Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Ab-Titchaz na Invisible naomba mumpe access Mwl Kichuguu kwenye huu ukumbi........samahani kwa usumbufu.......
Maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "power in the right hands is good and indeed necessary for a new state" yanaweza kuwa sahihi kwa taifa jipya kama South Sudan. Lakini sidhani kama tunaweza kusema kuwa taifa letu ni jipya na hivyo tumpe madaraka mtu mmoja.
Tanzania siyo taifa jipya, bali demokrasia yake ndiyo bado changa. Demokrasia yetu bado ipo kwenye majaribio na kuna taasisi nyingi tuu, ikiwemo ya Rais, ambazo zinahitaji kufanyiwa review.
- Kwa upande mwingine, tatizo linaweza lisiwe kumpa Rais madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa "checks and balances" kuhakikisha kuwa hayo madaraka hayatumiwi vibaya.
- Nafikiri tatizo siyo Rais kuwa na madaraka makubwa, bali kutokuwepo kwa checks and balances kuhakikisha kuwa hayatumii hayo madaraka vibaya. Mbona Rais wa Marekani ana madaraka makubwa tuu kiasi kwamba anaweza ku-command the instant destruction of an entire city within minutes?
- Marekani ina maelfu ya missiles with nuclear warheads na ni Rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutoa signal to launch them. Ila checks and balances zinahakikisha kuwa anayatumia haya madaraka vizuri.
- Ukiondoa madaraka ya Rais na kumpa mtu mwingine, una uhakika gani kuwa hatayatumia vibaya? kwa mtu kama huyu?
- Kupunguza madaraka ya Rais haitasaidia sana unless tuwe na uhakika kuwa hao wengine tutakaowapa hayo madaraka watayatumia vizuri. Otherwise, itakuwa ni kulihamishia tatizo kutoka kwa mtu/taasisi m/moja kwenye kwa taasisi mtu mwi/nyingine.
- Sidhani kama tatizo lipo kwa Rais kuwa na madaraka makubwa bali kukosekana kwa checks and balances jinsi rais anavyotumia hayo madaraka. Kuwepo kwa strong checks and balances zitamfanya rais awe makini zaidi jinsi anavyotumia madaraka aliyopewa.
Kwa hiyo, swali la kujiuliza siyo kwa nini Rais asipunguziwe madaraka aliyonayo sasa, bali ni kwa nini madaraka ya Rais yasiwe subject to democratic review or checks and balances ambazo kwa sasa hazipo?
By the way, out of this topic. Can yon tell me serikali katika mwezi huu januari imefaya kazi gani ya maana inayohusiana na maendeleo ya nchi? Au rais au PM, tunaweza kujua wanafanya kazi gani kwa ajili ya maendeleo ya nchi? au ndio wanafanya kazi zile zile za kila siku za mambo yale yale ya siasa? just curious, labda wewe unajua kidogo on this.
Mkuu Mchambuzi;
(1) Kuhusu ukomavu wa Taifa, nadhani tutafanya makosa kutaka kufuata historia ya taifa lililokomaa la Marekani kama model yetu, bali tunatakiwa tujifunze kutoka kwenye historia hiyo. Marekani ilipitia historia ndefu kulingana na wakati na vile vile kulingana na namna taifa hilo lilivyoundwa; lilianza likiwa ni makoloni kadhaa yanayojitegemea halafu kwa pamoja yakaamua kuasi utawala wa kikoloni na kuuangana, ila kwa vile mawasiliano hayakuwa ya kasi kama leo, iliwachukua miaka mitatu kwa zile state 13 za kwanza kukamilisha utaratibu wa kuandikiana makubaliano ya kuungana. Halafu hali iliendelea hivyo pole pole hadi baada ya miaka 110 ndipo wakawa wamekamilika kuwa Taifa tunalolijua leo; kwa hiyo kufuata model yao kuwa miaka hamsini bado ni uchanga kitaifa tutakuwa tunafanya makosa; tujifunze kutoka kwao; au tujifunze kwa nchi kama India au Singapore ambazo hatukutofautiana sana kupata Uhuru; waliopokuwa na miaka 50 walikuwa wako mbele sana, na wana utaratibu ambao kiongozi wa nchi hana absolute power kama rais wetu sisi.
(2) Katika dunia ya leo ambayo imekuwa kama kijiji kidogo, ni lazima tuachane na mifumo ya utawala ya kizamani ambamo kiongozi mmoja tu ndiye anakuwa na madaraka yote; sababu zipo nyingi. Katika kujibu maswali yako mengine uliyouliza, ninakubaliana na wewe kuwa hatuwezi kumnyima rais madaraka, ni lazima rais wetu awe na madaraka lakini tunataka madaraka hayo yawe na mipaka yake. Baadhi vitu nilivyoguzia kuhusu mipaka hiyo ni pamoja na:
(a) Kumpunguzia mamlaka ya kuteua na kufukuza mtu wakati wowote; uteuzi anaofanya rais ni lazima uthibitiwe, na utaratibu wa kufukuza wateule pia ni lazima uthibitiwe kikatiba. Nadhani nimeeleza vizuri kuwa kufanya hivyo kutasababisha wateule wasiwe wanafanya kazi zao kwa kujipendekeza kwa rais. Kuna njia tatu za kuthibiti madaraka hayo: (i) kwanza ni kupunguza nafasi za kuteuliwa- rais asiteue nafasi za makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wabunge maalumu. Makatibu wakuu wawe ni wanataaluma watakaoomba nafasi hizo na kusailiwa kama wanataaluma wengine, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wachanguliwa na wanachi kwa kura. (ii) Pili ni kuwapo na muundo wa serikali kikatiba, yaani idadi ya wizara ziwe zimeandikwa ndani ya katiba. Kwa hiyo iwe inajulikana kabisa kuwa atateua mawaziri wangapi kulingana na idadi iliyoandikwa ndani ya katiba> (iii) Utezi wowote wa rais ni lazima uwe unakubaliwa na Bunge, yaani rais ana-nominate, na bunge lina-confirm; vile vile katika kumfukuza mteule, rais ata- recommend kumvua mteule madaraka, halafu bunge lina-confirm mteule huyo kuvuliwa madaraka.
(b) Kumpunguzia mamlaka ya kuamuru jeshi kufanya operesheni yoyote ya kijeshi. Operesheni zote za kijeshi ziwe zinapata baraka ya Bunge, na hapa niliongeza kuwa katiba inaweza kuweka mwanya maalumu wa rais kuanzisha operesheni za kijeshi kwa kushirikiana na viongozi wachache wa bunge bila kupata kibali cha bunge zima iwapo operesheni hiyo ni time-sensitive.
Ili kuondoa mgongano baina ya bunge na rais, katiba iweke utaratibu wa ziada baada ya kutokea mvutano baina ya rais na bunge. Kuna njia nyingi za kufanya hivyo ili kuhakikisha kuwa Bunge halimbani sana rais kama ambavyo Marekani leo hii Bunge lao limekuwa linamfanya Rais wao ashindwe kufanya kazi zake vizuri, siyo vigumu kuweka utaratibu huo.
Kwa Tanzania Parliamentary System ni Majanga.Ni ukweli usiofichika kuwa our parliament is full of useless figures.No disrespect to Prof.Majimarefu et.al,but such kinds of figures are just filling empty chairs.
Presidential form of government is a bit better at the moment until we reach a level where Tanzanians understands why they elect MP's and what caliber an MP should have/be.
Pamoja na Madhaifu yake yooote, Kikwete na taasisi nzima ya Uraisi is miles ahead better than our parliament collectively.We do have few probably a handful brilliant MP's thats about it.Ukiona Rais inabidi ateue mtu kuwa mbunge ili kujazia baraza la mawaziri, jua kuna tatizo kubwa, ukiona the likes of Mulugo and such wanakuwa mawaziri jua kuna tatizo kubwa kuliko.
With the way votes are conducted in our parliament,i wouldn't want those empty heads to decide if the country goes to war or not. Am sure if the malawi issue was put up to the parliament to decide,we would long be in war by now.WHY?because in our parliament a few noisy MP's influence the rest who just follow the beat.
Bongolander,
je, ni kwanini chini ya awamu ya Mwalimu Nyerere such powers tuliona zipo justified lakini sasahivi hatuoni umuhimu wake?
Swali linalofuata ni je, kwanini implementation ya economic reforms nayo haikufuata an incremental process (kidogo kidogo) kama mageuzi ya kisiasa na badala yake kiuchumi mambo yakawa implemented radically bila ya kujali madhara yake kwa wananchi?
Naomba nieleweke kwamba sitetei CCM au kupinga mabadiliko husika, bali najadili kwa maoni yangu tumefikaje hapa;
EMT,
Katika haya, nina masuala mawili - matatu ningependa kuyajadili; Kwanza, kwa mtazamo wangu, kuna utofauti baina ya taifa jipya na taifa changa; Iwapo utakubali nikuelekeze zaidi katika dhana ya uchanga kuliko upya, unatumia criteria ipi au zipi to gauge or to determine uchanga wa taifa - umri? Kama ni umri wa taifa, ni miaka mingapi?
Pili unaposema kwamba demokrasia yetu bado changa, una maanisha demokrasia ya aina gani na unaipimaje? Umri? Kama ni umri wa demokrasia, ni miaka mingapi?
Suala la tatu ambalo ningependa kulijadili kidogo lakini zaidi pia kwa mtindo wa Swali kwako ni kwamba - Ukichukulia Tanzania na Somalia, how would you describe these two kama mataifa in terms of upya, uchanga, or anything in these lines... Bear in mind kwamba Somalia ceased to be a British protectorate earlier than Tanganyika i.e. Somalia (1960) na Tanganyika a year later (1961);
Naomba nimalizie kwa swali lingine kwako:
Kwa mtazamo wako, in the context of all the above, tufuate mfumo gani chini ya katiba mpya na kwanini - presidential form of government au parliamentary form of government?
Kuna baadhi ya maamuzi kwa kweli ni muhimu yafanywe kwa haraka na Rais, na hayana haja ya kusubiria vikao vya bunge; Vinginevyo bunge ni muhimu pia kushirikishwa na hili linaweza kufanyika kupitia kupitia kamati husika za bunge ambazo zinaweza kushauri the executive branch juu ya maamuzi Fulani kasha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi husika kwa haraka; Bottom line ni kwamba - kuna baadhi ya maeneo ambayo ni muhimu yapunguzwe, lakini mengine ni muhimu yaachwe kama yalivyo LAKINI yadhibitiwe kikamilifu chini ya Katiba Mpya, hasa kwa kulipa bunge uwanja mkubwa zaidi katika maamuzi na uongozi wa nchi;
| Mwaka | Main Feature | Main Objective |
| 1961 – 1966 | Party State (TANU) | To establish order |
| 1967 – 1985 | Developmental State (TANU/CCM) | Progress |
| 1985 – Present | Contracting State | Control |
Raia Fulani, hili ndilo nimekuwa nalipigia upatu kila mara. Ni jambo la hatari sana kulundika madaraka ya uongozi kwa mtu mmoja. Kwa nchi za wenzetu wamefanikiwa kuufanya uongozi wa taifa kama kiungo cha Institutions na hviyo nasi ni wakati sasa tuachane na dhana ya uongozi wa jeshi la mtu mmoja.Na inakuwaje pale ambapo Rais yuko madarakani kimabavu kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika? Matatizo huongezeka zaidi. Tayari tulishashauriwa kuwa Afrika haihitaji strong men bali strong Institutions. Hii ina maana kupunguza nguvu na madaraka ya Rais! Tuna Bunge ambalo ni tofauti na Serikali na Mahakama. Tunachoshuhudia ni kwamba wabunge wanaamua kupinga muswada fulani ambao umependekezwa na serikali iliyopo madarakani. Wengi wa wabunge wako chama tawala. serikali ambayo watendaji wake wakuu ni wanachama wa chama tawala na ni wateule wa Rais (madaraka ya rais) inaamua kuwaita wabunge wake pembeni na kuwaonya juu ya kupinga kwao jambo fulani. Mwisho wa siku wabunge hulegea na kupitisha madudu kisa tamko lilitoka kwa Rais.
Leo Tume ya uchaguzi inakiri haiko huru. leo BOT inakiri kuingiliwa na wanasiasa. Leo UWT inafanya kazi za chama. Yote haya ni madhara ya nguvu iliyokithiri ya Rais. Taasisi zipewe nguvu na mamlaka ya kiutendaji.