Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Bongolander,

Majibu kwa bandiko lako namba 37;

Kuhusu uhatari wa kumpunguzia madaraka Rais, nilijadili hili ndani ya hoja iliyohusu jinsi gani Katiba ya JMT (1977) ilivyoiweka taasisi ya Rais kama ni living symbol of our Unity lakini pia custodian of our peace, stability & direction ya nchi; Sina maana kwamba haya yabakie kama yalivyo, nia yangu ni kuelezea tu tumetokea wapi na kwanini maamuzi haya yalichukuliwa ili tukija amua kufanya mabadiliko huko mbeleni ndani ya Katiba mpya, basi tusikurupuke na tufanye maamuzi kama watu ambao tupo well informed;

Kuhusu Kagame na Mengistu, ni kweli, na hoja hii, hasa juu ya Kagame ipo midomoni mwa watanzania wengi sana ambao wanatamani Rais ajae awe wa Caliber ya Kagamae huku wakitaja majina fulani fulani ya hapa nyumbani kwamba ndio yanafaa katika kufanikisha hilo, lakini pia ni hao hao ambao wamekuwa mstari wa mbele kujadili kwamba kuna umuhimu wa kupunguza madaraka ya Rais, na nimekuwa na argue kwamba this is self - contradictory kwani marais Kagame na Mengistu, literally ni their full executive powers ndio zimefanya wafanikishe yale, kwa maana nyingine, "power was/is in the right/good hands..."; Ni muhimu tukaelewa hili kwani kupunguza madaraka ya rais katika katiba ijayo kuutfanya tusiwe na nafasi ya kutumia ukagame au umengistu in the course of economic and social development;

Mwisho ni hoja yako kuhusu umuhimu wa separation of powers, rais kutokuwa sehemu ya bunge n.k; Je, nitakuwa sahihi iwapo uelewa wangu ni kwamba your concerns zitakuwa taken care of kwa ku strengthen notion ya separation of powers and such separation iwe na meno kikatiba yenye kung'ata katika shughuli za kila siku za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika taifa na pia kumtoa Rais kwenye bunge? Nauliza haya kwani bado sijaona exactly ni kitu gani unataka kiondolewe kwa Rais in terms of powers from your view; Pia nakuuliza tena - katika muktadha huo, tufuate which form of government ndani ya Katiba mpya - Parliamentary form of government or Presidential form of government?
 
Mkuu nguruvi3,

Haya ni majibu ya mchango wako mzuri kwenye bandiko namba 38 la mjadala huu; ningependa nianze na jinsi gani umehitimisha bandiko husika; umesema hivi:

  • Nimalize kwa kusema sababu zilizokuwepo kwasasa hazina mantiki.
  • Nadhani kundi linalosema rais alundikiwe madaraka lina hofu kubwa isiyo na sababu.
  • Hofu ya kuwa nchi ni Rais na si uongozi.
  • Mimi naamini wakati umefika tujitahmini na kuchukua mwelekeo mpya, miaka 50 ni mingi sana kusubiri.

Na mwanzo wa mjadala ulisema kwamba - concentration of powers za Marais Kikatiba katika bara la Afrika ulichangiwa na masuala yafuatayo:

1. Uwoga wa mapinduzi barani afrika katika kipindi cha 1960s - early 1980;
2. Hapakuwa na qualified manpower ya kutosha kuongoza mihimili yote kwa ukamilifu;
3. Kulikuwa na haja ya Viongozi wa nchi kuwa kiungo cha taifa ili kuwaunganisha wananchi baada ya ukoloni na madhara yake;

Kimsingi nakubaliana na hoja hizi, lakini swali langu kwako ni je, what was the overriding reason when it comes to Mwalimu Nyerere kati ya hizo factors tatu hapo juu? In my view, factor number three ndio ilibeba factors nyingine zote, kwahiyo iwapo tunaamua kuifanya kila factor hapo juu ijitegemee, obviously tutaona kwamba sababu husika kwa kiasi kikubwa sana zimepitwana wakati; Ni kutokana na sababu hii, bado naona kwamba sababu namba tatu is still heavy weight in today’s context, hence relevant; lakini unaonya kwamba can we afford kukaa na kusubiria kiongozi wa aina ya Mwalimu aje? That’s a very important question;

Vinginevyo sijui kama watanzania wanaelewa kwamba penetration ya west kiuchumi na kisiasa katika nchi yetu kupitia liberal democracy and economic principles has managed to divide and rule the society na ni ni moja ya sababu kubwa sana kwanini tunagongana vichwa nchini kwetu; Ili kuondokana na mgongano huu, we need Rais mzalendo, mwadilifu, na mwenye uwezo wa kukemea ubepari na soko huria pale unapokandamiza wananchi, sio rais wa kukenua kenua tu anaposikia masuala ya FDI and AID, hence sababu namba tatu hapo juu I find still rellevent leo, but again, swali lako pia muhimu kwamba – can we afford kumsubiria rais wa namna hiyo na kuachia Katiba wazi juu ya suala hili?

Hoja yako kwamba – maamuzi can be done kwa upesi zaidi huko huko walipo wananchi kuliko Dodoma na Dar-es-salaam, you are right lakini it depends unazungumzia maamuzi gani, vinginevyo as we speak, dhana ya decentralization tayari inafanikisha hilo ambapo kuna serikali za mitaa, serikali za vijiji, na pia kwenye ngazi za kata kuna madiwani ambao wanashirikiana na wabunge wa maeneo yao (wabunge wakiwa pia ni madiwani by default) wakifanya maamuzi mengi tu ya maendeleo katika maeneo yao pertaining to afya, elimu, miundo mbinu n.k;

I agree juu ya umuhimu wa kuvipatia more autonomy vyombo vya DCI, PCCB, DPP, CAG n.k; Lakini again, suingi mkono kuachia vitu hivi view huru kabisa bali kumthibiti Rais, kwani hatari ya kutumika vibaya na watu wenye fedha ni kubwa zaidi kuliko hatari ya Rais husika kuvi abuse; Just think about it; Ni muhimu the journey towards autonomy on these organs ianze with baby steps;

Kuhusu Mahakama kuwa huru naunga mkono hoja pia, ila iendane vilevile na kuanza kuupa mhimili huu fedha za kutosha kujiendesha and reward the judiciary personnel with good salaries and allowances ili kuwapa motisha zaidi na pia kupunguza rushwa katika mhimili huu; Kuna mtu nadhani mwanasiasa mmoja alishauri kwamba mhimili huu uwe na mamlaka ya kujiamulia bajeti yake yenyewe, sio serikali, naunga mkono hoja husika;

Kuhusu bunge kuwa na autonomy zaidi na kumwondoa Rais katika mhimili huo, naunga mkono hoja, lakini hatutakuwa tumefanya kazi ya maana iwapo hatua hii haitaenda sambamba na reforms ndani ya vyama vyetu vya siasa ambazo zitatambulika ndani ya Katiba ya nchi, vinginevyo Chama chochote chenye majority seats whether ni CCM, Chadema, CUF, vitaendelea kuikinga serikali yao hata katika masuala ambayo hayana maslahi kwa taifa; It is in this context pia nimekuwa nikijenga hoja separation of powers/checks and balance in our context is gaining a new face, ambayo ni the main opposition party (Chadema), na hii ni nje ya bunge;

Naomba nirudi kwenye hoja yako moja muhimu sana ambayo nilijadili kidogo hapo juu – nakubaliana na wewe kimsingi kwamba ni gharama na ni hatari zaidi kuachia Katiba ya nchi impe full executive powers Rais kwa matumaini kwamba Nyerere mwingine ipo siku atakuja; Lakini pia sina uhakika sana kwamba tukifanya a Cost – Benefit Analysis juu ya suala hili, costs will outweigh the benefits; In my humbe view katika hili – tupo salama zaidi kwa sasa tukiacha certain powers zibaki kama zilivyo huku tukiweka juhudi kubwa zaidi katika kuzidhibiti, hasa kupitia Bunge; Lakini again, Kimweri kwenye bandiko namba 39 ametoa angalizo muhimu sana kwamba we have a very incompetent legislature ambalo hatuwezi kuliamini kwa asilimia mia moja; Sasa sijui kama hii ina maana tujaribu kutengeneza mazingira ya competent legislature Kikatiba au vipi;

Na mwisho ni mjadala wako kuhusu Japan ambapo mawaziri wakuu saba walijiuzulu ndani ya kipindi cha miaka mitano; I agree kimsingi, na ndio maana nimeuliza swali langu kwenu kwenye bandiko namba 35; Ni kwamba, Japan wanafuata a parliamentary form of government, na mfumo huu inherently ni unstable kama nilivyojadili elsewhere, nadhani katika majibu yangu kwa bongolander; Parliamentary form of government is very unstable lakini brings more accountability on part of the executive; kwa mtazamo wako, na hili swali nalirudia tena (rejea bandiko langu namba 35), ila this time kwa version tofauti – JE:

Katika katiba mpya, should we trade accountability for stability (hence adopt presidential form of government) or we should trade stability for accountability (hence adopt parliamentary form of government?
 
Ni mchanganuo mzuri sana ila tatizo ni kuwa umeelekeza na kujikita kwenye fikra na utendaji ulioshindwa au kushindikana.

Kikubwa hapa ni kujadili upande mwingine wa hoja kwa kina ili tukija fanya maamuzi basi iwe tumeyafanya kama well informed citizens after exhausting all the factors and variables huku tukijaribu ku qualify au disqualify correlation baina ya variables na factors fulani fulani; Nia yangu ni hiyo tu, ndio maana kichwa cha uzi kimeuliza: Je tumeelewa hoja yake ya Msingi? Vinginevyo nia yangu sio kuaminisha wana JF kwamba Sefue is right, lakini pia sipo hapa kujadili how wrong he might be; I am trying to be objective na kuwa more of a moderator, na kama nina mapungufu katika hilo, naomba uniwie radhi na nieleze wapi nirekebishe;
 
"POWER IN THE RIGHT HANDS IS GOOD AND INDEED NECESSARY FOR A NEW STATE"

HAKIKA, na hapo ndipo ndipo kwenye FUMBO GUMU SANA KULIFUMBUA JUU YA WATAWALA WETU.

Ili kufikia mafanikio yoyote yale, ni lazima kuwepo na KAZI, si kazi tu ila NIDHAMU YA KAZI PIA! Sasa yupi wakusimamia nidhamu hiyo? Anatakiwa aweje? Laiti kama tungekuwa bado na Utamaduni wetu wa KUANDAA VIONGOZI WETU, kwa vigezo vyenye tija kwetu, basi tusingehofu kumpa rungu kubwa kiongozi wetu wa nidhamu kazini, kwani tungekuwa na hakika naye ya kulitumia vizuri! Tatizo linakuja sasa kuwa Mfumo uliopo unatuaminisha kuwa, kupata kiongozi bora ni mchezo wa BAHATI NASIBU, hatuna hakika ya kumpata bora au dhaifu. Ikiwa hvyo tutawezaje kumpa rungu kubwa mtu huyo, je hatogeuka kutuponda nalo?

LAKINI, hilo haliondoi ukweli kwamba, NIDHAMU KAZINI NI MSINGI WA MAFANIKIO, NA NIDHAMU HUSIMAMIWA NA MTU MWENYE NGUVU, MAANA HULKA ZA BINADAMU SI ZA KUFANANISHA NA UZITO HATA WA SHABA. Hivyo suluhisho ni kurudia TAMADUNI ZETU ZA KUANDAA NA KUPATA VIONGOZI (zaweza kuwa za tofauti lakin muhimu ni kuwa nazo), kisha tutawajibika KUWAAMINI HAO NA KUWAPA NGUVU INAYOSTAHILI! Tuwe na hakika na mikono yao kwa kuwaandaa wenyewe! TUSIJARIBU VIONGOZI au kuwapata kwa KUBAHATISHA! Madaraka finyu ya raisi ni hatari kwa UMOJA WETU KAZINI, na nidhamu ya kazi ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja kama timu, bunge, mahakama na serikali kila moja ikiwa na sauti yake binafsi, niaje tutaleta umoja kama sehemu ya nidhamu kazini?

Pia tukumbuke Raisi ni OFISI kwanza kabla ya MTU.

Mungu wetu anaita sasa!
 
Kikubwa hapa ni kujadili upande mwingine wa hoja kwa kina ili tukija fanya maamuzi basi iwe tumeyafanya kama well informed citizens after exhausting all the factors and variables huku tukijaribu ku qualify au disqualify correlation baina ya variables na factors fulani fulani; Nia yangu ni hiyo tu, ndio maana kichwa cha uzi kimeuliza: Je tumeelewa hoja yake ya Msingi? Vinginevyo nia yangu sio kuaminisha wana JF kwamba Sefue is right, lakini pia sipo hapa kujadili how wrong he might be; I am trying to be objective na kuwa more of a moderator, na kama nina mapungufu katika hilo, naomba uniwie radhi na nieleze wapi nirekebishe;

Hoja yake imeeleweka na inaambatana na nafasi aliyo nayo. Haoni na hataona madhara ya rais dhaifu kushindwa kumudu madaraka chini ya katiba inayofikiria kuwa rais ni malaika na mwenye uwezo.

Pro and cons za hoja yake ni mfu kwa sababu hata siku moja haelewi jinsi watu wanavyoathirika na rais anavyoshindwa kumudu madaraka yeye akiwa mtendaji ndani ya taasisi ya urais
 
Una maoni gani juu ya kauli hii ya Mwalimu:

"Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"
 
chiti_chitu,

pia ukiweza, tafadhali jadili maswali yangu manne katika hitimisho la bandiko namba moja kwani naona kila mtu ana yakimbia, hivyo tunashindwa kuja na hoja zenye maslahi ya taifa na badala yake inakuwa ni maslahi binafsi au ya vyama fulani;
 
Una maoni gani juu ya kauli hii ya Mwalimu:

"Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"

Alikuwa anazungumzia udhaifu wa katiba ambao kama rais angekuwa na hulka ya udikteta angewezeshwa na katiba hii mbovu kutawala kidikteta.

Uchaguzi kwa jamii isiyo na elimu nzuri na ni masikini ni bahati nasibu; kwa hiyo kuwa na Rais sahihi madarakani ni vyema au bahati kinyume chake ni 70% ukweli kuwa kibinadamu rais sahihi ni mfumo unaosimikwa na katiba. Na ni sahihi kuwa na katiba inayotoa madaraka ambayo hata rais mwenye uwezo chini ya 50% atamudu madaraka kupitia taasisi zingine zenye kumudu baadhi ya majukumu ambayo kwa sasa rais anayo. Mfano uteuzi wa wakuu mbali na ushikaji ushikaji unaweza kufanywa vizuri zaidi kama rais hatahusishwa. Mfano mwingine tume mbali mbali hususan tume ya uchaguzi na mengi mengine
 
"POWER IN THE RIGHT HANDS IS GOOD AND INDEED NECESSARY FOR A NEW STATE"
HAKIKA, na hapo ndipo ndipo kwenye FUMBO GUMU SANA KULIFUMBUA JUU YA WATAWALA WETU.
Ili kufikia mafanikio yoyote yale, ni lazima kuwepo na KAZI, si kazi tu ila NIDHAMU YA KAZI PIA! Sasa yupi wakusimamia nidhamu hiyo? Anatakiwa aweje? Laiti kama tungekuwa bado na Utamaduni wetu wa KUANDAA VIONGOZI WETU, kwa vigezo vyenye tija kwetu, basi tusingehofu kumpa rungu kubwa kiongozi wetu wa nidhamu kazini, kwani tungekuwa na hakika naye ya kulitumia vizuri! Tatizo linakuja sasa kuwa Mfumo uliopo unatuaminisha kuwa, kupata kiongozi bora ni mchezo wa BAHATI NASIBU, hatuna hakika ya kumpata bora au dhaifu. Ikiwa hvyo tutawezaje kumpa rungu kubwa mtu huyo, je hatogeuka kutuponda nalo? LAKINI, hilo haliondoi ukweli kwamba, NIDHAMU KAZINI NI MSINGI WA MAFANIKIO, NA NIDHAMU HUSIMAMIWA NA MTU MWENYE NGUVU, MAANA HULKA ZA BINADAMU SI ZA KUFANANISHA NA UZITO HATA WA SHABA. Hivyo suluhisho ni kurudia TAMADUNI ZETU ZA KUANDAA NA KUPATA VIONGOZI (zaweza kuwa za tofauti lakin muhimu ni kuwa nazo), kisha tutawajibika KUWAAMINI HAO NA KUWAPA NGUVU INAYOSTAHILI! Tuwe na hakika na mikono yao kwa kuwaandaa wenyewe! TUSIJARIBU VIONGOZI au kuwapata kwa KUBAHATISHA! Madaraka finyu ya raisi ni hatari kwa UMOJA WETU KAZINI, na nidhamu ya kazi ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja kama timu, bunge, mahakama na serikali kila moja ikiwa na sauti yake binafsi, niaje tutaleta umoja kama sehemu ya nidhamu kazini?
Pia tukumbuke Raisi ni OFISI kwanza kabla ya MTU.
Mungu wetu anaita sasa!

Jingalafalsafa,

Kwa hoja yako, unakubali kwamba "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State", lakini tatizo ni kupata the right hands tumpe such powers; Suluhisho kwa hili iwe nini juu ya madaraka ya Rais - Kuyaondoa na abakie tu a ceremonial figure? kuyapunguza? Kuyaacha mengi kama yalivyo lakini tuyadhibiti? Pia je, tufuate mfumo gani wa utawala - parliamentary? Presidential? Why? Why Not? Pia una maoni gani juu ya maswali yangu manne kwenye hitimisho la bandiko namba moja la uzi huu?
 
Mkuu nguruvi3,

Haya ni majibu ya mchango wako mzuri kwenye bandiko namba 38 la mjadala huu; ningependa nianze na jinsi gani umehitimisha bandiko husika; umesema hivi:

  • Nimalize kwa kusema sababu zilizokuwepo kwasasa hazina mantiki.
  • Nadhani kundi linalosema rais alundikiwe madaraka lina hofu kubwa isiyo na sababu.
  • Hofu ya kuwa nchi ni Rais na si uongozi.
  • Mimi naamini wakati umefika tujitahmini na kuchukua mwelekeo mpya, miaka 50 ni mingi sana kusubiri.

Na mwanzo wa mjadala ulisema kwamba - concentration of powers za Marais Kikatiba katika bara la Afrika ulichangiwa na masuala yafuatayo:

1. Uwoga wa mapinduzi barani afrika katika kipindi cha 1960s - early 1980;
2. Hapakuwa na qualified manpower ya kutosha kuongoza mihimili yote kwa ukamilifu;
3. Kulikuwa na haja ya Viongozi wa nchi kuwa kiungo cha taifa ili kuwaunganisha wananchi baada ya ukoloni na madhara yake;

Kimsingi nakubaliana na hoja hizi, lakini swali langu kwako ni je, what was the overriding reason when it comes to Mwalimu Nyerere kati ya hizo factors tatu hapo juu? In my view, factor number three ndio ilibeba factors nyingine zote, kwahiyo iwapo tunaamua kuifanya kila factor hapo juu ijitegemee, obviously tutaona kwamba sababu husika kwa kiasi kikubwa sana zimepitwana wakati; Ni kutokana na sababu hii, bado naona kwamba sababu namba tatu is still heavy weight in today's context, hence relevant; lakini unaonya kwamba can we afford kukaa na kusubiria kiongozi wa aina ya Mwalimu aje? That's a very important question;

Vinginevyo sijui kama watanzania wanaelewa kwamba penetration ya west kiuchumi na kisiasa katika nchi yetu kupitia liberal democracy and economic principles has managed to divide and rule the society na ni ni moja ya sababu kubwa sana kwanini tunagongana vichwa nchini kwetu; Ili kuondokana na mgongano huu, we need Rais mzalendo, mwadilifu, na mwenye uwezo wa kukemea ubepari na soko huria pale unapokandamiza wananchi, sio rais wa kukenua kenua tu anaposikia masuala ya FDI and AID, hence sababu namba tatu hapo juu I find still rellevent leo, but again, swali lako pia muhimu kwamba – can we afford kumsubiria rais wa namna hiyo na kuachia Katiba wazi juu ya suala hili?

Hoja yako kwamba – maamuzi can be done kwa upesi zaidi huko huko walipo wananchi kuliko Dodoma na Dar-es-salaam, you are right lakini it depends unazungumzia maamuzi gani, vinginevyo as we speak, dhana ya decentralization tayari inafanikisha hilo ambapo kuna serikali za mitaa, serikali za vijiji, na pia kwenye ngazi za kata kuna madiwani ambao wanashirikiana na wabunge wa maeneo yao (wabunge wakiwa pia ni madiwani by default) wakifanya maamuzi mengi tu ya maendeleo katika maeneo yao pertaining to afya, elimu, miundo mbinu n.k;

I agree juu ya umuhimu wa kuvipatia more autonomy vyombo vya DCI, PCCB, DPP, CAG n.k; Lakini again, suingi mkono kuachia vitu hivi view huru kabisa bali kumthibiti Rais, kwani hatari ya kutumika vibaya na watu wenye fedha ni kubwa zaidi kuliko hatari ya Rais husika kuvi abuse; Just think about it; Ni muhimu the journey towards autonomy on these organs ianze with baby steps;

Kuhusu Mahakama kuwa huru naunga mkono hoja pia, ila iendane vilevile na kuanza kuupa mhimili huu fedha za kutosha kujiendesha and reward the judiciary personnel with good salaries and allowances ili kuwapa motisha zaidi na pia kupunguza rushwa katika mhimili huu; Kuna mtu nadhani mwanasiasa mmoja alishauri kwamba mhimili huu uwe na mamlaka ya kujiamulia bajeti yake yenyewe, sio serikali, naunga mkono hoja husika;

Kuhusu bunge kuwa na autonomy zaidi na kumwondoa Rais katika mhimili huo, naunga mkono hoja, lakini hatutakuwa tumefanya kazi ya maana iwapo hatua hii haitaenda sambamba na reforms ndani ya vyama vyetu vya siasa ambazo zitatambulika ndani ya Katiba ya nchi, vinginevyo Chama chochote chenye majority seats whether ni CCM, Chadema, CUF, vitaendelea kuikinga serikali yao hata katika masuala ambayo hayana maslahi kwa taifa; It is in this context pia nimekuwa nikijenga hoja separation of powers/checks and balance in our context is gaining a new face, ambayo ni the main opposition party (Chadema), na hii ni nje ya bunge;

Naomba nirudi kwenye hoja yako moja muhimu sana ambayo nilijadili kidogo hapo juu – nakubaliana na wewe kimsingi kwamba ni gharama na ni hatari zaidi kuachia Katiba ya nchi impe full executive powers Rais kwa matumaini kwamba Nyerere mwingine ipo siku atakuja; Lakini pia sina uhakika sana kwamba tukifanya a Cost – Benefit Analysis juu ya suala hili, costs will outweigh the benefits; In my humbe view katika hili – tupo salama zaidi kwa sasa tukiacha certain powers zibaki kama zilivyo huku tukiweka juhudi kubwa zaidi katika kuzidhibiti, hasa kupitia Bunge; Lakini again, Kimweri kwenye bandiko namba 39 ametoa angalizo muhimu sana kwamba we have a very incompetent legislature ambalo hatuwezi kuliamini kwa asilimia mia moja; Sasa sijui kama hii ina maana tujaribu kutengeneza mazingira ya competent legislature Kikatiba au vipi;

Na mwisho ni mjadala wako kuhusu Japan ambapo mawaziri wakuu saba walijiuzulu ndani ya kipindi cha miaka mitano; I agree kimsingi, na ndio maana nimeuliza swali langu kwenu kwenye bandiko namba 35; Ni kwamba, Japan wanafuata a parliamentary form of government, na mfumo huu inherently ni unstable kama nilivyojadili elsewhere, nadhani katika majibu yangu kwa bongolander; Parliamentary form of government is very unstable lakini brings more accountability on part of the executive; kwa mtazamo wako, na hili swali nalirudia tena (rejea bandiko langu namba 35), ila this time kwa version tofauti – JE:

Katika katiba mpya, should we trade accountability for stability (hence adopt presidential form of government) or we should trade stability for accountability (hence adopt parliamentary form of government?
Mchambuzi, Ahsante sana kwa hoja zako mwanana.
Ukirudi nyuma post 39 Kimweri ameeleza vizuri sana na nakubaliana naye sana kuhusu bunge.

Kwa upande wangu, stability is a byproduct of accountability.
Katika mazingira yetu bunge limepoteza maana ya ''assembly of intellectuals'' limekuwa eneo la kutafutia vipato.
Unapokuwa na corrupt parliamentarians wasiojua kwanini wapo bungeni ni hatari sana kuwakabidhi nguvu za ziada.
Jibu langu linabaki prez form of government. I hope sijafanya contradiction na maelezo yangu ya awali.

Pili, power in the right hand is good and indeed necessary for a new state? Hapa nitauliza, should we take the risk hoping that ''right hand'' opportunity will present itself. Should we remain optimistic that the beautiful one is not yet born!
Is it worth taking the risk at this time when we need to run to catch up with the rest of the world.
I'm pessimistic than optimistic! No! let us take a new direction.

Tatu, sababu zilizomfanya Nyerere achukue hatua hizo ni 2, 3 na 1 ulivyozisema hapo juu.
Ukizitazam vizuri zote zimepoteza maana kwasababu zinategemea. Sababu namba 1 haipo kwasasa. Sababu namba 2 inapunguza ulazima wa sababu namba 3 kwa kiasi kikubwa sana. Sidhani kuwa tunahitaji mtu wa kutuunganisha, ila tunahitaji vyombo vya kulinda kile kilichotuunganisha ambacho Nyerere alikifanya.

Nne, Sababu zinazowakera wananchi ni matokeo ya uzoefu wa miaka 50 na hasa 25 iliyopita. Bila kujali chama gani kitachukua madaraka wananchi wanaona ni wakati sasa tuwe na mfumo tofauti kwasababu tumebadilisha viongozi na haionekani kutoa majibu. People are increasingly become impatient because ''no hope or signs for expected mothers in horizon' hence the beautiful one will not be born soon.
Doing the same thing over and over hoping for different result is a silly thing.

Tano, bila kujali kiongozi atatoka chama gani, Tanzania itabadilika kwa kubadili mfumo na si watu.
Uzooefu unatuonyesha kuwa mfumo uliopo ndio unabadilisha viongozi na si kinyume chake.
Akija Lipumba, Mbowe, Zitto n.k. they will play by the same book. The solution is to write the new one.
Mchambuzi, who knew that the ''son'' of Nyerere will turn to be a big snake and looter on Nyerere's land!!

Mkuu, nadhani tunaposema rais apunguziwe madaraka kuna kitu tunakikosa.
Hatumaanishi kuwa rais awe ceremonial figure! no thank you.

Mimi nina maanisha rais aondolewe yale yasiyomhusu au yanayomkwaza katika utendaji ili awajibike kwa mambo ya kitaifa. Taasisi nyingine kama mahakama zirudishiwe mamlaka na hadhi zao bila kuingiliwa na taasisi ya urais.
Kuwepo na system itakayomfanya rais awajibike zaidi kuliko ku-abuse power.

Kuwepo na functional decentralized system ili wananchi wapange na waaamue hatima ya mambo yao bila bureacracy ya taasisi ya Urais. Mfano uliotoa kuwa tunayo decentralized system ninatofautina nao kwasababu iliyopo ni cosmetic tu.
Wanannchi hawana nguvu zaidi ya mkurugenezi, mkuu wa wilaya au mkoa.

Haiwezekani tatizo la Tanzania nzima likawa shule za kata, kuna kwingine hawana Hospitali, maji n.k
Priority za nini wanataka zinapangwa Dar na hazitoki kwao, na hapo ni kuwanyima fursa ya maendeleo yao.

Huu mfumo wa sasa ni symbolic, ukweli ni kuwa rais anaingilia madaraka hata ya kuamua visima vya maji achilia mbali vyoo vya shule through his presidential power, trickling down.

Ni wakati sasa yeye abaki kuwa na executive power ya mambo ya kitaifa mengine yafanywe na taasisi nyingine.
Kwanini rais amiliki PCCB? Who will be a watch dog to his government!

Kwangu mimi kumpunguzia madaraka is to make him accountable under the check and balance system.
He should not have an open ended executive power! no! at some point there should be a ''watch dog'' against him.
 
Maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "power in the right hands is good and indeed necessary for a new state" yanaweza kuwa sahihi kwa taifa jipya kama South Sudan. Lakini sidhani kama tunaweza kusema kuwa taifa letu ni jipya na hivyo tumpe madaraka mtu mmoja.

Kwa upande mwingine, tatizo linaweza lisiwe kumpa Rais madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa "checks and balances" kuhakikisha kuwa hayo madaraka hayatumiwi vibaya.

Nafikiri tatizo siyo Rais kuwa na madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa checks and balances kuhakikisha kuwa hayatumii hayo madaraka vibaya. Mbona Rais wa Marekani ana madaraka makubwa tuu kiasi kwamba anaweza ku-command the instant destruction of an entire city within minutes?

Marekani ina maelfu ya missiles with nuclear warheads na ni Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutoa signal to launch them. Ila checks and balances zinahakikisha kuwa anayatumia haya madaraka vizuri.

Ukiondoa madaraka ya Rais na kumpa mtu mwingine, una uhakika gani kuwa hatayatumia vibaya? kwa mtu kama huyu?

Imekuwa sasa kama mazoea kwa mkuu wa wilaya ya Lushoto ndugu Majid Mwanga(29) kuwaweka ndani watumishi wa umma mara kwa mara eti kwa madai kuwa hatekelezi ilani ya CCM. Amekuwa akifanya hivyo mbele ya wananchi kama sehemu ya kujizolea umaarufu,huku akijua kuwa anadhalilisha taaluma za watu

Mbaya zaidi amekuwa akifanya hivyo hata kwa madaktari, jana tu amemuweka ndani mganga mkuu wa wilaya(DMO), ETI kwa madai kuwa hakusimamia usafi wa soko mpaka saa 12 jioni.

Kwa mtu kama huyu unaweza kumpa hayo madaraka ya Rais? Maana hata mwenyekiti wa kijiji ana madaraka yake na wapo wengi tuu wanayatumia vibaya. In fact, raia wa kawaida wananyanyasika zaidi na viongozi wa ngazi za chini kuwa na madaraka makubwa au kutumia madaraka yao vibaya.

Tanzania siyo taifa jipya, bali demokrasia yake ndiyo bado changa. Demokrasia yetu bado ipo kwenye majaribio na kuna taasisi nyingi tuu, ikiwemo ya Rais, ambazo zinahitaji kufanyiwa review.

Kupunguza madaraka ya Rais haitasaidia sana unless tuwe na uhakika kuwa hao wengine tutakaowapa hayo madaraka watayatumia vizuri. Otherwise, itakuwa ni kulihamishia tatizo kutoka kwa mtu/taasisi m/moja kwenye kwa taasisi mtu mwi/nyngine.

Sidhani kama tatizo lipo kwa Rais kuwa na madaraka makubwa bali kukosekana kwa checks and balances jinsi rais anavyotumia hayo madaraka. Kuwepo kwa strong checks and balances zitamfanya rais awe makini zaidi jinsi anavyotumia madaraka aliyopewa.

Kwa hiyo, swali la kujiuliza siyo kwa nini Rais asipunguziwe madaraka aliyonayo sasa, bali ni kwa nini madaraka ya Rais yasiwe subject to democratic review or checks and balances ambazo kwa sasa hazipo?
 
Bongolander,

Majibu kwa bandiko lako namba 37;

taasisi ya Rais kama ni living symbol of our Unity lakini pia custodian of our peace, stability & direction ya nchi;

Pia nakuuliza tena - katika muktadha huo, tufuate which form of government ndani ya Katiba mpya - Parliamentary form of government or Presidential form of government?

Mchambuzi kwanza the very idea that the president is a living symbol is highly problematic, it may have been valid then, but for the moment the president must be more than that, not just a symbol. Unajua maendeleao ni jambo la muhimu sana, bahati mbaya ni kuwa rais wetu ana kazi nyingi sana kiasi kuwa kazi zinazohusu maendeleo na hata usalama kama anaziacha pembeni that is why we see lots of weaknesses on that front.

Nilichokuwa namaanisha kwenye bandiko # 37 ni kuwa rais wetu ana madaraka makubwa kupita kiasi. Madaraka ninayozungumzia hapa ni yale yanayovuka mipaka ya executive branch. Yaani Rais wetu ana uwezo wa kuingilia kazi za mahakama na kazi za bunge, even worse anaweza hata kuingilia kazi za fourth estate. Kufanya kazi ambazo kimsingi hazimhusu makes him unable to concentrate and deliver on his traditional duties.

Hata traditional duties alizonazo za executive powers ni nyingi kupita kiasi, Just imagine anateua mawaziri wangapi. Anateua Ma RC wangapi, na uniambie kama kweli anajua interests za watu wa mikoa husika na anapeleka watu wanaoweza kuaddress issues zao. Just think of how many DCs he appoints, na hiyo ni moja kati ya appointments muhimu sana, uangalie kama kweli anateua kwa interest za wilaya hizo au ni fadhila, urafiki, undugu na uswahiba, bila kujali interests za wana wilaya. Same goes on to nafasi za ukatibu mkuu wa wizara, etc etc. Anateua watu wengi sana kupita kiasi, kiasi kwamba hawezi kuwamonitor effectively wote anaowateua ili ajue kama wanaperform au wazuga tu. Kama uko serious it can take two good days kuasses kazi ya miezi sita ya mtu uliyemteua, can our president really do that? Even worse anaweza kuanzisha wizara as he wishes, kana kwamba nchi yetu haijui ni wizara gani tunazihitaji kwa kumhibu wa katiba. Kwa hiyo hata executive duties zenyewe ni nyingi kupita kiasi kwa mtu mmoja kuweza kutekeleza

Kwa hiyo itakuwa ni vizuri kama rais atakuwa anafanya kazi ya urais (executive roles tu anazoweza kuzimudu), na sio kazi za mahakama na bunge. Ingawa kikatiba inaonekana kuwa tuna separation of powers, lakini de facto all powers have been vested not only to the executive branch, but also to President himself. That is terribly bad. Umoja, uhuru na utulivu unaweza kulindwa hata bila kuwa na rais Mungu. The idea of power in good hands makes a lot of sense, lakini kwa sasa na kwa Tanzania hatuna hakika kama kweli tunaweza kuwa na Kagame au Mengistu, if we gamble on that we may end up in big mess and lose all what we think we have achieved. Hakuna mtu mwenye uhakika kama Rais aajaye atakuwa kama Nyerere, kagame, au atajali nchi kuliko maslahi binafsi. Inawezekana akaja na inawezekana asije.

Pia rais anatakiwa awekewe rules of game, sio akiwa rais anaamua tu kusafiri kama anavyopenda, ateue watu kama anavyopenda, atumie madaraka kama anavyopenda na kwa maslahi ya chama chake na yake binafsi badala ya maslahi ya nchi yake, aamue kuwa hoja hii ijadiliwe na hii isijadiliwe, hili liachwe ni hili lisiachwe, aamue kuwasamehe wezi na bunge na mahakama wakae kimya tu. Hili ni tatizo kubwa.

Rais anatakiwa awekewe rule of conduct ambazo ziko wazi na ajue kabisa kuwa hayuko above rules, na apewe kazi za kufanya na anoenekane kuwa anafanya kazi hizo anazotakiwa kuzifanya. Kwa sasa kimsingi hayo hakuna.

Unajua mkangano uliopo Tanzania kwa sasa ni kuwa hatuna presidential system as it is in America na hatuna Parliamentary system as it is in UK. Ni kama tuna hybrid system, close to the one the French people are following. Lakini ya Ufaransa inafanya kazi katika mazingira ya Ufaransa na historia yake, na katiba tofauti sana na ya Tanzania. Definately haiwezi kudeliver kwa Tanzania.

Naona mode ya government wanayoadvocate Chadema, kama itazingatia zaidi umoja wa taifa na usalama wake, kwa kiasi kikubwa inaendana kiasi na mazingira yetu. Serikali kuu yenye nguvu isiyoingilia kazi za mihimili mingine, kuimarisha mihimili yote inaweza kukaguana, inayoweza kusambaza maendeleo ya nchi na sio Tanzania kuwa Dar es salaam na Dar es salaam kuwa Tanznaia. Which is very stupid thing Tanzania is still doing. Hii njia ya sasa tunayofuata haioneshi mwelekeo wowote wa nchi kupiga hatua za maana.

I hope you get my point on where i stand on this and why i suggest that President should have less powers.

By the way, out of this topic. Can yon tell me serikali katika mwezi huu januari imefaya kazi gani ya maana inayohusiana na maendeleo ya nchi? Au rais au PM, tunaweza kujua wanafanya kazi gani kwa ajili ya maendeleo ya nchi? au ndio wanafanya kazi zile zile za kila siku za mambo yale yale ya siasa? just curious, labda wewe unajua kidogo on this.
 
Ama kwa hakika nimejifunza sana katika huu uchambuzi wako ,yapo mengi ya kujiuliza,-watu wanadai bunge lenye meno,mahakama yenye meno,halafu wanataka taasisi ya urais iwe kibogoyo???!!!
 
Bongolander, hapo #52 umenigusa vema. Katika nchi yetu rais ni kila kitu ingawa tunasema ipo mihimili mingine.
CJ ameto maoni na kueleza kuhusu mhimili wa mahakama. Ukimsoma vizuri ni kama vile ansema mhimili siyo huru.
Kuna wakati waliomba hata bajeti iwe yao wasitegemee kukinga mikono ili kuwaweka huru.

Ukija upande wa bunge, with all due respect naweza kusema ni la hovyo sana.
Nalo kama mahakama linafanya kazi kama branch ya taasisi ya urais na wala nisingeshauri mambo muhimu yakabidhiwe bunge! bunge letu ni mkusanyiko wa wafanyabiashara za mafao! I'm sorry huo ndio ukweli.

Nikiulizwa sasa punguzo la madaraka ya rais liende wapi, mimi ningesema liende katika taasisi muhimu kwa kuzifanya zifanye kazi bila kumtegemea mtu mmoja (rais).
Hivi India wanawezaje ku-survive miezi 3 wakiwa hawana bunge effective wala PM?

Hofu inayowakumba wengi ni dhana kuwa rais ataondolewa nguvu kama za ulinzi na usalama.
Bongolander ameaInisha vizuri sana tatizo la kulundikiwa madaraka.
Ni mara ngapi wananchi wamekataa kiongozi lakini ameendelea kubaki kwasababu tu rais hajaamua.

Ni mara ngapi tumeona rais aki-abuse power kwasababu tu yupo juu ya kila jambo. Anaamua nani aende mahakamani nani asishtakiwe. Imefika mahali marafiki wahalifu wa rais wanapewa pensheni na kiinua mgongo cha ubalozi.

Hivi kwanini rais asi focus katika mambo makubwa ya kitaifa badala yake ajikite kuchagua mkurugenzi wa VETA.
Ilipoamuliwa kuwa rais hatakuwa mkuu wa Chuo kikuu kuna tatizo gani limetokea kwa kumuondolea ''uwezo'' huo.

Kati ya makatibu wakuu, wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi, ni nani anayeweza kufanya jambo kulingana na ubunifu au mazingira aliyopo bila ridhaa ya rais. Na nchi itaendelea vipi kukiwa hakuna fursa ya kutenda bila woga au hofu.

Mimi sidhani kuwa kumpunguzi rais madaraka ni kumfanya awe kibogoyo. la haha! zaidi ni kumpa meno machache makali.
Tunataka rais abaki kuwa na meno, lakini uwepo utaratibu wa kuhakikisha kuwa anayatumia meno hayo kwa njia sahihi(check and balance)

Lakini pia kinywa kizuri ni kile chenye meno 32, kikiwa na 76 hicho si kinywa ni tatizo. Ndio maana tunashauri ang'olewe baadhi ya meno yasiyo na ulazima.

Rais atabaki na executive power ikiwa ni pamoja na commander in chief, mkuu wa nchi na serikali na madaraka mengine kama ya kusimamia usalama wa nchi na uwezo wa kuilinda nyakati za dharura, kusimamia uchumi wa nchi na utangamano wa taifa. Hatuhitaji apunguziwe motorcade au body guard, isipokuwa asifanye kazi za kesi za tembo waliotoroshwa kwenda Qatar, kuteua wakuu wa VETA, kusimamia watendaji wa uchimbaji wa visima na matundu ya vyoo.

Tunahitaji rais atakayefanya kazi pamoja na mahakama na bunge na sio rais anayefanyiwa kazi na vyombo hivyo.
Most important ni lazima aelewe kuwa kuna ''watch dog''
 
Mkuu Nguruvi

Unajua kuna mambo mengi sana tunaona yanakwenda ovyo, na tunajua yanakwenda ovyo lakini tunayaacha tu kwa sababu za kisiasa. It is such a shame eti kwa kuwa ni mbunge wa CCM mwanaCCM akihujumu nchi unakaa kinywa kwa excuse ya party solidarity.

Ukiangalia vijana wengi tunafanya makosa sana tunaposifia kuwa Lissu ni mbunge safi mpiganaji, Mwakyembe mbunge safi, lakini tunasahau kuwa the system in which the parliament itself is operating is horrible. So whether a member of parliament is high class or whatever, wote wako kwenye mazingira mabaya kikazi, wametekwa na political system inayoserve interests za Rais na chama tawala.

Unajua kuna madaraka ambayo tupende au tusitake ni lazima yawe ya rais, tena labda yanatakiwa kuimarishwa. Rais ni lazima awe commander in Chief, ni lazima awe chief executive na head of state. Sasa rais akipewa kazi ya kuchagua wabunge ambayo ni kazi ya constituents, au naye akiwa mbunge wakati sisi tunataka awe rais, au akiwa ofisa elimu mkuu that is problematic.

yeye mwenyewe anateua wabunge, yeye mwenyewe ni mbunge kama sehemu ya bunge yeye mwenyewe anaweza kuvunja bunge, ukiangalia yote hayo huwezi kuelewa maana yake hasa ni nini, na lengo lake hasa ni nini. yeye mwenyewe anatunga sheria na yeye mwenyewe anatekeleza sheria na yeye mwenye alinda haki. That is way too much.
 
Katika mchango wake wa hivi karibuni juu ya Katiba Mpya, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue amekuja na hoja kwamba “Kupunguza Madaraka Ya Rais Ni Hatari Kwa Usalama Wa Nchi”, na kusisitiza kwamba kuna umuhimu wa madaraka hayo kubakia kama yalivyo chini ya Katiba Mpya;

Mchambuzi wakuu wa wilaya si waachiwe wapigakura wachague wamtakaye..................huyu balozi anadongo hata hapo/..........wakurugenzi wa halamashauri si waachiwe madiwani wachagu wamtakaye?

uteuzi wa majaji na mahakimu si ufanywe na tume yao ambayo wao wenyewe wadau wake watakuwa wamewachagua na bunge lihakiki zoezi hilo kwa kushirikisha wananchi...........................hapo iko shida gani?

madaraka ya kumpunguzia raisi ni ya uteuzi wa viongozi kwa maana kushirikisha raia na wawakilishi wao ili tupate viongozi bora.

la ajabu raisi huteua watu wengi ambao hata hawafahamu na hivyo kubebeshwa lawama mambo yanapokwenda mrama bila ya sababu ya msingi.........................kikubwa ni uongozi wenye uwazi, shirikishi na wenye kuhakikiwa na umma wote kluwa haki imentendeka..........
 
Mkuu Nguruvi

Unajua kuna mambo mengi sana tunaona yanakwenda ovyo, na tunajua yanakwenda ovyo lakini tunayaacha tu kwa sababu za kisiasa. It is such a shame eti kwa kuwa ni mbunge wa CCM mwanaCCM akihujumu nchi unakaa kinywa kwa excuse ya party solidarity.

Ukiangalia vijana wengi tunafanya makosa sana tunaposifia kuwa Lissu ni mbunge safi mpiganaji, Mwakyembe mbunge safi, lakini tunasahau kuwa the system in which the parliament itself is operating is horrible. So whether a member of parliament is high class or whatever, wote wako kwenye mazingira mabaya kikazi, wametekwa na political system inayoserve interests za Rais na chama tawala.

Unajua kuna madaraka ambayo tupende au tusitake ni lazima yawe ya rais, tena labda yanatakiwa kuimarishwa. Rais ni lazima awe commander in Chief, ni lazima awe chief executive na head of state. Sasa rais akipewa kazi ya kuchagua wabunge ambayo ni kazi ya constituents, au naye akiwa mbunge wakati sisi tunataka awe rais, au akiwa ofisa elimu mkuu that is problematic.

yeye mwenyewe anateua wabunge, yeye mwenyewe ni mbunge kama sehemu ya bunge yeye mwenyewe anaweza kuvunja bunge, ukiangalia yote hayo huwezi kuelewa maana yake hasa ni nini, na lengo lake hasa ni nini. yeye mwenyewe anatunga sheria na yeye mwenyewe anatekeleza sheria na yeye mwenye alinda haki. That is way too much.

Bongolander absolute power corrupts absolutely..................tunachohitaji ni shirikishi na uwazi ya teuzi mbalimbali
 
...............Hoja yako kwamba – maamuzi can be done kwa upesi zaidi huko huko walipo wananchi kuliko Dodoma na Dar-es-salaam, you are right lakini it depends unazungumzia maamuzi gani, vinginevyo as we speak, dhana ya decentralization tayari inafanikisha hilo ambapo kuna serikali za mitaa, serikali za vijiji, na pia kwenye ngazi za kata kuna madiwani ambao wanashirikiana na wabunge wa maeneo yao (wabunge wakiwa pia ni madiwani by default) wakifanya maamuzi mengi tu ya maendeleo katika maeneo yao pertaining to afya, elimu, miundo mbinu n.k;

................... should we trade accountability for stability (hence adopt presidential form of government) or we should trade stability for accountability (hence adopt parliamentary form of government?

Sipendi kuamini......either form of government haziwezi kuwa accountable and/or stable.......huku kutakuwa ni kujinyima na kutojitendea haki kifikraKwanini.......na sipendi kuamini au kufuata mfumo mmoja at expense of the other.....We as nation can do and detremine what is required for our future.......

Kwa mfani ukiwauliza CCM leo wanafuata mfumo gani wa siasa watakuambia "Ujamaa"......kwa watu wanaofahamu Ujamaa halisi ni nini watashangaa kuona yanayoendelea Tanzania kisiasa na kiuchumi......kwani tumeenda zaidi ya Ujamaa na ku-formulate kitu ambacho si wewe/ mimi au CCM wenyewe wanaojua kuwa ni mfumo gani wa siasa.........my point is.....ninaamini Taifa letu limeelimika kiasi cha kuamua ni namna gani nchi yetu iongozwe ili kutuletea maendeleo tunayoyataka..........hizo elimu za mifumo mbali mbali itusaidie kuunda "MODELI" yetu......ili nasi tutoke......

........nadhani umeshasikia nchi nyingi zinazoendelea zinapenda kujifunza kutoka kwenye "modeli" ya Singapore........lets learn from others and create our own "modeli"...itakayotu-suit....

Kuhusu massuala ya decentralization.....nchi yetu bado sana......bado directives zinatoka Dar/Dom .....hizo serikali za mitaa na vijiji ziko kama picha tu.........kama umeishi kule wilayani na vijijini utaelewa ni kitu gani nazungumzia........kama serikali za mikoa, wilaya na vijiji zingekuwa zina-function inavyotakiwa...leo hii issues kama za gesi ya Mtwara, machimbo ya dhahabu au issues kutoka mikoa ya Rukwa/Katavi, Mbeya na Ruvuma zingekuwa somehow "history"............CCM wamehodhi utashi wa wananchi....kwa excuse ya stability....wakati huo huo wanawafisadi wananchi.......

kama CCM wanataka kuendelea kuhodhi utashi wa wananchi na wananchi wakawaelelewa......... inabidi wawe responsible and accountable....period!
 
Mchambuzi, Ahsante sana kwa hoja zako mwanana.
Ukirudi nyuma post 39 Kimweri ameeleza vizuri sana na nakubaliana naye sana kuhusu bunge.

Kwa upande wangu, stability is a byproduct of accountability.
Katika mazingira yetu bunge limepoteza maana ya ''assembly of intellectuals'' limekuwa eneo la kutafutia vipato.
Unapokuwa na corrupt parliamentarians wasiojua kwanini wapo bungeni ni hatari sana kuwakabidhi nguvu za ziada.
Jibu langu linabaki prez form of government. I hope sijafanya contradiction na maelezo yangu ya awali.

Pili, power in the right hand is good and indeed necessary for a new state? Hapa nitauliza, should we take the risk hoping that ''right hand'' opportunity will present itself. Should we remain optimistic that the beautiful one is not yet born!
Is it worth taking the risk at this time when we need to run to catch up with the rest of the world.
I'm pessimistic than optimistic! No! let us take a new direction.

Tatu, sababu zilizomfanya Nyerere achukue hatua hizo ni 2, 3 na 1 ulivyozisema hapo juu.
Ukizitazam vizuri zote zimepoteza maana kwasababu zinategemea. Sababu namba 1 haipo kwasasa. Sababu namba 2 inapunguza ulazima wa sababu namba 3 kwa kiasi kikubwa sana. Sidhani kuwa tunahitaji mtu wa kutuunganisha, ila tunahitaji vyombo vya kulinda kile kilichotuunganisha ambacho Nyerere alikifanya.

Nne, Sababu zinazowakera wananchi ni matokeo ya uzoefu wa miaka 50 na hasa 25 iliyopita. Bila kujali chama gani kitachukua madaraka wananchi wanaona ni wakati sasa tuwe na mfumo tofauti kwasababu tumebadilisha viongozi na haionekani kutoa majibu. People are increasingly become impatient because ''no hope or signs for expected mothers in horizon' hence the beautiful one will not be born soon.
Doing the same thing over and over hoping for different result is a silly thing.

Tano, bila kujali kiongozi atatoka chama gani, Tanzania itabadilika kwa kubadili mfumo na si watu.
Uzooefu unatuonyesha kuwa mfumo uliopo ndio unabadilisha viongozi na si kinyume chake.
Akija Lipumba, Mbowe, Zitto n.k. they will play by the same book. The solution is to write the new one.
Mchambuzi, who knew that the ''son'' of Nyerere will turn to be a big snake and looter on Nyerere's land!!

Mkuu, nadhani tunaposema rais apunguziwe madaraka kuna kitu tunakikosa.
Hatumaanishi kuwa rais awe ceremonial figure! no thank you.

Mimi nina maanisha rais aondolewe yale yasiyomhusu au yanayomkwaza katika utendaji ili awajibike kwa mambo ya kitaifa. Taasisi nyingine kama mahakama zirudishiwe mamlaka na hadhi zao bila kuingiliwa na taasisi ya urais.
Kuwepo na system itakayomfanya rais awajibike zaidi kuliko ku-abuse power.

Kuwepo na functional decentralized system ili wananchi wapange na waaamue hatima ya mambo yao bila bureacracy ya taasisi ya Urais. Mfano uliotoa kuwa tunayo decentralized system ninatofautina nao kwasababu iliyopo ni cosmetic tu.
Wanannchi hawana nguvu zaidi ya mkurugenezi, mkuu wa wilaya au mkoa.

Haiwezekani tatizo la Tanzania nzima likawa shule za kata, kuna kwingine hawana Hospitali, maji n.k
Priority za nini wanataka zinapangwa Dar na hazitoki kwao, na hapo ni kuwanyima fursa ya maendeleo yao.

Huu mfumo wa sasa ni symbolic, ukweli ni kuwa rais anaingilia madaraka hata ya kuamua visima vya maji achilia mbali vyoo vya shule through his presidential power, trickling down.

Ni wakati sasa yeye abaki kuwa na executive power ya mambo ya kitaifa mengine yafanywe na taasisi nyingine.
Kwanini rais amiliki PCCB? Who will be a watch dog to his government!

Kwangu mimi kumpunguzia madaraka is to make him accountable under the check and balance system.
He should not have an open ended executive power! no! at some point there should be a ''watch dog'' against him.

Nilimsikiliza Obama majuzi ile wakati anaongelea kuhusu US ku-pays 'Bills" zao..........pale ndio utaona kuwa ni kwa jinsi gani Rais anavyoheshimu mihimili mingine ya Uongozi.........
 
Mchambuzi

Ningependa sana kuchangia kwenye thread yako ya uliyoweka hapa ila sina privileges za kufanya hivyo, ndiyo maana nimeona nikujibu kwa kutokea huku:

Umegusia madaraka ya raisi yanayoongelewa kuwa haya:
• He/she is the head of state with Full Executive Powers and Commander in Chief of the Armed Forces;
• The Cabinet which he appoints largely from MPs is ‘only' advisory to him;
• He has full powers to appoint, promote, dismiss and to exercise disciplinary control over the Civil Service including the Judiciary and so forth;
• He/She also has an overall responsibility for Government Organization and Direction;

Ni kweli madaraka hayo ni makubwa sana na ndiyo yanayosababisha nchi isikose mwelekeo kwa vile yanafanya mwelekeo mzima wa nchi umtegemee rais tu, na iwapo rais huyo atakuwa ni dhaifu basi nchi nzima inaharibika. Hatuwezi kujifanya kuwa kila mara tutakuwa na viongozi thabiti tu, la hasha kufanya hivyo tutakuwa tunajidanganya; tutawapata maraisi dhaifu wengi sana na hasa hawa watakokuja huko mbele yetu ambao wamelelewa kisiasa na viongozi dhaifu hawa wa sasa.

Madaraka ambayo ni lazima rais apunguziwe ni pamoja na haya yafuatayo:

• He/she is the head of state with Full Executive Powers and Commander in Chief of the Armed Forces;

Pamoja na kuwa rais ndiye Commander In Chief of Armed Forces, ni vibaya kumpa madaraka yote ya kuamrisha jeshi kufanya operation yoyote ya kijeshi bila kupata kibali cha bunge. Rais anaweza kutumia madaraka hayo kwa lengo binafsi kama vile kwenda kupigana nchi ya jirani ili kumsaidia rafiki yake kisiasa, anaweza kutumia madaraka hayo vibaya ili kuwazima wapinzani wake wa ndani kisiasa, na vile vile anaweza kutumia madaraka hayo vibaya ili kujipatia mali binafsi kutoka nchi jirani. Kwa hiyo ni lazima kupunguza wigo wa madaraka ya rais katika kutoa amri za kijeshi; amri zote zinazohusu operations za kijeshi ni lazima zipitie bungeni ili kupata ridhaa ya wananchi. Kunaweza kuweko na utaratibu wa kikatiba wa kuhakikisha kuwa kibali cha dharura cha bunge kinatolewa iwapo itaonekana kuwa muda ni critical katika operation hiyo.

• He has full powers to appoint, promote, dismiss and to exercise disciplinary control over the Civil Service including the Judiciary and so forth;

Hapa ndipo kwenye utatinishi mkubwa sana unaotakiwa kufumbuliwa:

Ijulikane kuwa wateule wote wa rais siyo watumishi wa rais bali ni watumishi wa umma; watumishi hao wa umma wanatakakiwa wawajibike kwa umma huo siyo kwa rais aliyewateua, na hivyo basi katika uteuzi huo, ni lazima kuwe na baraka za umma kupitia kwa wabunge wao. Isiwe rahisi kwa rais kuwafukuza watumishi wa umma aliowateua bila kupata kibali cha bunge ili kuondoa mwanya kwa watumishi hao kufanya kazi kwa lengo la kumfurahisha rais tu badala ya kufanya kazi ya kufurahisha umma.

Vile vile kwenye watendaji wa kwenye Civil Service wasiwe wa kuteliwa tu; nafasi nyingi ziwe za contract (renewable) ambapo mtu ataomba kulingana na qualifications zake. Mwishoni mwa contract hiyo, performance yake inakuwa evaluated na iwapo hairidhishi basi anakuwa replaced.

Nafasi nyingine nyingi za kuteuliwa kama wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ziondolewe kabisa, badala yake ziwe za kuchaguliwa.

• He/She also has an overall responsibility for Government Organization and Direction;

Rais hawezi kujiundia serikali atakavyo; mara anaunda baraza la mawaziri 50 mara anaounda baraza la mawaziri kubwa kusudi ndugu na marafiki zake tu wapate madaraka. Ni lazima kuwa na utaratibu wa kikatiba unaoweka bayana muundo wa serikali, halafu rais atatakiwa kuunda serikali hiyo kwa mujibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom