Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani nchini Tanzania: Serikali ihakikishe usalama wa Viongozi wa Upinzani, iwaachie waliokamatwa na kurejesha mawasiliano kwa wananchi

Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani nchini Tanzania: Serikali ihakikishe usalama wa Viongozi wa Upinzani, iwaachie waliokamatwa na kurejesha mawasiliano kwa wananchi

Balozi huyo ameandika:

Reports of arrests of opposition leaders are extremely concerning. I urge the Government to ensure the safety and security of all opposition leaders, cease these targeted arrests, release detainees, restore telecommunications, and afford due process under the law to all citizens.

View attachment 1617807
Go and tell your government. Ignorant ambassador
 
Huyu balozi serikali imemuendekeza sana, ni muda muafaka ajue Tz ni nchi huru, wakati hao wajinga wake wanajaribu kutoa matamko ya kuleta vurugu hakusema neno, kuendelea kumuendekeza balozi wa namna hii ataleta matatizo , afanye anachotaka ila hao wajinga wa CDM sheria ichukue mkondo wake, hamna kucheka na ujinga.
Kabisa anajijengea tabia ya kuingilia siasa za Tanzania; huku anajifanya kiziwi kwa matamshi hatari yanayotolewa ya kuvunja amani na hao anaowatetea.
 
Mkuu huoni wao wanatuchokoa? kwao wana uchaguzi, kura za mgombea wao mmoja zinaibwa na kutupwa majalalani, vikundi vya wanamgambo wazungu wenye siraha nzito wapo wanajifua eti wanatetea maslahi ya weupe dhidi ya waafrika na wakuja wengine...polisi wazungu wanakandamiza shingo za weusi na kuwapeleka kuzimu fasta...kuku kwetu ni wanasiasa wenye njaa wanapigania ruzuku tu acha tuwaweke ndani magaidi hawa!
Kabisa kwani viongozi wanaojali matumbo yao tu na sio Watanzania kwani hata familia zao wao wameshazinusuru kwa kuwaondoa alfu wanawaambia watanzania waandamane ili waumie wafe Tanzania ibakie yao tu
 
Hivi huyu baba hanaga kazi zingine? Kwa Kenya huwaga wanaside na serikali kukandamiza wapinzani kwa Tz wanaside na wapinzani dhidi ya serikali. Wamerekani wanafiki sana jamani
Tuseme ukweli tu SERIKALI YA TANZANIA awamu ya tano ni Serikali dhalimu sana. Yani huwezi kutofautisha Tanzania na Burundi au Rwanda kwa sasa. Tanzania ni nchi iliyojijengea heshima kubwa kidemokrasia Leo hii tumekuwa kituko.

Swali unalotakiwa kujiuliza, je wanayoyasema marekani ni ya kweli au wanamsingizia MAGUFULI???

Mitandao imezimwa au haijazimwa??? Kura zimeibiwa au hazijaibiwa??

UCHAGUZI ulikuwa huru au uhuni tu??

Je magufuli asingefanya dhulma ya yote haya Marekani wangemsema vibaya? ?

Tatizo ni MAGUFULI...ni MAGUFULI tu
 
Balozi huyo ameandika:

Reports of arrests of opposition leaders are extremely concerning. I urge the Government to ensure the safety and security of all opposition leaders, cease these targeted arrests, release detainees, r
Serikali inafahamu inachofanya hivyo asijaribu kuingilia maamuzi yetu kama ambavyo hatuingilii maamuzi yao
 
Back
Top Bottom