Balozi wa Denmark nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Mette Nørgaard Dissing-Spandet aitembelea JamiiForums

Huwa najaribu kuangalia forums nyingine huko Duniani ila nakiri JamiiForums ni home of great thinker na ni best of the best mimi nawaambia bongo tuna akili za mbele sana sema tunashindwa zitumia tu.

Yaani endapo tukiwa serious tutafika mbali hili jukwaa ni zaidi ya World Enclopedia yaani kila kitu kishajadiliwa na kina maoni kwa angles tofautitofauti na kuna mengine chanzo ni humu tu hutakuta pahali pengine Duniani,
Artificial intelligence ikifika kwenye peak watu wakitaka info kuhusu mambo mbali mbali lazima itakuja kua Moja ya source mhimu!
 
Kiingereza chako na cha Kiranga ndicho kilinivutia kujiunga na JF 2014.

Na hoja zenu pia zilikuwa murua sana.
 
Tunafurahi kuona wageni wameona kitu kwenye taasisi hii ya Jamii Forums, ndio maana safari za kuitembelea kwa ajili ya kujifunza , kupongeza, kitia moyo na kuwezesha zimekuwa nyingi.

Ni bahati mbaya sheria na kanuni za nchi yetu zimekuwa sio rafiki sana lakini ungekuwa ni mtandao mkubwa sana hapa Afrika na nje ya afrika pia.

Siasa na wanasiasa wamekuwa sos ya kurudisha nyuma jitihada za wabunifu wengi yote kwa maslahi ya kisiasa kwa kivuli cha maadili ya jamii na usalama wa taifa.

Miaka karibu 20 ya Jf kama sio misukosuko ya kisheria mahali ingekuwa imefika Jf pangekuwa si haba.
Hata hivyo pongezi kwako Maxence Melo najua jitihada hazizidi kudra, umejitahidi mno, lakini kwa kudra za Mungu kuna sehemu umefika ukikaa ukiangalia nyuma na ulipo sana kisha ukatazama mbele hutaacha kusema asante Mungu, nami binafsi nakutakia kufanikiwa juu ya matarajio yako.

Ombi langu unapoelekea mwaka wa 20 fanya kitu, pia usiwasahau wale wanachama walioanza nawe Ambao wengi wao bado wapo wala uwaambie asante kwa majina yao hata kama wengine hawapo , au wametangulia lakini asante yako itakuwa zawadi kubwa sana kwao .
 
Hahaha, mkuu!

Sio wote wanahusika na platform management.

Kuna programu 8, ya platform hii ni mojawapo. Wengine wapo kwenye programu nyingine mbalimbali
Kiukweli hao mabinti wawiwili mkono wa kulia hasa huyo wa pili kutoka kulia kwakweli ndio hunifanya nifungue haraka thread za wageni wanao tembelea jf ili nijue kama yupo na anaendeleaje! Huyo ndio atanifanya siku moja niitembelee jf!😂😂😂😂😂
 
Ni faraja kuona mabalozi wanajali kazi mnayoifanya.

Hivi Ubalozi wa Denmark Tanzania bado upo katika mchakato wa kufungwa? Kuna wakati walisema wanataka kufunga ubalozi.
Hatutashangaa na siajabu hata hatutaelezwa kinachoendelea.
This is Bongo. A typical banana republic!
 
Deservedly. Why not?! It's mind opening, free speech and yes an education platform ever founded in TZ. Kudos JamiiForums
 
Mi naomba nisiwe MUONGO.Nimeona wagfanya kazi wengi tu, Lakini naomba kujuzwa, Jamiiforums wanafanya kazi gani hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…