GE2025 Balozi Polepole aapa kutorudi nyuma hadi mchakato wa Wagombea Urais CCM kuanza Upya. Amuonya anayezima Mtandao

GE2025 Balozi Polepole aapa kutorudi nyuma hadi mchakato wa Wagombea Urais CCM kuanza Upya. Amuonya anayezima Mtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Polepole!! Huyuhuyu polepole ambaye bunge lililopita yeye ndiye alikuwa msatari wa mbele kuhakikisha wapinzani hawaingii bungeni!!

Ni walewale tu kama ilivyo kwa wilbroad na haruna
Leta ushahidi acha Maneno....
 
Polepole!! Huyuhuyu polepole ambaye bunge lililopita yeye ndiye alikuwa msatari wa mbele kuhakikisha wapinzani hawaingii bungeni!!

Ni walewale tu kama ilivyo kwa wilbroad na haruna
Ameweza kuteka akili za mabumunda
 
Narudia..Hoja na Mtu vinaenda sambamba...Hoja itaenda peke yake ikiwa tu hyo mtu ameachana na siasa au kaanzisha chama chake..Hvyo mnaosema Polepole asijadiliwe bali jadili hoja zake kuna kitu mnataka kutukwepesha..
 
Kwa hiyo Uzalendo wa Polepole umekuja baada ya kuona maslahihi yake yamebinywa?
Hatuangalii masrahi ya polepole Wala masrahi ya kikwete au masrahi ya mama na hata Lizi 1.

Tunaangalia masrahi ya taifa. Uwajibikaji na Uzalendo.

Kwa kujidai vipofu na viziwi myaweza sana
 
Mimi binafsi, nikiwa na Akili yangu Huru, Moyo safi, bila upendeleo wowote , Ninamkubali sana Polepole , Polepole ni Moja ya Watanzania wenye Akili nyingi sana .

Uwezo wake kupangilia Hoja.
Uwezo wake wa kuthubutu.
Uwezo wake wa kuchambua mambo.
Uwezo wake wa maono.
Uwezo wake wa Ushawishi.
Uwezo wake Mvuto anapokua anaongea.

Uwezo wake wa Kujiamini .
Uwezo wake wa Utambuzi wa Dunia.

Sina mashaka kabisa, kua Polepole ni Moja ya watu ambao akiwa Rais huwezi kua naye Mashaka yaan ni hivi

Polepole
LISSU
Mpina
Gwajima

Hawa Mmoja wao akiwa Rais, Furaha itakua ni sehem ya kawaida ya Maisha ya mwanadam.

Akikazia muda huu juu ya Hotuba yake Kwa Taifa usiku wa Leo.

1- Kawataka watanzania Leo kujionea USHAHIDI wa kwanini Rais Samia hatakiwi kuendelea .

2-Amuonya Muhusika wa Kuzima Mtandao, akisema, Once Nchi imenyooka , Atawajibishwa Kisheria Kwa kaliingizia Taifa Hasara ya Bilion Tano .

Wakuuu ni Saa mbili kamili usiku.

Mnakumbuka niliwaambia humu, Katu ya Tarehe 1-7 Nchi itasimama?.
Mkuu nimeskitika wazee wazima wameufyata japo mzee Butiku nae amejifanya kuongea lakini kawa muoga anazunguka mbuyu, labda mzee anaogopa kuambiwa na wewe una mawaa kwenye Kigoda cha Mwalimu.
 
Namuombea sana Ndugu polepole, naamini katika yeye wapo watu wa vyombo vya usalama. Hakurupuki, ni vile tu jeuri wa hao familia.

Akipata uungwaji mkono na watanzania waliowengi itakua poa sana. TZ sio ya familia flani tu kuongoza, ni ya Watz wote. CCM sio yao, Ccm ni chama cha siasa cha UMMA. Wasijimilikishe nchi na chama, hivyo vyote wamevikuta na wataviacha.
Kabla CCM haijawepo Tanzania na Baraza la usalama was taifa lilikuwepo,kabla samiah na jk hawajashika hatamu Ccm na Tanzania Walishakuwepo kitambo plus Baraza la usalama lilishakuwepo!

Ukweli mchungu ambao watz hawaambiwi ni kwamba system za kiusalama zimefanya compromise na utovu wa nidhamu wa viongozi waliopewa dhamana nankuharibu utaifa wetu!

System ya kisalama ifumuliwe coz imeshindwa kuwa pro active kwenye hatma na maswala mtambuka ya kitaifa ndio maana tumeangukua kwenye ujinga uliopo!!

Mini simumunyi maneno nasema hivi Baraza la usalama na deep state kama wapo wametusaliti watanzania na taifa letu!!

Haiwezekani leo mafisadi wanateka chama na wanafanya wafanyavyo na hatuna Cha kuwafanya na wanaharibu Kila kitu na wote wanajiona wanaweza kufanya lolote!!

Tumia akili na wenzake na nyuzi zao wametuangusha sana aiseh!!

Nasubiri kuona!!
 
hao uliowataja ni CCM ni vile inajibadilisha humo humo kiutendaji na kichama..
 
Acheni kutudanganya watanzania!

Nchi haiwezi simama kwa press za kina pole pole!

Labda kama ingekua kamandi ya kijeshi ikiitisha press hiyo na sio wanasiasa!!

Ifike mahali mwache kuleta tension zisizo na maana kwa watanzania!

Tumekubaliana kama taifa,tuwe taifa la rushwa,siasa ilipe sana kuliko taaluma,familia kubwa kubwa ndio zishike siasa zetu,tuzalishe chawa !pia wanajeshi walinde mipaka huku ndani ya nchi wizi nanufisadi uwepo wa kutosha!

Hayo ni maamuzi ya wenye mamlaka Hali iwe hivyo na huo ndio uwe utambulisho was taifa letu Hadi kimataiga kwamba ni taifa la wapiga deal na mafisadi!!
Kwa kweli 🤣
 
Hizi propaganda tu zinazofanywa na CCM kuteka tention za watu kipindi hiki cha uchaguzi, hawa watakuwa ktk fungu lao na wameandaliwa kabisa kuisema vibaya CCM alafu baada ya uchaguzi utawaona wanakuja na hoja ya maridhiano. ni kama lowasa kipindi cha Magu.
Sure indeed ,

Inaitwa devide and rule
 
Mwenye link ya press ya Balozi tafadhali
 
Hizi propaganda tu zinazofanywa na CCM kuteka tention za watu kipindi hiki cha uchaguzi, hawa watakuwa ktk fungu lao na wameandaliwa kabisa kuisema vibaya CCM alafu baada ya uchaguzi utawaona wanakuja na hoja ya maridhiano. ni kama lowasa kipindi cha Magu.
huu mchezo wawafanyie wenye akili ndogo, akili kubwa wanajua ni mchezo gani unachezwa
 
Back
Top Bottom