Sasa kama Kipa Djigui Diara ( Yanga SC ) ni mdaka Mishale na kila Siku Magazeti ya Kinafiki ya Mwanaspoti na Championi yanajipendekeza Kumpamba ( Kumsifia ) mbona tokea aitwe na Mali huko AFCON ya Cameroon anaozea tu Benchi / Mkekani?
Cha Kushangaza yule Mchezaji Bora na asiyeimbwa na Magazeti ya Kinafiki Championi na Mwanaspoti Peter Banda ( Simba SC ) ndiyo ameweza Kucheza huko AFCON ya Cameroon na kuingarisha vyema Simba SC kwani kila alipokuwa na Mpira Watangazaji walikuwa wakisema anachezea Simba SC ya Tanzania.
Nina Rafiki yangu Mmoja wa Kikongo ( kutoka Congo DR ) huwa anatushangaa sana Watanzania kwa Kuwasifia na Kuwapamba Kutwa akina Mayele, Moloko, Makambo, Bangala, Djuma, Mukoko na huyu Mbovu wa Juzi Ushindi wakati Wote hawa huko Kwao Congo DR ni 'Makapi' tupu na hata tukisikia wanaitwa Timu ya Taifa ni kujaza tu Idadi ila huishia Mkekani ( Benchini ) tu Kuchoma Mahindi.
Hata hivyo Mchezaji pekee huko Kwao Congo DR anaimbwa sana, ameshapata mpaka Tuzo kadhaa katika Ligi Kuu ya Congo DR na kwamba hata hapa Simba SC alipo saaa anapita zake njia kwani muda wowote anaelekea zake Ulaya ( hasa Ufaransa, Uhispania na Ubelgiji ) ni Beki Henock Inonga peke yake na ndiyo Mkongo anayejua Mpira kati ya Wachezaji wote wa Kikongo walioko hapa Kwetu Tanzania.