Balozi Dkt. Slaa awakosoa waandishi kwa kuandika habari tofauti na alichokisema

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari, Dr Wilbroad Slaa amewalaumu waandishi wa habari kuwa walipewa fedha ili kuandika habari kuwa Dr. Slaa akubali mkataba wa bandari. Ambapo amesema kuonesha kuwa wamepokea fedha hata vichwa ya habari vilifanana kwa magazeti saba. Slaa ameongeza kuwa anayetaka hotuba aliyoandaa atampatia softcopy kuliko kwenda kutumia gharama ku-print copy halafu waandishi wasiandike.

Slaa amesema kwa sababu hiyo, ktk hotuba hii hatoisoma bali ataongea kwa uhuru na amesisitiza kuwa yeye hapingi uwekezaji bali anapinga masharti ya mkataba. Hicho ndicho anachoomaanisha.

Aidha ametoa wito kwa rais kuteua watu kutokana na uwezo na sio kwa sababu ya uchawa akitolea mfano wa Msigwa ambaye amemuona kama ni chawa.

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
 
NJAA waandishi nao wanafanya kazi nafikiri kilichoamua ni marupurupu.(waandishi fanya kazi kwa uaminifu tafadhari)
 
Akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari, Dr Wilbroad Slaa amewalaumu waandishi wa habari kuwa walipewa fedha ili kuandika habari kuwa Dr. Slaa akubali mkataba wa bandari. Ambapo amesema kuonesha kuwa wamepokea fedha hata vichwa ya habari vilifanana kwa magazeti saba. Slaa ameongeza kuwa anayetaka hotuba aliyoandaa atampatia softcopy kuliko kwenda kutumia gharama ku-print copy halafu waandishi wasiandike.

Slaa amesema kwa sababu hiyo, ktk hotuba hii hatoisoma bali ataongea kwa uhuru na amesisitiza kuwa yeye hapingi uwekezaji bali anapinga masharti ya mkataba. Hicho ndicho anachoomaanisha.

Aidha ametoa wito kwa rais kuteua watu kutokana na uwezo na sio kwa sababu ya uchawa akitolea mfano wa Msigwa ambaye amemuona kama ni chawa.

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
Dr atulie ale mafao ya kuhongwa ili akimbie vita akitokea chadema au hela alohongwa imeisha anatafuta kick wamhonge tena
 
Back
Top Bottom