Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
Daah weeh kweli kichekesho hizo meli sahv zilizojaa mizigo inaelekea wapi?
 
Mkakati my ass@#$%*&!

Kwa nini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Weeh jamaa mtu wa ajabu unaishi dunia gani hivi unajua kama meli sahv ni sawa na uwezo wa viwanja 3 mpk 4 vya mpira wa miguu sasa ule uchochoro zikija 4 tu zitageuza vipi?
 
Weeh jamaa mtu wa ajabu unaishi dunia gani hivi unajua kama meli sahv ni sawa na uwezo wa viwanja 3 mpk 4 vya mpira wa miguu sasa ule uchochoro zikija 4 tu zitageuza vipi?
zipo kubwa kama zanzibar yote, so kugeuza sio dili ni dili ni uwezo wa kwenda kulia - kushoto-nyuma-mbele (zina reverse kotekote), sasa sijui hujielewi au ni wale keyboard worrior
 
Haya aliwahi kusema mwenda zake kuhusu Bandari ya Bagamoyo.

Tujikumbushe
 
Tuutafute wote, lakini bado ukweli utabaki kuwa, maradi unafaida kubwa sana suala la masharti linazungumzika mbona kwenye madini tulikaa tukazingumza sasa tunaona faida yake
Chief kusema tu mradi unafaida kubwa bila kusema masharti yake yapoje siyo sawa.Faida kubwa ni zipi?? Lets say mfano mwa faida ulizozitaja ni ujenzi wa viwanda ndani ya EPZ.Je ikiwa miongoni mwa sharti ni lager number ya ajira zitoke nje ya nchi( Nchi wawekezaji).Uoni kama tutakuwa tumepigwa?
 
Ingawa umeandika analyitically lakini unapigia debe mradi wa bandari ya Bagamoyo utekelezwa kinyume na maamuzi ya JPM kuwa usitekelezwe. Name naona nikujibu kiuchambuzi kwa nini usijengwe. Katika uchambuzi huu nitatumia pia hoja za wengine wenye mawazo kama yako.

Kwanza, Ndugai mwanzoni kabisa alisema kuwa Magufuli alishauriwa vibaya. Wote tunamfahamu Magufuli kama mtu makini sana katika kusoma document hata iwe kubwa kiasi gani si rahisi kumchomekea kitu asikione, pili kati ya Ndugai na JPM ambaye anaweza asiwe na access ya document ni Ndugai lakini sio JPM kwa kuzingatia nafasi yake hivyo hoja ya Ndugai kuwa Magufuli alishauriwa vibaya haina mantiki kabisa ila Ndugai aliitumia kama gia ya kutaka kujenga uhalali wa kureverse maamuzi ya Magufuli kuhusu kukataa kujengwa kwa bandari hiyo.

Mnaoupigia debe mradi huo mnadai kuwa bandari ya Bagamoyo ina kina kirefu maji hayajai na kupwa hivyo ndio sehemu inayofaa kujengwa bandari ya kupokea meli hizo kubwa na kuwa bandari ya DSM haiwezi kupanuliwa kuchukua meli kubwa za mita mia tatu au mia nne. Sasa kwa nini mkataba ukataze kujenga bandari ya DSM au nyingine yeyote kuanzia Tanga hadi Mtwara? Haowawekezaji na nyinyi mnaogopa nini hiyo bandari ya Bagamoyo kushindana na bandari zingine za Tanzania? kwa nini mnaikingia kifua dhidi ya banfari zingine? Busara ya kawaida hapa ni kuwa wao kama wangewekeza (japo mimi napinga) basi wangekuwa tayari kwa ushindani na sio kutaka upendeleo wa kipekee.

Mnadai meli kubwa ndizo zitakuwa zinatia nanga bandari ya Bagamoyo sasa kwanini hamtaki hizo meli mnazoziita ndogo ziendelee kutia nanga katika bandari ya Dsm, Tanga na Mtwara? Kwa nini mnataka kuziua bandari zingine ikiwa lengo ni bandari ya Bagamoyo kuhudumia meli kubwa za mita mia tatu au mia nne?

Pia mnadai kuwa meli kubwa zitaleta mizigo Bagamoyo kisha baada ya kupakuliwa mizigo hiyo itabebwa na meli ndogo kupelekwa sehemu zingine! Uongo ulioje! Hizo sehemu ni zipi? Jiografia ya Tanzania ni kuwa sisi tumezungukwa na nchi sita zisizo na bandari ambazo ni Malawi, Zambia, Congo Mashariki (ingawa atlantic ocean wanayo), Rwanda, Burundi na Uganda. Nchi tatu za mwisho huwa tunashindana na Kenya katika kugombania mizigo yao hivyo wanaotutegemea kabisa ni nchi tatu za mwanzo. Pia hata kwa Zambia huwa tunashindana na bandari ya Durban. Mizigo inapoletwa katika bandari zilizopo hubebwa kwa reli na malori kupelekwa huko katika nchi hizo hivyo suala la meli ndogo ndogo kuichukua mizigo na kuisambaza haina mantiki kabisa, Pia jiografia ya Africa, mizigo inayokwenda Africa kaskazini au Magharibi kutoka Asia ni rahisi kupita Suez canal, mediteranian kisha kwenda huko hivyo haiwezekani mizigo yao ije huku East Africa kisha irudi huku North au west Africa. Hali kadhalika kwa mizigo inayotoka bara la America haiwezi kuletwa huku kwetu kisha ipakiwe tena kwenda West Africa aau hata South Africa. Pia mizigo ya Africa Kusini inayotoka Asia haiwezi kuletwa Bagamoyo kisha ipakiwe tena kwenda Africa Kusini. Ni wazi mizigo ya Africa Kusini kutoka Asia moja kwa moja inapelekwa bandari ya Durban ambayo ni bandari kubwa. Hivyo hoja kuwa sisi tutakuwa tunahudumia mizigo ya nchi zenye bahari kama sisi ni hoja mufilisi isiyo na mashiko. Sisi urefu wa Kamba yetu utaendelea kuwa nchi zisizo na bandari zinazotuzunguka tu na ambazo zinahudumiwa vyema na bandari za DSM, Tanga na Mtwara vizuri na kwa ufanisi.

Reli ya kutoka bandari ya Mtwara hadi Mbababay ikikamilika, tutakuwa na uhakika wa kuihudumia Malawi kwa ufanisi zaidi kuliko bandari ya Bagamoyo. Hali kadhalika bandari ya Tanga imepanuliwa na SGR ikikamilika mizigo ya Congo Mashariki, Rwanda, Burundi, Uganda itahudumiwa kwa ufanisi zaidi.

MAPATO

Serikali kupitia mamlaka ya bandari inapata pesa za handling na storage ya mizigo pamoja na kodi/tozo mbali mbali za forodha zinazokusanywa na TRA kutokana na meli zinazotia nanga katika bandari ya DSM, Tanga na Mtwara; lakini bandari ya Bagamoyo ikijengwa mamlaka hizo hazitakusanya mapato huko na wakati huo huo bandari hizo zitakuwa zimeminywa meli zisitie nanga huko, badala yake mapato hayo na mengine ambayo projections zinaonyesha yataendelea kukua yatakuwa yanachukuliwa na wawekezaji hao toka China na Oman kutokana na meli kutia nanga bandari ya Bagamoyo, ujinga ulioje. Tuwe wakweli hata bandari hiyo ya Bagamoyo ikijengwa asilimia kubwa ya meli zitakazokuwa zinatia nanga ni hizi hizi zinazoitwa meli ndogo ambazo kwa sasa zinatia nanga bandari za Dsm, Tanga na Mtwara. Wakina Ndugai wanapigia debe hata haya mapato tunayoyapata sasa kupitia bandari zetu tuyakose badala yake yakusanywe na kuchukuliwa na wachina kwa kisingizio mradi una manufaa. Mbona hawatauambii quantifiable revenue amount ambayo tutakuwa tunapata bandari ya Bagamoyo ikifanya kazi badala yake wamekalia kusema mradi una manufaa sana lakini hawatupi figure?



UJENZI WA VIWANDA

Hoja nyngine ambayo inapigiwa debe na kufungamanishwa na ujenzi wa bandari ni ujenzi wa viwanda katika ukanda huo wa Bagamoyo. Swali rahisi hivi ni lazima mtu akitaka kujenga viwanda lazima ajenge na bandari? Kama hao wawekezaji wana nia ya kujenga hvyo viwanda hawajakatazwa kwani eneo la Bagamoyo ni moja ya meneo yaliyoainishwa kama EPZ, Hivyo wanaweza kuja kupitia TIC na kupewa ruhusa ya kujenga viwanda. Jambo la msingi wajenge viwanda kwa terms zilizo sawa na wawekezaji wengine katika EPZs zingine na wasipewe upendeleo wa kipekee kuliko wawekezaji wengine wanaojenga viwanda. Ukipita barabara ya Kilwa kuelekea Mkuranga, njia ya Chalinze na Tanga, utaona kuna viwanda vya wachina vimejengwa/vinaendelea kujengwa; mbona hao hawakufungamanisha ujenzi wa hivyo viwanda na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo?

Ujenzi wa viwanda na ujenzi wa bandari ni vitu viwili tofauti ambavyo mwekezaji hana uhalali wa kulazimisha kuwa lazima afanye vyote. Amekataliwa bandari ajenge hivyo viwanda. Kama atahitaji bandari za kuimport raw materials au export ya bidhaa zake atatumia bandari zilizopo. Hoja kuwa bandari ya Bagamoyo ikijengwa na viwanda 700 vitajengwa haina mashiko kwa sababu hayo mambo mawili siyo lazima yafanyike pamoja.

Hoja yako kuwa China inaitambua Bagamoyo katikampango wake wa Belt and Road sisi haituhusu kwani hiyo ni mikakati yao ya kuitawala na kuinyonya dunia. Kwani hata kama tungeamua kujenga bandari ya Bagamoyo ni lazima wajenge wachina? Hatuwezi kujenga kwa nguvu zetu?

Watu wanapopata nafasi za uongozi wajifunze kuiga uzalendo kama ambavyo viongozi wa mataifa ya Uchina na mengine yaliyoendelea wanavyoweka maslahi ya nchi zao mbele hata kama ni kwa kunyonya nchi zingine.

Bandari ya Baagamoyo ikifanikiwa kujengwa basi itakuwa ni ufisadi kama ufisadi mwingine uliokuwa unafanyika huko nyuma hususan awamu ya nne.
 
Na kama tushasema investor anaruhusiwa kuajiri watu anaoona wanamfaa...hivi matumaini ya job creation kwa wazawa itakuwaje? Maana mchina habagui kazi hata reachstacker operator bandarini anaweza mleta mchina….

Naomba huo mkataba wanapoujadili tuweke wazi ajenda ya local content....
Kwenye hili mama asipokuwa makini atakaribisha dili nyingi sana zisizoeleweka.
 
Ndugu-yai hapo na mjenzi wa Bandari anavishwa Lubega kuwa chief wa Wagogo
[emoji2][emoji3][emoji38]
Screenshot_20210415-205545_WhatsApp.jpg
 
Kwanini chapisho lenye maandishi ya mkataba wa mradi huo yasitolewe kwa umma ili tuwe na picha kamili?
Mimi nimemsikia Magufuli akiuponda sana huo mradi,lakini nilimsikia Spika Ndugai aksifia huo mradi.
 
Japokuwa zimeelezwa faida nyiingi za mradi huo, Kwenye maelezo yote kwangu nilona Shida ipo kwenye tax collection!

Je ni kweli TRA will not be allowed to correct tax kwenye hiyo bandari?

Kwamba moja ya masharti yanaonyesha TRA hawatakiwi kukanyaga pale for 33 years ???

Kama ilo sharti nilauongo, hiyo bandari ijengwe haraka sana eti!!
 
Mkakati my ass@#$%*&!

Kwa nini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Watanzania mlishaambiwa mtumie kichwa kufikiria sio kufugia nywele. Matokeo yake ndio haya.

Ushawahi kufika bandarini Dar? Au unaishi mkoa gani ndugu?
 
Japokuwa zimeelezwa faida nyiingi za mradi huo, Kwenye maelezo yote kwangu nilona Shida ipo kwenye tax collection!

Je ni kweli TRA will not be allowed to correct tax kwenye hiyo bandari?

Kwamba moja ya masharti yanaonyesha TRA hawatakiwi kukanyaga pale for 33 years ???

Kama ilo sharti nilauongo, hiyo bandari ijengwe haraka sana eti!!
Mchina hawezi kuwa mjinga kuweka kipengele ambacho kitamkosesha fursa. Mimi naona mkataba ukiwekwa wazi tutaenda kuvunja lile kaburi pale...
 
Dah ninachoka ninapotaka kuaminiahwakwamba bandarinya dar haina uwezo wa kupokea meli kubwa Wala makontena Yale....


Ambayo makontena Yale na meli zile zitakuja baada ya bandari mpya kujengwa....


Kuweni makini..mtauza nchi....pale. ambapo factor ya biashara sio ubora wa bandari Bali uwezo wa wanannzengo kuagiza mizigo na kutumia.bamdari
 
Kwa masharti hayo huyo Mary Nagu atafutwe huko halipo na kuwekwa Segerea walau mwezi mmoja, how dumb was she kukubali mambo kama hayo.
Mkuu Mary Nagu kama waziri na katibu mkuu wake hao ni kuwaonea tu. Alisaini huku mkuu wake wa kazi JK akiwa amesimama nyuma yake kushuhudia anatekeleza makubaliano kati ya JKM wa Tanzania na Xi Jinping wa China.

Tanzania hata ikiwa na rais mzuri au mbaya kiasi gani na akayatumia madaraka yake kama yalivyoainishwa kwenye katiba na sheria bila kupindisha kulinda udhaifu wa kibinadamu lazima atang'olewa na genge fulani lenye hati miliki ya mamlaka (The wealth and power elites).

Ndio, lipo na linafanya kazi usku na mchana wakifuatilia mwenendo wake, kiapo na athari zinazotokana na matokeo ya utekelezaji wa katiba, sheria, mila, desturi na kanuni za mifumo utawala wa nchi.

1. Ukiwa kiongozi utafurahisha watu wengi lakini utekelezaji wa majukumu hupunguza tija na ufanisi
2. Ukiwa mtawala utachukiza kadhaa (manung'uniko, kubeza, juhudi za kukwamisha na viapo vya visasi huongezeka) na kufurahisha kadhaa kwa fursa ambazo , lakini utekelezaji wa majukumu ya dhamana aliyokabidhiwa wenye matokeo chanya kwa muda mwafaka huonekana bayana

Ili kuondosha mianya na madhara yatokanayo na utekelezaji wa katiba na sheria pamoja na kinga kwa viongozi wakuu wanazopewa kusimamia dhamana kama taifa lazima kwa pamoja liwe na sera ya kipekee, maono, dhamira, mwelekeo na malengo yanayoweza kutekelezeka.

Utashi na vipaumbele vya rais vyenye malengo binafsi ya kisiasa vidhibitiwe ili kudumisha ustawi wa jamii nzima.
 
Mchina hawezi kuwa mjinga kuweka kipengele ambacho kitamkosesha fursa. Mimi naona mkataba ukiwekwa wazi tutaenda kuvunja lile kaburi pale...
Vitu vifuatavyo ni HATARI kwa USALAMA wa TAIFA na UCHUMI kuzidi UKIMWI kuvikabidhi kiukamilifu bila miongozo ya kisheria ua udhibiti, (ubora, usalama, usahihi, utimilifu/utoshelevu, uzingatiwaji wa maadili na miiko) kwa mwekezaji ama wa ndani au nje ya nchi
1. Kiwanja cha ndege
2. Bandari (kama ipo)
3. Mipaka ya nchi
4. Jeshi
5. Polisi
6. Uhamiaji na usajili uraia
7. Benki kuu
8. miundo mbinu ya Reli/barabara
9. Usalama wa taifa
10. Mawasiliano
11. Maliasili, nishati na madini
12. Mahakama
13. Bunge
14. Usalama wa chakula na afya
Nk
 
_118047256_4d949889-4818-407f-8ee6-c8b1d38fe37c.jpg
Aliyekuwa Rais waTanzania Hayati John Pombe Magufuli alisema mradi wa bandari ya Bagamoyo ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.

MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.
Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wan chi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.

Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari.

_118047257_b08d82e7-8a67-48ff-87b6-a3fe69f44e50.jpg

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari
Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari. Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.

Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika.

Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.

Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji.

Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.

Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka.

Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.

Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

_118047258_2987e81f-d2f1-478b-a150-2e5ce4ff0396.jpg
Ramani inayoonesha bandari mahala ilipo ya Bagamoyo na bandari nyingine katika nchi za Afrika Mashariki
Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).

Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited(China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute(STEPI)Korea Kusini.

Hofu ya Mradi wa Bagamoyo

Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka.

Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.

_118047260_d2d05b4b-8834-415c-8846-13f505e27ddf.jpg

Spika Job Ndungai aliwahi kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa
Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.

Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?

Mmoja wa viongozi wa juu katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambao mradi huo ulikuwa unaelekea kukamilika, ameniambia mengi ya yanayoyosemwa kuhusu mradi huo hayana ukweli na kwamba kulikuwa na upotoshaji mkubwa.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yake, kiongozi huyo alisema gharama pekee kubwa ambayo serikali ingetakiwa kuingia katika mradi huo ni ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa kupisha ujenzi wa bandari hiyo ambao kwa makisio ya mwaka 2016 yalikuwa kiasi cha dola takribani dola milioni 20.9 (shilingi bilioni 43).

" Gharama yetu ni hizo dola milioni 20 za kulipa wananchi lakini mengine yote ni siasa tu. Wanaokuja wanaleta shilingi trilioni 23 na ni uwekezaji wala si mkopo. Ni sawa na kampuni zinazokuja kuchimba madini hapa kwetu. Huwezi kusema wanakuja kutukopesha hela za kuchimba madini. Ni biashara yao.

" Jambo la muhimu kuliko yote ni kwamba huo mpango wa kuwa na Bandari ya Bagamoyo tulikuwa nao hata kabla wawekezaji hawajaja. Na wala hakuna masharti ya kutuzuia kujenga barabara wala miundombinu mingine. Hilo suala la miaka 33 ni la kawaida, yaani mtu aweke shilingi trilioni 23 na halafu asiweke muda wa kurudisha hela zake? Mwisho kabisa, baada ya miaka 33, bandari na hivyo viwanda havitahamishwa Tanzania na nina imani nchi yetu itakuwepo bado," alisema kiongozi huyo.

Huku Lamu, kule Bagamoyo
Kenya, kwa muda mrefu, ilikuwa ikitegemea Bandari ya Mombasa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo kwa wateja wake wa ndani na katika eneo la maziwa makuu. Kwa sababu ya ongezeko la mahitaji, yenyewe pia ikaamua kujenga Bandari ya Lamu - kwa sababu zilezile ambazo zimeifanya Tanzania kuwa na mpango wa Bagamoyo.

Hadi sasa, nchi hizi mbili zinashindana katika kuhakikisha ipi inakuwa ya kwanza kufanikisha mradi huo ambao unatarajiwa kuleta picha mpya ya ukuaji wa uchumi wa mataifa haya mawili jirani.

Bandari ni mojawapo ya maeneo ambayo yana fursa kubwa katika ukuaji wa uchumi na majirani hawa wote sasa wanatafuta wawekezaji katika miradi ya bandari lakini kwa kuiunganisha na ile ya miundombinu ya reli za kisasa.

Hata hivyo, kwa maana ya ukubwa na umuhimu, mradi wa Bandari ya Bagamoyo una faida kubwa na muhimu zaidi kwa Tanzania kwa sababu ya faida kubwa za viwanda na kilimo zitakazosababishwa moja kwa moja na uwepo wa bandari hiyo.

Rais Samia atafanya nini?
Katika muda wote aliowahi kuwa Makamu wa Rais, Samia hajawahi kutoa kauli yake rasmi kuhusu mradi wa Bagamoyo. Hata hivyo, sasa akiwa Rais, ni wazi washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.
_118047262_8ee77ad5-1e48-4daf-b8e4-66ac5e672595.jpg

Akiwa Rais, huenda washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na CCM , watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

Dhana ya hofu dhidi ya Wachina ina mashiko miongoni mwa Watanzania wengi na ukweli kwamba hofu hiyo ilitangazwa na Rais Magufuli hadharani na katika namna ambayo ilikuwa rahisi kueleweka kwa Watanzania, inampa Rais Samia fursa ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuondoa mambo ambayo yanaweza kuwa hayana maslahi kwa taifa lake.

Bahati nzuri ambayo Watanzania wanayo kwasasa ni kwamba Samia ana asili ya Zanzibar na anajua nini maana ya bandari - pengine kuliko viongozi waliozaliwa mbali na pwani.


Chanzo: BBC SWAHILI
 
Hizo picha nimepiga leo.
Ni aibu mpaka leo bandari kubwa hakuna bagamoyo.
Na bado wanatumia JAHAZI
IMG_20210417_091131507.jpg
IMG_20210417_091134504.jpg
IMG_20210417_091137305.jpg
IMG_20210417_091158543.jpg
 
Back
Top Bottom