Hivi ile Televisheni ya Zanzibar ipo siku hizi?
Nakumbuka miaka ya themanini tulikuwa tunaangalia taarab TVZ.
Ni kitu tofauti kabisa na hii taarab ya mipasho ya siku hizi.
Taarab ya asili Zanzibar ni muziki wa kuheshimika sana. Na ndiyo maana hata sherehe kubwa kama hii watu wanataja taarab.
Huu ni kama muziki wa Zanzibar.
Nakumbuka mahojiano fulani alifanyiwa Dr. Salim Ahmed Salim, katika kumuonesha kuwa ni mtu anayependa asili yake, wakasema, licha ya kuzunguka dunia nzima, lakini muziki alioupenda zaidi ulikuwa taarab.
Sent using
Jamii Forums mobile app