Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Yaani mtu anaweka mtaji wa Trillion 23 we unaweka bilioni 46 thn asiweke masharti ya ku secure pesa yake?

Masikini anajifungia sana ndani anaogopa kuchekwa.
 
Umesema tujadili ilimanisha utaweka hapa ushahid wote kuhusu huo mradi ila umeonesha dhahiri kuwa upo upande gan. Hii mada umeiharibu mwenyewe umeonesha porojo na ushabiki tu.
Mleta mada hayupo upande wowote, amechukua nakala kutoka kwenye link hii hapa chini ya BBC

Hakuna chochote ulichokijibu hapa badala yake na wewe umeonesha unamaslahi. Jielekeze kwenye maswali yaliyoulizwa sio kuleta longolongo nyingi zisizo na ushawishi wa namna yoyote ile. Jibu swali kwa swali wana jamvi watapembua unatetea kitu gani.
 
Hiko kitu hata mwendazake hakufanya mboni
Sasa yeye alitueleza yaliyo ndani ya mkataba,sasa nyinyi mnatetea bandari iwe chini ya mchina kwa 33 miaka.na hutakiwi kuendeleza au marekebisho yoyote ya bandari za ukanda wa pwani,
Nyinyi mtuambie hapana,mkataba hausemi hivyo
 
Kwa masharti yaleyale ya wachina aliyoyasema hayati Dr. Magufuli? 😳
 
Hapa nachokiona sio mkataba kuoneshwa, ni issue ya Trust labda unazungumzia..

Unamuamini nani zaidi.
 
Watuwekee hapa huo mkataba nasi tuusome 🙄
 
Hapa nachokiona sio mkataba kuoneshwa, ni issue ya Trust labda unazungumzia..

Unamuamini nani zaidi.
Namuamini aliyekataa na akatoa sababu za kukataa huo uwekezaji wa kitapeli
 
Namuamini aliyekataa na akatoa sababu za kukataa huo uwekezaji wa kitapeli
Of course, ni sahihi kwa upande wako binafsi na wengine wenye maono Kama yako.. if you put in that terms
 
Kwa masharti yaleyale ya wachina aliyoyasema hayati Dr. Magufuli? 😳
Zito kabwe ningemuelewa sana endapo angelisema hili kipindi MAGU yupo hai,ili tuujue ukweli,wamengoja hayupo wa kutusemea wananchi ndio wanaanza utapeli wao
 
Zito kabwe ningemuelewa sana endapo angelisema hili kipindi MAGU yupo hai,ili tuujue ukweli,wamengoja hayupo wa kutusemea wananchi ndio wanaanza utapeli wao
Wote wanaong'ang'ania huo mradi wa bandari, kwann hawakusimama na kumpinga mzee alipotoa pingamizi na akatoa sababu zake?
 
Mleta mada haujawa fair katika kuchambua, umeleta maelezo ya upande mmoja sana, maelezo ya kutetea ujenzi wa hiyo bandari tu. Hapa kuchambua mbivu na mbichi ni ngumu sana.
 
Maneno mengi ambayo ni upuuzi mtupu. Hayati JPM aliweka wazi masharti ambayo aliyaita ni kichaa tu anaye weza kusaini huo mkataba. Kwa maneno mengine vichaa ndio walioandaa mkataba na vichaaa ndio wanaoweza kuutetea huu mradi.

Bandiko lako limejaa maneno faida kubwa, faida kubwa ,faida kubwa, faida kubwa. Husemi lolote kuhusu masharti ya wawekezaji wa mradi huu. Ugomvi uko kwenye masharti semeni chochote kuhusu masharti maana yanajulikana na yalitwa ya hovyo na Watanzania wakakubaliana na Hayati, kasoro mijizi na mafisadi ndio inayo endelea kumpinga.
 
Back
Top Bottom