mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Hivi unaijua lugha ya mabeberu!! Kwa mabeberu mahali panaponyonyeka hapo ndipo wanapopasifu kuwa ni salama kuwekeza!! Kwa mfano Richmond ilivyotunyonya katika kuiuzia tanesco umeme kwa bei mbaya hapo, kwao ndiyo salama. Wanakuuzia kwa kigezo cha capacity charges!! Richmond ikabadilika jjna ikawa Dowans! Dowans ikabadilika jina ikawa Symbion!! Mitambo ile ile. Kwa kigezo cha capacity charges, uwezo wa mitambo yao kuzalisha umeme ndiyo unayolipia na siyo kiasi cha umeme ulioutumia!! Kwa jamaa hawa capacity charge kwa siku moja ni sh.152,000 000/=, Hata kama haujatumia kabisa umeme wao, lakini bado utalipa kiasi ambacho wana uwezo wa kuzalisha na siyo waliozalisha!! Kwa hiyoTanesco walikuwa wanalipia umeme ambao hawajautumia na hawauhitaji hasa wakati wa masika ambapo mabwawa ya kufua umeme kama mtera, nyumba ya Mungu na kidatu yakiwa yanazalisha umeme wa kutosha !Kupitia chombo fulani cha habari, nimemsikia Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberatha Mulamula akidai kwamba kwa sasa Wamarekani wanaamini kuwa ni salama kuwekeza Tanzania, lakini hasemi ni wakati gani Wamarekani waliona si salama kuwekeza Tanzania.
Mabeberu wakikusifu tayari ujue wameshaona mwanya wa kukunyonya!! Ndiyo maana mabeberu hawampendi mchina maana mchina hanyonyeki!!