Mimi siwezi kumtetea chochote yeyote nje ya Tanzania. Kila nchi ina mipango yake na maslahi yake.
Lakini siyo kweli kuhusu hilo la Ukraine. Inaonyesha hufuatilii taarifa kuhusu swala hilo. Misaada aliyo pewa Ukraine hadi wakati huu kutoka Marekani huwezi kamwe kuibeza. Ni mamia ya mabilioni ya dollar. Kwa hiyo siyo kweli kusema Mmarekani hasemi chochote.
Na inaonyesha kuwa huna hata ABC kabisa za mkasa huo wa Ukraine, na kinacho piganiwa hasa ni nini.
Hili la kwetu,... acha tu; sioni sababu ya wao kujiingiza kwa maana sioni kuwa wanao msaada wowote mbali tu ya kupiga kelele.
Lakini ukweli ni kwamba huyu mama yenu huenda safari hii atatuvusha na kutuingiza ngazi ambayo bado hatujawahi kuifikia kama taifa.