Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Mkuu Ab-Titchaz na Invisible naomba mumpe access Mwl Kichuguu kwenye huu ukumbi........samahani kwa usumbufu.......

Ndugu yangu nashukuru kwa kuniombea kibali hiki; kwa muda mrefu nilikuwa sijui limits zangu hadi wiki chache zilizopita nilipogundua kuwa kuna jamvi ambalo nilikuwa siruhusiwi. Nimekuwa nasoma post nyingi bila kuzichangia, lakini hii imenigusa sana kwani niliwahi kuindika jamvini hapa mwaka 2007.

Tukumbuke tena kuwa "Absolute power corrupts absolutely"
 
Ogah - bandiko lako namba 38,

Suala la stability versus accountability in inherent kwa mifumo husika – mfumo wa kibunge katika utawala wa nchi by default hupelekea more accountability lakini less stability; Accountability kwa maana moja tu kwamba Waziri Mkuu anapovurunda, bunge lina uwezo wa kumwondoa straight away kupitia vote of no confidence na kuitisha uchaguzi mkuu mpya, na ni suala hili la uwezekano wa chaguzi kujitokeza mara kwa mara ndio hupelekea mfumo huo kubatizwa kwamba ni unstable lakini upo vizuri katika masuala ya accountability; Kwa upande mwingine, presidential system of government huwa more stable kwani uchaguzi wa Rais husubiria vigezo vya kikatiba, hence kufanya nchi na utawala kwa ujumla kutokuwa unstable licha ya kwamba katika kuelekea uchaguzi mkuu unaofuatia kwa mujibu wa Katiba, mfumo unaweza pelekea less accountability kwa umma iwapo Rais atakuwa hawajibiki ipasavyo lakini analindwa na Katiba unlike mfumo wa kibunge ambapo Waziri Mkuu anaweza kutimuliwa hata mara kumi ndani ya miaka mitano;

The bottom line hapa ni kwamba mfumo mmoja unapelekea hali ya more accountability kuliko stability na mwingine unapelekea hali ya stability kuliko accountability kwa reasoning hiyo, na hapa hakua siasa wala maneno yenye chumvi bali it is a fact; Ni muhimu umma ukajua unataka nini between the two katika mchakato wa kupata Katiba mpya, kwani tunaweza kuja juta sana iwapo tutafanya maamuzi ya kumpunguzia madaraka Rais bila ya kuangalia athari zake katika muktadha wa parliamentary versus presidential form of government; Kwa maana nyingine, tukifanya maamuzi ya kumpunguzia madaraka rais kikatiba, ni muhimu maamuzi hayo yaende sambamba na yale yanayuhusu aina ya mfumo ambao utaendana na Katiba mpya; Tusijisahau tukaacha suala hili la aina ya mfumo liishie hewani au lifanyiwe maamuzi na watu wengine;

Kuhusu decentralization, kimsingi nakubaliana na hoja yako; Kumekuwa na utekelezaji mdogo sana wa suala zima la decentralization, hasa katika suala la bajeti au fedha; maamuzi juu ya mahitaji na matumizi ya fedha ngazi za chini yameendelea kubakia ngazi za juu; Ni kawaida kwa kwa mwaka mpya wa fedha (mwezi juni) kuwasili huku Idara au Mikoa fulani bado haijapata fedha zote zilizoidhinishwa kwa ajili yao katika mwaka wa fedha uliopita;
 
Kichuguu,

Karibu katika mjadala na pole sana kwa heka heka za kutafuta access to Great Thinkers Forum;

Majibu yangu yanahusiana na hoja zako kweney bandiko namba 60 la mjadala; Kwanza, nikubaliane na hoja yako kwamba "absolute power corrupts absolutely"; Vile vile nakubaliana na hoja yako kwamba its risky kuacha katiba impe madaraka Rais huku tukiomba mungu kwamba ipo siku atakuja Rais mwenye sifa za kutuokoa chini ya imani kwamba "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"; Lakini pamoja na hayo, mimi bado naamini katika dhana hii, hasa kwa taifa dogo na changa kama letu; Wengi wanajadili kwamba Tanzania sio taifa changa kwa vile lina umri wa miaka 50;

Tukiangalia taifa la Marekani, taifa hili lilikuwa na umri wa miaka 50 ilipofika mwaka 1826, chini ya Rais wa sita wa nchi hiyo John Quincy Adams; Ningependa pia mchangiaji mwenzetu humu bobuk anisome katika hili, hasa kutokana na hoja yake kwamba Tanzanai sio Taifa Changa, na kwamba kwake yeye Taifa Changa Afrika ni South Sudan pekee;

Iwapo Marekani kama Taifa wangejiona wameshakomaa at age of 50, leo wasingekuwa hapa walipo; Kumbuka kwamba by the year 1826 (mwaka wa hamsini wa Marekani kama Taifa), matukio makubwa kama American Civil War na mengineo mengi yalikuwa bado hayajatokea, Civil War ilikuja kutokea zaidi ya miaka themanini baada ya kuzaliwa kwa taifa hili; Kwa Tanzania, ni kama tuseme tupaet tatizo kubwa la vita ya wenyewe kwa wenyewe miaka ya kukaribia 2050;

Vile vile, katika umri wa miaka hamsini ya Marekani kama Taifa – bado kulikuwa na mvutano mkubwa sana ndani ya jamii juu ya mfumo bora wa kufuata baina ya Presidential form of government versus Parliamentary form of government; Ilipofika mwaka 1849, the 12[SUP]th[/SUP] President wa taifa hilo ambae awali alikuwa ni Jenerali wa Jeshi – Zachary Taylor, akaingia madarakani kupitia chama cha Whig ambacho leo hakipo tena katika siasa za nchi hiyo kutokana na mitazamo yake kupitwa na wakati; Sera zilizoipa nguvu candidature ya Jenerali Taylor pamoja na Chama Chake Cha Whig ni pamoja na msimamo wao wa kuunga mkono kwamba Bunge liwe na madaraka zaidi ya Rais – yani taifa lifuate a Parliamentary form of government; Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya taifa hili kuja gundua kwamba walikuwa wanafanya makosa kwani kasi ya kuipeleka nchi mbele zaidi katika dunia ya ushindani ilihitaji a president with full executive powers hence adoption of a Presidential form of government iliyo ambatana na effective checks and balance;

Ni katika muktadha huu ndio nimekuwa nikihimiza umuhimu wa kufikiria mara mbilimbli suala la kumpunguzia Rais madaraka kabla ya kufanya maamuzi haya chini ya Katiba mpya; Sipingi mabadiliko lakini natoa angalizo tu kwamba tufanye maamuzi baada ya kuwa well informed, tusikurupuke tu kutokana na hasira au uchovu unaotokana na madudu yanayoendelea katika uongozi wa taifa letu katika nyakazi hizi;

Nikirudi katika hoja zako nyingine juu ya madaraka ya Rais Kikatiba, ni kama ifuatavyo:
Kwanza ni hoja yako kwenye kipengele cha - He/she is the head of state with Full Executive Powers and Commander in Chief of the Armed Forces;

Hapa nakubaliana na wewe, kuna umuhimu wa Rais kuwekewa checks and balance katika suala hili; Wakati wa Mwalimu, tuliingia katika Vita dhidi ya Amin, na Vita hivi vilikuwa justified (vilikuwa ni halali); Gharama ya Vita hivi kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni kwamba viligharimu taifa $500 Million (kwa thamani ya mwaka 1980); Kwa mujibu wa wataalam wa uchumi juu ya masuala yaku convert dollar ya wakati uliopita ili kujua thamani ya hiyo dollar katika nyakazi ya sasa, $1 Mwaka 1980 ni sawa na kama $2.70 mwaka 2012; Kwa maana hii, vita vya Kagera kwa gharama za leo takriban $1.4 billion, na kwa shillingi za kitanzania ni sawa na shilling trillioni mbili na ushee; Kwa Kagera inaeleweka, lakini kwa Vita vya ovyo ovyo ambavyo Rais anaweza tu kujiamulia kutoka usingizini, huu ni mzigo mkubwa saa kwa walipa kodi, hivyo naunga mkono hoja yako kwamba ni muhimu Katiba iwe na restrictions juu ya hili kwani mbali na gharama kubwa kwa walipa kodi, Vita pia inaathiri sana shughuli za kijamii na kiuchumi ndani ya nchi;

Hoja yako ya pili juu ya kipengele cha - He has full powers to appoint, promote, dismiss and to exercise disciplinary control over the Civil Service including the Judiciary and so forth;
Katika hili, nakubaliana na hoja zako kama zilivyo katika bandiko lako namba 60 lakini ningependa kufahamu je - hapa madaraka ya rais yaondolewe au yadhibitiwe? Pia nini ni mtazamo wako juu ya aina gani ya mfumo ungependelea uwepo ndani ya Katiba mpya kuendana na mabadiliko unayojadili - tufuate Presidential au Parliamentary form of government?

Na hoja yako ya mwisho katika bandiko lako namba 60 - He/She also has an overall responsibility for Government Organization and Direction;
Hapa pia nakubaliana na wewe mstari kwa mstari; katika hili pia, je kwa maoni yako, madaraka ya rais yaondolewe au yadhibitiwe? Pia nini ni mtazamo wako juu ya aina gani ya mfumo ungependelea uwepo ndani ya Katiba mpya kuendana na mabadiliko unayojadili - tufuate Presidential au Parliamentary form of government?

Nimalizie kwa haya:

Nadhani tunakubaliana juu ya umuhimu wa rais kuwa na nguvu kimaamuzi lakini kupitia checks and balance husika, hasa bunge; Unalizungumziaje hili katika mazingira ambayo unaweza kukuta chama kimoja ndio kina majority bungeni na chama husika hakijafanya reforms ambazo zinatakiwa kiwe na maamuzi yenye kuweka maslahi ya taifa mbele na badala ya maslahi ya Chama? Tuna tatizo hili ndani ya CCM, Chadema, CUF, n.k, kila maamuzi huwa ni partisan; Kwa mtazamo wangu, tunafanya makosa makubwa sana kukimbilia kwenye mabadiliko ya Katiba huku tukidharau umuhimu wa reforms ndani ya vyama vya siasa, kwani chini ya Katiba za Sasa za Vyama vyetu Vya Siasa ambazo Katiba ya nchi inaendelea kutojishughulisha nazo, under the majority bungeni, Ikulu ya Chadema, CCM, au CUF ndio itakayotoa maamuzi ambayo bungeni yataenda kupitishwa kama yalivyo kwani wabunge watatakiwa kuunga mkono maamuzi ya Chama vinginevyo watakuwa wanaenda kinyume na misimamo ya Chama;

cc nguruvi3, EMT, bongolander
 
Mkuu Mchambuzi;

(1) Kuhusu ukomavu wa Taifa, nadhani tutafanya makosa kutaka kufuata historia ya taifa lililokomaa la Marekani kama model yetu, bali tunatakiwa tujifunze kutoka kwenye historia hiyo. Marekani ilipitia historia ndefu kulingana na wakati na vile vile kulingana na namna taifa hilo lilivyoundwa; lilianza likiwa ni makoloni kadhaa yanayojitegemea halafu kwa pamoja yakaamua kuasi utawala wa kikoloni na kuuangana, ila kwa vile mawasiliano hayakuwa ya kasi kama leo, iliwachukua miaka mitatu kwa zile state 13 za kwanza kukamilisha utaratibu wa kuandikiana makubaliano ya kuungana. Halafu hali iliendelea hivyo pole pole hadi baada ya miaka 110 ndipo wakawa wamekamilika kuwa Taifa tunalolijua leo; kwa hiyo kufuata model yao kuwa miaka hamsini bado ni uchanga kitaifa tutakuwa tunafanya makosa; tujifunze kutoka kwao; au tujifunze kwa nchi kama India au Singapore ambazo hatukutofautiana sana kupata Uhuru; waliopokuwa na miaka 50 walikuwa wako mbele sana, na wana utaratibu ambao kiongozi wa nchi hana absolute power kama rais wetu sisi.

(2) Katika dunia ya leo ambayo imekuwa kama kijiji kidogo, ni lazima tuachane na mifumo ya utawala ya kizamani ambamo kiongozi mmoja tu ndiye anakuwa na madaraka yote; sababu zipo nyingi. Katika kujibu maswali yako mengine uliyouliza, ninakubaliana na wewe kuwa hatuwezi kumnyima rais madaraka, ni lazima rais wetu awe na madaraka lakini tunataka madaraka hayo yawe na mipaka yake. Baadhi vitu nilivyoguzia kuhusu mipaka hiyo ni pamoja na:

(a) Kumpunguzia mamlaka ya kuteua na kufukuza mtu wakati wowote; uteuzi anaofanya rais ni lazima uthibitiwe, na utaratibu wa kufukuza wateule pia ni lazima uthibitiwe kikatiba. Nadhani nimeeleza vizuri kuwa kufanya hivyo kutasababisha wateule wasiwe wanafanya kazi zao kwa kujipendekeza kwa rais. Kuna njia tatu za kuthibiti madaraka hayo: (i) kwanza ni kupunguza nafasi za kuteuliwa- rais asiteue nafasi za makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wabunge maalumu. Makatibu wakuu wawe ni wanataaluma watakaoomba nafasi hizo na kusailiwa kama wanataaluma wengine, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wachanguliwa na wanachi kwa kura. (ii) Pili ni kuwapo na muundo wa serikali kikatiba, yaani idadi ya wizara ziwe zimeandikwa ndani ya katiba. Kwa hiyo iwe inajulikana kabisa kuwa atateua mawaziri wangapi kulingana na idadi iliyoandikwa ndani ya katiba> (iii) Utezi wowote wa rais ni lazima uwe unakubaliwa na Bunge, yaani rais ana-nominate, na bunge lina-confirm; vile vile katika kumfukuza mteule, rais ata- recommend kumvua mteule madaraka, halafu bunge lina-confirm mteule huyo kuvuliwa madaraka.

(b) Kumpunguzia mamlaka ya kuamuru jeshi kufanya operesheni yoyote ya kijeshi. Operesheni zote za kijeshi ziwe zinapata baraka ya Bunge, na hapa niliongeza kuwa katiba inaweza kuweka mwanya maalumu wa rais kuanzisha operesheni za kijeshi kwa kushirikiana na viongozi wachache wa bunge bila kupata kibali cha bunge zima iwapo operesheni hiyo ni time-sensitive.


Ili kuondoa mgongano baina ya bunge na rais, katiba iweke utaratibu wa ziada baada ya kutokea mvutano baina ya rais na bunge. Kuna njia nyingi za kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa Bunge halimbani sana rais kama ambavyo Marekani leo hii Bunge lao limekuwa linamfanya Rais wao ashindwe kufanya kazi zake vizuri, siyo vigumu kuweka utaratibu huo.
 
EMT,

Maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "power in the right hands is good and indeed necessary for a new state" yanaweza kuwa sahihi kwa taifa jipya kama South Sudan. Lakini sidhani kama tunaweza kusema kuwa taifa letu ni jipya na hivyo tumpe madaraka mtu mmoja.

Tanzania siyo taifa jipya, bali demokrasia yake ndiyo bado changa. Demokrasia yetu bado ipo kwenye majaribio na kuna taasisi nyingi tuu, ikiwemo ya Rais, ambazo zinahitaji kufanyiwa review.

Katika haya, nina masuala mawili - matatu ningependa kuyajadili; Kwanza, kwa mtazamo wangu, kuna utofauti baina ya taifa jipya na taifa changa; Iwapo utakubali nikuelekeze zaidi katika dhana ya uchanga kuliko upya, unatumia criteria ipi au zipi to gauge or to determine uchanga wa taifa - umri? Kama ni umri wa taifa, ni miaka mingapi?

Pili unaposema kwamba demokrasia yetu bado changa, una maanisha demokrasia ya aina gani na unaipimaje? Umri? Kama ni umri wa demokrasia, ni miaka mingapi?

Suala la tatu ambalo ningependa kulijadili kidogo lakini zaidi pia kwa mtindo wa Swali kwako ni kwamba - Ukichukulia Tanzania na Somalia, how would you describe these two kama mataifa in terms of upya, uchanga, or anything in these lines... Bear in mind kwamba Somalia ceased to be a British protectorate earlier than Tanganyika i.e. Somalia (1960) na Tanganyika a year later (1961);

  • Kwa upande mwingine, tatizo linaweza lisiwe kumpa Rais madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa "checks and balances" kuhakikisha kuwa hayo madaraka hayatumiwi vibaya.
  • Nafikiri tatizo siyo Rais kuwa na madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa checks and balances kuhakikisha kuwa hayatumii hayo madaraka vibaya. Mbona Rais wa Marekani ana madaraka makubwa tuu kiasi kwamba anaweza ku-command the instant destruction of an entire city within minutes?
  • Marekani ina maelfu ya missiles with nuclear warheads na ni Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutoa signal to launch them. Ila checks and balances zinahakikisha kuwa anayatumia haya madaraka vizuri.
  • Ukiondoa madaraka ya Rais na kumpa mtu mwingine, una uhakika gani kuwa hatayatumia vibaya? kwa mtu kama huyu?
  • Kupunguza madaraka ya Rais haitasaidia sana unless tuwe na uhakika kuwa hao wengine tutakaowapa hayo madaraka watayatumia vizuri. Otherwise, itakuwa ni kulihamishia tatizo kutoka kwa mtu/taasisi m/moja kwenye kwa taasisi mtu mwi/nyingine.

  • Sidhani kama tatizo lipo kwa Rais kuwa na madaraka makubwa bali kukosekana kwa checks and balances jinsi rais anavyotumia hayo madaraka. Kuwepo kwa strong checks and balances zitamfanya rais awe makini zaidi jinsi anavyotumia madaraka aliyopewa.

Kwa hiyo, swali la kujiuliza siyo kwa nini Rais asipunguziwe madaraka aliyonayo sasa, bali ni kwa nini madaraka ya Rais yasiwe subject to democratic review or checks and balances ambazo kwa sasa hazipo?

Kimsingi, nakubaliana na wewe katika yote hapo juu, hasa umuhimu wa kutazama ni wapi tupunguze madaraka ya Rais kufanikisha nini na ni wapi tusipunguze bali tudhibiti madaraka ya rais na kwa lengo la kufanikisha kitu gani.Ubovu wa utawala mmoja usitufanye tuje na maamuzi ambayo baadae tunaweza juta;

Naomba nimalizie kwa swali lingine kwako:

Kwa mtazamo wako, in the context of all the above, tufuate mfumo gani chini ya katiba mpya na kwanini - presidential form of government au parliamentary form of government?
 
By the way, out of this topic. Can yon tell me serikali katika mwezi huu januari imefaya kazi gani ya maana inayohusiana na maendeleo ya nchi? Au rais au PM, tunaweza kujua wanafanya kazi gani kwa ajili ya maendeleo ya nchi? au ndio wanafanya kazi zile zile za kila siku za mambo yale yale ya siasa? just curious, labda wewe unajua kidogo on this.

Bongolander,

Hoja zako kwenye bandiko namba 52, nyingi nakubaliana nazo - kwamba taasisi ya urais inakabiliwa na changamoto nyingi sana tofauti na miaka ya nyuma, hivyo kuna ulazima wa kuiangalia upya kwa maslahi ya nchi/wananchi; Lakini tukirudi nyuma kidogo na kujiuliza, je, ni kwanini chini ya awamu ya Mwalimu Nyerere such powers tuliona zipo justified lakini sasahivi hatuoni umuhimu wake? Hili ni swali ambalo wengi wanajaribu kulijibu kwa kuzunguka, hasa kwa kujenga hoja kwamba its risky kuiachia katiba impe rais wa nchi mamlaka husika kwa matumaini kwamba siku moja atakuja rais anayetufaa na kuikomboa nchi yetu; Pia hapa nina swali - je mahitaji ya such powers chini ya mwalimu ni kwamba yamepitwa na wakati? yameshafanikisha kazi yake? au ni suala la risk kuendelea na project husika?

Vinginevyo kimsingi naelewa hoja za watu mbali mbali juu ya umuhimu wa kuimarisha systems za checks and balance lakini at the the same time, we are not sober enough kujadili matatizo yaliyopo ndani ya vyama vyetu vya siasa na tusipokuwa waangalifu, tutamaliza mchakato wa katiba bila kuhakikisha kwamba inazungumza mambo fulani fulani kuhusu conduct za vyama vyetu vya siasa ambapo as we speak, any majority bungeni (iwe CCM, CUF, Chadema) inaweza kufanya maamuzi ambayo ni partisan zaidi kuliko yanayojali zaidi maslahi ya taifa; Vyama vyetu ni muhimu vifanye mageuzi ya ndani huku yale ya msingi yakiwekewa kanuni au utaratibu kwa mujibu wa katiba ya nchi;, vinginevyo bila umakini, tutarudi kule kule hata chini ya utawala wa chama kingine cha siasa;

Kuhusu suala la taifa letu kuwa na hybrid ya mfumo wa utawala baina ya presidential na parliamentary, ni kweli; Mapema 1960s tuliamua kuondokana na mfumo wa kibunge na kuanza kuwekeza zaidi kwenye mfumo wa Urais na hili likawa cemented zaidi baadae baada ya adoption ya mfumo wa chama kimoja cha siasa, na baadae zaidi kwenye Katiba ya muda ya 1965, kisha katiba ya kudumu ya 1977; Ilipofika mwaka 1985 wakati mwalimu anaondoka kupisha economic reforms, political reforms ziliendelea kuwekwa kapuni; political reforms have been trekking economic reforms for almost a decade; Iwapo tungefuata mapendekezo yote ya tume ya nyalali miaka ya mwanzo ya tisini, CCM isingekuwa katika shimo hili la sasa kwani iliendelea kuamini kwamba itaweza Ku-implement liberal democracy at her own pace, in a top-down fashion, kwa hoja kwamba kwenda pupa itaharibu hali ya amani na utulivu - of which kwa mujibu wa katiba ya 1977, rais ndio custodian wa hilo;

Swali linalofuata ni je, kwanini implementation ya economic reforms nayo haikufuata an incremental process (kidogo kidogo) kama mageuzi ya kisiasa na badala yake kiuchumi mambo yakawa implemented radically bila ya kujali madhara yake kwa wananchi? Yote haya mawili - yani incremental implementation of liberal democracy na radical implementation of economic reforms ndio yamepelekea CCM to meet in collision course na umma kwani kwa sasa, umma umeaminishwa kwamba wao ni maskini kwa sababu ya kuchechemea kwa mabadiliko ya kisiasa ambapo ilitakiwa yaje kwa kasi kama ile ya mageuzi ya kiuchumi - in other words, umma una aminishwa kwamba iwapo mageuzi ya kisiasa yangeenda kwa spidi kali kama mageuzi ya kiuchumi, basi hali zao (wananchi) zingekuwa bora zaidi; je kuna ukweli kiasi gani katika this argument? huo ni mjadala mwingine;

Ningependa kumalizia kwa kusema yafuatayo:

Kwanza, tumefikia hapa kutokana na sisi CCM kuchelewa to realize that - mfumo wa vyama vingi unahitaji a neaw arrangement baina ya the party in power and organs of the state; Tunaendelea kuwa na kitu kinachofanania na corporate structure ambapo mihimili mingine na taasisi muhimu za za ulinzi na usalama, lakini pia za kiraia zinaendelea kufanywa kama ni idara ya Chama Cha mapinduzi;

Pili - ni muhimu kwa CCM kukubali tu matokeo and transform from kudhania kwamba CCM is the only political expression of the state .It is prudent tubadilike, tena haraka (kabla hatujatokomezwa na umma for good) na kuwaa political party (among other political parties which have equal rights and privileges before the constitution) contending with other parties within that very same state; In short, tukubali kwamba sasa we are contenders kama wengine;

Ni masuala haya mawili ambayo kwa kiasi kikubwa ndio yanaipa CCM headache when it comes to mabadiliko ya Katiba;

Naomba nieleweke kwamba sitetei CCM au kupinga mabadiliko husika, bali najadili kwa maoni yangu tumefikaje hapa;
 
Mkuu Mchambuzi;

(1) Kuhusu ukomavu wa Taifa, nadhani tutafanya makosa kutaka kufuata historia ya taifa lililokomaa la Marekani kama model yetu, bali tunatakiwa tujifunze kutoka kwenye historia hiyo. Marekani ilipitia historia ndefu kulingana na wakati na vile vile kulingana na namna taifa hilo lilivyoundwa; lilianza likiwa ni makoloni kadhaa yanayojitegemea halafu kwa pamoja yakaamua kuasi utawala wa kikoloni na kuuangana, ila kwa vile mawasiliano hayakuwa ya kasi kama leo, iliwachukua miaka mitatu kwa zile state 13 za kwanza kukamilisha utaratibu wa kuandikiana makubaliano ya kuungana. Halafu hali iliendelea hivyo pole pole hadi baada ya miaka 110 ndipo wakawa wamekamilika kuwa Taifa tunalolijua leo; kwa hiyo kufuata model yao kuwa miaka hamsini bado ni uchanga kitaifa tutakuwa tunafanya makosa; tujifunze kutoka kwao; au tujifunze kwa nchi kama India au Singapore ambazo hatukutofautiana sana kupata Uhuru; waliopokuwa na miaka 50 walikuwa wako mbele sana, na wana utaratibu ambao kiongozi wa nchi hana absolute power kama rais wetu sisi.

Mkuu kichuguu,

Katika hili, nia yangu sio kupendekeza kwamba tuwaige marekani bali tujifunze kutoka kwao ili mwisho wa siku tuje na maamuzi ambayo yapo more informed; Kimsingi, hiyo ni moja ya nia zangu za msingi katika mjadala huu; Vinginevyo mifano ya Marekani na India ni mizuri kwani kwa upande mmoja, marekani ni demokrasia yenye mafanikio makubwa kuliko yote duniani kiuchumi, huku india ikiwa ni demokrasia kubwa kuliko zote duniani; Marekani inafuata mfumo wa Urais ambao inherently kama nilivyofafanua huko nyuma, mfumo huu upo more stable lakini una matatizo katika accountability; Tatizo la accountability katika muktadha wa utawala wa marekani tuliuona wakatio wa Bush (rejea maamuzi mbalimbali katika utawala wa Rais Bush); India wao wanafuata mfumo wa kibunge )parliamentary form of government ambao inherently ni more accountable lakini less stable; tumeona jinsi gani India inavyokabiliwa na instability ingawa on the accountability front, ipo mbali sana; Sijui sana kuhusu Singapore zaidi ya kuielewa juu juu, nikiwaelewa zaidi, ntakurudia juu ya hilo kwani nadhani Singapore ni muhimu sana katika hoja zako kwani umeijadili kama mfano zaidi ya mara moja sasa;


(2) Katika dunia ya leo ambayo imekuwa kama kijiji kidogo, ni lazima tuachane na mifumo ya utawala ya kizamani ambamo kiongozi mmoja tu ndiye anakuwa na madaraka yote; sababu zipo nyingi. Katika kujibu maswali yako mengine uliyouliza, ninakubaliana na wewe kuwa hatuwezi kumnyima rais madaraka, ni lazima rais wetu awe na madaraka lakini tunataka madaraka hayo yawe na mipaka yake. Baadhi vitu nilivyoguzia kuhusu mipaka hiyo ni pamoja na:

(a) Kumpunguzia mamlaka ya kuteua na kufukuza mtu wakati wowote; uteuzi anaofanya rais ni lazima uthibitiwe, na utaratibu wa kufukuza wateule pia ni lazima uthibitiwe kikatiba. Nadhani nimeeleza vizuri kuwa kufanya hivyo kutasababisha wateule wasiwe wanafanya kazi zao kwa kujipendekeza kwa rais. Kuna njia tatu za kuthibiti madaraka hayo: (i) kwanza ni kupunguza nafasi za kuteuliwa- rais asiteue nafasi za makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wabunge maalumu. Makatibu wakuu wawe ni wanataaluma watakaoomba nafasi hizo na kusailiwa kama wanataaluma wengine, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wachanguliwa na wanachi kwa kura. (ii) Pili ni kuwapo na muundo wa serikali kikatiba, yaani idadi ya wizara ziwe zimeandikwa ndani ya katiba. Kwa hiyo iwe inajulikana kabisa kuwa atateua mawaziri wangapi kulingana na idadi iliyoandikwa ndani ya katiba> (iii) Utezi wowote wa rais ni lazima uwe unakubaliwa na Bunge, yaani rais ana-nominate, na bunge lina-confirm; vile vile katika kumfukuza mteule, rais ata- recommend kumvua mteule madaraka, halafu bunge lina-confirm mteule huyo kuvuliwa madaraka.

(b) Kumpunguzia mamlaka ya kuamuru jeshi kufanya operesheni yoyote ya kijeshi. Operesheni zote za kijeshi ziwe zinapata baraka ya Bunge, na hapa niliongeza kuwa katiba inaweza kuweka mwanya maalumu wa rais kuanzisha operesheni za kijeshi kwa kushirikiana na viongozi wachache wa bunge bila kupata kibali cha bunge zima iwapo operesheni hiyo ni time-sensitive.

Nakubaliana na wewe katika hoja zote hapo juu, lakini hasa iwapo focus ipo zaidi katika kuthibiti nguvu za rais, sio kuziondoa; Lakini pia naomba ulifikirie hili katika muktadha wa mageuzi ndani ya vyama ambapo nilijadili kwamba tunaweza kuendelea kujisahau na kuacha kuthibiti vyama vya siasa ndani ya Katiba ya nchi, na kupelekea vyama kuendelea kufanya maamuzi partisan ahead of maslahi ya taifa; Chadema au CUF ikiingia sasahivi ikulu, literally itafanya maamuzi mengi ya kichama kama CCM; Kwahiyo ni muhimu katika kudhibiti nguvu za rais kikatiba, pia tukathibiti vyama vya siasa kikatiba;

Ili kuondoa mgongano baina ya bunge na rais, katiba iweke utaratibu wa ziada baada ya kutokea mvutano baina ya rais na bunge. Kuna njia nyingi za kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa Bunge halimbani sana rais kama ambavyo Marekani leo hii Bunge lao limekuwa linamfanya Rais wao ashindwe kufanya kazi zake vizuri, siyo vigumu kuweka utaratibu huo.

Naelewa hoja yako hapa, lakini tukumbuke pia kwamba huko nyuma, marekani ilikuwa na mfumo wa kibunge hasa chini ya chama cha Whig lakini baadae mfumo huu ukaonekana kwamba haufai, hivyo wakaamua kuwa na an executive president; Unajua suala muhimu ambalo tunalisahau ni kwamba sisi kama Taifa, nini ni values, vision and ethos zetu? Haya ni masuala ambayo hayatakiwi kuwa na any compromise na badala yake, lazima kuwe na bipartisan stance badala ya kufanya maamuzi or take ideological positions kuendana na vyama; wenzetu marekani kuna masuala ambayo hayana mjadala, kwa mfano national security n.k, haya hayana itikadi; je kwetu sisi yawe masuala gani? Katiba iyaweke haya sasa, itasaidia sana kupunguza migongano isiyokuwa na tija baina ya taasisi ya Urais na Bunge;

cc nguruvi3, EMT, bongolander
 
Kwa Tanzania Parliamentary System ni Majanga.Ni ukweli usiofichika kuwa our parliament is full of useless figures.No disrespect to Prof.Majimarefu et.al,but such kinds of figures are just filling empty chairs.

Presidential form of government is a bit better at the moment until we reach a level where Tanzanians understands why they elect MP's and what caliber an MP should have/be.

Pamoja na Madhaifu yake yooote, Kikwete na taasisi nzima ya Uraisi is miles ahead better than our parliament collectively.We do have few probably a handful brilliant MP's thats about it.Ukiona Rais inabidi ateue mtu kuwa mbunge ili kujazia baraza la mawaziri, jua kuna tatizo kubwa, ukiona the likes of Mulugo and such wanakuwa mawaziri jua kuna tatizo kubwa kuliko.

With the way votes are conducted in our parliament,i wouldn't want those empty heads to decide if the country goes to war or not. Am sure if the malawi issue was put up to the parliament to decide,we would long be in war by now.WHY?because in our parliament a few noisy MP's influence the rest who just follow the beat.

Kimweri,

Asante sana kwa mchango wako, hasa kwa ujasiri wa kujadili kwanini mfumo mmoja kwa mtazamo wako ni bora kuliko mfumo mwingine i.e. presidential form of government vis a vis parliamentary form of government; Wachangiaji wengi wana hamasa kubwa sana juu ya uthibiti wa nguvu za rais kikatiba na ikiwezekana kuziondoa kabisa lakini ukiwauliza je suala hilo liandane na adoption ya mfumo gani wa utawala baina ya parliamentary na presidential, na kwa hoja zipi, wengi swali hili wanajaribu sana kulikwepa;

Kimsingi naunga mkono hoja zako hapo juu kwamba bila ya uangalifu, tukilipa bunge madaraka kuliko Rais chini ya Katiba Mpya, tunaweza jikuta nchi inaendeshwa na bunge la ovyo kabisa, likiwa na mchanganyiko wa wendawazimu, illiterates, wachumia tumbo n.k;

Mwalimu huko nyuma alikuwa anaonya sana juu ya hili, hasa kwa kuzingatia kwamba alikuwa anahitaji wabunge wazuri ili aunde serikali yenye watu wenye uwezo, wachapa kazi, waadilifu na wazalendo; Kwa mfano, katika hotuba yake mwaka 1970 wakati wa uchaguzi mkuu, mwalimu Nyerere alinena haya:

"The Members of the Government are chosen, or rather the government is formed by the President; But the President chooses his Government from among the leaders you have nominated. Our Constitituion says that the people choose their members of parliament and the President selects the Ministers from among the MPs; If you select good leaders the President can select the government from among them; It is harder if the People you select are not suitable to be Ministers."

------

Binafsi nadhani laiti viongozi wote wangekuwa na umakini katika hili, leo tusingekuwa na mjadala kwamba mawaziri wasitokane na wabunge;

Mbali ya hili, Mwalimu pia alikuwa makini sana kutotumia madaraka yake vibaya, at least bila ya kushirikisha mihimili mingine, hasa bunge; Kwa mfano, katika uchaguzi wa mwaka 1970, Marehemu Paul Bomani alianguka katika kura za maoni kiti cha ubunge Mwanza Mjini; Pamoja na kuanguka kwake, Mwalimu bado akamteua kuwa Mbunge ili ampe uwaziri; Lakini kabla ya kufanya hayo, Nyerere alienda kwanza kutoa hotuba ndefu na makini sana katika kulizindua bunge halafu mle mle akatangaza kwamba anataka kufanya uamuzi wa kumteua Paul Bomani kuwa Mbunge ingawa ameanguka kura za maoni, na kuomba bunge limwelewe katika maamuzi yake kwani anamhitaji sana katika serikali yake; Siku chache baadae Bomani akateuliwa na akapewa uwaziri kwa malengo ya Mwalimu, hasa kusimamia masuala ambayo aliamini Bomani yupo more competent lakini pia kuhakikisha kwamba mkoa anaotoka Bomani unakuwa na mwakilishi mzuri bungeni na kwenye serikali;

Leo ndugu yangu Kimweri, ili uteuliwe kuwa Mbunge sidhani kama mchakato huo utapelekwa bungeni zaidi ya kujadiliwa kwenye vikao vya kahawa baina ya mamlaka ya uteuzi na wapambe; Vile vile unaweza kupewa na uwaziri hapo hapo, sasa whether unazo sifa au hauna sifa, au whether umesha apishwa kwanza kuwa Mbunge kwa mujibu wa kanuni au haujaapishwa,who cares, wewe tayari ni Mbunge na Waziri bwana...
 
Kichuguu nakubaliana na hoja zako hasa pale ulipoonyesha kwa namna tofauti nini maana ya kumpunguzia rais madaraka.

Mchambuzi, mimi nadhani kuwa unapoweka check and balance tayari umeshampunguzi rais madaraka, tofauti na wenye hofu check and balance haimfungi mikono lakini pia haimwachii ''afanye apendavyo''

Mchambuzi ametolea mfano wa taifa kama Marekani na matatizo iliyopitia hadi kuwa na kitu stable kama walicho nacho.
Nakubaliana nawe lakini pia niseme naishangaa sana India kwa utaratibu ilio nao.

Nadhani tunafahamu kuwa India ni big democracy in the world. Pamoja na ukubwa na matatizo yao, wao wameweza kutengeneza kitu chao ambacho dunia inakishangaa.

India iliwahi kukaa miezi 3 bila effective PM au Parliament. Narudia sana mfano huu maana nakumbuka Lowasa alipojiuzulu Rais aliita mkutano na kusema nchi imetikisika. Real! kwamba mtu mmoja kajiuzulu. Hapo niliingiwa sana na hofu nikijua kuwa kumbe nchi hii si uongozi ni viongozi. Ndipo wazo la India na Japan likawa linanijia kila mara.

Nadhani tufikirie zaidi kwa kuangalia kwingine na mazingira yetu. Marekani, Rais anateua mabalozi lakini hadi wathibitishwe na kamati ya bunge ya mambo ya nje. Ni kupitia hapo uteuzi unaweza kukubaliwa au kukataliwa.
Sisi tumefanya nafasi kama za ubalozi kuwa sehemu za kupunguzia machungu au kufaa rafiki. Si rais ana uwezo wa kuteua au kutengua?

Nadhani mnakumbuka hata DC mmoja ambaye amemaliza shule tu wala hajawahi kuwa kiranja.
Kwasababu tu rais ana uwezo basi akamteua. Sasa ukiangalia kwa makini rais amepewa nguvu sana lakini wanavyo zi-abuse nguvu hizo sidhani kuwa wakinyang'anywa wataathirika au kutakuwa na athari.

Kuna chuo kikuu kimoja kina mjumbe wa kuteuliwa na rais mwenye umri wa miaka yapata 75.
ushiriki wake umekuwa wa matatizo kutokana na umri. Bado rais amemwacha katika nafasi hiyo mwaka wa 10 sasa.

Nina hakika hawezi ku-deliver lakini basi tu yupo. Sasa tukiondoa nguvu ya rais kuteua watu wasioweza tutakuwa tunamyima nini kwasababu hata sasa hivi wapo na hakuna wanchofanya.
Kwanini wajumbe wa bodi kama za vyuo wasipatikane kwa utaratibu mwingine.

Lakini cha hatari zaidi ni pale rais anapokuwa na nguvu zaidi ya bunge. Rais anapokuwa na maamuzi yanayoathiri utendaji wa mahakama na rais anapokuwa na ubia na vyombo vya mihimili mingine ikiwemo fourth state.

Hatari ya kumlundikia mtu mmoja madaraka tumeshaona matokeo yake.
If we still keep our hope that at a certain point in time this may change, then we are playing a bad card.
If we still hope that the beautiful one will be born soon we're taking risks hence cost-benefit analysis is not in our favor.

There should be a fine trim of his power without compromising security and social fabric which bound us together yet allowing him/her to enjoy the executive power vested on him.
 
Kwa jinsi mjadala unavyoendelea, maoni ya wengi ni kwamba – kuna haja ya kudhibiti mamlaka ya Rais kupitia Bunge, badala ya kupokonya madaraka husika all together; Hii ni ishara kubwa kwamba tofauti na kipindi cha nyuma, watanzania wengi wanazidi kupoteza imani na taasisi ya Urais; Awali, niliuliza maswali kadhaa kama njia yaku – stimulate mjadala hasa kwamba je – sababu zilizopelekea Katiba ya nchi kumpa mamlaka husika Rais wa nchi, je leo, sababu hizi bado zipo relevant au zimepitwa na wakati? Wachache wamejadili swali hili, lakini mchango wa nguruvi3 katika hili ulikua ni mzuri sana;

Swali lingine likawa – je, sababu husika zilifanikiwa kutekeleza malengo yaliyowekwa au hazikufanikisha, na je kuna masuala ambayo tungependa kuya pursue kama awali hivyo kumwachia Rais madaraka kadhaa kama ilivyokuwa chini ya Mwalimu? Maoni ya wengi, hasa pia niki recall hoja za nguruvi3 katika hili ni kwamba this is a risky business na hatuna muda wa kufanya trial and error katika nyakazi hizi, we have important tasks to pursue and accomplish kama taifa; Kwa maoni haya, kilicho dhahiri hapa ni kwamba watanzania wamechoka, na hawana imani tena na taasisi ya Urais kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, hivyo wanahitaji mabadiliko, whether yawe ni ya kudhibiti madaraka ya rais kikatiba au kumpokonya, kikubwa ni kwamba taasisi hii ni muhimu ifanye kazi under scrutiny; Hii ni hoja ya msingi sana na hata mimi mtoa hoja niseme tu kwamba naiunga mkono;

Kabla ya kufunga pazia (at least for now) juu ya wapi tumetoka na maamuzi haya Kikatiba kama nchi ili tuhamie kwenye masuala mengine muhimu, ningependa niseme machache juu ya hili; Chini ya mfumo wa chama kimoja (TANU na baadae CCM), sababu ya msingi ya kuwa na chama kimoja cha siasa ilikuwa ni ku – institutionalize national unity based on a strong central government; Kwa mujibu wa hotuba ya Mwalimu Nyerere iliyochapishwa na gazeti la nationalist (1970), Mwalimu aliliweka suala hili namna hii:

["The Tanzanian system of one party democracy is designed to enable the people to elect a competent government which reflects their wishes and desires and to do so without damaging the society and the long – term objectives that they have set for themselves"].

Katika nukuu hapo juu, tunaona jinsi gani Mwalimu alikuwa anazingatia sana suala la competency katika wateule wake na kwa kweli he delivered viongozi wengi wenye uwezo, wenye uzalendo na uadilifu; Lakini katika nyakazi za leo, madhaifu katika hilo ni moja ya sababu kubwa na za msingi kwanini watanzania wanataka mabadiliko katika mamlaka hii ya Urais;
Mwalimu alifanya taasisi ya Urais kuwa the single most important office in Tanzania, na ndio maana uchaguzi wa Urais carried with it so much significance kwani Rais was not only the living symbol of our unity bali pia alikuwa ni kiungo muhimu baina ya Chama, Serikali na Wananchi; Kwa kifupi, the supreme powers of the President were used to consolidate the integrity of the state na pia at the same time to build a new nation within a framework of popular participation and national unity;

Kwa kumalizia section hii, tofauti na miaka ya nyuma, katika nyakazi hizi taasisi ya Urais imeonyesha incompetence katika utendaji wake lakini pia katika wateule wanaotokana na mamlaka hii; Pili, our country has not only lost its integrity but it longer has its own vision (Vision 2025 sio yetu bali ni based on Washington Consensus); Na tatu, mamlaka ya Urais imeyumba sana katika kujenga umoja na mshikamano, hasa katika mazingira ya hali ngumu ya maisha ambayo yamechangiwa sana na uwepo wa soko huria holela na azimio la Zanzibar ambayo yamezaa ufisadi wa kupindukia n.k; Katika mazingira haya, ni vigumu sana kuuza idea kwa wananchi kwamba tunahitaji mamlaka ya rais yaendelee kama yalivyo chini ka Katiba mpya kwa manufaa ya Taifa wakati in practice, manufaa hayo yamekuwa ni kwa wachache tu;

Pamoja na mapungufu haya, bado kuna umuhimu wa kuzingatia haja ya kuchagua zaidi katika kuthibiti baadhi ya mamlaka ya rais kikatiba kuliko kuyapunguza au kuyaondoa kabisa; Na ni katika muktadha huu ndio nimekuwa nauliza swali lakini sipati majibu kutoka kwa watu wengi sana kwamba – je, kiu yetu juu ya mabadiliko haya iendane na mfumo gani wa utawala chini ya Katiba mpya na kwa sababu gani – je, iwe ni Presidential form of government ambayo kwa kawaida huwa ni MORE STABLE BUT LESS ACCOUNTABLE? au parliamentary form of government kwa kawaida huwa ni MORE ACCOUNTABLE BUT LESS STABLE?

Ningependa kujadili kidogo juu ya mifumo hii miwili; tukianza na parliamentary form of governance, kanuni ya msingi hapa ni uthibiti wa bunge over the executive action (mhimili wa Urais); Katika hili, Serikali inakuwa obliged to reveal, explain and justify kwa bunge juu ya maamuzi yake yote – from teuzi mbalimbali katika nafasi za uongozi to development of public policies; Bunge linapata fursa to scrutinize shughuli zote muhimu za serikali hivyo kujiridhisha kwamba teuzi, public policies etc zinaenda sambamba na needs and aspirations za wananchi kwa mujibu wa katiba iliyotokana na wao, lakini pia uwepo wa effective implementation ya miradi ya serikali; Kwahiyo, chini ya mfumo huu – Katiba makes the executive accountable to bunge in all matters pertaining to law making, policy formulation and implementation, financial regulations etc;

Swali linalofuatia ni je – how do we balance between accountability and stability huku tukiwa na ufahamu kwamba presidential form of governance is MORE STABLE BUT LESS ACCOUNTABLE while parliamentary form of government is MORE ACCOUNTABLE BUT LESS STABLE?

Content and form of parliamentary control over the executive hutofautiana from country to country; Kwa mfano, kwa nchi ambayo ime adopt the theory of separation of powers kikamilifu kama USA, parliamentary control over the executive ni tofauti kabisa na nchi kama India kwa mfano, ambayo Baraza la mawaziri lipo accountable moja kwa moja kwa bunge; Katika mfumo wa Marekani, Mawaziri hawaitwi mbele ya bunge kujieleza kama ilivyokuwa chini ya mfumo wa kibunge, na pia bunge halina mamlaka ya kuwa dismiss mawaziri ambao wanalega lega katika utendaji wao; Lakini kwa India inayofuata parliamentary form of government ambapo mawaziri wapo accountable kwa bunge, their existence (mawaziri) hutokana na matakwa ya bunge kupitia vote of confidence or no confidence;

Under the Presidential form of government in the USA, the executive (Rais) is quite stable for the entire duration of which he/she is elected (miaka minne), and he is only answerable to the people (especially after every four years) not bunge; And he can't be removed from office for any wrong policies au anything done by him under his capacity kama Rais wa nchi; However, Rais can be impeached for his personal misconduct BUT not for formulating or implementing wrong or bad policies; Ni katika mazingira haya, presidential form of government ensures MORE STABILITY BUT IGNORES ACCOUNTABILITY OF THE EXECUTIVE KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI (WABUNGE); Pia chini ya presidential form of government, mawaziri sio wabunge, pia sometimes, the executive (Rais) can by-pass bunge, na huwa inaweza ikatokea kwamba the executive action isn't in-line with the desires and aspirations of the people (kwa mujibu wa katiba inayotokana na wananchi), lakini this problem is less intense (if not remote) chini ya parliamentary form of government;

Swali bado linabakia lile lile – how do we balance between STABILITY AND ACCOUNTABILITY?

Wengi pengine wanaweza kupendekeza kwamba tuwe na dual system ya kuchukua mazuri ya bunge na mazuri ya Rais; Kama alivyojadili awali mwenzetu bongolander, sisi tunafuata dual system, lakini mimi kwa mtazamo wangu ni zaidi ya hapo – hatujielewi kwani CCM kwa muda mrefu ilikuwa inafuata presidential form of government (kuanzia 1962) na baada ya mageuzi ya kiuchumi in mid 1980s, tuliendeleza mfumo huu kwa imani kwamba kubania mageuzi ya kisiasa ingeendelea kutuweka in control to determine the pace of democratization in the country in a top – down fashion; Tume ya Nyalali ikaja na mapendekezo ishirini na kitu kwamba kuna baadhi ya sheria na vifungu vya Katiba ni muhimu vifanyiwe marekebisho ili taifa liweze kuendeshwa na kukidhi mahitaji ya demokrasia ya uliberari inayofuata mfumo wa vyama vingi; Lakini CCM tukapiga dana dana mapendekezo mengi kwa justification kwamba kuingia kwa pupa katika mageuzi ya kisiasa kutaaribu hali ya Utulivu na Amani nchini;

Wengi tunabakai kujiuliza, kwanini mageuzi ya kiuchumi yalifanywa kwa kasi ya ajabu na baadae kushindiliwa kwa msumari wa Azimio la Zanzibar? Kati ya mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi, kipi kinatishia zaidi amani na utulivu nchini? Jibu ni mageuzi ya kiuchumi ingawa viongozi wengi wa CCM wasingependa kukubaliana na hoja hii;

Nikirudi kwenye hoja juu ya jinsi gani tunaweza ku balance between STABILITY & ACCOUNTABILITY, tutazame wenzetu wa Ufaransa wanafanyaje katika hili; Rais nchi Ufaransa hupita iwapo anapata zaidi ya 50% ya idadi ya kura zilizopigwa na hii ni kwa mujibu wa Katiba; Ikitokea mgombea urais hafikishi idadi hii ya kura, basi uchaguzi hurudiwa baina ya mshindi wa kwanza na wa pili, ndani ya siku saba; Vinginevyo for the next seven years, Rais is in office, hence Stability for seven years on part of the executive; However, Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, na zinahitajika two thirds ya kura za wabunge kufanikisha hilo; Ikitokea hivyo, Rais anavunja bunge na uchaguzi mkuu unaitishwa; Baada ya uchaguzi mkuu mpya, iwapo wabunge waliopita watampigia tena kura of no confidence kwa two thirds, basi Rais husika anaachia madaraka na kuondoka zake moja kwa moja;

Kwa ufupi, tumeona kwamba parliamentary form of government ensures STABILITY of the executive and consequently to the PEOPLE; Parliamentary form of government ensures greater STABILITY;

Kwa kumalizia, sio kwamba the inherent weakness of the parliamentary form of government ndio sababu kubwa kwanini mfumo wa Kibunge huwa ni ‘UNSTABLE'; Kuna sababu nyingi zinazochangia uwepo wa INSTABILITY, hasa katika mataifa machanga au yanayoendelea, kwa mfano absence of adequate electoral reforms, tendency or threats of factionalism and/or defections ndani ya vyama vikubwa vya Siasa n.k; Ili kuthibiti haya, huwa kuna umuhimu wa kufanya electoral reforms kwa mujibu wa Katiba ya nchi, lakini vile vile suala la defections katika vyama, zipo nchi zenye anti – defection laws ambapo kunakuwa na masharti jinsi gani wabunge can defect; Mbunge haujiamkii tu na kuamua kuhamia chama kingine ovyo ovyo;

cc EMT, nguruvi3, ogah, kichuguu, bongolander
 
Bongolander,

je, ni kwanini chini ya awamu ya Mwalimu Nyerere such powers tuliona zipo justified lakini sasahivi hatuoni umuhimu wake?


Swali linalofuata ni je, kwanini implementation ya economic reforms nayo haikufuata an incremental process (kidogo kidogo) kama mageuzi ya kisiasa na badala yake kiuchumi mambo yakawa implemented radically bila ya kujali madhara yake kwa wananchi?

Naomba nieleweke kwamba sitetei CCM au kupinga mabadiliko husika, bali najadili kwa maoni yangu tumefikaje hapa;

Mchambuzi kipindi kile absule powers kwa Nyerere ilikuwa tolerated kwa kuwa ilikuwa rahisi kumwamini mwalimu, hakuwa mwizi, hakuwahi kujilimilikisha benki au migodi, wala kutuuza watanzania. Mwalimu hakuwa mhuni alikuwa akitumia madaraka kwa ajili ya nchi si kwa ajili ya maslahi yake binafsi. Japokuwa kuna wakati alionekana kutojua what is right for Tanzania and Tanzanians, lakini alifanya anachoamini kuwa ni sahihi. Kwa sasa hoja hiyo ina utata inategemea kudra za mungu kumpata mtu mkweli, kwa hiyo ni bora kubank kwenye katiba kwa sheria zinazomdhibiti, rais kuliko kuchamtuwe na Rais mungu mtu ambaye anaweza kuchezea madaraka kama anavyopenda.


Mchambuzi nadhani unaweza kukumbuka kuwa bila Nyerere kusema Tanzania ifuate mfumo wa vyama vingi, huenda Tanzania ingechelewa kuingia kwenye siasa za vyama vingi, labda tungeingia kwa mitulinga kama walivyofanya Kenya. Kimsingi CCM ilikuwa na mazingira ya kukataa vyama vingi kwa msingi wa matokeo ya kura za maoni. lakini labda tungebanwa na benki ya dunia. Lakini ukumbuke kuwa (na hili wengi hadi leo hawataki kujua) CCM ina wenyewe, wenye ni wachahce wanaonufaika na nchi, ukianza kuangalia utasikia babu alikuwa fulani, baba alikuwa fulani, na mtoto sasa ni fulani, wanaendelea walewale....mfano mzuri ni kina Nape, Nchimbi, Mwinyi, Msuya etc etc.

Ilikuwa ni rahisi kuliberalize uchumi ili waangalie wapi kumeiva, ili watumie nguvu ya kisiasa kuingia huko. Ndio maana ukiangalia mpaka leo utaona mkurugenzi wa bodi fulani ni wale wale waliokuwepo wakati wa mageuzi, na mpaka sasa mwekezaji mgeni akija angalia ajira zinavyotolewa, zinazunguka kwanza kwa wale wale wenye madaraka ya kisiasa, zile mbaya mbaya ndio zinaenda kwa wasio wenyewe.

They believed that and they still want to show that singular politics can work in plural economy. lakini tumeona kuwa hata sasa tunahitaji plural politics za kweli iliziendane na hali ya sasa ya uchumi. Kivitendo Tanzania bado ni nchi ya chama kimoja, kwa kuwa bado opposition kazi yao ni kupiga kelele tu, hawana meno. Wangekuwa na meno labda issue ya EPA, Richmond etc zingekuwa zimetatuliwa kihalisi.

Kwa hiyo mchambuzi sio kuwa tumefika hapa kwa bahati mbaya. Tumefika hapa kwa makusudi, walitufikisha hapa sio kuwa wamefanya bahati mbaya. Ni makusidi.

Jaribu kusikiliza hotuba za Mkapa alizotoa baada ya kupewa ripoti za tume. utaona wazi kuwa maslahi ya wanaCCM wa juu yalizingatiwa zaidi kuliko ya nchi au ya chama.
 
EMT,

Katika haya, nina masuala mawili - matatu ningependa kuyajadili; Kwanza, kwa mtazamo wangu, kuna utofauti baina ya taifa jipya na taifa changa; Iwapo utakubali nikuelekeze zaidi katika dhana ya uchanga kuliko upya, unatumia criteria ipi au zipi to gauge or to determine uchanga wa taifa - umri? Kama ni umri wa taifa, ni miaka mingapi?

Kwanza kabisa kwenye hiyo nukuu, Nyrere alikuwa ana refer taifa jipya au taifa changa? Kwenye thread yake ya "Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa Changa ni Vitu Viwili Tofauti" Raia Fulani anasema kuwa bado hajajua "kwa usahihi mpaka wa uchanga wa umri wa Taifa lolote ni miaka mingapi, ila [aki]ikiitazama Tanzania bado [a]naona miaka 50 bado taifa hili ni changa." Source: https://www.jamiiforums.com/great-t...-kwa-taifa-changa-ni-vitu-viwili-tofauti.html

Kwa maana hiyo, sidhani kama alikuwa pia ana maanisha kuwa Tanzania bado ni taifa jipya. Kwa mfano, sidhani kama unaweza kulinganisha South Sudan na Tanzania kwa kusema zote ni nchi mpya.

Lakini tukija kwenye suala la uchanga wa taifa, Tanzania/Tanganyika, kwa mfano, ina umri wa miaka 50 ambao ni mkubwa zaidi ya Rwanda, Kenya, Singapore, Yemen, Jamhuri ya Czech na South Sudan. Bado Taifa lenye umri wa miaka 50 tunaweza kusema ni changa?

Ukipitapita kwenye korido za majumba ya kisiasa unawasikia wanasiasa wakisema kuwa taifa letu bado ni changa. Lakini wapo watu wanaona dhana ya uchanga kama ni kisingizio cha viongozi kushindwa kueleza ni kwa nini bado tuko hapa tulipo. Kusema kuwa Tanzania ni taifa changa kunaweza kuchukuliwa na wengine kama kisingizio cha kuhalalisha umasikini wa taifa.

Kuna nchi luluki ambazo tulipata nazo uhuru wakati mmoja lakini leo nchi hizi ziko mbali kimaendeleo. Pia kuna nchi tulikuwa nazo sawa kiuchumi wakati tunapata uhuru lakini leo ziko mbali. Je, maendeleo ni criteria yak u-determine uchanga wa taifa? Kwamba taifa ilikendelea zaidi linakuwa siyo changa tena?

Hili suala la Tanzania kuitwa taifa changa limeshajadiliwa wakati huyu huyu Balozi Sefue alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Jaribu kupitia michango ya wachangiaji kwenye hii link uone jinsi wachangiaji walivyotaharuki kwa Tanzania kuitwa taifa changa: MICHUZI: PONGEZI ZA WANANEW YORK KWA MHE. BALOZI OMBENI SEFUE

Kwenye hiyo link kuna mchangiaji mmoja amejaribu kutetea uchanga wa Tanzania kwa kutumia vigezo kuwa bado Tanzania ni maskini, elimu bado ipo chini, hakuna usawa wa jinsia, kuna vifo vingi vya wachanga na akina mama, kuna ukimwi, kutokuwepo na ustawi wa mazingira na kutegemea misaada ya wafadhili.

Fadhy Mtanga, kwenye article yake "Miaka 50 taifa haliwezi kuwa changa"ambapo anasema "Ukijaribu kutazama kwa makini, utaona kuwa sehemu kubwa sana ya mataifa ya ulimwengu huu yamepata uhuru wake katika karne ya 20, sisi tukiwa mmojawao. Na katika mataifa hayo, sehemu yake kubwa yamepata uhuru katika nusu ya pili ya karne hiyo, ama tuseme baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Lakini sisi ni masikini zaidi pamoja na fursa nyingi nyingi tulizo nazo.

Wenzetu bado wanajiita wachanga? La hasha! Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Tanzania ni taifa changa. Nirekebishe kauli, sitokuwa mtu wa mwisho, bali sitoamini kamwe, kuwa taifa letu ni taifa changa.

Kwa kisingizio hiki cha uchanga kama namna bora ya kuhalalisha umasikini wetu bandia (ni umasikini bandia kwa kuwa tuna utajiri wa rasilimali), hata baada ya miaka 100, 150, 200 na kadhalika, bado watu watasema ni taifa changa." Source: mwananchi mimi!: Miaka 50 taifa haliwezi kuwa changa

Pili unaposema kwamba demokrasia yetu bado changa, una maanisha demokrasia ya aina gani na unaipimaje? Umri? Kama ni umri wa demokrasia, ni miaka mingapi?

Kwenye thread yake, Raia Fulani anaendelea kusema kuwa "Demokrasia yetu hadi sasa ipo katika nadharia tu hasa tukitilia maanani yale yanayotokea sasa na yaliyotangulia. Tangu kuanza kwa Taifa hili chini ya Uhuru toka wakoloni, pamekuwa hapana demokrasia ya uwazi kiasi cha kutosha kusema kuwa jambo hili linafanyiwa kazi kivitendo. Azimio la Arusha halikuwa na mrengo wa demokrasia japo lengo lilikuwa jema. Singependa kurudi sana huko awali. Mivutano ya leo katika siasa zetu ni picha ya wazi ya kukosekana hiyo demokrasia-utawala wa Raia na uhuru wa maoni, uhuru wa kuamini dini na itikadi pasina kuvunja sheria za nchi. Matokeo yake tunashuhudia mivutano, mitafaruku, mikandamizo, vitisho, na mauaji. Siasa ndio mwongozo wa taratibu za nchi. Siasa ndio maisha ya kila siku. Katika Demokrasia tumeshindwa."

Pia katika kitabu chake, "Uongozi wetu na hatma ya Tanzania" Mwalimu Nyerere aliandika "Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake".

Lakini ukiongalia leo, pamoja na kuanzishwa kwa vyama vingi, bado ubovu wa viongozi ndani ya CCM upo pale pale. Wapo waliotumaini kuwa mfumo wa vyama vingi ungeondoa CCM madarakani au ungeilazimisha CCM kujisafisha uongozi wake. Lakini ukiangalia sivyo kama Nyerere na wengine walivyotarajia. Pamoja na kuwepo kwa vyama vingi, bado watu wengi wanaamini kuwa hali ya uongozi ndani ya CCM haijabadilika na vyama vya upinzania bado havina nguvu ya kuindoa CCM madarakani.

Hapa ndipo linapokuja suala zima la maana ya demokrasia. Watu wengi wanadhani kuwa demokrasia ni kuwa na mfumo wa vyama vingi, kuwa na free and fair election kila baada ya miaka fulani, kuweka kikomo cha mtu kuwa rais, n.k. Ndiyo maana ukipita kule kwenye jukwaa la siasa utakuta watu wengi wanaongelea zaidi siasa za vyama, kugombea urais, uchaguzi mwaka 2015, n,k. Wengi wao hiyo ndiyo demokrasia.

Lakini values za demokrasia ni zaidi ya vyama vingi, periodic elections, urais, n.k. Demokrasia yetu ni changa kwa maana kuwa it is still in its very infancy stage. Bado sana. Ndiyo maana hata watawala wetu wanapinga sana watu wa kusini ku-exercise their right to internal self-determination in the exploitation of their natural resources. The right to internal self-determination is part and parcel of democracy.

Suala la tatu ambalo ningependa kulijadili kidogo lakini zaidi pia kwa mtindo wa Swali kwako ni kwamba - Ukichukulia Tanzania na Somalia, how would you describe these two kama mataifa in terms of upya, uchanga, or anything in these lines... Bear in mind kwamba Somalia ceased to be a British protectorate earlier than Tanganyika i.e. Somalia (1960) na Tanganyika a year later (1961);

Maelezo yangu hapo juu kuhusu uchanga yatakuwa yamejibu hili. Siamini kama Tanzania na Somalia ni nchi changa au mpya.

Naomba nimalizie kwa swali lingine kwako:

Kwa mtazamo wako, in the context of all the above, tufuate mfumo gani chini ya katiba mpya na kwanini - presidential form of government au parliamentary form of government?

Tukifuata parliamentary system, nafasi ya rais itabidi iwe ceremonial. Waziri Mkuu ndiye atakayekuwa mkuu wa serikali huku Rais akiwa mkuu wa nchi tuu. Maamuzi yote yakiwemo yale ya kuteua mawaziri itabidi yafanywe na Waziri Mkuu ambaye pia anakuwa responsible kwa bunge.

Uzuri wa parliamentary system ni kwamba unaweza kupitisha sheria kwa haraka na kwa urahisi zaidi. Chama ambacho kina majority ya wabunge kitakuwa kinapitisha miswada kwa kuwa na kura nyingi. Faida nyingine ni kuwa chama ambacho kitakuwa na majority bungeni ndicho kitakachounda serikali. Kwa hiyo, the will of the people inaweza kuwa instituted more into parliamentary system. Uzuri mwingine wa parliamentary system against presidential system ni kwamba, watu watakuwa wanakipigia kuwa chama badala ya mtu.

Hasara ya parliamentary system ni kuwa mkuu wa nchi aka rais hachaguliwi moja kwa moja na wapiga kura. Tatizo lingine, hakuna body nyingine inayoweza kuli-challenge bunge. Nakumbuka Uingereza wamejaribu kufanya reform kwenye House of Lords (tena reform nzuri tuu na zenye mantiki) lakini serikali ya zamani ya Labour na sasa ya Conservative na Liberal Democrats wameshindwa kabisa maana kila wakipeleka mswada bungeni unatupiliwa mbali. Matokeo yake, serikali imeamua ku-abandon kabisa the reform of the House of Lords: David Cameron retreats on House of Lords reform - Telegraph

Kwenye parliamentary system unaweza kuwa na strong prime minister kama ilivyo Uingereza na Japani, lakini kuna nchi nyingine ambazo parliamentary system imekuwa unstable. Mfano, mzuri ni matokeo ya uchaguzi uliofanyika Israel juzi. Kwa nchini kama Italia, Ujerumani, na Canada, sometimes parliamentary system imefanya serikali ishindwe kupitisha hata mambo ya msingi kabisa kutokana na kutokuwa na majority bungeni (coalition governments).

Lakini nadhani ili uwe na an effective parliamentary system hasa kwa nchi kama Tanzania inabidi uwe na wabunge imara na wenye msimamo dhabiti na siyo wabunge wanaofuata upepo. Hii ni kwa sababu bunge ndilo litakalokuwa linatoa maamuzi mazito mengi ya mustakabadhi ya nchi. Waziri Mkuu hatakuwa na prerogative powers kama anazokuwa nazo Rais kwenye presidential system. Badala lake atakuwa analitegemea bunge kufanya maamuzi.

Je, tayari tunao wabunge imara kwenye bunge ambao tunaweza kuwa-trust kabisa na kuwakabidhi mustakabadhi wa maamuzi makubwa ya nchi au yatakuwa yale yale ya kuhamishia tatizo kutoka institution moja kwenda nyingine bila kuangalia effectiveness ya institution yenyewe?
 
Kwanza niseme wazi kuwa binafsi siamini hata kidogo katika Demokrasia, maana nina uhakika kuwa haina inachosadifu kwetu, si fikra zetu, mazingira yetu, wala chochote chetu, ni UBATILI TU! Hivyo, siungi mkono mchakato wowote ule unaofanywa kwa vigezo vya kutekeleza Demokrasia! Maana hilo ndilo KABURI letu watoto wa Afrika! Huwa mara nyingi nasema, ukishakubali demokrasia basi huna budi kufungwa na kanuni na taratibu za demokrasia.

Kanuni hizo ndizo zinazojaza Wabunge wenye kusutana bungeni, wabunge wanaongozwa na mahaba ya vyama vyao kwenye maswala nyeti ya taifa, mawazili wenye kujaza nafasi tu pasi kuwa na fikra zozote endelevu, maraisi wenye kusujudu wezi wetu na kuwaangukia wanyonyaji, kwamaana huchaguliwa kwa umaarufu wao si ufanisi wao, wapo wachungaji, wanamuziki, wafanyabiashara, wanajeshi, ili mradi tu aliweza kuteka hisia za watu kwa umaarufu wake! Wengine wanalazimika kugawa kanga na kofia na watu wanawachagua wanaenda bungeni, wizarani, ama ikulu. Bado tunaimba wimbo wa Demokrasia kwa Maendeleo! Ni KUJIDANGANYA hilo halipo kwetu!

POWER IN THE RIGHT HANDS.... Ni namna bora ya kusimamia maendeleo kulingana na Mazingira yetu na Nyakati zetu(FIKRA). Tutapataje right hands...ni kwa KUANDAA VIONGOZI WETU! Ni viongozi ni watu, na watu ndio sisi! Kumbe jamii kwa ujumla inapaswa kuandaliwa kuzalisha viongozi bora watakaoaminiwa! Tunaposema waandaliwe, inamaanisha "the whole system of life" inapaswa kumjenga mwanajamii kule kunakofaa. Hapo sasa ni janga, maana watanzania tumezoea sana kuhangaika na matawi na kuacha mizizi ya tatizo, lakini ukweli ni kwamba mfumo mzima wa maisha unapaswa kumjenga raia kuwa kiongozi na raia bora, huwa hatuwezi kutoka nje ya upatikanaji wa ITIKADI KUU YA TAIFA LETU! Hakika kabisa, hakuna suluhisho lolote lile la unyonge wetu kama hatujazingatia Itikadi ya Taifa! (Sijawahi kuwa na wimbo tofauti na huu katika ukombozi wa mtu mweusi, mtaniwia radhi kama mmeuchoka maana unakera) Huwa naamini kuwa, "MAISHA NI FALSAFA KABLA YA CHOCHOTE KILE"

Demokrasia ndio iliyofanya watu wahangaikie kuunda serikali badala ya kujenga nchi, maana ndiyo iwapayo nafasi wabomoa nchi kuvaa kanzu ya wajenga nchi na wakaingia nayo harusini. Tutawashangaaje leo?

Bado hatujatambua UZITO wa HULKA ZA BINADAMU, ndio kikwazo kikubwa! Lakini ni lazima tutambue Umimi/Ubinafsi unao-shape HULKA zetu, una nguvu kubwa sana kamwe haiwezekani kuuzuia kwa njia ya demokrasia. TUSIDANGANYIKE na wapuuzi wa magharibi, hakika wanaweza kuelewana kidemokrasia kwa kuwa sisi wanyonge tupo. Laiti kama tungeweza kuificha Afrika japo kwa miaka 5 tu, tungeona ubinafsi wao unavyowakiana wenyewe kwa wenyewe na kama hiyo demokrasia ingesimama tena, NEVER. Wasitudanganye kuwa wao wanapatana kidemokrasia, ni kwa sababu sisi tupo. Sasa sisi hatuna wa kummalizia HULKA zetu, tunawakiana wenyewe kwa wenyewe, na huko ndio KUANGAMIA KWETU!

Demokrasia isitumike kama kigezo cha kuhalalisha ama kuhalamisha chochote kile, tutazame mazingira yetu, watu na fikra zetu na kupima nini kinatustahili. Na hiyo ndio MANTIKI.

Mungu wetu anaita sasa.

D
 
Kuna baadhi ya maamuzi kwa kweli ni muhimu yafanywe kwa haraka na Rais, na hayana haja ya kusubiria vikao vya bunge; Vinginevyo bunge ni muhimu pia kushirikishwa na hili linaweza kufanyika kupitia kupitia kamati husika za bunge ambazo zinaweza kushauri the executive branch juu ya maamuzi Fulani kasha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi husika kwa haraka; Bottom line ni kwamba - kuna baadhi ya maeneo ambayo ni muhimu yapunguzwe, lakini mengine ni muhimu yaachwe kama yalivyo LAKINI yadhibitiwe kikamilifu chini ya Katiba Mpya, hasa kwa kulipa bunge uwanja mkubwa zaidi katika maamuzi na uongozi wa nchi;

Labda nitokezee hapa, japo sijasoma maoni ya wadau wote humu ila nimeona nihoji kitu hapa kabla sijaendelea zaidi.

Kwenye post hii ambayo ulikuwa unamjibu Nguruvi3.
Mchambuzi, mi nilidhani "kumpunguzia nguvu" Rais kutaendana na decentralization katika maamuzi mengi.
Labda siwezi kupata picha kamili ya mfano wa maamuzi yanayotaka uharaka unayoyazungumzia hapo.

Ila nadhani kama taifa kama tutafikia kupunguza nguvu za rais (kama wengi wanavyotamani na mimi nikiwa mmoja wao) bila kufikiria kwa pande zote mianya inayoweza kutokea kwa matukio mbalimbali ya kimaamuzi, basi tutakuwa taifa la wajinga hasa na wapuuzi wa hali ya juu.

Naamini mapendekezo ya kupunguza nguvu lazima yaende sambamba na uundaji wa vyombo, mamlaka na taasisi mbalimbali kuziba ombwe hilo, bila kusahau kanuni mbalimbali au kama ni bunge maana yake halitakuwa bunge hili tena tulilolizoea.

Pia kama tukiwa kweli tunalenga kujenga taifa linalotegemea mifumo yake badala ya watu fulani katika taasisi fulani basi hamna namna ya kukwepa kujifunza kwa mifano wenzetu fulani wamewezaje kwenye jambo fulani ilihali Rais wao akiwa katika namna ya mamlaka yasiyompa ufalme na utukufu....

Mi ninachoona kwenye hoja imezungukwa na uoga wa watu fulani kwenye nchi ambao mara zote wamekuwa wakituona wananchi na matakwa yetu kama bado hatujafikia kiwango cha kujiamulia,
Kundi hili ndio limekuwa na ushawishi kwa watawala wetu, ni kundi kama hili ndio hata kwenye uchaguzi mkuu mara zote wamekuwa wakitoa miongozo kwa tume zetu kuwa mshindi wa urais atangazwe nani (rejea ushahidi wa mazingira kwa uchaguzi wa mwaka 2010 kwa Slaa na chaguzi zote za Zanzibar kwa Maalim Seif).....


Hivyo hoja hii inataka kupelekwa kupotosha ili kuleta sura ya uasi au kupotoka au kwamba taifa litaangamia, na hii inafanywa makusudi kwa ku-overlook masuala ya msingi kabisa kuwa kuongoza ni team na sio suala la mtu mmoja hata awe na nguvu kiasi gani, pia wana overlook suala la mifano na kujifunza kutoka kwa wenzetu wengine!

Kwenye bold red, sina maana ya kuhamisha mjadala ila tu najaribu kuonyesha nguvu ya nyuma ya watawala katika kuamini mara zote kuwa wao wana uwezo wa kuwafikiria wananchi wengine
 
Last edited by a moderator:
EMT,

Nianze na suala la uchanga wa taifa; Bandiko hili linalenga zaidi kuchokoza mada based on mjadala wako kwenye bandiko namba 73;

Nikianza na suala la uchanga wa taifa, hoja zangu katika hili zinatokana zaidi na kutatizwa kwangu na tabia ya watanzania wengi kuchanganya dhana mbili kama vile ni kitu kimoja – dhana ya ‘state' and ‘government'; Nilijadili dhana hizi kwa undani kwenye uzi mwingine ufuatao https://www.jamiiforums.com/great-t...wa-rais-kikwete-mjadala-wa-nadharia-tete.html

Tukirudi kwenye mada husika, iwapo tutakuwa tutaangalia Tanzania kama nchi iliyokuwa chini ya ‘Sovereign GOVERNMENT' for the past 52 years, then hoja kwamba Tanzania sio Taifa Changa, ni hoja yenye mashiko; Lakini tukiamua kujadili Tanzania ‘As a STATE', mtazamo wangu ni kwamba we are still very young; Mifano ya Kenya, Rwanda n.k, hasa juu ya jinsi gani wamepiga hatua katika kipindi cha miaka 50 bado hakibadili ukweli kwamba as states, nchi hizi bado zipo very vulnerable and things may reverse at any time - hakuna guarantee of sustenance; Kenya, Rwanda, Tanzania, zote ni problematic states, one step away from being failed states; Suala la Tanzania being a problematic state pia nilishajadili kwa kirefu katika uzi mwingine huko nyuma;

Nikirejea sehemu ya mjadala wangu huo nilisema kwamba - Kwa upande mmoja – A Government (Serikali) ni taasisi ambayo jukumu lake kubwa ni kutunga na kutekeleza sheria na sera mbalimbali ndani ya jamii husika; Muhimu pia ni kwamba taasisi hii ina nguvu na mamlaka ya kutawala eneo husika la kijiografia pamoja na wakazi wanaoishi eneo hilo; Mamlaka na nguvu hii imegawanyika katika maeneo makuu matatu:

Legislative (Bunge) – nguvu ya kutunga sheria na sera mbalimbali;
Executive – nguvu ya kurututisha utiifu wa sheria (enforce law);
Judiciary (Mahakama) – nguvu ya kufafanua au kuanisha Sheria mbali mbali ili kuongoza shughuli za kila siku katika uendeshaji wa serikali - kisiasa, kiuchumi na kijamii;

Kwa upande mwingine, nilijadili kwamba maana ya ‘State' ni ‘a geographic entity' ambayo ina fiscal system yake mahususi, ina Katiba Yake na Soveregnity (freedom from external control);

Katika haya mawili (state vis a vis government), we certainly have an aged government but the story is different when it comes to Tanzania as a state;

Ili nieleweke vizuri zaidi natokea wapi na wasiwasi wangu kuhusu hoja kwamba Tanzania sio Taifa changa, pengine niulize swali lifuatalo: Je, kwa miaka 52 iliyopita (tangia uhuru wa kisiasa), Tanzania imekuwa ikifanya kitu gani kinachofanania na State Building? Kwani bila ya uangalifu, tutaendelea kupuuza juu ya umuhimu wa kurudia juhudi za state building, hasa strengthening of formal and civic institutions za kuendesha maisha ya kisiasa, kijamii na kiuchunmi; Hivi sasa, informal and community based institutions ndio zinaendesha nchi, huku formal and civic institutions zilizopo zikitumika tu kama rubber stamps; Iwapo kuna mtu anaweza ku-point kwamba tumekuwa katika harakati za state building kwa mifano hai, basi hivyo ndivyo tutaweza kupata hoja zenye mashiko kwamba sisi sio wachanga kwani when it comes to this and that, we have mileage;

Vinginevyo naendelea kuamini kwamba we have hardy done much to build Tanzania as a State, instead, we have been busy forming new governments for the past 50 years; State building efforts zilifanyika katika kipindi kidogo sana na zikafa (1967 – early 1980s); it is in this light that I am strongly convinced kwamba as a STATE, Tanzania bado ni wachanga sana (not necessarily experience in forming governments for political leadership and administration purposes)';

The following table might help nieleweke zaidi:

MwakaMain FeatureMain Objective
1961 – 1966Party State (TANU)To establish order
1967 – 1985Developmental State (TANU/CCM)Progress
1985 – PresentContracting StateControl

Kufuatana na the table above, - baada ya uhuru, the ultimate objective ya mwalimu na TANU was to create and sustain a new order; Ingawa Mwalimu was optimistic about the future, he had no experience of exercising power; He was anxious to secure his own position at the helm of the "inherited colonial state', thus the rise of TANU (later CCM) as the Party State;

In 1967 throughout 1985, Mwalimu's objective shifted from ORDER to DEVELOPMENT; he (and TANU) realized that he had to show wananchi that he and TANU) had abilities to develop the country; it is in this context that Nyerere developed an interest in grabbing control of the State for the purpose of guiding progress – kwahiyo hapa the party state was replaced by the Developmental State;

From 1985 to the present – hapa we see the World Bank and IMF taking over; Serikali imeondolewa katika suala zima la State building, na suala hilo kuachia nguvu za soko, huku serikali ikifanya facilitation and to a smaller extent, regulation; The bottom line ni kwamba throughout this period, our government have become increasingly dependent on policy advice and funding for economic reforms from external sources;

Ukitazama kwa ukaribu vipindi hivi vitatu, as a STATE, Tanzania is still in its infancy stage kwani katika miaka 52 ya uhuru, ni kwa miaka 18 tu (1967 – 1985) ambapo we had home grown policies and vision; For the remainder of the period, some other forces have been in control;

Kwahiyo hoja zangu za msingi juu ya kwanini sikubali moja kwa moja kwamba sisi sio wachanga kama Taifa ni based on arguments kuu mbili hapo juu – kwanza ni dhana ya problematic state, pili ni mjadala wangu kuhusu evolution yetu kama Taifa kutokea party state – to developmental state to contracting state; Na hoja nyingine ya kuongezea hapa ni kwamba – bado tunaishi under the first generation of leaders, and I believe kwamba it is also an important variable or unit of analysis katika kubaini uchanga au ukomavu wetu kama Taifa;

Hoja zako kuhusu parliamentary form of government vis a vis presidential form of government nakubaliana nazo kimsingi, ila nina machache ya kuchangia nikipata muda baadae;


Cc: JingalaFalsafa, Nguruvi3, Raia Fulani, jouneGwalu, Bongolander, Kichuguu, Ogah, Mkandara, Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa,

Asante sana kwa mchango wako bandiko namba 74; Kimsingi, kama nimekuelewa, uachojaribu kujadili ni jinsi gani collapse of our democracy is imminent; Kama ni po sahihi, basi naunga mkono hoja; Ni masuala kama haya ndio yananifanya niamini kwamba Tanzania as a STATE bado ni changa sana kama nilivyojadili elsewhere; Likelihood ya democracy to collapse huchangiwa na inequality, poverty, ethnic and religious polarization and fragmentation, etc, na yote haya yapo Tanzania kwa vile we never finished our State Building Project (hence uchanga wetu kama taifa);

Wajibu wa State Building ulikuwa ni wa CCM, lakini badala ya kuendeleza juhudi za STATE Building and Consolidation alizoanzisha Mwalimu, CCM imejikuta ikijikita zaidi katika kushinda chaguzi ili kukamata dola na kuunda serikali ambayo literally imekuwa ikiendesha a problematic state; Na situation after 1985 ambayo ilipelekea a shift from developmental state to contracting state (rejea mjadala wangu bandiko namba), ndio imekuwa ni beleshi la kuichimbia CCM kaburi lake; Kwa sasa CCM ipo in a catch - 22 situation - LACKING LEGITIMACY, IT CANT BE EFFECTIVE; LACKING EFFECTIVENESS, IT CANT DEVELOP LEGITIMACY;

Lakini pamoja na yote haya, CCM survives kwa sababu - katika demokrasia zilizokomaa, wapiga kura evaluate utendaji wa vyama vilivyopo madarakani mainly kwa kigezo cha economic outcomes; Lakini katika demokrasia na Taifa Changa kama Tanzania, wanasiasa wanatafuta kuungwa mkono by exploiting nationalism and unity, exaggerating internal threats kwa umma kutokana na uwoga wa CCM kwa upinzani mkali wa Chadema, matumizi ya nguvu ya dola kuthibiti uprising (kinyume cha katiba), na pia manipulating media; Ploys kama hizi kwa kiasi kikubwa zinafanikiwa kwani wapiga kura walio wengi Tanzania kwanza ni - they are inexperienced na pili, ni - they are unsophisticated;Tatizo lililopo ni kwamba watanzania wameweka matumaini yao yote katika Katiba mpya kama vile huo ndio mwarobaini;
Wanajidanganya kwani thats only the half, the other half ni kwamba (i quote Dr. Ambedkar on this one:

"However a good constitution may be, it is sure to turn out bad because those who called to work on it happen to be a bad lot; However a bad constitution may be, it may turn out to be good if those who are called to work on it happen to be a good lot; The working of the constitution does not depend wholly on the nature of the constitution; The constitution can provide only the organs of the State such as the Legislature, the Executive and the Judiciary. The factors on which the working for these organs of the State depend are the people and the political parties."

Nakubaliana na hoja ya Dr. Ambedkar, na ndio maana katika mijadala mingi nimekuwa nikihimiza juu ya umuhimu wa kuhakikisha kwamba electoral reforms zinaenda sambamba na political party reforms huku masuala muhimu ya kuhakikisha kwamba Katiba za vyama vya Siasa zinakuwa harmonised na sheria za nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi, yanazingatiwa;

cc:
jouneGwalu, Bongolander, Kichuguu, Ogah, EMT, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Nami ninapotazama hili suala kwa namna yangu naona wazi kuwa hakuna upande ambao utasimama sahihi aidha Rais akipunguziwa madaraka ama akiongezewa madaraka. Viongozi huongoza watu. Watu wana mitazamo tofauti. Nipendacho mi tofaiti na upendacho wewe. Maridhiano (consensus) huja baada ya upande mmoja kukubali kupoteza haja fulani. Nimewahi kusoma sehemu kuwa ''Democracy and Development are mutually exclusive''. You cannot exercise both at the same time. Either you cannot reach a consensus. Likewise these two variables are not infinite. It reaches a time they confluence. That time is when the State is mature enough as far as the meaning of a state is concerned.

Madaraka ya rais yawe wakati gani? Serikali iko ndani ya Taifa. Ukomavu wa taifa na ukomavu wa serikali vinapimwaje? Kwa upande wa Tanzania, serikali na Taifa vilianza wakati mmoja, yaani mara tu baada ya uhuru. Kwa mujibu wa ufafanuzi huko juu tunaambiwa kuwa taifa letu ni changa lakini serikali ina umri wa kutosha. katika mpishano huu tunawezaje kujadili madaraka ya Rais anayeongoza serikali iliyo na umri kuliko taifa analoliongoza? Au umri wa serikali huanzia pale Rais mpya anapoingia madarakani? Uhuru (demokrasia) ukizidi maendeleo huwa yanachelewa. Kadhalika kuna mambo mengi ambayo tunaweza kudhani kuwa yamo katika kundi la demokrasia halafu ukifika wakati serikali chini ya madaraka ya Rais ikaamua kufanya jambo (mathalani kujenga miundombinu, kutenga hifadhi za Taifa, kuhamisha/kuvuna rasilimali, n.k) na wananchi wakagoma kisha nguvu ya Dola ikatumika kutekeleza madaraka ya Rais, kuna mambo ya kujiuliza. Hao wanaobugudhiwa kupisha maendeleo wako katika maeneo hayo kihalali au kimakosa? Kama wako kihalali, serikali imechukua hatua gani kuona maridhiano (consensus) yanafikiwa? kama hawako kihalali, wako hapo kwa muda gani? Ilikuwaje wakawa hapo? Mipango miji na vijiji ilishaainisha maeneo ya makazi na maeneo kwa ajili ya maendeleo?

Rais anaongoza watu katika Taifa. Watu ndio walioamua fulani ndio awe kiongozi wa Taifa letu kwa niaba yetu. Sote tusingeweza kuongoza. katika kufanya kazi ya Rais kuwa rahisi, Rais anateua wasaidizi wake. Hapa ndipo matatizo huanza. Katika Taifa letu mfano mzuri na ulio wazi ni utendaji wa usalama wa Taifa. Tnashuhudia kila wakati wapinzani wakilalamika kwa usalama wa taifa unatumika kuhujumu upinzani. Kwa maana nyingine mfumo uliopo unaruhusu uwt kutumika na kundi fulani katika jamii. Mkuu wa uwt anateuliwa na Rais. Mkuu wa majeshi anateuliwa na Rais. Mkuu wa jeshi la polisi anateuliwa na Rais. Rais wa nchi ndiye mwenyekiti wa chama. Hawa wateule watamwambia nini Rais cha kumpinga?

Na inakuwaje pale ambapo Rais yuko madarakani kimabavu kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika? Matatizo huongezeka zaidi. Tayari tulishashauriwa kuwa Afrika haihitaji strong men bali strong Institutions. Hii ina maana kupunguza nguvu na madaraka ya Rais! Tuna Bunge ambalo ni tofauti na Serikali na Mahakama. Tunachoshuhudia ni kwamba wabunge wanaamua kupinga muswada fulani ambao umependekezwa na serikali iliyopo madarakani. Wengi wa wabunge wako chama tawala. serikali ambayo watendaji wake wakuu ni wanachama wa chama tawala na ni wateule wa Rais (madaraka ya rais) inaamua kuwaita wabunge wake pembeni na kuwaonya juu ya kupinga kwao jambo fulani. Mwisho wa siku wabunge hulegea na kupitisha madudu kisa tamko lilitoka kwa Rais.

Leo Tume ya uchaguzi inakiri haiko huru. leo BOT inakiri kuingiliwa na wanasiasa. Leo UWT inafanya kazi za chama. Yote haya ni madhara ya nguvu iliyokithiri ya Rais. Taasisi zipewe nguvu na mamlaka ya kiutendaji.
 
Raia Fulani,

Asante kwa mchango wako *bandiko namba 78); Nimebaini hoja kuu tatu na ningependa kuzijadili kama ifuatavyo:

Kwanza ni kuhusu suala la State vis a vis Government ambapo you have raised interesting points kuhusu jinsi gani tunaweza kupima ukomavu wa STATE na SERIKALI, lakini pia kuhusu Umri wa SERIKALI NA STATE; Before we embark into a discussion about the criteria, determinants, indicators on these matters, if i may borrow neno lako for a second i.e. consensus, can we first reach a consensus kwamba state formation and government formation ni vitu viwili tofauti? Kwa mfano, sisi kama watanganyika na baadae watanzania, we have never formed our own state, kilichotokea ni kurithi a state established na mkoloni to serve matakwa ya mkoloni wakati ule; Tulichokifanya ilikuwa ni formation of a new and indigenous government to run institutions zile zile za mkoloni; Zilitokea changamoto nyingi na Mwalimu alizijadili kwa kirefu kwenye chapisho lake na TANU na RAIA na kwingineko;

Leo, it may happen that we get a strong government depending nani yupo madarakani (example Mkapa, Nyerere, hawa walitupatia serikali ambazo tunaweza kusema zilikuwa much stronger than Kikwete na Mwinyi, but huu ni mjadala mwingine); Lakini uwepo wa ‘a strong government' from time to time haina maana kwamba we also have a strong state; Tanzania as a state is inherently weak, soft and problematic – hata wakati wa Nyerere na Mkapa; Ushahidi juu wa hili ni kuhangaika kwetu na hili lijiti linaloitwa STATE tangia uhuru ambapo kama nilivyojadili awali, tulianza na PARTY STATE miaka sita ya mwanzo baada ya uhuru, lakini kutokana na the inherent softness, weakness and associated problems and challenges that faced GOVERNMENT ya wakati ule running STATE institutions, Mwalimu na TANU wakahamia kwenye DEVELOPMENTAL STATE; Lakini kwa vile hili lijitu STATE ni inherently weak, soft and problematic, DEVELOPMENTAL STATE under Azimio la Arusha failed to deliver, and since 1985, tumekuwa na ‘a CONTRACTING STATE' kama nilivyojadili kwenye bandiko namba 76, na kwa miaka 28 sasa ya hii CONTRACTING STATE Per Washington Consensus, bado tunaona lijiti hili linaloitwa STATE likiwa inherently weak, soft and problematic, kupelekea hoja ya Mnyika na wengineo kwamba Rais wa awamu ya NNE NI DHAIFU;

Hoja yako ya pili inahusu democracy and development – nakubaliana na wewe katika hili, na ushahidi upo kwenye practicality ya neo liberal democracy and neo liberal economic principles ambazo zinaendelea kuwa implemented katika nchi zinazoendelea kupitia a variety of reforms, huku matokeo yake yakiendelea kutonufaisha walio wengi;

Hoja yako ya mwisho inahusu madaraka ya Rais na naunga mkono hoja, hasa juu ya umuhimu wa kupatia taasisi muhimu zinazo deal na masuala ya uchumi na fedha, ulinzi na usalama more autonomy, vinginevyo tutashuhudia political democracy ikisambaratishwa na the demos (people kupitia peoples power) before our eyes, kwani ‘a STATE' emerges in response to needs that groups/individuals have in a society; and such needs may rise from problems related to security, welfare and solving the conflicting demands of scarce resources – particularly kutatua the economic problem of scarcity ambapo kunakuwa na limited resources facing unlimited wants in the society; mishandling of matters in this context can turn a country into flames…; Pia tukiwa katika hoja hii ya madaraka ya rais, kama ulivyojadili, kuna umuhimu wa ku strike the right balance between a stable government and an accountable government – the former relies on presidential form of government and the latter on parliamentary form of government;
 
Na inakuwaje pale ambapo Rais yuko madarakani kimabavu kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika? Matatizo huongezeka zaidi. Tayari tulishashauriwa kuwa Afrika haihitaji strong men bali strong Institutions. Hii ina maana kupunguza nguvu na madaraka ya Rais! Tuna Bunge ambalo ni tofauti na Serikali na Mahakama. Tunachoshuhudia ni kwamba wabunge wanaamua kupinga muswada fulani ambao umependekezwa na serikali iliyopo madarakani. Wengi wa wabunge wako chama tawala. serikali ambayo watendaji wake wakuu ni wanachama wa chama tawala na ni wateule wa Rais (madaraka ya rais) inaamua kuwaita wabunge wake pembeni na kuwaonya juu ya kupinga kwao jambo fulani. Mwisho wa siku wabunge hulegea na kupitisha madudu kisa tamko lilitoka kwa Rais.

Leo Tume ya uchaguzi inakiri haiko huru. leo BOT inakiri kuingiliwa na wanasiasa. Leo UWT inafanya kazi za chama. Yote haya ni madhara ya nguvu iliyokithiri ya Rais. Taasisi zipewe nguvu na mamlaka ya kiutendaji.
Raia Fulani, hili ndilo nimekuwa nalipigia upatu kila mara. Ni jambo la hatari sana kulundika madaraka ya uongozi kwa mtu mmoja. Kwa nchi za wenzetu wamefanikiwa kuufanya uongozi wa taifa kama kiungo cha Institutions na hviyo nasi ni wakati sasa tuachane na dhana ya uongozi wa jeshi la mtu mmoja.

Ile hofu ya kwamba kumpunguzia rais madaraka kunaweza kuhatarisha usalama wa nchi, mimi sioni matiki yake kwa kufikiri kuwa hivi sasa rais ana madaraka hayo na bado wana-abuse bila kuhatarisha usalama.
 
Back
Top Bottom