View attachment 1754585
Aliyekuwa Rais waTanzania Hayati John Pombe Magufuli alisema mradi wa bandari ya Bagamoyo ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali...
Huu uzi umeurejesha nara ya pili ingawa kichwa cha habari slightly kimerekebishwa. Nami narudia kukujibu kama nilivyoipinga hoja ya kujenga bandari Baganoyo katika hoja ya awali.
Ingawa umeandika analyitically lakini unaupigia debe mradi wa bandari ya Bagamoyo utekelezwe kinyume na maamuzi ya JPM kuwa usitekelezwe. Nami naona nikujibu kiuchambuzi kwa nini usijengwe. Katika uchambuzi huu nitatumia pia hoja za wengine wenye mawazo kama yako.
Kwanza, Ndugai mwanzoni kabisa alisema kuwa Magufuli alishauriwa vibaya. Wote tunamfahamu Magufuli kama mtu makini sana katika kusoma document hata iwe kubwa kiasi gani si rahisi kumchomekea kitu asikione, pili kati ya Ndugai na JPM ambaye anaweza asiwe na access ya document ni Ndugai lakini sio JPM kwa kuzingatia nafasi yake hivyo hoja ya Ndugai kuwa Magufuli alishauriwa vibaya haina mantiki kabisa ila Ndugai aliitumia kama gia ya kutaka kujenga uhalali wa kureverse maamuzi ya Magufuli kuhusu kukataa kujengwa kwa bandari hiyo.
Mnaoupigia debe mradi huo mnadai kuwa bandari ya Bagamoyo ina kina kirefu maji hayajai na kupwa hivyo ndio sehemu inayofaa kujengwa bandari ya kupokea meli hizo kubwa na kuwa bandari ya DSM haiwezi kupanuliwa kuchukua meli kubwa za mita mia tatu au mia nne. Sasa kwa nini mkataba ukataze kujenga bandari ya DSM au nyingine yeyote kuanzia Tanga hadi Mtwara? Hao wawekezaji na nyinyi mnaogopa nini hiyo bandari ya Bagamoyo kushindana na bandari zingine za Tanzania? kwa nini mnaikingia kifua dhidi ya bandari zingine? Busara ya kawaida hapa ni kuwa wao kama wangewekeza (japo mimi napinga) basi wangekuwa tayari kwa ushindani na sio kutaka upendeleo wa kipekee.
Mnadai meli kubwa ndizo zitakuwa zinatia nanga bandari ya Bagamoyo sasa kwanini hamtaki hizo meli mnazoziita ndogo ziendelee kutia nanga katika bandari ya Dsm, Tanga na Mtwara? Kwa nini mnataka kuziua bandari zingine ikiwa lengo ni bandari ya Bagamoyo kuhudumia meli kubwa za mita mia tatu au mia nne?
Pia mnadai kuwa meli kubwa zitaleta mizigo Bagamoyo kisha baada ya kupakuliwa mizigo hiyo itabebwa na meli ndogo kupelekwa sehemu zingine! Uongo ulioje! Hizo sehemu ni zipi? Jiografia ya Tanzania ni kuwa sisi tumezungukwa na nchi sita zisizo na bandari ambazo ni Malawi, Zambia, Congo Mashariki (ingawa atlantic ocean wanayo), Rwanda, Burundi na Uganda. Nchi tatu za mwisho huwa tunashindana na Kenya katika kugombania mizigo yao hivyo wanaotutegemea kabisa ni nchi tatu za mwanzo. Pia hata kwa Zambia huwa tunashindana na bandari ya Durban. Mizigo inapoletwa katika bandari zilizopo hubebwa kwa reli na malori kupelekwa huko katika nchi hizo hivyo suala la meli ndogo ndogo kuichukua mizigo na kuisambaza haina mantiki kabisa, Pia jiografia ya Africa, mizigo inayokwenda Africa kaskazini au Magharibi kutoka Asia ni rahisi kupita Suez canal, mediteranian kisha kwenda huko hivyo haiwezekani mizigo yao ije huku East Africa kisha irudi huku North au west Africa. Hali kadhalika kwa mizigo inayotoka bara la America haiwezi kuletwa huku kwetu kisha ipakiwe tena kwenda West Africa au hata South Africa. Pia mizigo ya Africa Kusini inayotoka Asia haiwezi kuletwa Bagamoyo kisha ipakiwe tena kwenda Africa Kusini. Ni wazi mizigo ya Africa Kusini kutoka Asia moja kwa moja inapelekwa bandari ya Durban ambayo ni bandari kubwa. Hivyo hoja kuwa sisi tutakuwa tunahudumia mizigo ya nchi zenye bahari kama sisi ni hoja mufilisi isiyo na mashiko. Sisi urefu wa Kamba yetu utaendelea kuwa nchi zisizo na bandari zinazotuzunguka tu na ambazo zinahudumiwa vyema na bandari za DSM, Tanga na Mtwara vizuri na kwa ufanisi.
Reli ya kutoka bandari ya Mtwara hadi Mbababay ikikamilika, tutakuwa na uhakika wa kuihudumia Malawi kwa ufanisi zaidi kuliko bandari ya Bagamoyo. Hali kadhalika bandari ya Tanga imepanuliwa na SGR ikikamilika mizigo ya Congo Mashariki, Rwanda, Burundi, Uganda itahudumiwa kwa ufanisi zaidi.
MAPATO
Serikali kupitia mamlaka ya bandari inapata pesa za handling na storage ya mizigo pamoja na kodi/tozo mbali mbali za forodha zinazokusanywa na TRA kutokana na meli zinazotia nanga katika bandari ya DSM, Tanga na Mtwara; lakini bandari ya Bagamoyo ikijengwa mamlaka hizo hazitakusanya mapato huko na wakati huo huo bandari hizo zitakuwa zimeminywa meli zisitie nanga huko, badala yake mapato hayo na mengine ambayo projections zinaonyesha yataendelea kukua yatakuwa yanachukuliwa na wawekezaji hao toka China na Oman kutokana na meli kutia nanga bandari ya Bagamoyo, ujinga ulioje. Tuwe wakweli hata bandari hiyo ya Bagamoyo ikijengwa asilimia kubwa ya meli zitakazokuwa zinatia nanga ni hizi hizi zinazoitwa meli ndogo ambazo kwa sasa zinatia nanga bandari za Dsm, Tanga na Mtwara. Wakina Ndugai wanapigia debe hata haya mapato tunayoyapata sasa kupitia bandari zetu tuyakose badala yake yakusanywe na kuchukuliwa na wachina kwa kisingizio mradi una manufaa. Mbona hawatauambii quantifiable revenue amount ambayo tutakuwa tunapata bandari ya Bagamoyo ikifanya kazi badala yake wamekalia kusema mradi una manufaa sana lakini hawatupi figure?
UJENZI WA VIWANDA
Hoja nyngine ambayo inapigiwa debe na kufungamanishwa na ujenzi wa bandari ni ujenzi wa viwanda katika ukanda huo wa Bagamoyo. Swali rahisi hivi ni lazima mtu akitaka kujenga viwanda lazima ajenge na bandari? Kama hao wawekezaji wana nia ya kujenga hvyo viwanda hawajakatazwa kwani eneo la Bagamoyo ni moja ya meneo yaliyoainishwa kama EPZ, Hivyo wanaweza kuja kupitia TIC na kupewa ruhusa ya kujenga viwanda. Jambo la msingi wajenge viwanda kwa terms zilizo sawa na wawekezaji wengine katika EPZs zingine na wasipewe upendeleo wa kipekee kuliko wawekezaji wengine wanaojenga viwanda. Ukipita barabara ya Kilwa kuelekea Mkuranga, njia ya Chalinze na Tanga, utaona kuna viwanda vya wachina vimejengwa/vinaendelea kujengwa; mbona hao hawakufungamanisha ujenzi wa hivyo viwanda na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo?
Ujenzi wa viwanda na ujenzi wa bandari ni vitu viwili tofauti ambavyo mwekezaji hana uhalali wa kulazimisha kuwa lazima afanye vyote. Amekataliwa bandari ajenge hivyo viwanda. Kama atahitaji bandari za kuimport raw materials au export ya bidhaa zake atatumia bandari zilizopo. Hoja kuwa bandari ya Bagamoyo ikijengwa na viwanda 700 vitajengwa haina mashiko kwa sababu hayo mambo mawili siyo lazima yafanyike pamoja.
Hoja yako kuwa China inaitambua Bagamoyo katikampango wake wa Belt and Road sisi haituhusu kwani hiyo ni mikakati yao ya kuitawala na kuinyonya dunia. Kwani hata kama tungeamua kujenga bandari ya Bagamoyo ni lazima wajenge wachina? Hatuwezi kujenga kwa nguvu zetu?
Watu wanapopata nafasi za uongozi wajifunze kuiga uzalendo kama ambavyo viongozi wa mataifa ya Uchina na mengine yaliyoendelea wanavyoweka maslahi ya nchi zao mbele hata kama ni kwa kunyonya nchi zingine.
Bandari ya Baagamoyo ikifanikiwa kujengwa basi itakuwa ni ufisadi kama ufisadi mwingine uliokuwa unafanyika huko