Balile: Mzee Butiku aache uwoga atutajie majina ya Wauwaji wa Kibao aone kama hatutachapisha, aache kututukana Waandishi!

No zinamwelewa lakini uchawa sasa ndo tatizo
 
Waandishi wa habari wamekua mchongo mchongoma sana... yaani kwa giant media house aliyebaki anaejitahidi kubalance story ni Mwananchi communications
 
Cc
Huyu anatumika na ccm?, anataka mzee wa watu ataje majina ili wamzingire.
 
Balile asimlaumu Mzee Butiku. Yeye na NGO yake wamefanya uchunguzi gani na kufichua siri gani? Investigative Journalism hakuna kabisa ! Wamebaki kuhongwa semina na kulipwa mamilioni ili waandike makala za udaku na uchawa tu !! Makala za watangazaji tu !
 
huyu tangu dp world hana thamani tena
 

Balile aache Uongo.... At the same time alishafika bei. Kama hawaogopi, mbona hakuna Gazeti leonlililoandika habari za Chadema na Samia Must Go aka SAMIA MUST FALL.
 
Mzee alitahiriwa bila ganzi tuwe wakweli...ni nani ataweza kuongea kama Butiku ? Anakwambia unachokiogopa ndo kitakuua....sema wanasiasa wanakwambia uandamane na familia zao ziko ulaya.....inafikirisha.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amesema kuwa Mzee Batiku ana uoga na kuwa hatakiwi kulaumu vyombo vya habari kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo kuripoti kwa kina masuala mbalimbali ikiwemo vitendo viovu vya utekaji na mauaji.

Anadai kuwa vyombo vya habari vinaweza kuchapisha taarifa ya wanaodaiwa kuhusika kufanya vitendo vya utekaji na mauaji endapo wakiwatajwa.

Akizungumza na 'Drive Show' ya East Africa Radio anasema kuwa vyombo vya habari havipo kwa ajili ya kuomba habari, hivyo kwa wahusika wa vitendo wakitajwa wataandikwa.

"Hili la Mzee Butiku, mimi nadhani hatugeuziani kibao lakini yeye ndiye anatuonesha msingi wa uoga, kwa sababu hatutatijie majina sisi tutaandika, sisi hatupo kuomba habari, yeye kama anawafahamu hatutajie" anasema Balile

"Anongeza Alikuwa kwenye Press conference alipaswa aseme ni fulani fulani harafu aone kama kama vyombo vya habari havitaandika, sasa yeye anafanya uoga anajificha mbele ya uoga na amekuwa na kawaida akitaka kufanya jambo pengine jamii imsikilize anatukana vyombo vya habari ndio anadhani kwamba labda hapo amepatia." anasema

Amesema kuwa haelewi Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa sasa inafanya nini. Anadai amekuwa akimuona Butiku akitoa matamko yanapotokea matukio.

"Kwanini yeye hataji lakini anaenda kusema vyombo vya habari vina uoga, mimi nadhani Mzee wetu tunamuheshimu sana tunaheshimu taasisi anayofanyia kazi ya Mwl. Nyerere Foundation japo mimi ukiniuliza sijui taasisi hiyo inafanya nini sasa hivi, uwa namuona akitokea matukio ndio naona hayo matamko"

Itakumbukwa Joseph Butiku ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alidai kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikishindwa kutimiza wajibu wake kwa kufuatilia kwa kina baadhi ya mambo na kuyaripoti kwa umma.

-
-
 
Kwann mkuu visubiri kupewa taarifaa na wasitafute taarifaa wao km wao Kwa kina zaidii na kuitolea ufafanuzi na kuanzisha kampenzi Kwenye vyombo vyao vinavyopingaa hv vitendo vya utekajii
 
Habari za kiuchunguzi kwa matukio ya aina hii sio kazi rahisi, hivyo waandishi pia waeleweke wakibaki kimya.

Pascal Mayalla
 
Katika watu wa hovyo kwenye habari ni wewe balile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…