Balozi Bashiru Ally Sasa imeiva, Katende kazi,

Balozi Bashiru Ally Sasa imeiva, Katende kazi,

Papa1

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
2,017
Reaction score
2,210
Baada ya ufahamu wa siasa za kitanzania kwa muda mrefu, sasa nadhani baada ya kupata uzoefu wa taaluma yako kivitendo kupitia nyadhifa zako tano za kisiasa ndani ya muda mfupi, yaani 1) Kilanja wa tume ya kuchunguza mali za CCM, (2). Katibu mkuu wa CCM, (3) Mh, Balozi (4) Katibu Mkuu Kiongozi na sasa (5). Mh. Mbunge wa kuteuliwa, sasa taaluma yako uneitendea haki. Naamini ukirudi chuoni ukaendelea na kufundishia vijana utatupatia kilicho bora kabisa. Umeona figisu nyingi, umeona fitina za kutosha, umeona dhuluma za kufa mtu, umeshuhudia upigaji kura feki, imeshiriki matangazo hewa ya washindi wa chaguzi, imekaa Ikulu, na bungeni imekaa. Hakika wewe ni mwalimu tumtakaye. Nakushauri irudi kwenye ajira yako ya awali na ikimpendeza uje tena kutoa somo kwa wajumbe wa bunge la katiba mpya litakapoanza. Nakutakia kila lililo jema.
 
Simuombei mabaya ila hata hao wanafunzi ambao ataanza kuwafundisha baada ya misimu kadhaa ya kufaidi kwake, nao wanafunzi watakuwa wanajipigia tuition ya vipi jinsi ya kuwakwepa wanasiasa juu ya uongo wao hususani lecture wao ndani ya chuo.

Yaani usishangae akazalisha wanafunzi wapya ambao hawatoamini chochote baada ya kufundishwa na dokta balozi Bashiru.
 
Hakika wewe ni mwalimu tumtakaye. Nakushauri irudi kwenye ajira yako ya awali na ikimpendeza uje tena kutoa somo kwa wajumbe wa bunge la katiba mpya litakapoanza. Nakutakia kila lililo jema

Nyie wapigaji mnafikiri nchi hii ni ya majuha tutakaokubali kuwa na Bunge lingine la Katiba ili mpate ulaji kama ule aliowapa Vasco Dagama halafu hatukupata Katiba baada ya kutumia mabilioni ya shilingi? Kazi ya kumalizia ile ile Katiba iliyopendekezwa ndio imebaki na inaweza kumalizwa na wataalam wachache waliobobea kwenye masuala ya Katiba; mawazo ya watanzania yamo kwenye ile rasimu ya Warioba, iliyobakia ni kazi ndogo sana!!! No justification for bunge la Katiba!
 
Hahahahaha kila MTU anamuombea mabaya,na akiwa anapita kwenye mitandao atapata sonono.
 
Hahahahaha kila MTU anamuombea mabaya,na akiwa anapita kwenye mitandao atapata sonono.
Uzuri wa CCM, ni kwamba ukiwa mwanachama mtiifu, unaibuka tena - hata utende makosa makubwa aje! Mfano ni mingi: Kinana, Lowasa, Sofia Simba, Nape, Makamba, Mwigulu, Nyalandu, etc.
Hivyo siku za mbele kukuta Dr. Bashiru akiwa ameibukia wadhifa mwingine si ajabu.
 
Yaani, we acha tu.
Huyu alikua ameshikilia hatma ya wenye Nia wote wa kupata ubunge Tanzania nzima, mpaka ulinzi wa kutosha alikua nao, Leo ana hadhi sawa na mzee Halima. Wote Ni wabunge wakuteuliwa pendwa.
 
Bashir Hana vigezo vya hao wengine. Figisu zake zilikua too much.
 
Yaani, we acha tu.
Huyu alikua ameshikilia hatma ya wenye Nia wote wa kupata ubunge Tanzania nzima, mpaka ulinzi wa kutosha alikua nao, Leo ana hadhi sawa na mzee Halima. Wote Ni wabunge wakuteuliwa pendwa.
Kwamba hadi babu tale kamzidi
 
Back
Top Bottom