Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani nchini Tanzania: Serikali ihakikishe usalama wa Viongozi wa Upinzani, iwaachie waliokamatwa na kurejesha mawasiliano kwa wananchi

Acha kutisha watu balozi ana majukumu yake mahususi acha kumpakazia fikra zako ni finyu sana unafikiri ujinga hatuwezi kubali wapinzani waharibu amani ya nchi yetu kamwe afu watakao patashida ni watanzania wanyonge ambao hawawezi hata kukimbia
Huu unyonge mnaouzungumza kila uchwao ni upi? Au maana ya unyonge ni kukaa kimya hata pale ambapo mtu anaonewa?

Mitaani wapo watu waliokosa furaha wakilalamika uchaguzi kuhujumiwa kwa kiwango cha kutisha pia wapo wanaoshangilia hivyo tusiwe wasemaji wa wanyonge maana hii kauli yakuwaita watu wanyonge ni kuwadharau.

Unless unipe tafsiri halisi ya mnyonge.
 
Pia tuwe wakweli tu sio kwamba amani tunayohubiri ipo kwa kiwango hicho bali ni kule kuvumiliana tu na ustaraabu wa Watz ndo kunafanya kuonekane kuna amani.

Kama amani ingekuwa ipo kwa kiwango hicho basi pasingekuwa na haja yakumwaga askari kila kona ili mradi kuzuia kinachoitwa vurugu.

Amani kama ipo kwa kiwango kikubwa basi hata hao wachache wanaotaka kuivuruga wangepuuzwa tu na wapenda amani.

Kutapakaa kwa askari barabarani ni kipimo cha kulazimisha amani wakati uhalisia pengine ni kinyume chake.
 
Huu ni ushahidi mwingine huyu ndugu hawezi kutoka madarakani. Huwezi kutoka ikiwa unawaumiza wenzio kwa kiwango hiki. Mf mzuri ni kina Kagame,M7 na Mugabe.
 
Hii yaani hata bila miwani inaonekana kabisa. Ni muhimu sana isambazwe kwenye vyombo vyetu vya habari ili wananchi wote waujue ukweli huu
 
I Wish JPM siku moja avae viatu vya Kambarage na kumtangaza huyu Balozi "Persona non-grata" haiwezekani akawa anaingilia internal affairs za nchi yetu Jambo ambalo lipo against na Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961.
 
Huu upumbavu wa mabalozi wa kibeberu kuachwa tu wakijifaragua na matamko sijui kwa nini nchi za kiafrika huwa hawawachani live!
 
I Wish JPM siku moja avae viatu vya Kambarage na kumtangaza huyu Balozi "Persona non-grata" haiwezekani akawa anaingilia internal affairs za nchi yetu Jambo ambalo lipo against na Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961.
Mtangulizi wake alitolewa hivi hivi huyu nae kanza
 
huu ni ushahidi mwingine huyu ndugu hawezi kutoka madarakani. Huwezi kutoka ikiwa unawaumiza wenzio kwa kiwango hiki. Mf mzuri ni kina Kagame,M7 na Mugabe.
Huyu na genge lake ni mpaka na yeye aumizwe ndio tutaheshimiana
 
Huu upumbavu wa mabalozi wa kibeberu kuachwa tu wakijifaragua na matamko sijui kwa nini nchi za kiafrika huwa hawawachani live!
Wacheni kupeleka bakuli
 
Huko USA wanajeshi wazungu kazi ni kupiga risasi ndugu zetu weusi. Hapo wao wanaona sawa tu?
 
Huenda wakapelekwa mahakamani baada ya JPM kuapishwa.
 
Yeye kama nani yani, kwani hapa ni Marekani!!! Wao wanavofanya targeted arrests kwa blacks!!?? Kila mtu apambane na hali yake, chamsingi aongeze bidii kuhakikisha anawapa ujanja wamarekani wenzake wasolve korona kwa kuiga mfano wetu, mtu yupo nchini free bila barakoa alaf anabwabwaja tu. Watu hawana shukran kabisa
 
Huyu baba hanaga kazi zingine? Kwa Kenya huwaga aanaside na serikali kukandamiza wapinzani kwa Tanzania wanaside na wapinzani dhidi ya serikali. Wamerekani wanafiki sana jamani
Marekani ni Wanafki wa professional level kwelikweli
 
Usijali mdogo mdogo tutalia wote.
CCM hautomjua Wala mpinzani hautomjua wote tutakuwa sawa.
Wapinzani bhana, kwaio mnataka nchi nzima tulie, akili za kiLibya izo, wanaozipandikiza tunawajua.. mshafeli.
 
Kula like 10,000. Alafu utaona mipinzani bado haielewi tu
 
Muulizeni Guantanamo washaifunga au bado ipo? Akijibu hilo mlilete hapa.
Obama alitaka kuifunga kipindi chake kidogo wamtoe roho. Sasa hivi wanahujumiana kwenye kura huko utafikiria ni Banana Republic tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…