Balozi Seif Ally Iddi; Leo kutakuwa na tamasha la taarabu kwa wageni waalikwa wa sherehe za mapinduzi.

Balozi Seif Ally Iddi; Leo kutakuwa na tamasha la taarabu kwa wageni waalikwa wa sherehe za mapinduzi.

Kwani taarabu wewe unaichukuliaje!??
 
Nikwamba nimesikia vibaya ama ni halisi kile alichokisema Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally kuwa leo kutakuwa na tamasha maalumu la taarabu kwa wageni wa sherehe za mapinduzi.?

Hivi limekaaje hili wakuu, ni taarabu vidole juu ama ni aina tofauti ya taarabu wakuu.
Kama ni hivi basi tuna Safari ndefu sana watanzani, inamaana hawakuona burudani nyingine zaidi ya taarabu?

Nani katoa hili wazo??

Kumbe ndo mana namuona mkwele kaenda na bi mkubwa!!

Haya kila la kheri kwenye vidole juu.
Sisi tutakuwa ma DJ hapa JF na wapiga picha na majaji wa kutaja yupi amekuwa bingwa wa kulisakata.

Watch....

Hiyo vidole juu ni morden taarabu na iko bara kule Zanzibar kuna taarabu asilia na ndio muziki wao

Ni kama ushangae rais wa Congo kusema kuna muziki wa rhumba kwa wageni
 
Labda mkuu wewe ndio hujui taarab! Zanzibar taarab sio vidole juu kama bara, kule watu huketi na waimbaji huketi pia isipokua yule anae ghani mashairi ! Ni burudani sana hata marehemu Omar Ali Juma akipenda sana enzi hizo...Mambo ya vidole juu na kuchambana sijui kumwaga radhi ni huku bara kwa mashangingi na masakambwanga! Kule wastaarabu wana swing tu miili wakiwa wameketi raha mustarehe wakifuatilia maudhui murua ya mashairi ! Elewa mkuu !
Hivi ile Televisheni ya Zanzibar ipo siku hizi?

Nakumbuka miaka ya themanini tulikuwa tunaangalia taarab TVZ.

Ni kitu tofauti kabisa na hii taarab ya mipasho ya siku hizi.

Taarab ya asili Zanzibar ni muziki wa kuheshimika sana. Na ndiyo maana hata sherehe kubwa kama hii watu wanataja taarab.

Huu ni kama muziki wa Zanzibar.

Nakumbuka mahojiano fulani alifanyiwa Dr. Salim Ahmed Salim, katika kumuonesha kuwa ni mtu anayependa asili yake, wakasema, licha ya kuzunguka dunia nzima, lakini muziki alioupenda zaidi ulikuwa taarab.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TVZ bado Hua inaonesha taarab isipokua kipindi kifupi si kama zamani, maana kwa sasa mambo ni mengi sana ya kureport kwa TV.
 
Hakuna burudani nyingine zaidi ya taarabu tena kwenye tukio kubwa la kitaifa Kama hili.
Taarab ndio utamaduni wao visiwani, kabla mimi na wewe hatujazaliwa.

Haya masuala ya kisasa hayana ulazima kuwa ni ya muhimu kwa wenyeji wa visiwa hivyo.
 
Labda mkuu wewe ndio hujui taarab! Zanzibar taarab sio vidole juu kama bara, kule watu huketi na waimbaji huketi pia isipokua yule anae ghani mashairi ! Ni burudani sana hata marehemu Omar Ali Juma akipenda sana enzi hizo...Mambo ya vidole juu na kuchambana sijui kumwaga radhi ni huku bara kwa mashangingi na masakambwanga! Kule wastaarabu wana swing tu miili wakiwa wameketi raha mustarehe wakifuatilia maudhui murua ya mashairi ! Elewa mkuu !
Nadhani ni vema ulivotoa huo ufafanuzi hapo.
Kuchambana ndio nini mkuu.?
 
Mleta mada umekurupuka nadhani umevimbiwa kiporo.
Tukiacha mambo ya ccm na cuf/chadema, taarabu ina shida gani? Ni mziki tena ambao ni kama unaitambulisha Zanzibar sasa tatizo liko wapi wageni wakipatiwa burudani na watu wa Zanzibar? Au ulitaka mchana kutwa na usiku kucha wajadili mapinduzi tu??????
Kwani kuna sehemu nilitaja ccm na cuf hapo mkuu.
 
Hiyo vidole juu ni morden taarabu na iko bara kule Zanzibar kuna taarabu asilia na ndio muziki wao

Ni kama ushangae rais wa Congo kusema kuna muziki wa rhumba kwa wageni
Kwani hiyo modern taarab ilianzia wapi mkuu hadi useme huko Zanzibar haipo.?
 
Nadhani ni vema ulivotoa huo ufafanuzi hapo.
Kuchambana ndio nini mkuu.?
Ahaa ! Kumchamba mtu ni pale wanawake hasa wa pwani kuenda kumsema mwenzao ambaye ni muongo au mfitini ili akome! Tendo hili hufanywa mbele ya halaiki au kadamnasi ya watu. Wakati mwingine wachambaji hupendelea kuvaa nguo aina ya dira sare sare na kibwebwe kiunoni ili kukoleza mambo ! Mchambwaji Hua hapewi hata nafasi ya kujitetea na anaweza kusingwa vile vile. Inasemekana kabila la wazaramo ndio wataalam wa kuchamba maana huweza kumchamba mwenzao mpaka akazimia bila hata kuguswa! 😁 Nadhani nimefafanua vya kutosha.😎
 
Back
Top Bottom