Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Libya....haikua nchi huru?Kuliko kutumia muda mwingi kuchangia vitu huvijui, angalau soma kidogo kuhusu Sheria za kimataifa itakusaidia zaidi. Nchi huru zina haki na mamlaka zake, ikiwa ni mamlaka ya kujiamulia mambo yake.
Pro liberarist hawaKwaiyo Libya hakukuwa na sheria za kimaitafa, Syria, Iraq, Yemen je, hakuna izo sheria ila sheria isome leo kisa Russia kafanya sio?
Ww ndo uache ubwege, halafu uyo barozi mwambie Al Shabab wanataka kumega kule juu upande wa Kenya uwe Somalia tuone atasemaje?
Njaa inawaponza Sana ndugu zetu hawaHuyo balozi wa Kenya alikuwa hajamaliza chuo kweli wakati Kossovo inamegwa na umegaji huo kufanyika bila UN/US kukemea?
Au Belgrade ilivyovulumishwa mizinga bila kufuata sheria za kimataifa na mauaji yakitekekezeka Yugoslavia ya zamani, balozi huyo alikuwa anaandaa proposal ya dissertation yake?
Hizi 'guts' za balozi zilikosekanaje wakati Libya inaharibiwa territory yake na Mabomu ya NATO bila idhini ya UN?
Nashauri, balozi apitie historia kwanza.
Walete mkono kama wanabisha[emoji23][emoji23][emoji23]Baada ya kuwapima USA EU UN kaona hawamuwezi kichawi.....kijesh.....na kiuchumi
Putin amenogewa naona sasaivi ameomba idhini ya bunge kuruhusu jeshi lifanye kazi nje ya nchi na amekubaliwa,lat's stay tuned,many more to come.
UPia naona CHINA hajtoa comment yeyote pale UN
Kabisa mkuu.[emoji1787][emoji1787]kwamba hakikustahili
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kwamba sasa anatambua sehemu ya Ukraine kama Urusi na atatuma wanajeshi wake kuwa walinzi wa amani katika majimbo hayo mawili .
Uingereza ilichukua hatua ya haraka kutangaza vikwazo. Urusi ilikemewa na nchi nyingi zikiwemo Mexico, Ireland, Norway, Ghana, na nyinginezo. Lakini ni Kenya ndio iliyojitokeza kwa makali yake kwa jinsi ilivyojibu hatua hiyo ya Urusi.
Balozi wake kwa Umoja wa Mataifa Martin Kimani alitoa hotuba ambayo wengi wamejitokeza kuisifia kama iliyoeleza kwa urahisi na ukali unaostahiki ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa ambao urusi imetekeleza .
"Uhuru wa eneo na mamlaka ya Ukraine yamevunjwa," alisema Balozi Martin Kimani
"Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaendelea kudhoofika chini ya shambulio hilo lisilo na huruma. Kwa wakati mmoja unatolewa kwa heshima na nchi zile zile ambazo kisha zikaupa kisogo katika kutekeleza malengo yanayopinga amani na usalama.... Kenya inasikitishwa sana na tangazo lililotolewa na Urusi la kutambua maeneo ya Ukraine kama mataifa huru'
Aliendelea kusema kuwa Kenya ina wasiwasi mkubwa juu ya athari ambayo Urusi inaweza kuwa nayo ikiwa itaruhusiwa na UN kushambulia na kunyakua nchi zingine.
Mfano wake ni kwamba mipaka ya Afrika ilikubaliwa na nchi zote za huko, licha ya mipaka hiyo kulazimishwa na wakoloni. Alieleza kuwa mataifa ya Afrika yalifanya uamuzi huo badala ya kuwa na vita visivyoisha.
"Tulikataa upanuzi kwa misingi yoyote, ikiwa ni pamoja na rangi, kabila, au kitamaduni," Kimani alisema. "
Baada ya hotuba yake hiyo ,maoni yalianza kutolewa huku akisifiwa kwa hotuba yake hiyo .Watumiaji wa mitandao ya kijamii walituma jumbe za kuonyesha 'makali' ya ujumbe wake na jinsi Kimani alivyojieleza na kuwakilisha msimamo wa kenya kuhusu hatua ya Urusi ;
Balozi Martin Kimani ni nani?
Balozi kimani aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa mataifa mwaka wa 2020 .
Kabla ya uteuzi wake wa hivi punde zaidi, Bw. Kimani alikuwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Kukabiliana na Itikadi kali na Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi nchini Kenya kuanzia Septemba 2015.
Pia aliwahi kuwa Katibu wa Mikakati katika Ofisi ya Mtendaji wa Rais kuanzia Disemba 2018.
Bw. Kimani alikuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa huko Nairobi, Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Makazi (UN-Habitat) kati ya Desemba 2012 na Septemba 2015.
Mapema katika taaluma yake, Bw. Kimani alikuwa Mkurugenzi katika Mamlaka ya Kiserikali juu ya Maendeleo (IGAD) nchini Ethiopia, kuanzia Aprili 2011 hadi Disemba 2012.
Bw. Kimani alipata PhD na shahada ya uzamili katika masomo ya vita katika Chuo cha King's College, Chuo Kikuu cha London, mwaka wa 2010 na 2003, mtawalia, na pia shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha New Hampshire mwaka wa 1996
Source bbc swahili
Je ....kiutalaamu hili limekaaje ....au ni sawa na sisimizi kumpiga biti tembo[emoji23][emoji23]
View attachment 2127616
Wew nae hujui kitu, hizo sheria za kimataifa na hayo makundi ya jumuiya za kimataifa kwa taarifa yako, hawa wote ni machawa wa Umagharibi+USA kwaiyo agenda yoyote ktk jumuiya hizo zilishabarikiwa na wamagharibi+USA kuwa sheria&kanuni zitafanya kazi kulingana na matakwa ya wao wanavyopenda haijarishi ni muda gan.Kuliko kutumia muda mwingi kuchangia vitu huvijui, angalau soma kidogo kuhusu Sheria za kimataifa itakusaidia zaidi. Nchi huru zina haki na mamlaka zake, ikiwa ni mamlaka ya kujiamulia mambo yake.
Huwa napata taabu Sana kutofautisha ....majukumu ya USA na UN kwny world affairsThose puppets leaders na machawa wa USA lazma waunge mkono na kumshambulia Russia
Huko palestina, wamarekani walipora ardhi kibabe na kuikabidhi kwa matapeli wenzao hao wayahudi wa uongo, and no one cared, yaan hata UN ilibariki ili jambo as if lilikuwa zuri.
Sas Russia anapojaribu nae kujimilikisha ardhi anazodai zake, why mumuandame kiasi hicho?
Siasa za dunia ni hovyo sana yaan