KERO Bandari kavu zilizopo Kata ya Sandali, Temeke ni kero, malori yanapaki hovyo

KERO Bandari kavu zilizopo Kata ya Sandali, Temeke ni kero, malori yanapaki hovyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kata ya Sandali, Temeke kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Kilimo kuna bandari kavu imekuwa kero kubwa sana kwa njia ya kwenda Kanisa la KKKT kupitika sababu malori yamekuwa yanaziba njia na huduma ya usafiri imekuwa changamoto.
1789898593800.jpeg
Yanaharibu barabara yana park mpaka kwenye mitaa imekuwa kero kubwa, Serikali ilisema imezindua bandari ya Kwala ili kupunguza foleni ya malori, sasa kama kuna hizi bandari kavu huku mtaani je, Kwala itakuwa na kazi gani?

Pamoja na mkuu wa mkoa kufika eneo hilo ila hali imekuwa mbaya zaidi kwani ndiyo malori yamekuwa mengi sanaa kupitiliza, Wakazi wa Sandali wanateseka sana njia hiyo kuna shule mbili kuna zahanati toka kuwa na Bandari Kavu imekuwa kero sana njia haipitiki kabisa.
1789898612120.jpeg

1789898622461.jpeg

1789898634401.jpeg
 
Back
Top Bottom