Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Balozi Sefue, Madaraka ya Rais na Katiba Mpya: Je, Tunaelewa hoja yake ya msingi?

Mchambuzi,
Hapo juu kuna kitu umekisema check and balance, na hasa ndio msingi wa hoja yangu.
Suala la madaraka ya rais linachukuliwa vibaya. Wale wanaodhani asipunguziwe madaraka wana hofu kuwa Rais anaweza kushindwa kufanya kazi zake kwa vile tu atakuwa amepokwa uwezo.

Kundi hilo linadhani rais ataondolewa kuwa Amir jeshi mkuu wa vyombo vya usalama au atapunguziwa nguvu kama alivyopunguziwa Gobachev na mwisho wa siku atakuwa powerless.

Kundi hili lina fear of unknown kwasababu tu limebaki kuangalia tulikotoka na limefungia macho twendako na dunia tuliyo nayo. Kuna nchi kama Turkey na nyingine nyingi tu uwezo wa rais unakuwa na mipaka hasa katika majeshi na vyombo vingine kama mahakama na haionekani kuwa tatizo zaidi.

Taifa letu linakua na hivyo lazima lipitie katika mabadiliko kulingana na nyakati.
Kuna wakati tuliaminishwa kuwa vyama vingi maana yake ni Rwanda genocide, Bosnia Hezegovina n.k.
Leo ni mwaka wa 20 hakuna tatizo lolote zaidi ya kuimarisha demokrasia kwa kiwango fulani.

Kundi la pili ambalo mimi ni mmoja wao ni lile linalotaka Rais apunguziwe madaraka.
Ukitazama kwa umakini, nchi yetu haina bunge au mahakama kama vyombo huru.
Bunge na mahakama ni matawi au ''jumuiya za serikali''.

Rais anaweza kuvunja bunge lililochaguliwa na wananchi, akamuondoa Jaji mkuu na kuweka ampendaye hata kwa emergency kama alivyofanya Mwai Kibaki.

Kumpunguzi madaraka nina maana ya kumwekea mipaka ya kazi yake na vyombo vya check and balance.
Leo Obama anafanya mabadiliko ya umiliki wa silaha wakati huo huo akiwa ameshapata ushauri wa kutosha kuhusu second ammendment kwasababu kinyume chake ni impeachment.

Kumpunguzi madaraka ni kuwa na serikali inayozingatia katiba, kufanya kazi kwa ushirikiano na vyombo vingine huku kila kimoja kikiwa watch dog ya kingine.Hiyo ndiyo check and balance.

Ni katika hiyo check and balance ndipo rais atakapolazimika kuteua watendaji ambao baada ya kuthibitishwa si wake tena, watawajibika sehemu nyingine. Hii itatoa nafasi za umakini katika kupata viongozi na kumpa rais ''unafuu'' wa kuwaondoa kwani yeye hatahusika tena.
Hebu fikiria yaliyotokea bungeni ambapo PM alilazimika kuondoka na si kuondolewa na Rais

Lakini pia kumpunguzi madaraka kunalenga kuongeza ufanisi kwa Rais kwa kumpunguzi kazi zisizo za lazima na zingine zinazomtia katika kashfa. Kwanini Rais wa linchi likubwa kama Tanzania ahangaike na uteuzi wa wakurugenzi wa miji au bodi za mashirika na vyuo,kwa mfano.

Kwa ufupi kumpunguzia madaraka rais haina maana ya kumyang'anya nguvu za kiutawala bali kumpa nguvu za kiutawala kwa kuzingatia, sheria, taratibu na maadili.Ni kumpa uwezo wa kufanya mambo ya kitaifa zaidi, kumwepusha na migongano isiyo ya lazima na vyombo vingine hata wananchi.

Ni njia ya kumpa nafasi ya kuiangalia nchi kwa ujumla wake bila haya, kusimamia majukumu yake na wenzake kwa kutambua kuwa kuna watch dog. Na muhimu ni kumfanya atambue kuwa yeye ni mtumishi namba moja wa umma na wala si mtumikiwa namba moja.

Kupunguziwa madaraka kutazuia ''office abuse'' na kumfanya afikirie kwa umakini kila jambo linalogusa wananchi, rasilimali na usalama wao kila sekunde na dakika.

Hatuhitaji kiongozi tunahitaji uongozi na uongozi hautengenezwi na jeshi la mtu mmoja bali collective responsibility ya kila mmoja wetu katika nafasi yake.Endapo ni hivyo kwanini tuna woga wa kugawna madaraka ili tuwe na uongozi badala yake tunataka kumlundikia mtu mmoja ili tuwe na jeshi la mtu mmoja.
 
Mchambuzi

Hivi katibu kiongozi amemwakilisha na Rais JK kwenye hayo maoni? Kama ndio, sishangai kusikia hayo aliyoyasema kwani yatakuwa ni ya JK wa ukweli. Kama hapana, basi anataka kumfurahisha JK wa ukweli na wale wote ambao watafuatia kutoka CCM.
 
Last edited by a moderator:
Angalizo, Mchambuzi tunakuheshimu sana usitumike kwenye issue kama hii!

Hilo ni ombi langu binafsi hasa kuzingatia uzito wako hapa JF!

Mkuu, MTAZAMO...hebu funguka kidogo...ANGALIZO lako linalenga kuhusu nini?

I think MH. MCHAMBUZI has brought a very loving motion in-here, lets have deeper discussion and NOT warnings or threats of whatever style...

Plse my views......and without prejudice..!!
 
Natumaini pia umesoma msingi wa hoja yenyewe Mtazamo; Naomba upitie kipengele kimoja baada ya kingine kisha ueleze ni kipi hasa kinaonyesha kwamba kuna ishara za mimi kutumika na watawala katika hili; Kama ulikuwa makini kidogo katika kusoma hoja yenyewe, nacholenga ni kuangalia nguvu hizi za rais zilianzia wapi, na kwanini, na pia kwanini awamu ya nne inaonekana kuwa dhaifu kuliko awamu zilizopita; nadhani ni katika kujenga hoja hii ndio inaonekana kama vile namtetea rais wa sasa wakati ukweli ni kwamba kama udhaifu katika utawala wake, udhaifu upo na kupingana na hili ni kwa kutumia akili ya mwendawazimu;

Mchambuzi nimepitia juu juu bandiko lako, naona kuna pointi nyingi sana za muhimu, kwa hiyo siwezi kutarget point moja tu kwenye post yako. Lakini ningependa tuliangalie jambo hili kwa mapana zaidi.

Kwanza sioni kama ni sahihi kuiunganisha hoja hii na matumizi ya madaraka ya urais ya Jakaya Kikwete. Kikwete ni mmoja tu kati ya watu wanne waliotumia madaraka ya Urais hapa Tanzania. Kila mmoja wao anaweza kujadiliwa kwa kona zote kutokana na matumizi yao ya madaraka ya urais. Kwa hiyo kama tunataka kuangalia jambo hili, ni vizuri tuliangalie kwa mapana, yaani experience ya matumizi ya madaraka ya urais kwa marais hao wanne, na hatari zinazoweza kutokea baadaye kama mtindo wa sasa ukiendelea, au kama ukibadilishwa. Na tuangalie kama kweli kuna umuhimu kwa mtindo wa sasa kuendelea kama ulivyo au kuubadilisha.

Kwa maoni yangu katiba ya sasa hasa vipengele vyote vinavyohusiana na execitive powers vina matatizo sana, haviendani na hali halisi ya nchi. Bado vingi ni vile vinalinda maslahi ya gavana anayetawala koloni la Tanganyika, na sio vilanida maslahi ya mtanzania.

Tatizo lililopo ni kuwa, wakati wa Nyerere karibu watu wote walimwamini Nyerere kuwa ni mwenzetu na ni kijana wetu, anayefanya kazi kwa niaba yetu na kwa ajili ya maslahi yetu, and there was general agreement that the ruling CCM was there (and there was evidence) for the people and for the country. Japokuwa kulikuwa na manung'uniko hasa kutoka kwa watu waliokuwa na mtazamo tofauti kuhusu mwenendo wa kisiasa na kiuchumi (they were not wrong), lakini walio wengi walijua kuwa mtu wao yuko ikulu, waliamini kuwa anatumia madaraka kwa ajili ya manufaa yao.

Tatizo ni kuwa wakati ule hakuna aliyejua wala kufikiri kuwa kuna siku CCM itabadilika kabisa na kuwa chama chenye malengo mengine na kurepresent interest za watu wa tabaka fulani la watu, lakini ikaendelea kuwa na jina lilelile, na kujaa mafisadi. Hakuna aliyefirikiri hilo na inaonekana kuwa hata sisi wengi wenye kadi za CCM hatuoni hilo, na tunendelea tu kusifu as if bado tuko na CCM ya Nyerere/Karume.


My point is, we are here because we thought and believed that Presidents of Tanzania will exercise power vested on them by our Constitution for the interest of the country, people and the party. We were damn wrong.

Watu wanaomwangalia JK kama kioo cha kuamua kubadilisha katiba hasa vipengele vinavyohusiana na madaraka ya rais hawaoni mbali. Kikwete anaendesha nchi "kishkaji" ndio maana anaonekana weak. Hajaweza kuunda cabinet yenye nguvu, hajaweza kuunda safu stable ya uongozi wa chama, hajaweza kuprovide leadership, na hajaweza kulead as president, hajaweza kuonesha wazi serikali yake inafanya kazi gani. Anafanya mambo ambayo otherwise si presidential, kama kusafiri kwenye safari nyingi zisizo na tija, kwenda kwenye misiba ambayo labda hata mkewe si vizuri kwenda, kuwalinda na kuwafumbia macho mafisadi, kuwateua watu katika mazingira ya kushangaza na kuwapa nafasi kubwa bila hata kuwa na sababu za msingi zaidi ya personal connections, watu kuwekeana sumu na siasa nyingi ambazo labda zinaonekana za kitoto...unaweza kuorodhesha mengi sana.

Lakini can you imagine, with current constitution, how will the situation be like with John Magufuli as president mtu ambaye anapenda kuendesha mambo kwa amri bila reasoning, with Edward Lowassa as president ambaye anadhalilisha watumishi na kuwatukana bila hata kujua mazingira yao ya kazi, mtu ambaye anatajwa kuwa uchu madaraka na utajiri kwa gharama yoyote, au with Augustine Mrema as president, au with an Islamist as president. Can you think for a second about this? Are we real sure that these people (na wengine wengi ambao hatuwajui) will exercise their executive powers for the interest of Tanzania and Tanzanians, wangapi watakuwa kizuizini kwa mujibu wa Preventive Detention Act? Wengine ambao ni arrogant si watakuwa wanawatisha watu na kuwatukana kila siku? wengine si watawaua watu na kuwapora mali zao na kujaza akaunti zao?

Kwa katiba hii tunaweza kuona kuwa ni bora kwa JK mwenye interest ya ku-enjoy urais, kuliko yule atakayetumia urais kuwatesa maadui na kukandamiza watu wengi asiowapenda kwa mujibu wa madaraka aliyopewa kikatiba.

The point is we need to be clear with what President should do and what president should not do. Awe na kazi yake ya urais tu, asiwe hakimu yeye mwenyewe, polisi yeye mwenywe na mbunge mkuu yeye mwenywe.

Hapa Tanzania ukiangalia kelele zote wanazopiga wabunge hazimsumbi rais kwa kuwa riasi mwenye ndio bunge, anaweza kulivunja bunge as he wish, na anaweza kukataa chochote wabunge wanachotaka as he wishes. Anaweza kutengua uamuzi wa mahakama as he wish na tusifanye kitu, anaweza kuteua mkewe kuwa waziri mkuu, mtoto wake kuwa mkuu wa majeshi, shemieji yake kuwa kamanda wa polisi, etc etc na hakuna atakayepinga kwa kuwa katiba inamruhusu kufanya hivyo.

Sidhani kama ni vizuri kuendelea na utaratibu wa kumfanya rais asifanye hivyo kwa kuona noma, ni vizuri kuwe na utaratibu wazi kuwa rais anaweza kumteua mtu mwenye sifa fulani katika nafasi fulani, asiwe jaji mkuu mkuu zaidi, asiwe spika mkuu mkuu zaidi. Anatakiwa kupunguziwa madaraka mengi lakini madaraka hayo yapelekwe kwenye idara nyingine ambazo zinaweza kufanya kazi vizuru zaidi. Na no vizuri tujue kazi za rais za kila siku ni zip[i na tujue anafanya kazi gani.
 
Bongolander,

Asante kwa mchango wako - bandiko namba 24; Umeongea mengi ya msingi lakini kama ni kutoa summary basi ni kwamba – Utawala wa Kikwete ume - expose jinsi gani taasisi ya urais ilivyokuwa ‘WEAK' lakini pia unatoa angalizo kwamba it could have been worse, na hivyo unaonya tuwe waangalifu huko tuendako. Kimsingi naunga mkono hoja.

In Tanzania, Mageuzi ya kisiasa yanachechemea mageuzi ya kiuchumi kwa karibia miaka 10, na the most important aspect of democratic transition – liberal democracy chini ya Mfumo wa Vyama Vingi ni Constitution reforms. Tume ya Nyalali ilipendekeza mabadiliko ya sheria nyingi pamoja na vipengele vingi vya katiba ya nchi (1977) - including kufutwa kwa ‘Detention ACT' uliyojadili, ili taifa liwe na Katiba inayokidhi mahitaji ya mfumo wa vyama vingi ndani ya demokrasia ya ulibelari; Sifa za demokrasia ya namna hii ni pamoja na uwepo wa:


  • Utawala wa sheria, SIO UTAWALA KWA SHERIA – kwa maana kwamba kila mtanzania anatakiwa kuwa na haki sawa mbele ya sheria, tofauti na hali ya sasa ambapo katika makosa Fulani Mchambuzi anakuwa treated tofauti na Bongolander;
  • Uwepo wa Chaguzi huru, za wazi na za haki;
  • Uwepo Wa Haki za kibinadamu na za kiraia;
  • Utenganishwaji wa mihimili ya DOLA.

Pamoja na umuhimu wa mapendekezo yote haya, Serikali ya CCM ikayatupa kapuni mapendekezo mengi kwa imani kwamba Chama kitaweza kusimamia democratic transition kwa ‘pace' inayoona ndio inafaa yani ‘top – down implementation of political reforms, kwa hoja kwamba kufuata an incremental approach towards political liberalization badala ya a radical approach kama ilivyotokea kwenye economic liberalization cntext, kutasaidia Taifa kuendelea kubakia in ‘peace, order and unity', of which Rais wa nchi kwa mujibu wa utaratibu alioweka Mwalimu Kikatiba ndiye the living symbol. Kikwete amekuja badili hili aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya chini ya utawala wake kwani unlike wenzake waliomtangulia ambao walikuwa keen to see radical implementation of economic reforms BUT incremental implementation of political reforms ambayo yalikinga sana madhaifu ya taasisi ya Urais, Kikwete ni kama amekuja na version yake ya "RUKSA" lakini tofauti na ile ya Mwinyi Kiuchumi, ya Kikwete ni ya Kisiasa.

Given the fact kwamba Rais (hivyo as of now KIKWETE) continues to be the Living Symbol of our Unity, na kwamba yeye ndie CUSTODIAN of our unity, peace, stability and order huku pia Katiba ikimtazama yeye kama mtu ambae anatakiwa kulipatia Taifa a Vigorous Leadership, hii radical democratic transition under his administration pamoja na kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari, pia the lack of adequate electoral reforms, the increasing threats of defections within the party (CCM), and importantly, factionalism iliyojitokeza chini ya awamu yake ambapo wahusika wamekuwa wana nguvu kubwa kuliko taasisi ya Rais na pia Chama Cha Mapinduzi, hizi ni sababu za msingi kwanini Rais Kikwete amekumbwa na JANGA LA UDHAIFU; Mind you, huko nyuma, taasisi ya Rais na Chama Cha CCM (Rais akiwa pia ndiye mwenyekiti wa CCM) vilikuwa ni SUPERIOR kwa mihimili yote mingine ya dola – Bunge na Mahakama; Pia taasisi ya Rais na CCM vilikuwa ni SUPREME kwa Katiba ya JMT (1977); Kwa bahati mbaya sana, taasisi hii ya Rais pamoja na CCM katika nyakati hizi, vimegeuka kuwa INFERIOR kwa baadhi ya Wanachama wa CCM, na kupelekea suala la Rais kuonekana ni Dhaifu, nchi kuyumba, kuwa ni masuala inevitable chini ya awamu ya nne

Kwa sasa tupo njia panda ingawa wengi tayari wameshachagua upande wa kufuata katika hii njia panda (yani kupunguza madaraka ya Rais Kikatiba badala ya kuegemea zaidi katika kuyadhibiti au kuyaacha kama yalivyo hivi sasa); Kwa upande mmoja, kama tunataka kuendeleza stability huku tukihakikisha kwamba power remains in good hands in 2015 huku tukiweka effective systems of checks and balance, basi our choice ndani ya katiba mpya ni muhimu iwe katika kudhibiti zaidi kuliko kupunguza madaraka ya rais kikatiba – hii aina maana kwamba madaraka yote yanabakia kama yalivyo, hapana, suala la msingi hapa ni kuchagua ratio mfano 70% of the effort iende katika kuthibiti maeneo Fulani, 30% iende katika kuyaondoa kabisa (huu ni mfano tu kwa nia ya kufafanua hoja); lengo kuu hapa iwe ni kuhakikisha kwamba tunaegemea zaidi katika kutafuta njia nzuri ya kudhibiti powers za rais kuliko kuzipunguza; Kwa kufanya hivyo, ina maana tutahitaji kufuata a presidential form of government; Lakini katika hili, una hoja ya msingi sana katika bandiko namba 24 kwamba tukipata Rais mwenye matatizo, tutalia na kusaga meno kwani stability means Rais atabakia madarakani kwa miaka mitano kikatiba na hatutaweza kumuondoa hata akifanya madudu ya namna gani mpaka muda wake uishe;

Kwa upande mwingine (tukiwa bado kwenye hoja kuhusu njia panda inayotukabili), tukifuata a parliamentary form of government, hii ina maana kimamlaka, atakayekuwa na nguvu zaidi katika uongozi wa Taifa ni Waziri Mkuu, lakini je, ubinafsi wetu transpired katika hizi mbio za kutafuta Urais 2015 CCM, Chadema, wangapi watakubali kwamba kuanzia 2015 tufuate a parliamentary form of government na kumpa madaraka zaidi Waziri Mkuu? Sioni waliio tayari kuruhusu chini ya Katiba Mpya unless sipo sahihi katika hili; Vinginevyo a parliamentary form of government itatusaidia kudhibiti kikamilifu shughuli za taasisi ya Rais pamoja na wateule wake na kufanya utawala uwe more accountable to the people kwani wabunge watakuwa na fursa ya kutimua waziri mkuu ambae atakuwa anaongoza serikali legelege bila ya kusubiri uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba (kial baada ya miaka mitano), hivyo kupelekea uwezekano wa chaguzi kuu za dharura kwa nia ya kuunda serikali mpya; Hii itapelekea accountability lakini instability kwa nchi; Kwahiyo ni suala la kuchagua kusuka au kunyoa;

Lakini tukichukua mifano ya mataifa makubwa kuliko yote kiuchumi – USA & Japan (huku tukiachana na China on this one), pengine tunaweza kujifunza mengi kwani haya offer both extremes. Kwa upande mmoja, Marekani wanafuata presidential form of government hivyo wapo very stable na ndio maana pamoja na Rais Bush kuvurunda, ilibidi kusubiria amalize muda wake, licha ya gharama alizoliletea taifa lake akiwa Rais; Kwa upande mwingine, Japan wao wanafuata a parliamentary form of government, but there is more accountability than stability kwani ni kawaida kusikia mara Waziri Mkuu amejiuzulu, mara mwingine kajinyonga, yote kutokana na lack of accountability, hivyo kupelekea taifa hili mara nyingine kuwa na mawaziri wakuu hata wawili tofauti ndani ya miaka mitano;

MaSwali ambayo ningependa kupata maoni toka kwani ni je:

*Katika mazingira ya sasa, hoja ya Mwalimu kwamba: "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"

Unadhani hoja hii is still relevant? Why? Why Not?

*Je, mfumo upi ni bora in the context of kupunguza madaraka ya rais kwa mujibu wa hoja zako bandiko namba 24, presidential au parliamentary? Why? Why Not?
 
*Katika mazingira ya sasa, hoja ya Mwalimu kwamba: "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"Unadhani hoja hii is still relevant? Why? Why Not?

*Je, mfumo upi ni bora in the context of kupunguza madaraka ya rais kwa mujibu wa hoja zako bandiko namba 24, presidential au parliamentary? Why? Why Not?

Mchambuzi: To think that Power will be always in the RIGHT HAND that only is a FRIGHTENING IDEA. Here We're talking HANDS of PEOPLE not ANGELS.

Second. Tanzania is no longer a NEW STATE, my brain tells me a new state is SOUTH SUDAN.
 
Mchambuzi: To think that Power will be always in the RIGHT HAND that only is a FRIGHTENING IDEA. Here We're talking HANDS of PEOPLE not ANGELS.

Totally YES

Second. Tanzania is no longer a NEW STATE, my brain tells me a new state is SOUTH SUDAN.

Partially YES;

Tanzania is a state on whose terms? South Sudan and Eritrea in my view are the only truly states in Sub Saharan Africa, the rest are just political territories run by central governments inherited from the colonial past; its why our so called states have been problematic from day one;
 
Nguruvi3,

Karibu sana katika mjadala; umezungumza mengi ya msingi, hasa tuendako, na kimsingi nakubaliana na wewe; Lakini haujagusia sana tulipotoka, hasa kwanini ilikuwa ni muhimu kuwa na mfumo huu wa sasa Kikatiba katika awamu ya kwanza, hasa iwapo kulikuwa na haja, haja hiyo imetimizwa na iwapo kuna haja au hakuna tena haja ya suala husika katika nyakati za sasa;

Ushauri wako unaoendana na kuunga mkono hoja ya kupunguza madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba ni mzuri. Nia yangu mimi sio kupingana na kundi hili la hoja bali kujaribu kujadili pande zote mbili za hoja objectively ili huko mbeleni tukija fanya maamuzi basi itokee baada yak u digest na ku exhaust factors na variables mbalimbali badala ya kuja kujuta; I still maintain kwamba pamoja na umuhimu wa kupunguza madaraka husika, lakini bila ya kuwa waangalifu, tutajikuta na nchi isiyotawalika kwani I still believe kwamba if power is in the right hands, hasa katika masuala muhimu kwa taifa, maamuzi yataweza kufanyika haraka sana tofauti na iwapo powers kadhaa muhimu zitakuwa delegated kwenye organs nyingine;

Kuna baadhi ya maamuzi kwa kweli ni muhimu yafanywe kwa haraka na Rais, na hayana haja ya kusubiria vikao vya bunge; Vinginevyo bunge ni muhimu pia kushirikishwa na hili linaweza kufanyika kupitia kupitia kamati husika za bunge ambazo zinaweza kushauri the executive branch juu ya maamuzi Fulani kasha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi husika kwa haraka; Bottom line ni kwamba - kuna baadhi ya maeneo ambayo ni muhimu yapunguzwe, lakini mengine ni muhimu yaachwe kama yalivyo LAKINI yadhibitiwe kikamilifu chini ya Katiba Mpya, hasa kwa kulipa bunge uwanja mkubwa zaidi katika maamuzi na uongozi wa nchi;

Ni lazima tuseme ukweli kwamba kinachoudhi watanzania wengi na kupelekea vilio vyao vingi juu ya umuhimu wa madaraka ya rais kupunguzwa (tofauti na awamu zilizopita) ni sababu mbili – kwanza ni mchakato unaotumika kuteua watu mbalimbali pamoja na ubora wa wateule husika; Pili, ni kumekuwepo na ucheleweshaji wa maamuzi muhimu lakini pia ukimya wa taasisi ya Urais juu ya matukio na maendeleo mbalimbali katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii, masuala ambayo yameathiri sana wananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii; Lakini cha ajabu ni kwamba, tatizo hili limejitokeza sio kwa sababu Rais hana such Powers, bali ni kutokana na kitendo chake cha kutozitumia ipasavyo (aidha kwa nia nzuri au kwa bahati mbaya, jibu sio straight forward katika hili), lakini pia kwa kuachia political reforms zije more radically kuliko awamu za nyuma; Vilevile ni kutokana na factions ndani ya CCM ambazo zimeua kabisa dhana kwamba Rais ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM is SUPREME Kwa kila kitu kuanzia Bunge, Mahakama, na Hata Katiba ya JMT (1977); Kwa bahati mbaya na kwa sababu zisizo wazi sana nguvu juu ya vyombo hivi zimehamia kwa kiasi fulani Chadema, lakini zaidi mikononi mwa watu wengine (sio taasisi) informally and unconstitutionally;

Naomba kusikia mawazo yako kama nilivyoainisha kwenye paragraph ya kwanza hapo juu;
 
Katika mchango wake wa hivi karibuni juu ya Katiba Mpya, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue amekuja na hoja kwamba “Kupunguza Madaraka Ya Rais Ni Hatari Kwa Usalama Wa Nchi”, na kusisitiza kwamba kuna umuhimu wa madaraka hayo kubakia kama yalivyo chini ya Katiba Mpya;

Nimesoma uchambuzi wako juu ya hoja ya Balozi. Mimi nadhani Balozi anakuwa mwoga tu na uoga huo anauleta kwetu ili tuujadili. Hii inatokana na kujenga mifumo ambayo inategemea watu kuliko taasisi. Ndio iliyozaa yale mambo ya kipuuzi kama Rais Kuongea na Wazee wa Dar es Salaam(sarakasi za kisiasa). Mimi naona jambo na hoja ya msingi ni kujenga,ndani ya katiba ianayokuja, mfumo unaotegemea taasisi( Institutional System) ambayo haumtegemei mtu na ambayo unafanya kazi ya kujiangalia na kujisahihisha wenyewe" checks and balances. Mfumo ambao kama Rais akiwa dhaifu(kilaza) au mwenye nguvu mambo yanaenda kwa sababu mfumo upo na unafanya kazi.Tuache woga na ubinafsi anaozungumzia Balaozi Sefue na tuwekeze na kujenga mfumo wa aina hii. Na hii inawezekana kabisa, maana katiba si ya kipindi kifupi kijacho ila iwe ya miaka 200 ijayo. Stability iletwe na mfumo na si watu. Badala ya watu kusema "ndio mzee" waseme "ndio mfumo"(kama hiyo itamsaidia mtu kuwa mkuu wa wilaya!).

Tuache woga na ubinafsi na tuwekeze huko kwa dhati nasema hivyo kwa kuwa sina uhakika kama kweli lensi iloyotumia Balozi Sefue haina ukungu wa madaraka uliotanda wakati wa kutoa hoja yake
 
Mchambuzi
Nachokiona na kusikia zaidi kwa kweli kinachozungumzwa sio kupunguza madaraka ya raisi bali ni kuweka checks and balances katika nyingi (na hasa zile muhimu) ya teuzi za raisi. Mfano akiisha kuteua jaji, basi jaji anaenda kuidhinishwa na bunge(muhimili mwingine) huko wabunge watapitia profile yake na kuona kama hakuna shaka katika uwezo, uadilifu na maadili then ndo anakuwa jaji, hii inasaidia kuhakikisha kwanza tunapata jaji ambaye integrity na uwezo wake umepitiwa na wengi, pili inamfanya raisi anapofanya uteuzi anakuwa makini zaidi sababu anakuwa anajua uteuzi wake utapitia kwenye chujio lingine.

Kwa kuangalia mfano huu utaona kwamba bado madaraka ya raisi yamebaki pale pale. Ila tumeongezea checks and balances tu ili kupata viongozi wenye uwezo na maadili yanayokubalika na jamii pana.

Na hii inaenda kwenye mambo mengine pia yasio ya uteuzi. Mfano raisi akitaka kutangaza/kuingiza nchi vitani badala ya kuwa ndie mwamuzi wa mwisho katiba inaweza kuweka provision ambapo raisi atapeleka kwanza kusudio la kuingia vitani bungeni halafu wabunge watajadili na kupiga kura ya ama kukubaliana au kutokubaliana na kusudio la raisi. Utaona hapo bado rais(amiri jeshi mkuu) anabaki na madaraka yake lakini tuanepusha mfano kuiingiza nchi katika vita ambayo pengine haina ulazima na vile vile kwasababu jambo linakuwa limeamuliwa na wengi linakuwa na justification ya kutosha pia.
 
Citizens want these executive powers to be reviewed due to the reason that they have been misused by the now government to the point of no return.
 
Mchambuzi

Umenena vema, swala hili binafsi natatizwa nalo. Kwanza ni lazima tujadili madaraka hayo tunayatoa kwa rais na kuyapeleka wapi? Je sababu zile ambazo taasisi ya urais inalalamikiwa kwa madaraka hayo kurundikwa hazipo huko tunakotaka kuhamishia hayo madaraka?

Ni katika Tanzania hii hii ambapo kuna taasisi zinashutumiwa kwa ukabila na udini. Kuna taasisi ambazo pia ni mihimili zimeshutumiwa mchana kweupe tena nyingine baina ya wajumbe wake kwa rushwa na upendeleo. Hakuna taasisi hata moja ambayo kwa uchache tu wa vigezo vya utawala bora kama uwazi, uwajibikaji, nidhamu na ushirikishaji wananchi inaweza ikasimama kifua mbele katika nchi yetu. Kuyatoa madaraka haya mikononi mwa rais na kuyapeleka mikononi mwa taasisi hizi mfu si kumaliza tatizo bali kuliamisha tu na pengine kulikuza zaidi. Wengine tunazungumzia kupeleka madaraka kwa umma as if umma tunaouzungumzia ni sisi watanzania wote kwa umoja wetu. Hakuna kitu kama hicho popote pale duniani, bado tunazizungumzia taasisi zile zile kama ilivyo taasisi ya urais.

Hatuna budi kuupanua mjadala huu ukilenga pia kufumua mfumo mzima wa taasisi zetu ili at least ziwe na medium standards za utawala bora. Na hii ndio fursa, mjadala wa katiba mpya unahitaji kuelekezwa katika kuunda Tanzania ya kimfumo. Tanzania inayojengwa na taasisi imara zinazoweza kutoa maamuzi kwa uwazi pasipo shaka. Kwa hivi tunavyojadili kupunguza madaraka ya rais pasipo kujadili hizo taasisi zingine na udhaifu wake wa kimfumo bado nasimamia maneno yangu kuwa huko ni kukaribisha maafa.

Ivoya-Ngia
Nakubaliana nawe kujenga mfumo na taasisi imara. Tusikubali kurundika mamlaka/madaraka kwa mtu au taasisi moja. Katika karne hii na mazigira ya sasa haitawezekana na itakaribisha vurugu. Wale wanaosema kuendelea kwa mfumo wa sasa wa Rais siyo tu kiongozi wa 'executive' Bali ana madaraka hata ya kutawala miili mingine ya dola wanafikiria ndani ya kisanduku.

Huwezi kutumia sababu ya uchanga kutoweka mfumo ambao utagawanya mamlaka na kuzuia taasisi au mtu mmoja kumiliki madaraka yote. Je KM kiongozi alitaka tuendelee na Rais ambaye anateua majaji apendavyo, ana uwezo wa kuvunja Bunge, anateua watendaji wote wakuu wa taasisi muhimu n.k. Na hakuna wa kuhoji? Katika siasa za sasa za ushindani tudipoangalia tutatengeneza mazigira ambapo hatutakuwa na continuity. Tuukatae mfumo huu.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma uchambuzi wako juu ya hoja ya Balozi. Mimi nadhani Balozi anakuwa mwoga tu na uoga huo anauleta kwetu ili tuujadili. Hii inatokana na kujenga mifumo ambayo inategemea watu kuliko taasisi. Ndio iliyozaa yale mambo ya kipuuzi kama Rais Kuongea na Wazee wa Dar es Salaam(sarakasi za kisiasa). Mimi naona jambo na hoja ya msingi ni kujenga,ndani ya katiba ianayokuja, mfumo unaotegemea taasisi( Institutional System) ambayo haumtegemei mtu na ambayo unafanya kazi ya kujiangalia na kujisahihisha wenyewe" checks and balances. Mfumo ambao kama Rais akiwa dhaifu(kilaza) au mwenye nguvu mambo yanaenda kwa sababu mfumo upo na unafanya kazi.Tuache woga na ubinafsi anaozungumzia Balaozi Sefue na tuwekeze na kujenga mfumo wa aina hii. Na hii inawezekana kabisa, maana katiba si ya kipindi kifupi kijacho ila iwe ya miaka 200 ijayo. Stability iletwe na mfumo na si watu. Badala ya watu kusema "ndio mzee" waseme "ndio mfumo"(kama hiyo itamsaidia mtu kuwa mkuu wa wilaya!).

Tuache woga na ubinafsi na tuwekeze huko kwa dhati nasema hivyo kwa kuwa sina uhakika kama kweli lensi iloyotumia Balozi Sefue haina ukungu wa madaraka uliotanda wakati wa kutoa hoja yake

Hakika kwa asilimia 100. Tumshauri KM Kiongozi aanze yeye kwa kujenga taasisi yake civil service iwe imara kuweza kuudumia Serkali yoyote itakayochaguliwa. Ni sababu ya woga huu ambao umejengeka kutokana na mifumo yetu na dhaifu na taasisi dhaifu inawafanya waogope mabadiliko yatakayoweka chama tofauti na CCM madarakani. Tumeingia kwenye mfumo wa vyama vingi tuna wajibu wa kuweka mfumo na taasisi zitakazofanya kazi vyema regardless ya chama au Rais atakayewekwa madarakani.
 
Nadhani hoja ya kupunguza au kuacha madaraka ya Rais ni hoja nzito na muhimu,lakini kama ambavyo ulivyoainisha kwa rejea kadhaa za maelezo ya mwalimu ya nini kuwa na mfumo unaompa Rais madaraka makubwa,hatukuwa na resources za kutosha na hatukuwa ktk nafasi ya kuachia mihimili kujiendesha bali the Executive kuendesha.

Nyakati tulizonazo ni bora kuwa na mfumo uanotoa madaraka kwa rais ya wastani,kila muhimili upewe madaraka yake kwa namna ambapo hakuokuwa na muingiliano wa kimamlaka.so Amb.Sefue amejenga hoja kwa misingi ya kulinda mazingira yanayomnufaisha lakini hakuja na hoja nzito kwa ustawi wa Taifa hili.Mfume wa Utawala lazima ubadilike kwa manufaa ya nchi na wananchi wake si kwa manufaa ya chadema ama ccm au nccr mageuzi,ni kwa manufaa ya nchi yetu na watanzania kwa Ujumla.

Bado viongozi walio wengi hawajakubali kuwa na mfumo mpya wa utawala jambo ambalo imekuwa ngumu kwao kuhusisha fikra jengefu ktk kujenga hoja,wamekuwa wakitawaliwa na mazoea na ubinafsi!
 
Mgaya D.W, Muchetz, tubadilike-sasa, nguruvi3, bobuk, bongolander,

Kwa mtazamo wenu, kwa kuzingatia hoja kwamba tumpunguzie rais madaraka katika katiba mpya, je hatua hii iendane na mfumo gani wa utawala ndani ya Katiba mpya, je - Presidential form of government au Parliamentary form of government?
 
Citizens want these executive powers to be reviewed due to the reason that they have been misused by the now government to the point of no return.

So the issue here is that power has been in the wrong hands, right? otherwise you support Mwalimu's argument that - "Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State"?
 
Mchambuzi kuna baadhi ya watu wanaona kuwa Tanzania inahitaji dikteta mzalendo, ambaye akitaka tujenge barabara atasimamia ijengwe bila kujali projo za kisiasa, akisema hatutaki ufisadi hakuna ufisadi. Hapa nazungumzia viongozi kama Kagame na Marehemu Mengistu.

Ukiangalia jinsi walivyofanya kazi unaweza kuona kuwa hoja ya mwalimu ya
"Power in the right hands is good and indeed necessary for a new State" ina mashiko. Kwa sababu inaonekana kuwa kama jamii ina watu wasiojua vipaumbele vyao na kuna mmoja anajua vipauambele vyao, si viabaya kama akitumia nguvu kufanya hayo. Nenda Kigali leo au Addis Ababa unaweza kuona kuwa ni miji ambayo inaendeshwa na serikali usalama, usafi, upangaji etc etc. na kwa ujumla unaona ni nchi mabzo serikali zinafanya kazi kwa ajili ya wananchi wao.


Umeuliza kuhusu relevancy ya hija hii. Inategemea tuko katika mazingira gani na tunataka nini. Unajua Tanzania siku zote inasifiwa kwenye jukwaa la kimataifa kuwa ni nchi ambayo iko shwari lakini ukweli ni kuwa tunadanganaya watu, tunatumia demokrasia kuibia watu, au tuna mfumo mzuri wa kuhadaa jumuiya ya kimataifa kuwa tunademokrasia lakini ukweli ni kuwa haitusaidii kuadress tatizo kubwa la umasikini, isipokuwa wajanja wanaitumia kufanya.

Kwa hali ya Tanzania naona ni vizuri sana kuwe na mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili mitatu ya dola, Inagwa katiba yetu inasema kuna mihimili hiyo lakini ukiangalia kihalisi bado ni mhimili mmoja tu. Executive branch ina nguvu kuliko bunge, na katika inasehema wazi kabisa kuwa rais ni sehemu ya bunge, that is wrong, Executive haitakiwi kuingilia mahakama lakini Tanzania kwa sasa kivitendo Rais ndio jaji mkuu.

Ukiangalia haya yote unawezakuona kuwa ni mazuri kama rais ni Nyerere, lakini si mazuri kama rais ni mtu mwenye hasira na dharau kama Mkapa, mtu wa madili kama Mwinyi,

kwa hiyo ni bora miundo hii iimarishwe na iwe na nguvu kuliko mtu mmoja mmoja. Executive iwe checked sana, tofauti na sasa ambapo kivitendo bunge na mahakama haviwezi kuishughulikia Executive. Na hatujui ni nani atakuja baada ya JK, akiwa nduli itakuwa taabu sana,

Wanaosema kuwa itakuwa hatari kama rais akipunguziwa madaraka ni vizri waseme ni hatari gani, na mi vizuri waseme kama kutakuwa na utaratibu wa kumfanya rais awe mzalendo kama Nyerere ili tumuamini na maraka makubwa namna hiyo.
 
Nguruvi3,

Karibu sana katika mjadala; umezungumza mengi ya msingi, hasa tuendako, na kimsingi nakubaliana na wewe; Lakini haujagusia sana tulipotoka, hasa kwanini ilikuwa ni muhimu kuwa na mfumo huu wa sasa Kikatiba katika awamu ya kwanza, hasa iwapo kulikuwa na haja, haja hiyo imetimizwa na iwapo kuna haja au hakuna tena haja ya suala husika katika nyakati za sasa;

Ushauri wako unaoendana na kuunga mkono hoja ya kupunguza madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba ni mzuri. Nia yangu mimi sio kupingana na kundi hili la hoja bali kujaribu kujadili pande zote mbili za hoja objectively ili huko mbeleni tukija fanya maamuzi basi itokee baada yak u digest na ku exhaust factors na variables mbalimbali badala ya kuja kujuta; I still maintain kwamba pamoja na umuhimu wa kupunguza madaraka husika, lakini bila ya kuwa waangalifu, tutajikuta na nchi isiyotawalika kwani I still believe kwamba if power is in the right hands, hasa katika masuala muhimu kwa taifa, maamuzi yataweza kufanyika haraka sana tofauti na iwapo powers kadhaa muhimu zitakuwa delegated kwenye organs nyingine;

Kuna baadhi ya maamuzi kwa kweli ni muhimu yafanywe kwa haraka na Rais, na hayana haja ya kusubiria vikao vya bunge; Vinginevyo bunge ni muhimu pia kushirikishwa na hili linaweza kufanyika kupitia kupitia kamati husika za bunge ambazo zinaweza kushauri the executive branch juu ya maamuzi Fulani kasha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi husika kwa haraka; Bottom line ni kwamba - kuna baadhi ya maeneo ambayo ni muhimu yapunguzwe, lakini mengine ni muhimu yaachwe kama yalivyo LAKINI yadhibitiwe kikamilifu chini ya Katiba Mpya, hasa kwa kulipa bunge uwanja mkubwa zaidi katika maamuzi na uongozi wa nchi;

Ni lazima tuseme ukweli kwamba kinachoudhi watanzania wengi na kupelekea vilio vyao vingi juu ya umuhimu wa madaraka ya rais kupunguzwa (tofauti na awamu zilizopita) ni sababu mbili – kwanza ni mchakato unaotumika kuteua watu mbalimbali pamoja na ubora wa wateule husika; Pili, ni kumekuwepo na ucheleweshaji wa maamuzi muhimu lakini pia ukimya wa taasisi ya Urais juu ya matukio na maendeleo mbalimbali katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii, masuala ambayo yameathiri sana wananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii; Lakini cha ajabu ni kwamba, tatizo hili limejitokeza sio kwa sababu Rais hana such Powers, bali ni kutokana na kitendo chake cha kutozitumia ipasavyo (aidha kwa nia nzuri au kwa bahati mbaya, jibu sio straight forward katika hili), lakini pia kwa kuachia political reforms zije more radically kuliko awamu za nyuma; Vilevile ni kutokana na factions ndani ya CCM ambazo zimeua kabisa dhana kwamba Rais ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM is SUPREME Kwa kila kitu kuanzia Bunge, Mahakama, na Hata Katiba ya JMT (1977); Kwa bahati mbaya na kwa sababu zisizo wazi sana nguvu juu ya vyombo hivi zimehamia kwa kiasi fulani Chadema, lakini zaidi mikononi mwa watu wengine (sio taasisi) informally and unconstitutionally;

Naomba kusikia mawazo yako kama nilivyoainisha kwenye paragraph ya kwanza hapo juu;
Mchambuzi, labda niseme kuwa mazingira yaliyokuwepo awamu ya kwanza ni tofauti na sasa kwa kiasi kikubwa.

Utakumbuka kati ya 1960 na 1985 mapinduzi yalikuwa ni mambo ya kawaida Afrika. Hayo yalitokana na excitement na matarajio ya uhuru. Kutokana na political instability viongozi wa nchi hizo wakajilimbikizia madaraka ili kuwa na udhibiti.

Lakini pia kiwango cha ufahamu na uelewa wa kilikuwa kidogo sana.
Huko Bungeni walikwenda watu ambao elimu zao na uwezo wao hakuruhusu wapewe sehemu kubwa ya utawala wa nchi.
Pamoja na hayo kulikuwa na umuhimu wa kujenga taifa kwa umoja kwa kuwa na kiongozi atakayewaunganisha wananchi ili wasigawanywe na euphori, excitement na ''utopia'' za uhuru

Mazingira hayo sasa hayapo tena, tunapaswa tuangalie utaratibu mwingine.
Mazingira yaliyopo yanatulazimisha kufanya hivyo kwasababu miaka 50 ni mingi na tumejifunza sana.
Uwepo wa awamu nne umetusaidia sana kutambua wapi tumekwama na kwanini.
Kama tungekuwa tumefanikiwa ndani ya miaka 50 sioni hiyo kama hii ingekuwa hoja.

Pili, Kumpunguzia nguvu rais kunapelekea kuwa na maamuzi ya haraka sana kuliko ilivyo sasa.
Wananchi wanatakiwa waamue hatima ya maisha yao pale walipo na si Dodoma au Dar es Salaam.

Ni rahisi wananchi wa Korogwe chini ya viongozi wao waliowachagua na kuwajibika kwao kufanya maamuzi muhimu kuliko kusubiri bureacracy ya mkurugenzi, mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Katibu mkuu, Waziri ambao hawawezi kufanya maamuzi kuchelea kumuudhi mzee. Ndio maana mkuu wa wilaya anajiuliza atangaze janga la njaa au la!

Kwa nchi kama Marekani, magavana ndio wanawajibika kwa watu wao.
Gavana Christie wa New Jersy ndiye anayehangaika na kujenga jimbo lake baada ya kimbunga.

Obama alishiriki mwanzoni pale ambapo federal level intervention ilihitajika.
Sasa anashughulika na masuala makubwa ya kitaifa na si kimbunga Sandy

Ninaposema apunguziwe madaraka hii haina maana kuwa aondolewe ''executive power''.
Marekani bado Obama ana Veto hata kama Senate na Congress wameamua jambo.

Kinachofanyika ni kuwa Veto hiyo aiutumie kwa maana iliyokusudiwa kwasababu kinyume chake Senate na Congress wanaweza kumrudi. Check and Balance.

Kumpunguzi madaraka rais ni kumuondolea kazi ambazo zinaweza kufanywa kwa ufanisi na idara au taasisi nyingine.
Hii haina maana kulundika madaraka katika bunge, la hasha!

kuna state Organs zingine zinapaswa kufanya kazi zenyewe.
Mfano, Mkuu wa Upelelezi, Takukuru, mashitaka, CAG n.k hawa hawapaswi kuwajibika kwa rais.

Kwa vile wanawajibika kwa rais kwa wakati huu, Rais anahusishwa na utoroshaji wa nyara, pembe na wanyama achilia mbali madini. Kilichotakiwa ni kuwa rais alipaswa kuwa observer wakati hatua zinachukuliwa na kuingilia tu pale ambapo masilahi ya taifa zima yanapoingia matatani.

Kumpunguzia madaraka ni kuacha mihimili mingine ifanye kazi bila kuingiliwa.
Mahakama iwe na majukumu yake kama ilivyo bunge.
Huko bungeni kunatakiwa kuwe na utaratibu utakaohakikisha kuwa hakuna political filbuster katika masuala muhimu ya kitaifa.

Kinachonisukuma niunge mkono hoja ya kupunguza nguvu.
kwanza ni ''play book' ya miaka 50 na viongozi tofauti.
Ninaamini kuwa hutuwezi kuishi kwa kusubiri azaliwe kiongozi mwadailifu for power to be on the right hand.
Hapa itakuwa gambling yenye risk kwasababu historia hujirudia na miaka 50 tunaweza kuwa hapa tulipo leo.

Pili, mifano ya nchi kama Marekani, India, Uingereza na Japan inanifanya niamini kuwa check and balance ni jambo muhimu sana na kwamba lazima kila state organ au institution iwe watch dog wa mwenzake.

Japan imekuwa na mawaziri wakuu 7 katika kipindi cha miaka 5.
Kwa vile mfumo wao umejengwa katika taasisi na si mtu au watu Japan inasonga mbele kila siku kana kwamba hakuna tatizo. Wao wametengeneza mfumo kwamba, kiongozi akiingia ofisini kuna ABCD za kufanya.
Akiacha kazi mwingine ataendelea alipofikia. Hii ni kwasababu ya kuwa na independent organs as opposed na sisi ambapo PM kujiuzulu tu nchi ilitetemeka.

India, hii iliwahi kuendeshwa bila waziri mkuu kwa miezi 3, nothing happened na maisha yaliendelea hadi walipopata ufumbuzi wa tatizo lao la uchaguzi. Sababu kubwa ni kuwa uongozi wa nchi upo katika taasisi na si mtu mmoja.
Kwamba madaraka ya nchi yamegwawanywa na si kurundikwa kama fungu la nyanya kwa mtu mmoja.

Uingereza, taifa kubwa na muhimu sana katika siasa za dunia iliwahi kukaa bila PM kwa wiki nzima.
Kuna mtu alikuwa London wala hakujua kuwa nchi haina PM. Hii ni kwasababu udhibiti wa nchi upo katika sehemu mbali mbali na muhimu katika mgawanyo maalumu na si 10 Downing street peke yake.

Nimalize kwa kusema sababu zilizokuwepo kwasasa hazina mantiki.
Nadhani kundi linalosema rais alundikiwe madaraka lina hofu kubwa isiyo na sababu.
Hofu ya kuwa nchi ni Rais na si uongozi.
Mimi naamini wakati umefika tujitahmini na kuchukua mwelekeo mpya, miaka 50 ni mingi sana kusubiri.
 
Mgaya D.W, Muchetz, tubadilike-sasa, nguruvi3, bobuk, bongolander,

Kwa mtazamo wenu, kwa kuzingatia hoja kwamba tumpunguzie rais madaraka katika katiba mpya, je hatua hii iendane na mfumo gani wa utawala ndani ya Katiba mpya, je - Presidential form of government au Parliamentary form of government?

Kwa Tanzania Parliamentary System ni Majanga.Ni ukweli usiofichika kuwa our parliament is full of useless figures.No disrespect to Prof.Majimarefu et.al,but such kinds of figures are just filling empty chairs.

Presidential form of government is a bit better at the moment until we reach a level where Tanzanians understands why they elect MP's and what caliber an MP should have/be.

Pamoja na Madhaifu yake yooote, Kikwete na taasisi nzima ya Uraisi is miles ahead better than our parliament collectively.We do have few probably a handful brilliant MP's thats about it.Ukiona Rais inabidi ateue mtu kuwa mbunge ili kujazia baraza la mawaziri, jua kuna tatizo kubwa, ukiona the likes of Mulugo and such wanakuwa mawaziri jua kuna tatizo kubwa kuliko.

With the way votes are conducted in our parliament,i wouldn't want those empty heads to decide if the country goes to war or not. Am sure if the malawi issue was put up to the parliament to decide,we would long be in war by now.WHY?because in our parliament a few noisy MP's influence the rest who just follow the beat.
 
Ni mchanganuo mzuri sana ila tatizo ni kuwa umeelekeza na kujikita kwenye fikra na utendaji ulioshindwa au kushindikana

1. Uchaguzi uliopita rais aliyeko madarakani alimtuma mwanae kumkusanyia "approvals za chama" na alipozipata alifanya kampeni ya bmw kwa vile URAIS WAKE HAUNA UBIA. Tafsiri ni kuwa urais ni wake na nchi na vote vilivyomo ni vyake atafanya anavyotaka.

2. Kisaikologia na kisoshologia wanadamu tunaishi kwa maelewano na makubaliano hasa kuhusu namna ya "kuongozana/kutawalana?" Inapofikia mtu mwenye madaraka kama ya urais haelewi nafasi yake kwa jamii (ustawi), ndiyo tunafikia kudorora kwa uchumi na kutokujua cha kufanya kama sasa.

3. Madaraka yanapotumika kama hisani kwa washikaji ni kukengeuka kwa dhana nzima ya utawala taifa linakosa mwelekeo "orientatio".

Mimi nadhani turudi kwenye misingi ya kujitawala

1. Hatukumuondoa mkoloni/mtawala mzungu na kumweka mkoloni/mtawala muafrika.

2. Tulitaka uhuru wa uchumi ili wanachi wetu waishi maisha mazuri.

3. Tulikuwa tunathamini sana utu wetu na tamaduni zetu na tulipata fursa za kujitawala ili zidumishwe kwa manufaa yetu sote.

Kwa kukengeuka kutokana na taratibu "zilizoporwa na wajanja)siyo waadilifu)

1. Misaada tuliyopewa imeamuriwa na kutafunwa na wajanja(siyo waadilifu)

2. Tumeingiza itikadi ya UJANJA KUPATA badala ya itikadi ya kulitumikia taifa kwa manufaa ya kupata wote.

3. Tumeandika makaratasi mengi juu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hata miradi ya kiujana ujanja kuhalalisha wizi/ufisadi huku tunajiuliza kwani imekuwaje hatujapata tulichotarajia.

Balozi Sefue

1. Haendani ni "reality on the ground" na historia. Tanzania ya sasa imenyimwa elimu ya msingi juu ya utaifa kutokana na watawala kutawala kwa mtaji wa ujinga huo na madaraka yasiyo na njia ya kusimamiwa kwa sababu ya ubovu wa katiba.

2. Umasikini unatofautiana sana. Viongozi/watawala wetu wana umasikini wa mawazo na kama hawana umasikini basi ni wavivu wa kufikiri wasiokaribisha mawazo yenye changamoto kwa sababu ya ubovu wa katiba.

3. Wemetumia sana hayo mawili juu kupora haki za msingi za wananchi na kujibinafsishia maamuzi juu ya maisha ya watu wengine (ubovu wa katiba).

4. Wamekuwa na jitihada za kushika madaraka bila kuyaachia ili mbadala wa utawala ukose fursa ya kuwawajibisha.

5 Wenye nafasi zao kama huyu Katibu Mkuu Kiongozi yeye yuko karibu la waridi hajui mvua, jua wala harufu ya mvundo kwake yeye kila kitu shwari (ndiyo maana hata muda wao unapoisha wanajiongezea muda kwa kanuni na sheria za hovyo) kwa sababu ya ubovu wa katiba.

Hitimisho

Urais kwa sisi wengine ni utumishi ndani ya mfumo unaokubalika na sisi sote. Lakini Rais si malaika anahitaji checks and balances, ana limitations za kibinadamu zenye ukomo. Majukumu ya kitaasisi ya urais yana watu wabaya na wazuri kwa nchi yao. Ni vizuri rais asipewe madaraka mengi asiyoyamudu kama huyu wa sasa, na aliyepita akabinafsisha rasilmali nyingi za taifa, au hata chama tawala kushindwa kumudu wajibu wake wa kisiasa hadi umaarufu unaporomoka.

Mimi ningependa madaraka ya rais yawe yale tu anayoweza kuyamudu na mengi mengine yasimamiwe kwa uhuru na wawakilishi kama nchi nyingi zinazosonga mbele zinavyofanya.

Sifue "amebugi" hoja yake haina uhalisia amefikia ukomo wa kufikiri kwa rais wa sasa na haoni rais wake alivyomtata kwa kushindwa kumudu madaraka.
 
Back
Top Bottom