Mbona hawalielezi hata bungeni hilo, kumbe kuna mambo mengi hata bunge limefichwa na bunge letu jinsi lilivyo la hovyo, naomba radhi sana na waniite kwa hilo, kilichofanyika juzi ni uhuni.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh..., huyu Dr. Ameliita Bunge Letu ni Bunge la Hovyo, na kilichofanyika kuridhia IGA ni uhuni?. Nashauri Daktari aitwe mbele ya Kamati!. Mimi nilipouliza tuu Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? niliitwa Bungeni kuhojiwa na kamati!, sasa leo Bunge linaitwa la Hovyo!, na kilichofanyika ni uhuni!, mtu huyu hawezi kuachwa hivi hivi, aitwe mbele ya kamati kuthibitisha kauli yake!. Na ikitokea asipoitwa, hii itaaminisha alichosema ni kweli, hivyo nawauliza waungwana, jee ni kweli Bunge letu ni Bunge la Hovyo?. Jee ni kweli kilichofanyika kwa Bunge kuridhia hii IGA ya serikali yetu na Mwarabu wa Dubai ni uhuni?. Mtu anayefanya uhuni ni muhuni, jee waheshimiwa wabunge wetu ni wahuni?.
Dkt. Slaa: Natoa wito kwa Watanzania wote kwa pamoja tusikubali kupokea upotoshwaji aina yoyote katika mambo yanayotuhusu sisi wenyewe na vizazi vyetu vijavyo. Mkataba huu ujadiliwe upya, uangaliwe upya tuweze kukubaliana vitu gani vifanyike.
Inahitajika elimu kuhusu mikataba kwa Watanzania, kama hata Daktari Daktari Balozi mzima hajui kuwa IGA ni makubaliano tuu, MoU, na sio Mkataba, mkataba ni HGA!, hakuna haja ya IGA mpya, yote aliyoyasema yatazingatiwa kwenye HGA!.
Kila mkataba ni makubaliano, lakini si kila makubaliano ni mkataba!. Every contract is an agreement but not every agreement is a contract!. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

P.
 
Hivi Mushumbusi yuko wapi amemuacha huyu Paroko na sononeko
Nyie ndio mnatufanya tuonekane wapuuzi na tusio jielewa. Jadili hoja yake. Nchi inauzwa unaleta propaganda za kitoto.
 
Waandishi wenyewe akina Balile? Wapenda bahasha kama lote!!
 
Anayepinga uwekezaji wa bandari ni adui wa maendeleo. Mmeendesha bandari wenyewe miaka yote bila tija yeyote zaidi ya rushwa na urasimu tu. Maza akimaliza bandari zifuate airports wape wanaojua wanachokifanya na wenye nyezo za kazi.
Ila Bandari za Zanzibar zina ufanisi?
 
Paskali bado una kinyongo cha kuitwa bungeni, sahau wacha yapite.
 
Wadau hivi haiwezekani huyu mzee akarudi bungeni mwaka 2025.

Kuna moto inatakiwa uwashwe ili watu fulani waelewe haya yanayofanyika hayapo gizani, zaidi ya huyu kuna wale wengine kama Heche nk.
Ujinga ni kipaji aisee. Kitu gani kimefanyika gizani?πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…