Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Kwani deni linalipwa na pesa za nje?

Ni msaada tu ndio huwa za nje, borrowed zote ni za ndani. Unachanga unalipa... ukikamilisha mradi ni wako.

We ukikopa ukajenga nyumba then ukikamilisha mkopo ni bank imekujengea au we mwenyewe?
Ukiambiwa tunajenga kwa pesa zetu za ndani wew unaelewa ulichoandika? Wasukuma sijui mna matatizo gani.
 
Mkuu Samahani Nikuulize Vitu Gani Vinafanya Uchumi Ukue Ukitoa Hiyo Miundombinu Unayo Ikataa.

Unajenga reli kwa miaka 6 na bado haijakamilika. Haiingizi fedha yoyote na marejesho unapeleka si ukichaa huu. Mkopo ni ili kukamilisha mambo haraka haraka hela ianze kutengenezwa.
 
Tusipende lawama, amesema sasa inatosha. Muhimu ni kupima usahihi wa anachosema.

Mambo ya kulaumu kwann hukuwa shujaa hapo nyuma tukakusifia au kukucheka na fake id humu jamii forum hayana maana.
 
Kwa wakati huo alikuwa sahihi kulingana na mazingira yaliyokuwepo hivyo hakuna unafiki hapo.

Hata askari kuna wakati hurudi nyuma wakiwa vitani haina maana ni kushindwa vita huenda ni kwenda kujipanga upya au kuepuka kuangamizwa na adui mwenye nguvu ili kwenda kujipanga na kupigana vyema wakati mwingine.
 
Hayati alitwambia tunajenga hivyo vitu kwa pesa za ndani - Sasa deni la Taifa inakuwaje limekuwa kubwa namna hii?
Mkuu unajipotosha. Hili ni deni sio msada. Kama nchi inakopesheka means inauwezo wa kulipa kwa pesa italazozalisha. Means ina pesa zake
 
Unafiki na ujinga wake ni upi hapo?
Soma bandiko langu hapo juu nililo ambatanisha na document kutoka wizara ya fedha kuhusu deni la taifa..
Ndo uone huyo jamaa alivyo mjinga na mnafiki.
 
Hawa ndiyo wale wale boot lickers...Hapa hakuna kitu anatafuta kiki tu na kujipendekeza...Heshima yangu ndogo imeisha kwa huyu nshomile!
 
Ccm ni mashetani,ila Bro ulikuwa wapi wakati wa Maghu?
Haya hukuthubutu kuyasema?au
 
Hayati alitwambia tunajenga hivyo vitu kwa pesa za ndani - Sasa deni la Taifa inakuwaje limekuwa kubwa namna hii?
Kwani ni uwongo kwamba hakutumia pesa za ndani? Na mkopo pia alitimia mbona Direcyor wa ADB kila mara alikuja ku sign na alikuwa anasema tumepewa pesa sasa ADB inatoa misaada au mikopo?
Acheni maneno yenu...Tanzania kwa East Africa ndiyo nchi ilikuwa ina deni dogo kuliko nchi zote kubwa Kenya na uganda au na hilo mta bisha?

Angalia maendeleo na miradi hizo pesa imefanya...
 
Kama tunaweza kutumia ule wa kiraia wa Mwanza tunashindwaje kuutumia wa chato ambao umejificha kwenye macho ya wageni lakini bado unaweza kutumika kwa malengo yote mawili Kama ulivyo wa Mwanza kwa sasa.
Unajua uwanja wa Jeshi ulijengwa na nani?

Kuna miradi haipaswi kujengwa na watu wa kawaida kutokana na sensitivity Yake . Ndio maana hata ikuku ya Dodoma haijajengwa na makampuni ya nje ili wasijue Mambo mengi!


Nadhani utakuwa umeelewa

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mafisadi wameshambulia sufuria baada ya chakula kuisha wanakumbuka sasa kuwa hadithi haitasaidia kwakua raia wanachotaka nikuona miradi ikiendelea na siyo maneno wanakuja na cheap talks za deni
 
Hawa ndiyo wale wale boot lickers...Hapa hakuna kitu anatafuta kiki tu na kujipendekeza...Heshima yangu ndogo imeisha kwa huyu nshomile!
Kwamba asingekuwa yeye katiba isingefuatwa!!!
 
Sasa hilo la Magufuri kuacha 78T mleta mada kalitoa wapi Kama siyo ujinga na unafiki wa kipumbavu.
Au Hayati magufuli kafariki Jana,


Kwanini mnashindwa tu kusema kuwa mama ndani ya miezi sita kashakopa zaidi ya 10T iliyopelekea deni la taifa kupanda kutoka 60.9T April 2021 mpaka 78T October 2021.

Acheni tabia za kijinga za kuwasafisha wachafu walio hai kwa kuwachafua wafu walio Safi.
 
Huyu waziri wa Mipango asipoangalia hata hizo tozo zake atakosa chakueleza raia huko mbele ya safari...Pesa bila plan na jinsi ya kuizalisha kuleta tija zinaisha pasipokujua hasa kama wewe ni mtu wa maneno mengi bila matendo...Kumbuka benchmark aliyoiweka Hayati ipo juu sana na bila kubana matumizi haiwezekani kwakua ukweli ni kuwa nchi yetu ni masikini wa kipato....
 
Kipi kimekamilika?
Wewe makalio hujui hata kimoja kilichokamilika! Hizo hospitali za wilaya hazifanyi kazi? Flyover haifanyi kazi? Barabara haifanyi kazi? Shule za zamani hujaona zimekamilika na zina fanaya kazi?
 
Kwamba asingekuwa yeye katiba isingefuatwa!!!
Vyote pamoja na deni ambalo hajalidadavua lina maana gani kwakua kachukua tu absolute figures na kuzibandika hapo kisha kuwrka mtizamo wake bila kujali hiyo miradi iliyokopewa returns zake ni zipi....Je uchumi baada ya miradi kuisha mfano bwawa la Nyerere inge boost uchumi kiasi gani ukiunganisha na miradi yote ya kimkakati aliyoianzisha hayati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…