Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Eti nchi za kijamaa tatizo sana kuthubutu. Basi nyie jamaa muwe mnakuwa consistent kwenye hoja au kupinga kwenu, vinginevyo mnaboa sana. Serikali ikitake risk kuwekeza kwenye ndege mnapiga mayowe eti hasara, serikali ikiwa cautious kukataa uwekezaji wa kinyonyaji mnapiga mayowe eti nchi ya kijamaa.

Nimesoma hiyo makala sijaona popote panapoonyesha JPM alisema uongo kuhusu sababu za kukataa "uwekezaji" wa bandari ya Bagamoyo. Mradi wowote unaozuia msiendeleze bandari zenu zingine ni mradi wa kipuuzi. Kuna makala ya nje ilishawahi kumwita JK "easy going president", ama kweli ni easy going president peke yake anayeweza kuprioritize trillion 23 over sovereignty ya nchi yake.
 
Mkakati my ass@#$%*&!

Kwa nini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Bandar ya dar ili waingie wachina inabid ticts watoke na hapo ndipo pagumu
 
According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?

huu mradi unakuja na package ya viwanda 500 - 700......hiyo ndio feeder ya hiyo bandari..
 
Kwamba Bagamoyo itakuwa ni centre ya kupokea meli kubwa na kisha kupakua mizigo na kupakia kwenye meli ndogo kuzimbaza barani Afrika na Mashariki ya mbali.

Kwamba hata mizigo ya Tanzania itahudumiwa na bandari ya bagamoyo kisha mizigo kupakiwa kwenye malori kwenda mikoa ya Pwani na Bara.

Sasa bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara zitafanya kazi gani kwa sababu hata Malawi, Zambia Uganda Rwanda, Burundi na Congo watahudiwa na Bandari ya Bagamoyo!

Ramadhan Kareem.

hizo bandari zipo toka uhuru tumezifanyia nini?..

mbili ni kama zimekufa, hiyo moja tia maji tia maji kila siku tunashikana uchawi....
package ya viwanda 500 - 700 mzunguko wake ni zaidi ya hizo bandari zote tatu...ajira 200k serikali itachukua social security + Paye....mkoa wa Pwani + dar es salaam utakuwa busy maradufu..na biashara nyingine zitachangamka balaa...
 
1. Faidi kwa wananchi pamoja na bandari kutajengwa viwanda zaidi 700 ambapo kutazalisha ajira zaidi ya 250,000

2. Mwekezaji ndiyo anaweka fedha yake trilioni 23, sisi tunaweka 48b tu za kulipa fidia wananchi

3. Masharti yanazungumzika
Umeuona huo mkataba?
Kwanini unatuhadithia tu hapa, kwanini usitupe nasi tuuone huo mkataba?
Masharti ya mkataba ni yapi?
 
huu mradi unakuja na package ya viwanda 500 - 700......hiyo ndio feeder ya hiyo bandari..
Kama ni fix, basi hii ndio fully fix ya kuwaibia watu ikiwa kweli hicho kipengere kipo kwenye mkataba.

Yaani bandari ikijengwa tu na viwanda papo hapo vinajengwa! Maajabu ya dunia.
Hivyo viwanda vinatokea wapi?
Ni viwanda vya kuzalisha nini?
Ni mali ya nani?
Kwanini visijengwe sasa popote pale Tanzania mpaka visubiri bandari ijengwe kwanza?

Yaani kwa udogo wa mji wa Bagamoyo, viwanda zaidi ya 500 vinawekwaje?
 
hizo bandari zipo toka uhuru tumezifanyia nini?..

mbili ni kama zimekufa, hiyo moja tia maji tia maji kila siku tunashikana uchawi....
package ya viwanda 500 - 700 mzunguko wake ni zaidi ya hizo bandari zote tatu...ajira 200k serikali itachukua social security + Paye....mkoa wa Pwani + dar es salaam utakuwa busy maradufu..na biashara nyingine zitachangamka balaa...
Hizi hadithi ziliimbwa sana Mtwara wakati wa uchimbaji wa bomba la gesi.
Wakazi wa Mtwara waliimbishwa weee lakini wakakataa, mwishowe serikali ikishirikiana na Mchina ikatumia nguvu kubwa kuchukua gesi ya Mtwara.

Mpaka leo hii kiuhalisia ni kiwanda kimoja tu kimejengwa tena cha Dangote, hakuna cha viwanda wala bibi yake viwanda Mtwara. Sio serikali wala mchina aliyejenga kiwanda Mtwara baada ya kuvuna gesi.
 
Proposal ya hao Wachina ipo wapi? Source ya info yenyewe ni Kiongozi mkubwa enzi za JK ambaye hata kutaja jina lake tu aliogopa? Wezi tu hao

Wanaotetea hiyo project wajibu na kudispute alichokisema hayati Magufuli badala ya kudai tu keanba alipotosha

Lakini, from a layman’s point of view - Kwanini Bagamoyo? Kwa nini tusiende kujenga/kupanua bandari eneo ilipo bandari ya sasa ili kuadress hizo challenges za kuzidiwa? Does it make any sense kutaka kuwa na bandari mbili within a distance of 80km?
 
Katika hili la bandari ya Bagamoyo ngoja niwe neutral kwa sasa, maana ninasikia kila upande ukisema ya kwake lakini hakuna upande uliotupa huo mkataba hadharani tukauona na kuusoma.

Kwanini watu wasiuchapishe huo mkataba na kuuvujisha mtandaoni ili sote tukasoma na kuchambua sisi mwenyewe?

Kama mkataba ni siri, hao wanaotuambia uzuri au ubaya wa huo mkataba wao waliusoma wapi? Kwanini hawataki kutupa na sisi tukausoma?

MY TAKE
Hili suala kwa vyovyote vile ni suala la kimaslahi binafsi kwa wanasiasa (haijarishi ni upande wa kupinga au kutetea), na watanzania tunatumika tu kama ngazi.
Mnama hata inapotokea mtihan wa necta umevuja sio km unaletewa mtihan km mtihan unaweza letewa swali mbili tatu ktk karatasi ya kawaida ukazisolv bila kujua km ni mtihan husika
 
Bandari ijengwe kwa kushirikiana wawekezaji pamoja na serikali,Yaani serikali iwe tayri kuchangia kiasi fulani na wawekezaji wachangie kiasi fulani ili kusudi faida au hasara itakayopatika iweze kugawanywa kwa wote wawili kulingana na uwekezaji walio ufanya.
 
Huo n mkataba wa hovyo kabsa
Mkataba uwekwe wazi
 
Jomba hapo unataka kuchambua kuhusu mradi au umekuja kujustify ujenzi wa mradi huo? Mana naona umeegemea upande mmoja tu wa faida na bla bla nyingi juu ya huo mradi..kwa ufupi tunaamn maneno ya jpm mana yy ndo kausoma huo mkataba pasi na ww unaskiliza maneno ya kundi la msoga..itoshe kusema ili ukwel ujulikane..baas huo mkataba wa mradi tuletewe kisha tuusome ndipo typrove wrong maneno ya Rais.
Mana ukisema sijui ndugayai kasema hili..nani amuamn yule mtu? Kigeugeu haelewek..yaan kiufup yupo yupo tuu..
 
Tuoneshe hicho kipengele kwenye mkataba,propaganda za Jiwe
Kama ni propaganda za jiwe,waambie hao wapigadebe wakanushe waje na vipengele vya huo mkataba maana jiwe kaisha kufa kama sio kweli,sasa kama hauamini jiwe utamwamini nani? maana yeye ndiye aliyeusoma na kutuelezea yaliomo.
 
Wakuu,

Mtajadiliana maiti ilithibitishwa kuwekwa kwenye friji muda mrefu kisha ukatolewa muda kusubiri kama itahimili kutotoa harufu mbaya kisha washiriki wakazike kwa pamoja.

Cha ajabu upande mmoja wa mpango ulipewa nafasi ya kuthibitisha maiti itaoza baada muda fulani hawajawahi kuleta mrejesho.

Nina dondoo za masharti ya mkataba huo ambao ulisainiwa na Dr. Mary Nagu (Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji awamu ya nne mwaka 2013 mbele ya Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Rais wa China Xi Jinping.

Eneo ambalo bandari ya uwekezaji wa China ni miliki ya TPA na tayari walishalipa fidia kwa maeneo yaliyotwaliwa.

Kampuni inayohusika na mkataba huu inaitwa 'China Merchant Holdings International-CMHI' na 'Oman State General Reserve Fuve Fund-OSGRF'

Kuna masharti tata kumi na moja na masuala mbalimbali yanayohitaji mazungumzo ya kina na umakiniishirini na kenda (29) hapa nataja manane kwa wanajamvi kujadili kwa kina na kutoa uelekeo uliosahihi na kwa manufaa ya nchi sio kukimbilia ajira 1000 ya WaTanzania kama vibarua.
1. Mwekezaji anataka serikali ya Tanzania kurekebisha sheria za ardhi ili ziruhusu kukodishiwa ardhi hiyo kwa muda wa miaka 99 mfulululizo bila ya kuwepo mazungumzo mapya baina yake na serikali;
SERIKALI ILIPINGA ikitaka ukodishaji uwe miaka 33 tu baada ya hapo yanaweza kuwepo mazungumzo ya nyongeza ya miaka kati ya 66 au 99
2. Mwekezaji kutolipa kodi yoyote kwa kipindi chote cha uendeshaji wa bandari hiyo hadi pesa yake yake yote iliyowekezwa imerudishwa kwa faida;
SERIKALI IIKATAA ikisema hakuna msamaha wa kodi
3. Kulipwa fidia na serikali kama kampuni ya uwekezaji huo itapata hasara wajkati uendeshaji wa bandari hiyo;
4. Serikali hairuhusiwi kurekebisha chochote kwenye mkataba endapo mwekezaji atapata faida;
5.Kupunguziwa gharama za umeme na maji
SERIKALI ILIKATAA hakuna punguzo wala rzuku katika huduma ya umeme na maji
6. Hairuhusiwi bandari ya Dar Es Salaam kufanya shughuli za kibiashara kuhusiana na huduma ya upokeaji, utunzaji na usafirishaji wa shehena badala yake jukumu hilo litakuwa la bandari ya Bagamoyo inayoendeshwa na China Merchant Holdings International pekee kama kitovu cha usafirishaji wa shehena majini, Lakini pia Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zilizoko ukanda wa bahari ya hindi ikiwa pamoja na Dar Es Salaam, Tanga na Mtwara
SERIKALI ILIKATAA ikitaka masharti hayo yaondolewe kwa kuwa nchi ina haki kuendeleza maeneo yake ya kukuza uchumi
7. Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) hairuhusiwi kukanyaga eneo la uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo kwa nia ya kufuatilia, kukusanya au kudai kodi;
8. Serikali ya Tanzania hairuhusiwi kwenda kwa mwekezaji huyo kuhoji ni nani washirika wa uwekezaji wake. Mwekezaji anauwezo endapo ataona inafaa kulitwaa eneo hilo kuwa miliki yake badala ya kukodishiwa.
SERIKALI ILIKATAA ikitaka mwekezaji ni sharti awekeze na kuongozwa na sheria za Tanzania hivyo mamlaka ya nchi ina haki kuingilia kila panapoonekana hapaendi sawa ili kulinda maslahi na usalama wa nchi
Mazungumzo yaliendelea kati ya Tanzania na CMHI & SGRF mwaka 2017, lakini yavunjika Mei 2017. Hata hivyo mazungumzo yalifufuliwa tena kila upande ukiwa tayari kusikiliza hoja za mwenzake baadae wawekezaji wakashauriwa wafanyie marekebisho masharti waliyoweka ili mazungumzo yaendelee wakipewa muda maalum ukiisha, basi bandari ya Dar Es Salaam ina haki yakuendeleaa eneo lake kwa kutafuta mwekeaji mwingine mwenye tija kwa taifa.

Wanajamvi mchezo huo hapo juu...........
 
Zilezi akili za kuachia makanikia ya kisafirishwa. Huku ukisema wananchi watafaidika na msaada wa vyandarua. Vyandarua vitasaidia kupambana na mbu wa Malaria, kutengeneza vichanja vifaranga wa kuku wasichukuliwe na mwewe, vipanga na kunguru na watazitumia kama nyavu za kivulia samaki. Zote hizi ni faida za vyandarua.

Nani aliye kudanganya kuwa viwanda vinajengwa tu kwa sababu bandari iko karibu?
Soma vizuri makala mradi huo inaenda sambamba na u
Zilezi akili za kuachia makanikia ya kisafirishwa. Huku ukisema wananchi watafaidika na msaada wa vyandarua. Vyandarua vitasaidia kupambana na mbu wa Malaria, kutengeneza vichanja vifaranga wa kuku wasichukuliwe na mwewe, vipanga na kunguru na watazitumia kama nyavu za kivulia samaki. Zote hizi ni faida za vyandarua.

Nani aliye kudanganya kuwa viwanda vinajengwa tu kwa sababu bandari iko karibu?
Zilezi akili za kuachia makanikia ya kisafirishwa. Huku ukisema wananchi watafaidika na msaada wa vyandarua. Vyandarua vitasaidia kupambana na mbu wa Malaria, kutengeneza vichanja vifaranga wa kuku wasichukuliwe na mwewe, vipanga na kunguru na watazitumia kama nyavu za kivulia samaki. Zote hizi ni faida za vyandarua.

Nani aliye kudanganya kuwa viwanda vinajengwa tu kwa sababu bandari iko karibu?

Ijenzi huo unatia mdani ujenzi wa viwanda zaidi ya 700 na vitaajiri zaidi watu 250,000
 
kwa upande wangu naona bado hatuna uwezo wa kujenga kwa pesa zetu za ndani na kama tunaweza basi itachukua muda mrefu sana kukamilika, maana hio pesa ni karibia bajeti yetu ya mwaka mzima. Hivyo naona wakae chini wafanye tasmini upya kama bado una weza kuendelea basi uendelee tu. Bila shaka utaleta tija kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom