Balozi wa Marekani: Kwa Miaka 3 Marekani imetoa msaada Tanzania Dola Bilioni 7.5 sawa na Trilioni 25 za Tanzania. Sio Mkopo ni Msaada tu

Balozi wa Marekani: Kwa Miaka 3 Marekani imetoa msaada Tanzania Dola Bilioni 7.5 sawa na Trilioni 25 za Tanzania. Sio Mkopo ni Msaada tu

Mimi mwenyeji wa Ngara Kagera lakini sina hulka za kibaguzi. Kwanini vitambulisho vya kununua ardhi vionekane muhimu wakati wa awamu inayoongozwa na Samia mwenyeji wa Kizimkazi?.

Wakati wa Magu uliomba hivyo vitambulisho?. Hulka zile zile za visasi na za kibaguzi.
Acha uongo wewe ni UWT upo mjini magharibi, hakuna mtu mjinga Kagera/bara kama wewe
 
C
Mama ana nguruma hadharani akitoka, anatuma wasaidizi wake wakimbie haraka balozini wakatafsiri alichomaanisha..... kuwa wasim quote vibaya yeye ni muasisi na pioneer wa rrrr na ndio maana bado Chadema ipo kwenye payroll ya serikali ..kwakweli kwa uduchu wakodi zetu siku misaada ikikoma ni lazima tuite maji mma........
Cdm wanalipwa na serikali kwa kazi ipi wanafanya?? Matumizi mabaya ya hela za walipa kodi
 
kwahiyo alikua anahitaji sifa, alikua anahitaji kuabudiwa na kupigiwa makofi?

au kuna siku au mahali nchi yake ililazimishwa kuleta misaada Tanzania na kwengineko duniani?🐒

au ni kimbelembele tu na kutaka sifa za kijinga?🤣
Walileta tu au baada ya kutembeza bakuli kenge wewe 😄 🤣 😂 ile hospital ya Dareja na Hydom ulijenga wewe
 
Mbona Magufuli alikuwa anasema kutwa , hakuna lolote msaada sio lazima ...Wangeacha tungeishi maana hata pesa wanaprint wao ....Hatuwezi kufa njaa ng'o hizo pesa wanakula wachache .

Ukweli ni kwamba hwana ubavu wa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yoyote hatutaki machafuko ....Afrika inaweza kuwepo bila ya hao , wanaimarisha uhusiano tu ...Huko kwao kuna homeless si wafute umaskini usome zero .! watu ambao wanafadhili mpaka vita ili wengine wauawe.
Mnakufaa njaa vizuri tu bila misaada unajua impact ya trillion 25?! Kama hujui Tanzania pesa za miradi zote ni za wafadhili na madafu yetu yanaishia kwenye kulipana mishahara
 
"Mabeberu" wametupa pesa nyingi sana!
 
Mimi siwezi kumtetea chochote yeyote nje ya Tanzania. Kila nchi ina mipango yake na maslahi yake.

Lakini siyo kweli kuhusu hilo la Ukraine. Inaonyesha hufuatilii taarifa kuhusu swala hilo. Misaada aliyo pewa Ukraine hadi wakati huu kutoka Marekani huwezi kamwe kuibeza. Ni mamia ya mabilioni ya dollar. Kwa hiyo siyo kweli kusema Mmarekani hasemi chochote.
Na inaonyesha kuwa huna hata ABC kabisa za mkasa huo wa Ukraine, na kinacho piganiwa hasa ni nini.

Hili la kwetu,... acha tu; sioni sababu ya wao kujiingiza kwa maana sioni kuwa wanao msaada wowote mbali tu ya kupiga kelele.
Lakini ukweli ni kwamba huyu mama yenu huenda safari hii atatuvusha na kutuingiza ngazi ambayo bado hatujawahi kuifikia kama taifa.
Kila Rais husakamwa anapokuwa ikulu na husifiwa anapoondoka ikulu. Kuna mamia ya viwanda vinaendelea kujengwa muda huu na vitakuja kusaidia katika kupambana na tatizo kubwa la ajira ndani ya miaka miwili au mitatu ijayo.

Nilisoma chuo kikuu Ukraine miaka ya 90 katikati naijua na najua siasa ya USA ya kutumia CNN na vyombo vyake vya propaganda katika kujipa maujiko siku zote.

Mmarekani anastahili kunyooshewa vidole sawa na anavyooshea mataifa mengine.
 
Hii misaada yao ndiyo inawapa kiburi cha kutukoromea utafikiri sisi ni makoloni yao.
Ni wakati muafaka wa kujielekeza GLOBAL SOUTH ili tuondokane na Hegemony ya mabeberu.
 
Kila Rais husakamwa anapokuwa ikulu na husifiwa anapoondoka ikulu. Kuna mamia ya viwanda vinaendelea kujengwa muda huu na vitakuja kusaidia katika kupambana na tatizo kubwa la ajira ndani ya miaka miwili au mitatu ijayo.

Nilisoma chuo kikuu Ukraine miaka ya 90 katikati naijua na najua siasa ya USA ya kutumia CNN na vyombo vyake vya propaganda katika kujipa maujiko siku zote.

Mmarekani anastahili kunyooshewa vidole sawa na anavyooshea mataifa mengine.
"Viwanda" ndivyo viwe gharama ya maisha ya waTanzania? Hoja yako hapa inakushusha daraja. Kulalamikiwa uongozi/rais hakujawahi kufikia kiwango hiki na kwa mambo mengi mbalimbali kiasi hiki. Samia kashuka sana. Mbaya zaidi, badala ya kuelewa yanayo lalamikiwa, hotuba zake zinazidi kuchochea moto, akidhani kuvimba kwake ndiko kutatia watu hofu.

Ndiyo, Mmarekani anastahili kunyooshewa vidole kwa mengi yanayofanywa nje ya nchi hiyo; lakini hakuna kiongozi aliye thubutu kufanya ujinga ndani ya nchi hiyo akabaki salama kama hawa wa kwetu. Kwa hiyo, hawa wakikoromewa na huyo huyo Mmarekani, pamoja na ubaya wake unao julikana nje, raia wanaonyanyaswa na viongozi wao kama Samia ni lazima washangilie.

Kama umesoma Ukraine, halafu ukaandika yale uliyo andika kule mwanzo, inaonyesha hukujifunza vizuri uhusiano wao na Urusi/Marekani ulivyo geuka kuwa sasa hivi.
 
Hii misaada yao ndiyo inawapa kiburi cha kutukoromea utafikiri sisi ni makoloni yao.
Ni wakati muafaka wa kujielekeza GLOBAL SOUTH ili tuondokane na Hegemony ya mabeberu.
Haisaidii kitu. Huko Global South ndiko wanakotaka ujinga uijnga wanaofanya akina Samia? Wananchi wakichachamaa, hao Global South wataleta jeshi kuja kumsaidia Samia kubaki madarakani kwa nguvu?
 
Huko Marekani walitaka kumuua Trump sababu mpinzani.. and he has audacity lecturing us about mauaji na utekaji
 
Back
Top Bottom