Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Tetesi: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu

Siasa za kidemokrasia katika nchi za Demokrasia ni dhahiri wananchi wanajigawa katika pande mbili .Upande wa giza na upande wa nuru yaani Wema na ubaya .

Kwa sasa wetu wanamtaka Lisu ili siasa za Tanzania zihame kutoka kwenye siasa za upande wa wapigaji tu na anayeonekana kinyume na ufisadi anauawa au kushughulikiwa kisasa. Hii imejenga taifa la watu waovu na uovu unaonekana ndio dili. Rushwa imekua ni kama fasheni kwenye nchi hii. Watu wanaofanya biashara halali wanadharaulika ,watu wanaosema na kukemea ufisadi wanaitwa wabangaizaji . Yaani tumerudi zama za giza za kutukuza mali na kudharau haki na hekima . Mtu mwenye pesa hata akitema pumba kama Mbowe anaonekana ana busara .

Mbowe amesababisha mauaji na ulemavu wa watu wengi sana hapa Tanzania lakini hajawahi kusemwa serikali wala kukamatwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji isipokuwa ni wakati wa JPM tu ndio alihukumiwa na kupigwa faini kwa kusababisha mauaji ya Akwiline . Familia ya Akwelini ilitakiwa ufungue Kesi ya madai dhidi ya Mbowe baada ya hukumu kuonyesha kuwa Mbowe na wenzake walisababisha kifo cha Akwiline.


Mbowe kama anafikiria kuwa damu za wenzake ndio mtaji wake basi akimlazimisha ushindi wa Rushwa ndio mwisho na anguko la Chama chake na SACCOs yake .kwani Atakua alepoteza watu wengi na hivyo kupoteza Ruzuku kubwa .
CDM sio ya kufa leo wala kesho mkuu...

Hizi hoja za Rushwa na Ubaridi kwenye Vyama vya upinzani lazima tujiulize tunefikajd hapa?

Magufuli alisababisha kwa kias kikubwa sana huu ubaridi wa Upinzani, lazima tukubali muda ni element muhimu sana kwenye kuchambua mambo
 
Mbowe imekula kwake. Hizo hela wajumbe wamesema watachukua lkn kura zitaenda kwa Lisu
 
Mchakato wa uchaguzi huu umeonyesha kwa kiasi kikubwa mno namna gani vyama vyetu vipo compromised

Whether huu ni uzushi au la, tayari reputation ya FAM na CHADEMA yake ipo tainted perhaps beyond repair
 
Libaba lizima linang'ang'ania madaraka kitu ambacho kimemshinda zaidi ya miaka 20 sasa

Kipi kipya atafanya sasa?
Agenda yake kuu ni kuchukua tena na kuondoka akifikisha miaka 68. Akifikisha miaka 68, anaweza kudai ameombwa sana asiachie chama na wampe mitano tena ya mwisho🙂

It is madness kung’ang’ania madaraka kwa 21+ years unless hii taasisi ni mali binafsi ya familia
 

View: https://youtu.be/lU_QbyAtMUM?si=Qdt19WOd_IGi962F

Duuh, mimi sikuwahi kufikiri wala kudhani kabisa kuwa kamanda wa anga na mwanaharakati wa siasa za mageuzi Tanganyika ndugu Freeman Mbowe kuwa ni shetani wa CCM - kijani aliyejificha kwenye gwanda la khaki la CHADEMA...!!

Katika VideoAudio Clip hiyo, Balozi Dr. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA kwa miaka 12 (2003 - 2015) na kufanya kazi chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe anafichua siri ya vikao kati ya Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CCM (Taifa) ambaye pia ni Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan...

Dr Wilbroad Slaa anasema, amepewa taarifa na vijana wake ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) juu ya kikao kati Rais Samia/CCM na Freeman Mbowe kujadili namna atakavyosaidiwa kushinda uenyekiti...

Anaendelea kusema kuwa, Rais Samia amekubali kumuongezea pesa Freeman Mbowe ili kugharamia mikakati ya ushindi wake na kwa hiyo wajumbe wajiandae kula pesa za bure za Samia Suluhu Hassan...

Aidha ameitahadharisha kambi ya Tundu Lissu kufahamu kuwa, Freeman Mbowe atapata msaada toka TISS, polisi na UVCCM wengi wataingia kama wajumbe wapiga kura na watavalishwa magwanda au jezi rasmi za CHADEMA...

Je, wajumbe 1,200 watashindwa kufahamiana na kudhibitiana ndani ya ukumbi? Timu Tundu Lissu fahamuni hili, jiandaeni kwa mapambano. Fanyeni kama TLS walivyofanya kumpigani Boniface Mwabukusi na kuibuka mshindi wa u - Rais wa TLS...

Yeye Mbowe afanye hivi, kwenye huu uchaguzi arudishe hela zake tu mana akishinda atapunguza mashabiki wa upinzani kumuelewa, atabaki na hao wanaokula naye ruzuku. Hata akiitisha mkutano wa hadhara wa zile kampeni zao kama kipindi kile watakuwa wanahudhuria wachache au hakuna kabisa.
 
CDM sio ya kufa leo wala kesho mkuu...

Hizi hoja za Rushwa na Ubaridi kwenye Vyama vya upinzani lazima tujiulize tunefikajd hapa?

Magufuli alisababisha kwa kias kikubwa sana huu ubaridi wa Upinzani, lazima tukubali muda ni element muhimu sana kwenye kuchambua mambo

Magufuli hakuwahi kuwa Mungu.
Ubaridi ulisababishwa na Mbowe maana alizoea rushwa ya awamu ya Nne na ushikaji. Biashara za kukwepa kodi n.k.Akajenga chuki na kutafuta urafiki kwa mahasimu wa JPM . Hapo moto ukawaka
 
Yeye Mbowe afanye hivi, kwenye huu uchaguzi arudishe hela zake tu mana akishinda atapunguza mashabiki wa upinzani kumuelewa, atabaki na hao wanaokula naye ruzuku. Hata akiitisha mkutano wa hadhara wa zile kampeni zao kama kipindi kile watakuwa wanahudhuria wachache au hakuna kabisa.
Mbowe akiwa tena mwenyekiti atakuwa kama huyu hapa chini
 

Attachments

  • GfuY-ekXQAAK7pI.jpeg
    GfuY-ekXQAAK7pI.jpeg
    68.5 KB · Views: 4
Silaa kila kitu kinaishia katikati upadre,Uccm,ukatibu mkuu,ndoa,ubalozi na mengineyo,bora Lisu asingemhusisha,mzee muongo na anazeeka vibaya.Nani anaweza kumwamini hata Rostam alimshangaa sana
 
Hakuna ukweli kwenye siasa

Ndiyo mwamba anavyoamini? Kama ndivyo basi haina shaka u CUFU uleeee unazidi kujongea:

GfuY-ekXQAAK7pI.jpeg


Tuna imani na Li-ssu, oya oya oya ..!
Lissu kweli, ..!
Oya oya oyaa!

Siasa za kiujanja ujanja, machale machale, zisizokuwa na sera nani anataka?
 
Ndiyo mwamba anavyoamini? Kama ndivyo basi haina shaka u CUFU uleeee unazidi kujongea:

View attachment 3196732

Tuna imani na Li-ssu, oya oya oya ..!
Lissu kweli, ..!
Oya oya oyaa!

Siasa za kiujanja ujanja, machale machale, zisizokuwa na sera nani anataka?
Yupo location anafanya bongo movie au yupo kwenye mtukano?
 
Back
Top Bottom