Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Serikali ingejenga bandari ya Bagamoyo kwa kushirikiana na oman na wa China kwa mfumo wa PPP badala ya kuachiwa wao pekee. Bandari na Airport ni malango ya kuingia na kutoka kiusalama serikali lazima iwe na jicho lake hapo.
Kabisa mkuu. Huwezi kuachia sehemu nyeti kama hizi ziwe mikononi mwa wageni. Hakuna nchi inayoweza kufanya ujinga kama huu. By the way mimi sijashawishika kabisa kuwa hiyo bandari ina ulazima ukitilia maanane tayari tuna bandari tatu ambazo ziko locations nzuri tu na zikipanuliwa zitakidhi mahitaji kabisa tena ya muda mrefu. Sikiliza. Asikudanganye mtu eti yatakuja mameli makubwa makubwa yatashusha mzigo na meli nyingine ndiyo zije kupakia. Hizo meli nyingine zitatoka wapi? Ukiangalia njia kuu meli meli duniani utaona hakuna nchi itakayohitaji bandari yetu iwe ndiyo kianzio cha safari ya bidhaa zake kwani itakuwa ni kuongeza gharama bila sababu. Hii bandari wachina wanalenga kuitumia kutoroshea malighafi ya nchi za Tanzania, Congo ya Zaire nk. Mengine ni changa la macho tu.
 
Watu mmetumwa kubadili upepo😀😀. Kuna vitu umeviruka hapo sijui ni makusudi au bahati mbaya. Yaani wakae/wamiliki eneo hilo na bandari kwa miaka 99 baada ya hapo wafidiwe ghalama za uwekezaji ndio wawaachie au kumilikisha/kuirudisha hiyo bandari MIKONONI mwa serikali. Yaani baada ya miaka hiyo watuuzie Tena. Ungekuwa na maana Kama baada ya maelezo yako hayo ungebandika na hiyo mikataba hapa ili na sisi tuone Kama unachokisema ndicho ulichokisoma kwenye hiyo mikataba... Jiulize kwa nini hauwekwi wazi kuondoa utata? KAZI IENDELEE/ KAZI IMENOGA
 
Watanzania karibu wote wanakubali kwamba Tanzania inahitaji bandari nyengine. Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.

Tatizo la Bandari y Bagamoyo ni hilo neno"Bagamoyo" ndio linachukiwa sana kesho wakibadilisha waseme Bandari ya Pwani ikajengwe Sadani hao wanaoipinga wote kimya.
 
Kuna wapuuzi wanakubali kujengewa bandari wakati wanajijua Kodi zao pale TPA ni Mzigo, TUNAENDA KUUA BANDARI YA DAR ES SALAAM wenyewe na kukabidhi uchumi wetu kwa wageni,

Haiwezekani tujiletee changamoto kwa tamaa za wachache ambao hawafikirii maslahi mapana ya Taifa hili, hizo trillion 23 hatuwezi kuzipata ndani ya miaka 33 tukajenga kwa pesa zetu? Hata ndani ya miaka 10 tu. Tunaweza kuzipata na tukajenga bandari kwa pesa zetu za ndani.

Tukikubali kujengewa bandari ya Bagamoyo,tumekubali mizigo yote inayoenda kwa majirani tutaikosa katika bandari yetu ya Dar, hizi billions ambazo zinapatikana Kama mapato mpaka nyingine zinaibwa tutazisoma mtandaoni tu.
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa bandari aliyeondolewa alisema bandari ya Bagamoyo ni kwa ajili ya viwanda vinavyojengwa pale.
 
😀😀😀😀 Kuna jamaa alibanwa sana na kifua kweli ilikuwa dalili za COVID 19 aliapa kamwe asipelekwe hospitali ya Mloganzila, hilo jona hapendi kulisikia kabisa anasema hilo jina si rafiki kwa wagonjwa yeye anafupishaga Mloga.
 
Aisee mna akili ngumu Sana kuelewa nyie watu khaa
Labda waeleweshwe kwa lugha ya bakora. Ujue inachosha
 
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa bandari aliyeondolewa alisema bandari ya Bagamoyo ni kwa ajili ya viwanda vinavyojengwa pale.
Hivi Trillion za kujengea bandari zimetushinda Kama Taifa kwa huo muda ambao wao watatukabidhi bandari kuwa yetu katika kuingizia Pato Taifa?

Pengine pesa tu zilizotumika kununua ndege zingetosha kujenga bandari

Hata tukijenga kwa miaka 20 Sawa tu, kikubwa iwe yetu isiyokuwa na masharti.
 
Hivi Trillion za kujengea bandari zimetushinda Kama Taifa kwa huo muda ambao wao watatukabidhi bandari kuwa yetu katika kuingizia Pato Taifa?

Hata tukijenga kwa miaka 20 Sawa tu, kikubwa iwe yetu isiyokuwa na masharti.
Hamna political will ya kujenga hiyo bandari swala sio pesa.

Ingekuwa tatizo ni mkataba na wachina wangesema mchina amezingua sasa tunaongea na mjerumani au mjapani.
 
Dar eneo dogo sana hapana uwezo wa kuchukua meli nyingi na ndio maana kuna ma ICD huko nje ya bandari.
 
Bwana KURUNZI Wenzenu wako huku. Yaani wachina wameajiriwa kwenye jeshi lao la polisi. Zambia( endelea kutumika)

 

Kumbuka idea ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni ya kwetu sio ya wachina, sisi ndio tuliwauzia wao wanaleta hela. Je wakati tunapanga kuhusu huu mradi hatukuona haya?
 
watu wanapaswa wajiulize ni nini tumepata so far kutokana na mkataba wa ukodoshaji wa sehem ya bandari kwa TICS before hatujawaza kuwaachia bandari yote wachina sisi tubaki kuchukua gawiwo?
Au ndo hatupendi kujifunza kwa makosa yetu wenyewe...tunataka tufanye makosa mengine ili tupate nafasi nyingine ya kujilaumu na kuilaumu serikali ya ccm?[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…