Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Kuna wakati ukiona maisha ya viongozi wakubwa wakisiasa yalivyo ya luxury unatamani ungekuwa mmoja wao au pengine hata watoto wako mmoja wao aje kuwa kiongozi mkubwa wa kisiasa kwasababu huko kuna hela na maisha ni hela
Magari wanayotembelea, nyumba wanazoishi, maisha wanayoishi, ilivyo rahisi kwao na wanafamilia wao kupata kazi, kupata huduma za kijamii zilizo bora, upendeleo kwa kila kitu, heshima, hadhi nakadha wa kadha
Vyote hivyo vinaweza kukufanya uvutiwe na maisha yao
Hata hivyo ukitafakari visanga na mikiki mikiki wanayoipitia unaanza kuwaonea huruma wao na familia zao na kupenda maisha yako uliyo nayo
Kuna siku nimejikuta natoa machozi kwa kumkumbuka Polepola na namna familia yake wakiongozwa na Mama yao mzazi walivyomlilia kipindi kile ametwaliwa na wasiojulikana kutoka alipokuwa anaishi
Ndugu kuondokewa na ndugu yao bila kuona kama amekufa au amekuwaje inaumiza sana
Hakuna anayejua familia ya Dr. Balozi Emmanuel Nchimbi inapitia wakati gani kwa mtu wao kujiondoa ghafla kwenye madaraka makubwa huku ikifuatiwa na kutimuliwa uanachama
Kwa vyovyote vile, huyu ana ndugu ambao nao ni wanachama wa chama chake; swali ni je wanaishije huko kwa sasa? Wanaangaliwaje? Wanawaangaliaje waliomtimua ndugu yao?
Vivyo hivyo bilashaka ana ndugu, jamaa na marafiki wanaofanya kazi serikalini pengine kwenye idara au sekta nyeti nyeti.
Swali ni lile lile; wanaangaliwaje? Wanawaangaliaje waliosababisha ndugu yao kuachia ngazi? Wanaangalianaje huko waliko?
Kuna hawa wanasiasa wa upinzani ukiona wanavyoburuzwa na mapolisi kila kukicha, wanavyopandishwa kwenye makarandinga, kila siku ni lock-up lock-up na wao, mahakamani kumejaa kesi zao na kadhalika kiasi kwamba huwezi kutamani maisha yao
Kitu pekee kinachoweza kukufanya ufanikiwe ni kuwa mnafiki, chawa na kujifanya zwazwa kwa wakubwa zako ili uendelee kuwepo
Kwenye siasa hutakiwi kwenda na akili zako timamu wala kuwaza na kutenda haki
Kwenye siasa hutakiwi kuwa mzalendo kwa nchi yako badala yake unatakiwa kuwa mzalendo kwa chama chako na viongozi wa chama chako. Hapa ni kwa wote, wa chama tawala na vile vya upinzani
Mfano mzuri ni Balozi Hamphrey PolePole na Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi
Hawa manguli kuna namna wametuachia maswali mengi ya kutafakari kabla haujaamua kuwa mwanasiasa au mwanafamilia wako kutamani kuwa mwanasiasa
Hawa ni somo tosha kwa wote wanaotaka na kutamani kushika nyadhifa kubwa za kisiasa
Walikuwepo kina Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, David Kafulila, kina Massele na wengineo.
Waliwatetemesha watawala, waliwavutia watawaliwa.
Lakini kwasasa ni kama kwao kuna machache sana ya kujifunza kuliko kwa kina Polepole na Nchimbi
Kupitia hawa inabidi jamii iamke na ijue kwamba Nyerere na wenzake hawakupata uhuru kirahisi hivyo bila mashinikizo kwa watawala itakuwa vigumu kwao kutenda haki
Watawala wa kisiasa wanafanana!! Wakishakalia viti kwao haki kwa wananchi inageuka anasa!
Hawataki kuambiwa na anayethubutu kuwaambia anageuka mhaini adui mkubwa. Hiki ndicho kilicho wakuta ndugu zetu Nchimbi na Polepole