Ndugu zangu Watanzania,
Wakati vyama kama CHADEMA viking'ang'aniana na kila mtu alijitangaza kuwa ndiye mgombea Urais,wakati CHADEMA ikiendelea kupukutika na kukimbiwa na wanachama wote wenye akili Timamu na wanaojitambua,wakati vyama kama CHADEMA vikiwa vimepoteza kabisa mitaani kutokama na kuishiwa ajenda na sera,wakati CHADEMA ikiwa imepoteza ushawishi nakupuuzwa na watanzania pamoja na hivyo kushindwa hata kufanya ziara mikoani.
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Jasusi Mbobezi wa kisiasa,Mwamba wa kusini,kiboko ya upinzani, Kiongozi Mwenye misimamo na mzalendo wa kweli asiye teteleka wala kuyumba ,aliyejenga nidhamu na heshima ndani ya CCM kwa kushirikiana na Mwenyekiti wetu Shujaa na Jemedari wetu hodari Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Anatarajia kufanya ziara nzito sana mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi akiongozana na wajumbe wa secretarieti.Ambapo katika ziara hiyo nzito atazungumzia na kugusa masuala mbalimbali pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwasikiliza wananchi kero zao kama ilivyo kawaida ya usikivu wa CCM kwa watanzania.ikumbukwe ya kuwa kwa utafiti imeonyesha huyu ndiye katibu mkuu bora Mwenye nguvu , Ushawishi,anayeheshimika ,kukubalika na kusikilizwa sana kwa vyama vyote vya ukombozi kusini Mwa jangwa la Sahara.
Ni Katibu Mkuu ambaye haogopi kusema ukweli na kumkemea mtu yeyote yule atakayekwenda kinyume na maadili,ni kiongozi ambaye kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi.Kwake cheo ni dhamana na utumishi kwa watu. tutarajie makubwa katika ziara hiyo na kuona utofauti wa katibu Mkuu wa chama Tawala na vile vyama vya kuokoteza vijihoja na usaka Tonge kama ilivyo kwa CHADEMA.
View attachment 3053315
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.