Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Tuna macho na baadhi yetu wanajua kusoma..., hivi kuna shida gani hii mikataba isiwekwa public ili tuweze kuona yote yaliyomo kuliko kutegemea kuambiwa ni nini kipo/hakipo ?
 
Mkakati my ass@#$%*&!

Kwa nini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Hii komenti imefanya kitimoto changu, konyagi ndogo mixer Pepsi kushuka vzuri sana.
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
Hizo Trilioni 23 ni matumizi ya serikali yote ikiwemo na misaada tunayopewa. Kwa kifupi huwezi kutengeneza huo mradi ndani ya miaka 6.
 
Yaani itakuwa ni aidha China , Oman air Korea kusini ndani ya Tz. Jw watalinda mipaka vipi Sasa wakati Kuna sehemu hawaruhusiwi kufika
 
Hakuna mwenye mkataba kujua kama alichoongea Jiwe ndicho ,ndio maana mtoa mada amesema mambo yaliyosemwa na Jiwe ilikuwa ni siasa maana hakuna aliyeuweka huo mkataba hadharani tukauoana si Jiwe au wewe hapa

Nachoona mimi siasa za kukosa ten percent na kutaka kuendeleza kwao ndio zilifanya sukuma gang kuachana na mradi wa bandari

Pia Kuhusu kuunganisha miundombinu na reli na barabara sidhani kama ni hoja maana hiyo ni wajibu wa serikali ambapo hata sasa wanatakiwa kufanya hivyo.

Kwa nini ni muhimu kwa serikali kujenga ile bandari jibu ni rahisi tuu Ili ku share costs na wawekezaji kupunguzia mzigo walipa kodi .

Mwisho uwekezaji wa hizo dola za marekani bilioni 10 haihusu kujenga bandari pekee kumbuka pale ni EPZ,na anaewekeza EPZ sio Serikali bali private sekta Kazi ya serikali ni kujenga mazingira wezeshi ikiwemo miundombinu.
 
Maneno meeengi wala sikuyasoma.
Ila vizuri zaidi mtoa mada ungeuliza:

TUNAHITAJI MAENDELEO AU TUKAE TU, TUKISUBIRI KUDRA YA MOLA?
TUNAHITAJI MAENDELEO YANAYOKUJA KWA KUTUMIA AKILI NA SIO KUDANGANYWA KUWA TUNALETEWA MAENDELEO KUMBE NI MUENDELEZO ULE ULE WA KUTUNYONYA KWA KUWATUMIA VIONGOZI WETU MAFISADI!!
 
Katika hili la bandari ya Bagamoyo ngoja niwe neutral kwa sasa, maana ninasikia kila upande ukisema ya kwake lakini hakuna upande uliotupa huo mkataba hadharani tukauona na kuusoma.

Kwanini watu wasiuchapishe huo mkataba na kuuvujisha mtandaoni ili sote tukasoma na kuchambua sisi mwenyewe?

Kama mkataba ni siri, hao wanaotuambia uzuri au ubaya wa huo mkataba wao waliusoma wapi? Kwanini hawataki kutupa na sisi tukausoma?

MY TAKE
Hili suala kwa vyovyote vile ni suala la kimaslahi binafsi kwa wanasiasa (haijarishi ni upande wa kupinga au kutetea), na watanzania tunatumika tu kama ngazi.
 
Afrika ipi inayoitaja, sisi bidhaa zetu zinakwenda sana Congo DRC na Zambia na Malawi sasa kumbuka kuna Bandari za Lami, Mombasa (zinahudumia South Sudan, Ethiopia na Uganda), Beira Mozambique inahudumia zaidi Malawi, Zimbabwe, Zambia na hata Congo, Durban S.A inahudumia Bitswana, Zimbabwe nk sasa jiulize je tunauhitaji wa Bandari ya Bagamoyo ambayo inamsharti ya hovyo hata wajukuu zetu watakuja kutushangaa kwa namna tutakavyokubali masharti yale
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
Na deni la taifa linaongezeka kwa nn?
 
Kila mtu ana maoni yake juu ya huu mradi, wapo wanao upinga, wapo wanao ungana na huu uwekezaji na wapo walio neutral.

Kila mtu atatoa sababu zake. Wengine wanatoa sababu reasonable , wengine watakurupuka kutoa sababu rubbish na wengine watabaki ku observe.

Ila ukweli inabidi upatikane quick decision making juu ya huu mradi maana ni Macro Economic Project Investment, wawekezaji wasije wakatoa maamuzi kabla ya watanzania..

Inabidi ijulikane kama iwe mbivu au mbichi haraka.
 
According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
Ref viwanda 700 vitakavyojengwa eneo law bandar
 
Kwanini mnatufanyia presentation ya picha kama aliyofanyiwa Ndugai wakati mkataba unaweza kuwekwa wazi bungeni kila kitu kikaonekana!
 
Utajuaje kwamba unanyonywa kama hukujaribu hata mradi enyewe.
The safest man is a dead man!

SIO LAZIMA UJARIBU ILI KUJUA UTANYONYWA, UKIWA NA AKILI VILE VIASHIRIA [ MASHARTI YA MRADI] VYA KUNYONYWA VITAKUJUZA KUWA HAUKO SALAMA!!!
 
Umesema tujadili ilimanisha utaweka hapa ushahid wote kuhusu huo mradi ila umeonesha dhahiri kuwa upo upande gan. Hii mada umeiharibu mwenyewe umeonesha porojo na ushabiki tu.
 
Back
Top Bottom