Baada ya ufahamu wa siasa za kitanzania kwa muda mrefu, sasa nadhani baada ya kupata uzoefu wa taaluma yako kivitendo kupitia nyadhifa zako tano za kisiasa ndani ya muda mfupi, yaani 1) Kilanja wa tume ya kuchunguza mali za CCM, (2). Katibu mkuu wa CCM, (3) Mh, Balozi (4) Katibu Mkuu Kiongozi na sasa (5). Mh. Mbunge wa kuteuliwa, sasa taaluma yako uneitendea haki. Naamini ukirudi chuoni ukaendelea na kufundishia vijana utatupatia kilicho bora kabisa. Umeona figisu nyingi, umeona fitina za kutosha, umeona dhuluma za kufa mtu, umeshuhudia upigaji kura feki, imeshiriki matangazo hewa ya washindi wa chaguzi, imekaa Ikulu, na bungeni imekaa. Hakika wewe ni mwalimu tumtakaye. Nakushauri irudi kwenye ajira yako ya awali na ikimpendeza uje tena kutoa somo kwa wajumbe wa bunge la katiba mpya litakapoanza. Nakutakia kila lililo jema.