Balozi Ujerumani kushuhudia michezo Jumuishi kwenye Viwanja vya Filbert Bay, Novemba 25, 2024

Balozi Ujerumani kushuhudia michezo Jumuishi kwenye Viwanja vya Filbert Bay, Novemba 25, 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
BALOZI wa Ujerumani Nchini Tanzania, Thomas Terstegen anatarajia kushuhudia michezo jumuishi itakayoshirikisha vijana zaidi ya 45, michezo itakayofanyika Novemba 25, 2024 kwenye Viwanja vya Filbert Bay, Kibaha Mkoani Pwani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays balozi huyo atasindikizwa na Mjumbe wa Kamati ya Olimpiki ya Ujerumani, Tomas Anton na viongozi wengine wa michezo wa ndani na nje ya nchi.
Thomas Terstegen.png
Rays alisema watendaji hao watashuhudia michezo jumuishi kwa michezo mitatu ikiwemo soka, Volleyball na Basketball.

Alisema kwenye Soka, timu ya vijana ya Azam FC itaoneshana kazi na timu mchanganyiko ya SOT.

Rays alisema ushuhudiaji huo wa michezo umekuja baada ya mafunzo kwa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Arusha ambako makocha na walimu walipatiwa mafunzo kupitia mradi wa michzo Jumuishi kupitia Kamati ya Olimpiki Ujerumani (DOSB) na Lions Club Ulaya.

Alisema mbali ya mradi huo kufanyika Tanzania pia ulifanyika Kenya, Burundi na Uganda.
 
Back
Top Bottom