Banda la kuku

Alvin Slain

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
6,375
Reaction score
3,663
Hello jf mabibi na mabwana natumai ni wazima wa afya baada ya wikiendi.
Ndugu mwanajamii baada ya kuomba ushauri hapa jukwaaa la ujasiriamali, nimeamua kwa ridhaa yangu kuwa mfugaji wa kuku wa kienyeji tiyari nimenunua jogoo(5) na makoo(12) .
Naombeni mnipe ramani ya kuweza kuwalea ktk banda ikizingatiwa baada ya muda mfupi watasaliana kwa wingi.
Muhimu zaidi na banda la vifaranga ambavyo havilelewi na mama yao.

Up dates--------------Baada ya kuandaa banda sasa nimewaleta kuku 25,
kazi hii si rahisi kwani kuku hawa wote ni wakubwa kwani wanapigana nitawaletea kila kinachojiri katika huu mradi,
-----------------------------
Kuku wameanza kutaga muda mchache baada ya kuwaweka kwenye banda, Haikupita wiki (2)Kuku wakaanza kutaga,Lakini kinachonishangaza kuna siku inapita sipati Mayai, Hii imekaaje.
 

Hongera sana kwa kuingia kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. Sina ramani ya banda la kuku ila naamini wataalamu hapa watakupatia; nina ushauri tu kwako kuwa ratio ya kawaida ya jogoo kwa mitetea ni 1:10 lakini hapa naona wewe umeanza na ratio ya 1:2.4, nadhani umenunua majogoo wengi sana. Unaweza kuzalisha mayai yasiyo na vifaranga kwa sababu muda mwingi majogoo yatakuwa yakionyeshana ubabe. Hongera sana.
 
Kadiria tu kutokana na wingi wa kuku wako. Mimi nimejenga 10 kama hilo ambapo kwa kila mita za mraba 9(3X3) wanaingia kuku 100. Hapo kwenye wavu wanashindia ni mita za mraba 15(5X3)


Vizuri mkuu labda kwa mimi ninayeanza unanishauri nijenge la ukubwa gani kwa kuku 15.
 


Kwa maana hio kama ni majike (30) majogoo inatakiwa (3)tu???
 
hilo eneo la uwazi unaotesha mboga na majani ambayo kuku wanakula. banda nzuri sana
 
Mpwa hili banda nimelipenda sana sana, juzi jumamosi nilikua shambani kwangu na ninaanzisha ufugaji wa kuku pia japo mimi nataka nifuge wote wote, nisaidie gharama za jumla kujenga banda moja kama hili lenye uwezo wa kubeba kuku kama mia moja hivi, this is now a Bright Monday.......thanks
 

Inategemea na materials utakazotumia. Mimi hutembelea sana site kubwa za ujenzi nako hupata mabati na mbao zilizotumika. Kifupi utahitaji bati 14; mirunda (au mikenge ndio imara zaidi) kama 40; Mabanzi ya mbao kama 30; Wavu kama roll moja pamoja na misumari ambayo siikumbuki. HAPO ndani nimetia sakafu ya simenti ni kama mifuko 2 na hapo nje ni vumbi tu au ukiweza weka maranda ya mbao juu yake....
 
Hayo majani yataota saa ngapi wakati kuku watakua wanalittumia?

Ni point nzuri........majani (mchicha) nauotesha katika mabeseni ya plastiki nje ya bandana unapokuwa baada ya kama wiki nawaingizia ndani(unahitaji kuwa na seti mbili ili kukamilisha mzunguko).
 
pouwa ungekuwa dar ninauza vifaranga vya kienyeji vya siku moja sh.1700 na vina chanjo ya( marex) huu ni ugonjwa wa kuku baada ya miezi sita (wanapoanza kutaga) wanapata kansa ya uzazi na huwa kuku anataga yai na uzazi wote kutoka nje na na kusababisha kuku kufa.

na hawa kuku wanaanza kutaga wakifikisha umri wa miezi sita na hawana uwezo wa kuaatamia kazi yao kubwa ni kutaga tu.

okey kwa hiyo ratio ya majogoo na mitetea ni kubwa sana kama unategemea hao kuku kuatamia, jogoo mmoja mwenye mbegu at least awe na mitetea mitano mpaka saba ikizidi zaidi kumi kwa hapo majogoo watapigana na mitetea itakosa mbegu au mitetea kufanywa sana kiasi kwamba kuchosha njia ya uzazi na kuja kushindwa kutaga baadae. ni ushauri tu.
 
Ni point nzuri........majani (mchicha) nauotesha katika mabeseni ya plastiki nje ya bandana unapokuwa baada ya kama wiki nawaingizia ndani(unahitaji kuwa na seti mbili ili kukamilisha mzunguko).

Yaani wewe mkuu ni zaidi ya chuo hongera sana
 
nadhani hilo eneo ni la kufungulia kuku wakati wa jioni au mchana waote jua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…