Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Katika mchango wake wa hivi karibuni juu ya Katiba Mpya, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue amekuja na hoja kwamba “Kupunguza Madaraka Ya Rais Ni Hatari Kwa Usalama Wa Nchi”, na kusisitiza kwamba kuna umuhimu wa madaraka hayo kubakia kama yalivyo chini ya Katiba Mpya;

Hoja ya Balozi Sefue imepokelewa kwa hisia mbalimbali, lakini hisia zinazotawala mijadala mingi ni za kupinga hoja kuliko kuunga mkono hoja Ni muhimu pande zote mbili za hoja zikapewa nafasi ya kusikilizwa, lakini ni muhimu zaidi ikaeleweka kwamba wanaopinga hoja ya ya Balozi Sefue ni wahanga wa kuyumba kwa uongozi wa nchi kwa muda mrefu sasa – kisiasa, kiuchumi na kijamii, hasa katika suala zima la maamuzi muhimu na magumu katika uongozi wa taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii, vinginevyo hakuna dalili yoyote kwamba wapinga hoja ya balozi Sefue ni watanzania waliokosa Uzalendo kwa Taifa lao au ni watanzania wasio litakia mema Taifa lao. Kimsingi, watanzania wengi wanazidi kuamini kwamba tatizo la kuyumba kwa uongozi wa taifa pamoja na madhara makubwa kwao kisiasa, kiuchumi na kijamii litapatiwa ufumbuzi iwapo tu taasisi ya Urais itapunguziwa madaraka yake chini ya katiba ya sasa.

Ni muhimu tukatambua kwamba Katiba ya nchi iliundwa kwa makusudi ya kufanya Rais wa nchi awe ‘the living symbol of our National Unity”. Kwa mtazamo wangu, hili ndio chimbuko la hoja ya Balozi Sefue. Mjadala kuhusu jinsi gani taasisi ya Urais imefanikiwa au imefeli katika hili, ni mjadala mwingine. Vinginevyo hili ni suala ambalo pengine linachangia kwa kiasi kikubwa kuibuka kwa hoja nyingi juu ya udhaifu wa taasisi ya Urais katika nyakazi hizi za Mageuzi ya Kisiasa kuelekea Mfumo wa Demokrasia ya Uliberali inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, mageuzi ambayo nilijadili sehemu nyingine kwamba - kitendo cha Rais Kikwete kuyaruhusu yatokee kwa kasi zaidi kuliko Marais waliomtangulia, kimechangia sana kwa Kikwete kuonekana ni Rais dhaifu kwa mujibu wa hoja ya Mh. J.J Mnyika, mwaka 2012.

Vinginevyo tangia uhuru, taasisi ya Urais imekuwa ikikabiliwa na UDHAIFU MKUBWA, lakini tofauti na Kikwete, Marais waliomtangulia walificha madhaifu haya kwa njia mbalimbali, hasa kupitia udhibiti wa mageuzi ya kisiasa na kuruhusu democratization kuingia nchini kwa mtindo wa Top – Down Approach (badala ya Bottom – Up), kwa mfano implementation ya maoni mengi ya tume ya Nyalali ‘incrementaly’ badala ya ‘radically’, ambapo tume ilipendekeza sheria kadhaa pamoja na vifungu fulani fulani vya Katiba ya 1977 vifanyiwe marekebisho ili Katiba ya nchi iendane na mhaitaji ya mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lakini badala yake, mapendekezo mengi (pamoja na suala la Katiba Mpya) yaliwekwa pembeni na serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka ishirini. Suala lingine linaruhusu ‘Uhuru wa Vyombo vya Habari’ ambavyo katika awamu za nyuma, lilidhibitiwa kikamilifu.

Kwahiyo incremental implementation ya demokrasia ya uliberali nchini pamoja na udhibiti wa vyombo vya habari vilisaidia sana kwa marais wa awamu za nyuma kukinga madhaifu ya taasisi ya Urais yasijitokeze, madhaifu ambayo kimsingi ni ‘inherent to our problematic state since the first day of independence in 1961’. Uamuzi wa Rais Kikwete kuruhusu yote haya chini ya utawala wake ndio imemfanya awe mhanga wa maamuzi yake mwenyewe na kuonekana dhaifu per Mnyika’s argument.

Ili kujikinga na madhaifu yanayoendana na taasisi ya Urais (The Executive) inayoongoza ‘A PROBLEMATC STATE OF TANZANIA’, ndio maana Mwalimu alikuwa akisisitiza na ku ‘justify jinsi gani:

“Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State”.

Madaraka husika ya Rais ambayo yamezidi kuzua controversy katika awamu ya nne ambayo pia kimsingi ndio yanabeba hoja ya Balozi Sefue includes:

• He/she is the head of state with Full Executive Powers and Commander in Chief of the Armed Forces;
• The Cabinet which he appoints largely from MPs is ‘only’ advisory to him;
• He has full powers to appoint, promote, dismiss and to exercise disciplinary control over the Civil Service including the Judiciary and so forth;
• He/She also has an overall responsibility for Government Organization and Direction;

Under a new and young Nation, Mwalimu aliona umuhimu wa kuweka haya katika Katiba i.e. the country’s Constitution was deliberately designed to create a powerful Chief Executive who would give the nation vigorous national leadership. Lakini pia, Mwalimu understood of the challenges ahead and in one of his speeches he argued that:

“We recognize that the system of checks and balances is an admirable way of applying the brakes to social change. Our need is not for brakes – our lack of trained manpower and capital resources, and even our climate, act too effectively already. We need accelerators powerful enough to overcome the inertia bred of poverty, and the resistance which are inherent in all societies.”

Source: J.K Nyerere, “How Much Power For a Leader”, The Observer, June 1962. Reprinted in African Report, Vol. 7, No. 7, July 1962, p.5.
________

Mwalimu also understood of the threats that lied ahead, and in one of his speeches he contended that:

“Our Union has neither the long tradition of nation-hood, nor the strong physical means of national security, which older countries take for granted. While the vast mass of people give full and active support for their country and its government, handful individuals can still put our nation into jeopardy, and reduce to ashes the efforts of millions.”

Source: President’s Speech at the Opening of University College, Dar-es-salaam, 21 August 1964, Dar-es-salaam, Ministry of Information and Tourism, p.17.
____

Nyerere assumed ‘full executive powers’ kutokana na ukweli kwamba baada ya uhuru, kazi ilikuwa ni Economic Development that was supposed to deliver also on the social front, bila ya kuathiri ‘UMOJA WA KITAIFA’. According to Mwalimu:

“New Nations like Tanganyika are emerging into independence as a result of a struggle for freedom from colonialism…Once the first free government is formed, its supreme task lies ahead, the building up of the country’s economy, so as to raise the living standards of the people, to eradicate diseases, to banish ignorance and superstition. This is no less than the struggle against colonialism, calls for the maximum united effort by the whole country if it is to succeed. There can be no room for difference or division…This is our time of emergency and until our war against poverty, ignorance and disease has been won, we should not let our unity be destroyed by a desire to follow somebody else’s book of rules”.

Source: ‘One Party Rule’, Spearhead, Dar-es-salaam, November 1961. Reprinted in Paul E. Sigmund Jr., ed., The Ideologies of Developing Countries, New York: Frederick A. Praeger, 1963, pp. 197 – 202.
_______________

Ili kuweza kufanikiwa katika kazi hii, to Mwalimu, it was necessary for the country to become a ‘ONE PARTY STATE’. In one of his speeches, Mwalimu argued that:

“The Tanzanian System of one party democracy was designed to enable people to elect a competent government which reflects their wishes and desires and to do this without damaging the society and the long term objectives they have set for themselves”

Source: The Nationalist, July 1970.
___________

However, Mwalimu also warned that:

“In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU”.

Source: Socialism & Participation: Tanzania’s 1970s National Elections: The Election Study Committee, University of Dar-es-salaam, 1974.
_________________

Na mwisho ni juu ya URais na Usultani/Ufalme na Udikteta. Miaka michaceh baada ya uhuru, watanzania wengi walikuwa wanajenga hoja kwamba kuna umuhimu wa Mwalimu Nyerere kuwa “Rais wa Maisha” na kwamba Katiba itamke kwamba hapatakuwa na uchaguzi katika ngazi ya Urais nchini Tanzania. Mwalimu alijibu hoja hizi kama ifuatavyo – akilenga Katiba ya nchi:

“It should be able to fit any person tall or short, fat or slim. It is not like a dress which is cut to fit a particular person. The people often inspired to the idea of having a life president because they trust their leaders but the present constitutional provision that every five years we should have a presidential election is quite convenient. May be after five years of office the electorate will want another leader or may be the leader himself will want to be relieved. It should be clearly understood that people change…the way is – if we want him we will elect him again after five years; if not, then we say ‘sorry’ to him. We are not electing to the President a Sultan but a worker”

Source: The Standard, 12 September 1970.
________________

HITIMISHO

Tukirudi kwenye hoja ya Balozi Sefue juu ya umuhimu wa kubakisha madaraka ya Rais kama yalivyo katika Katiba Mpya, kuna masuala kadhaa muhimu ya kujadili, ikiwa ni pamoja na haya yafuatayo:

• Moja: How Far Do We Still Agree With Nyerere that:

“POWER IN THE RIGHT HANDS IS GOOD AND INDEED NECESSARY FOR A NEW STATE?

Hili ni swali muhimu hasa kwa watanzania ambao bila ya kujijua wamekuwa ni kigeu geu kwani kwa upande mmoja wanataka rais ajaye asiwe na madaraka kama ilivyo chini ya katiba ya sasa, lakini kwa upande mwingine, hao hao wana hamasa kubwa ya kutaka rais ajaye awe na uwezo wa kufanya maamuzi magumu, huku wakipendekeza umuhimu wa kuwa na Kiongozi kama Rais Kagame wa Rwanda na kutaja taja baadhi ya Wanasiasa ambao wanadhania watakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Ni muhimu kundi hili likatambua kwamba – UKAGAME utakuwa ni mgumu sana chini ya Katiba Mpya iwapo madaraka ya sasa ya Rais yatapunguzwa kama wanavyopendekeza.

• Mbili – Kinachokera wananchi wengi kuhusu ukubwa wa madaraka ya Rais Kikatiba ni nini hasa: Je, ni kwamba bado tunahitaji Rais mwenye ‘full executive powers’ lakini tatizo ni kwamba such power is in the wrong hands? Au ni kwamba haijalishi nani au chama gani kinatoa Rais wa Tano, Suala la Rais kuwa na ‘full executive powers’ kwa Tanzania limeshapitwa na wakati?

• Tatu – Kwa wale wote wenye mapenzi na vyama vya upinzani – hasa Chadema, kwa maoni yenu, ili Rais atakayetokana na Chadema (kwa mfano) awe na uwezo wa kuirudisha nchi katika mstari, je atafanikiwa zaidi iwapo ataendelea kuwa na ‘full executive powers’ kama ilivyo ndani ya Katiba ya sasa ambapo atakuwa in a better position kutekeleza majukumu yake ya Urais kwa ufanisi zaidi au uwezo wake kurudisha nchi katika mstari na pia kuongoza kwa ufanisi zaidi utajitokeza iwapo nguvu na mamlaka ya Rais yanapunguzwa chini ya Katiba mpya?

• Nne – kutokana na dhana iliyojijenga miongoni mwa vyama vyote vya siasa kwamba umuhimu mkubwa wa Chaguzi Kuu ni kushinda ili kukamata dola na kuunda serikali - na iwapo tunakubaliana kwamba “Tanzania As State is Problematic” kwani tangia uhuru tumejikita zaidi katika kuunda serikali badala ya STATE BUILDING & CONSOLIDATION, Je, juhudi zetu towards State Building zitafanikiwa zaidi chini mwenye full executive powers au asiyekuwa na such powers?
 
Ninavyoelewa issue ya madaraka ya Rais iliwahi kutolewa ufafanuzi mzuri tu na Mwl Julius Nyerere!

Swali ni je mazingira yale ya Mwl yapo hadi sasa? Msingi wa nchi hii bado changa kama alivyochagiza Mh Malecela una ukweli?

Mwisho mimi naunga mkono hoja ya kupunguza madaraka kwa Rais walau kwa mihimili muhimu!
 
Ninavyoelewa issue ya madaraka ya Rais iliwahi kutolewa ufafanuzi mzuri tu na Mwl Julius Nyerere!

Swali ni je mazingira yale ya Mwl yapo hadi sasa? Msingi wa nchi hii bado changa kama alivyochagiza Mh Malecela una ukweli? Mwisho mimi naunga mkono hoja ya kupunguza madaraka kwa Rais walau kwa mihimili muhimu!

Mazingira ya nchi ni tofauti sana na enzi za mwalimu, vilevile historia na matukio ya siku za karibuni zinaonyehsa wazi yanaonyesha wazi kuwa kuna haja ya kumpunguzia madaraka raisi ili kupata ufanisi katika utawala bora na kuboresha demokraisa.
 
Mchambuzi hii ni hoja ya msingi sana uliyoleta hapa.

Kwa maoni yangu Kikwete ametusaidia sana kujua madhara ya raisi kuwa na madaraka makubwa sana. Amekuwa akiteua washikaji zake pamoja na washikaji wa mwanae rizimoko kushika nyadhifa mbalimbali za kiserikali, mashirika ya umma na taasisi mbalimbali ambao wengi wao wamethibitika kuwa na uwezo mdogo sana wa utendaji kazi na wengine wamebainika kuwa hawana uwezo kabisa wa kutekeleza majukumu yao.

Hata hivyo imebainika raisi kuingilia utendaji na ufanisi wa mihimili mingine hasa mahakama na bunge kwa kuteua watendaji wakuu wa mihimili hiyo na kuifanya isiwe na uhuru kamili katika kutoa maamuzi.

Kwahiyo ni muhimu sana madaraka ya raisi yadhibitiwe kama kuyapunguza itahatarisha usalama wake ama usalama wa nchi/wananchi kwa namna yoyote ile.
 
Last edited by a moderator:
Hawezi kutoa maoni tofauti na yaliyopo sasa,JK hatamuelewa,na sababu inawalinda watenda maovu,hawezi kusema lolote!ukitaka aseme subiria akitoka au atoe kwa maandishi na asitaje jina lake,hapo sawa!
 
Angalizo, Mchambuzi tunakuheshimu sana usitumike kwenye issue kama hii!

Hilo ni ombi langu binafsi hasa kuzingatia uzito wako hapa JF!
 
Mchambuzi

Umenena vema, swala hili binafsi natatizwa nalo. Kwanza ni lazima tujadili madaraka hayo tunayatoa kwa rais na kuyapeleka wapi? Je sababu zile ambazo taasisi ya urais inalalamikiwa kwa madaraka hayo kurundikwa hazipo huko tunakotaka kuhamishia hayo madaraka?

Ni katika Tanzania hii hii ambapo kuna taasisi zinashutumiwa kwa ukabila na udini. Kuna taasisi ambazo pia ni mihimili zimeshutumiwa mchana kweupe tena nyingine baina ya wajumbe wake kwa rushwa na upendeleo. Hakuna taasisi hata moja ambayo kwa uchache tu wa vigezo vya utawala bora kama uwazi, uwajibikaji, nidhamu na ushirikishaji wananchi inaweza ikasimama kifua mbele katika nchi yetu. Kuyatoa madaraka haya mikononi mwa rais na kuyapeleka mikononi mwa taasisi hizi mfu si kumaliza tatizo bali kuliamisha tu na pengine kulikuza zaidi. Wengine tunazungumzia kupeleka madaraka kwa umma as if umma tunaouzungumzia ni sisi watanzania wote kwa umoja wetu. Hakuna kitu kama hicho popote pale duniani, bado tunazizungumzia taasisi zile zile kama ilivyo taasisi ya urais.

Hatuna budi kuupanua mjadala huu ukilenga pia kufumua mfumo mzima wa taasisi zetu ili at least ziwe na medium standards za utawala bora. Na hii ndio fursa, mjadala wa katiba mpya unahitaji kuelekezwa katika kuunda Tanzania ya kimfumo. Tanzania inayojengwa na taasisi imara zinazoweza kutoa maamuzi kwa uwazi pasipo shaka. Kwa hivi tunavyojadili kupunguza madaraka ya rais pasipo kujadili hizo taasisi zingine na udhaifu wake wa kimfumo bado nasimamia maneno yangu kuwa huko ni kukaribisha maafa.
 
Kwa hoja yako, ina maana kwamba ili kuepuka matatizo husika tuna mbadala wa kuyadhibiti madaraka ya Rais na kwamba jawabu lake sio kuyapunguza; hoja hii ni nzuri kwa kweli kwani kwa nchi zinazofuata presidential system kama marekani, Rais wa nchi ana madaraka makubwa sana lakini wenzetu wamefanikiwa sana kuyadhibiti kupitia checks and balances mbalimbali;
 
Angalizo, Mchambuzi tunakuheshimu sana usitumike kwenye issue kama hii!

Hilo ni ombi langu binafsi hasa kuzingatia uzito wako hapa JF!

Natumaini pia umesoma msingi wa hoja yenyewe Mtazamo; Naomba upitie kipengele kimoja baada ya kingine kisha ueleze ni kipi hasa kinaonyesha kwamba kuna ishara za mimi kutumika na watawala katika hili; Kama ulikuwa makini kidogo katika kusoma hoja yenyewe, nacholenga ni kuangalia nguvu hizi za rais zilianzia wapi, na kwanini, na pia kwanini awamu ya nne inaonekana kuwa dhaifu kuliko awamu zilizopita; nadhani ni katika kujenga hoja hii ndio inaonekana kama vile namtetea rais wa sasa wakati ukweli ni kwamba kama udhaifu katika utawala wake, udhaifu upo na kupingana na hili ni kwa kutumia akili ya mwendawazimu;
 
Mchambuzi

Umenena vema, swala hili binafsi natatizwa nalo. Kwanza ni lazima tujadili madaraka hayo tunayatoa kwa rais na kuyapeleka wapi? Je sababu zile ambazo taasisi ya urais inalalamikiwa kwa madaraka hayo kurundikwa hazipo huko tunakotaka kuhamishia hayo madaraka?

Ivonya-Ngia,

Hii ni hoja ya msingi sana - tunayapunguza ili tuyapeleke wapi? Hili ni swali ambalo hatujatumia muda wa kutosha kulijadili kama jamii; vile vile tumekuja na mapendekezo mengi sana juu ya nini kiwepo katika katiba mpya, lakini tumeshindwa kuja na mawazo juu ya nini kifanyike ili mapendekezo yetu yawe practiced katika maisha yetu ya kila siku badala ya kuwa tu a list of items mentioned kwenye katiba mpya; Nikirudi kweney hoja yako kwamba tuyapunguze tuyapelekea wapi madaraka ya rais, pamoja na umuhimu wa swali hili, haina maana kwamba basi tuyaache kwenye taasisi ya Rais kama ilivyo sasa bali tutafute njia ya kuyasambaza kwingine kupitia an effective system of checks and balance; Vinginevyo kwa kweli majibu ya watu mbalimbali kwamba katiba mpya italitatua hili na lile zinakera kwani Katiba sio mwarobaini, hasa ikiwa tutashindwa ku match theory and practice;

Ni katika Tanzania hii hii ambapo kuna taasisi zinashutumiwa kwa ukabila na udini. Kuna taasisi ambazo pia ni mihimili zimeshutumiwa mchana kweupe tena nyingine baina ya wajumbe wake kwa rushwa na upendeleo. Hakuna taasisi hata moja ambayo kwa uchache tu wa vigezo vya utawala bora kama uwazi, uwajibikaji, nidhamu na ushirikishaji wananchi inaweza ikasimama kifua mbele katika nchi yetu. Kuyatoa madaraka haya mikononi mwa rais na kuyapeleka mikononi mwa taasisi hizi mfu si kumaliza tatizo bali kuliamisha tu na pengine kulikuza zaidi. Wengine tunazungumzia kupeleka madaraka kwa umma as if umma tunaouzungumzia ni sisi watanzania wote kwa umoja wetu. Hakuna kitu kama hicho popote pale duniani, bado tunazizungumzia taasisi zile zile kama ilivyo taasisi ya urais.

Kwa kuongezea tu, ni muhimu tukaanza kuwa serious katika ujenzi wa taasisi za kiraia kwani shughuli ni aidha hiyo imetushinda au tumeitelekeza;Hatuna strong civic institutions za kusimamia mambo mbalimbali ya kitaifa na badala yake taifa linaendeshwa na informal institutions ambazo zipo huko kwenye communities na hizi ndio zinazaa wabunge, madiwani, marais, na hata mawaziri huteuliwa kutokana na nguvu za hizi community based institutions ambazo zinaendeshwa kwa misingi ya udini, ukabila na ukanda, itikadi za vyama, among others;

Hatuna budi kuupanua mjadala huu ukilenga pia kufumua mfumo mzima wa taasisi zetu ili at least ziwe na medium standards za utawala bora. Na hii ndio fursa, mjadala wa katiba mpya unahitaji kuelekezwa katika kuunda Tanzania ya kimfumo. Tanzania inayojengwa na taasisi imara zinazoweza kutoa maamuzi kwa uwazi pasipo shaka. Kwa hivi tunavyojadili kupunguza madaraka ya rais pasipo kujadili hizo taasisi zingine na udhaifu wake wa kimfumo bado nasimamia maneno yangu kuwa huko ni kukaribisha maafa.

Naunga mkono hoja, ni suala zima la kuhakikisha kwamba taifa linajenga na kuimarisha civic institutions badala ya kuzipiga vita, taasisi kama mabaraza ya vijana, kina mama, wazee n.k ambayo hayafuati mrengo wowote wa kisiasa; Pia nadhani suala la utawala bora linafifisha umuhumu wa uongozi bora; hatuhitaji watawala bora bali viongozi bora;
 
Hawezi kutoa maoni tofauti na yaliyopo sasa,JK hatamuelewa,na sababu inawalinda watenda maovu,hawezi kusema lolote!ukitaka aseme subiria akitoka au atoe kwa maandishi na asitaje jina lake,hapo sawa!

Kimsingi naunga mkono hoja, lakini suala la msingi hapa ni je, kama taifa tumetoka wapi katika hili? Chimbuko lake nini? na je katika awamu hii, tatizo kwa wengi ni kwamba power is in the wrong hands vinginevyo tunakubaliana na mwalimu kwamba - "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"? Au Mtazamo wa mwalimu umeshapitwa na wakati?

Kimsingi, hoja yangu ndio inalenga hayo, ingawa wapo baadhi ya wachangiaji wameanza kuhisi kwamba nimetumwa na CCM kuja kutetea suala husika, na hii inatokana zaidi na wahusika kutotulia vizuri na kusoma hoja yangu ya msingi na kuielewa;
 
Mazingira ya nchi ni tofauti sana na enzi za mwalimu, vilevile historia na matukio ya siku za karibuni zinaonyehsa wazi yanaonyesha wazi kuwa kuna haja ya kumpunguzia madaraka raisi ili kupata ufanisi katika utawala bora na kuboresha demokraisa.

Kwa maana hii, haukubaliani na hoja ya Mwalimu katika mazingira ya sasa kwamba:

"Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"
 
Rais anapoteua binadamu aina ya Philipo Mulugo kuwa waziri (tena wizara ya elimu) utanishawishije kuwa madaraka ya rais yasipunguzwe? Tuache matani! Kama rasimu italeta upuuzi huu hatutaipitisha hadi utawala mwingine utakaokuwa na nia ya mageuzi ya kweli ya katiba.
 
Kwanini mnaendelea kukwepa maswali yangu kwenye hitimisho langu hapo juu kwenye bandiko namba moja na badala yake mnakuja na hoja rasha rasha?
 
Mchambuzi,

..mimi kama mshabiki wa CDM, "kuirudisha nchi kwenye mstari", maana yake ni kumrudisha Raisi/serikali kwenye mstari.

..kwa maana nyingine kuwepo mazingira ambayo yatam-discourage Raisi kutumia madaraka yake vibaya.

..ili mazingira hayo yawepo, kwanza tunapaswa kuweka mfumo mzuri wa checks and balance. vilevile tunapaswa kuzipa MENO na UHURU taasisi zetu za uchunguzi, bunge, pamoja na mahakama zetu.

NB:

..Raisi anayekuja anaweza kuwa na miaka 18, sasa r we ready to risk it na kumlundikia madaraka aliyokuwa nayo Raisi wa sasa??
 
Kwa hoja yako, 'Power might be necessary especially if it is in the right hands', au nimekosea? Sijaelewa sana iwapo you are for madaraka ya Rais kudhibitiwa au madaraka ya Rais kupunguzwa;
 
Mchambuzi,

..both; yapunguzwe na kudhibitiwa.

..wengi wanafikiri lengo ni kumuweka Raisi ktk mazingira magumu.

..mimi kwa upande wangu nadhani tutakuwa kunamlinda Raisi from self destruction, na zaidi asituumize wananchi.

..fikiria kama tungeweza kumdhibiti/kumlinda/kum-protect Mkapa asiingie mikataba mibovu, au asifisadi.

..lakini siyo Raisi tu. hata mihimili mingine kama mahakama na bunge nayo lazima idhibitiwe.
 
Mchambuzi,

..both; yapunguzwe na kudhibitiwa.

..wengi wanafikiri lengo ni kumuweka Raisi ktk mazingira magumu.

..mimi kwa upande wangu nadhani tutakuwa kunamlinda Raisi from self destruction, na zaidi asituumize wananchi.

..fikiria kama tungeweza kumdhibiti/kumlinda/kum-protect Mkapa asiingie mikataba mibovu, au asifisadi.

..lakini siyo Raisi tu. hata mihimili mingine kama mahakama na bunge nayo lazima ithibitiwe.

Katika muktadha huu, unashauri tufuate mfumo gani, Parliamentary system of government au Presidential System of government?
 
Katika muktadha huu, unashauri tufuate mfumo gani, Parliamentary system of government au Presidential System of government?
Mchambuzi,

..zote zina pros and cons, bahati mbaya havent taken time kuangalia ni mfumo upi unatufaa.

..labda niseme presidential kwasababu to some extent mfumo huo uko more stable.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

..zote zina pros and cons, bahati mbaya havent taken time kuangalia ni mfumo upi unatufaa.

..labda niseme presidential kwasababu to some extent mfumo huo uko more stable.

Ni kweli, presidential form of government, faida yake kubwa ni more stability na parliamentary form of government, faida yake kubwa ni more accountability;

Mara tu baada ya uhuru (1961), tuli adopt parliamentary form of government lakini muda mfupi baadae tukabadilisha iwe presidential form of government kwa sababu mbalimbali including nilizojadili awali (see bandiko namba moja la uzi huu); Swali muhimu linalofuatia ni je, how can we strike the balance ili kuendeleza stability lakini at the same time kuongeza accountability ya serikali? Ni muhimu tuchague na kuwa tayari to incur an opportunity cost, hatuwezi kuchagua both - kuthibiti na kupunguza madaraka ya rais, ni lazima tuchague moja - kwamba, should we aim for more accountability than stability or stability than accountability? In my view, jibu kwa hili litatokana na uchaguzi wetu on either kufuata parliamentary au presidential system of government chini ya katiba mpya; Kwa maana nyingine, tutakuwa tunafanya makosa sana iwapo tutajadili sana suala la kupunguza madaraka ya rais huku tuki ignore suala zima la form of government - presidential vis a vis parliamentary, na hali hii inaendelea kujitokeza kwani katika mchakato wa katiba mpya, hakuna anayejali kulijadili;

Vinginevyo mengine yatategemea jinsi gani tunaimarisha suala la checks and balance, lakini itambulike pia kwamba ingawa checks and balance na separation of powers ni kitu kimoja, utekelezaji wa checks and balance may go beyond three pillars za state; kwa mfano, opposition parties (hasa major opposition political party) offers a new face of separation of powers, hence checks and balance, ingawa formally wengi hawalitazami suala hili kwa mtindo huu;
 
Back
Top Bottom