Umeiweka vizuri sana, Magufuli alililisema hili hadharani, na siyo siri kuwa Kikwete alikuwa madarakani wakati mchakato huu unaanza na pia China inahusika na mradi huu. Kama ni hivyo, kwanini China haijajitokeza hadharani kukanusha? China hawajawahi kuwa na unafiki, kila siku wanaparurana na Marekani huko kwenye MSM. Kwa nini Kikwete hajatoka hadharani kukanusha? Bila shaka wanajua alichosema Magufuli ndio ukweli. Hata yule Kakoko wa bandari alisema the same, sijaona aliyekanusha.
Ya Chato ni muktadha tofauti na huu. Tumalize hili kwanza.
Hivi inaingia akili kwamba watanzania wanaweza kuchukulia maoni ya Kakoko seriously - kwani uchunguzi wa CAG umetoa picha gani kuhusu projects za kimangamushi za TPA alizo zi-sign Kakoko mwenyewe - kuanzia ujenzi Bandari kwenye Lakes zote Tanzania pamoja na Bandari za Bahari za kuu ie Dar, Tanga na Mtwarahusu Taifa letu,hapo tunazungumzia masuala ya ujenzi wa infrastructures,je,tukija kwenye ununuzi wa flow meters bei walizo nunulia ndio bei alisi kweli? After sales contract ya flow meters inasemaje, je, kulikuwepo ulazima wowote wa kununua flow meter mpya pale Dar Port badala ya kukarabati ya zamani, mwaka juzi nilimuona JPM akiwahoji ma data entry clerks wa container scanners, aliwakuta wapo kwenye chumba ambacho hakuna dirisha la kuangalia kinacho endelea kwenye kwenye zoezi la ku-scan makonteina hawajui maconteina magapi yanapitishwa bila ya kukaguliwa,na Taifa linapoteza revenue kiasi gani kutokanax na hujuma hizi zilizo dhahiri - si rahisi udanganyifu huu ukawa unaendelea hapo Bandarini bila ya top managment anayo ongoza na Kakoko bila kujuwa, haya tuje kwenye manunuzi na ufungaji wa survaillance and secyurity systems hapo bandari,je, Serikali ikitumia an independent consultant akakagua vifaa vyote na system nzima wanaweza kusema gharama za manunuzi na ufungaji wa security sysyem haukuwa highly inflated?
Juzi hapa nilimsikia CAG aki question some projects zinazo fanyika TPA lakini hazikamiliki miaka nenda rudi wajanja wanaendelea kupiga hela tu under Kakoko's watch,CAG alizungumzia vile vile suala la kuwapa tenda makampuni ambayo hayana sifa mwishowe wanashindwa kumaliza kazi wanazo pewa,o hii inaleta picha gani, ni wazi tenda hizo wanapewa makampuni/watu kwa kujuwana na si ufanisi wa kazi, how about TPA (IT) system going down for days on end na wahusika wana manufacture lame excuses za kutaka kuendelea kufanya kazi manually thereby bypassing computer system ili waendeleze wizi na udanganyifa mwisho wa siku kulikosesha Taifa letu mapato - mtu ungetegemea Taasisi kama TPA inge-install a robust backup system with an equally impregnable "FAILOVER" system ya kuwezesha mitambo ifanye kazi uninterrupted 24X7 , badala yake wanawachia wajanja waingilie system wakiwa na lengo la kuikosesha mapato Serikali.
Nayasema haya yote kutokana na kauli ya Kakoko aliyo itoa akiwa Mkoani Mwanza aliwakandia Wachina kuhusu mradi wa ujenzi wa Bandari ya B'moyo alionekana wazi wazi yuko overly determined kuhakikisha mradi huo unazikwa au wenda ikawa alitaka wachina waje wawekeze katika ujenzi wa Bandari ya B'moyo kwa pesa zao halafu mwisho wa siku Bandari ikabidhiwe TPA chini ya Uongozi wa Kakoko mambo ya ndio sivyo ya shirika la TPA yajirudie tena kwenye Bandari mpya ya B'moyo, wakati akijuwa wazi kwamba Serikali haitachangia hata senti tano kwenye project nzima - na ukweli wa mambo hakuna mwekezaji mwenye akili timamu anaweza kubariki masharti ya ajabu kama hayo.
One more thing, former TPA Director General si msemaji wa Serikali, si katibu mkuu wa Wizara au Waziri wa uchukuzi - yeye ana moral Authority gani ya kutaka kuzima mradi ambao ungeweza kupaaisha Taifa letu kimaendeleo in terms of ujenzi wa viwanda vingi vya kisasa kuzunguka bandari, Korea kusini ilikuwa tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa high tech factories karibu na bandari, bandari ya B'moyo ingekuwa incoporated kwenye mpango kabambe wa ku-link reli za Continental Europe, Uingereza, Urusi, Asia (Iran,Korea nk) pamoja na Uchina kwenyewe - mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli popote Duniani bila ya kutegemea usafiri wa meli ambao ni dead slow - sasa wachina kutaka kuiweka bandari ya B'moyo in the loop ya silk road project hilo waswahili hawalioni,wamekazania ujenzi wa Bandari ya B'moyo ipigwe chini.
Maoni yangu, mama Samia na wazalendo wengine wanao litakia mema Taifa letu wahakikishe mradi huu unafufuliwa kwa hari mpya na kasi mpya, msiwasikilize waswahili wanao kuwa driven na kampein chafu zinazo ratibiwa na vyombo vya habari vya magharibi na intel agencies zao kuwahujumu Wachina kiuchumi na kidiplomasia, fufueni mradi wa bandari ya B'Moyo kama kuna mapungufu ya hapa na pale kwenye mkataba basi wahusika wakae chini na ku-resolve kistaarabu mapungufu yatakayo jitokeza na sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kuanzisha kampein chafu za kuwasema vibaya wachina mnarudia kampein zile zile za Waingereza na Wanerikani za kuwakandia Wachina 24X7.