Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Mleta mada umewahi kuuona huo mkataba?
Umeusoma wewe mwenyewe au umehadithiwa?

Kama umeona huo mkataba, tuonyeshe na sisi huo mkataba ili tuusome kwanza. Na kama umehadithiwa, basi achana kwanza na hizo hadithi, jipe muda ya kuutafuta huo mkataba kwanza.
 
Mleta mada kachukua nakala ya BBC

Maneno mengi ambayo ni upuuzi mtupu. Hayati JPM aliweka wazi masharti ambayo aliyaita ni kichaa tu anaye weza kusaini huo mkataba. Kwa maneno mengine vichaa ndio walioandaa mkataba na vichaaa ndio wanaoweza kuutetea huu mradi.

Bandiko lako limejaa maneno faida kubwa, faida kubwa ,faida kubwa, faida kubwa. Husemi lolote kuhusu masharti ya wawekezaji wa mradi huu. Ugomvi uko kwenye masharti semeni chochote kuhusu masharti maana yanajulikana na yalitwa ya hovyo na Watanzania wakakubaliana na Hayati, kasoro mijizi na mafisadi ndio inaendelea kumpinga.
Kama ulisikia Ndugai uwanja wa majadiliano upo juu ya hayo masharti ila ukweli utabaki kuwa huo maradi unafaida kubwa.
 
Siku zote mkataba wa kibiashara huwa na pande kuu tatu za mchanganuo, ambazo ni gharama, faida na masharti.

Sasa basi tunataka tuuone kwanza huu mkataba na tuusome ili kufahamu pande zote, halafu ndio tuchambie kwa kufanya mjadala.
 
Kwamba Bagamoyo itakuwa ni centre ya kupokea meli kubwa na kisha kupakua mizigo na kupakia kwenye meli ndogo kuzimbaza barani Afrika na Mashariki ya mbali.

Kwamba hata mizigo ya Tanzania itahudumiwa na bandari ya bagamoyo kisha mizigo kupakiwa kwenye malori kwenda mikoa ya Pwani na Bara.

Sasa bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara zitafanya kazi gani kwa sababu hata Malawi, Zambia Uganda Rwanda, Burundi na Congo watahudiwa na Bandari ya Bagamoyo!

Ramadhan Kareem.
Njoo upate futru hapa
 
Mleta mada umewahi kuuona huo mkataba?
Umeusoma wewe mwenyewe au umehadithiwa?

Kama umeona huo mkataba, tuonyeshe na sisi huo mkataba ili tuusome kwanza. Na kama umehadithiwa, basi achana kwanza na hizo hadithi, jipe muda ya kuutafuta huo mkataba kwanza.
Tuutafute wote, lakini bado ukweli utabaki kuwa, maradi unafaida kubwa sana suala la masharti linazungumzika mbona kwenye madini tulikaa tukazingumza sasa tunaona faida yake
 
Nikukumbushe tu aliyesema masharti ya proposal ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni mabovu alikuwa ni Rais wa JMT, kwa maneno mengine mtu aliyekuwa na access ya taarifa zote zinazohusu taifa wakati wowote; na kwa taarifa yako tu, si kuwa alikuwa anakuwa briefed tu, alikuwa anasoma yeye mwenyewe page kwa page most of the sensitive documents. Unahitaji niongeze sauti???
 
Kama ulisikia Ndugai uwanja wa majadiliano upo juu ya hayo masharti ila ukweli utabaki kuwa huo maradi unafaida kubwa.
Una faida kubwa kwa nani?
Uwekezaji huo unawagusa wananchi, serikali na mwekezaji(mgeni). Sasa nani atavuna faida kubwa zaidi.

Yote kwa yote, uwekezaji wowote wenye kuweza kuleta faida kubwa pia una hatari ya kuleta hasara kubwa ikiwa mambo yatakwenda kombo!

Pia uwekezaji wenye kuleta faida kubwa huwa ni uwekezaji wa gharama kubwa pia. Nani atazilipa hizo gharama za uwekezaji?

Mwisho kabisa, uwekezaji mkubwa huenda sambamba na masharti makubwa (magumu!) na hufungwa (bond) kwa mkataba wa muda mrefu zaidi. Why? Kulinda mtaji wa mwekezaji.

Kufupisha story, tupewe huo mkataba sote tuuone, tuusome na kuuchambua.
 
Kama ulisikia Ndugai uwanja wa majadiliano upo juu ya hayo masharti ila ukweli utabaki kuwa huo maradi unafaida kubwa.

Sasa kwa nini wasishughulikie hayo masharti yakaboreshwa kwa faida za pande zote mbili. Wamekazana na kuitaka serikali ikubali kusaini huo mkataba. Ninge muelewa Ndungai kama angesema kwa uwazi kwamba masharti ya bandari ya Bagamoyo yana walakini mkubwa. Bunge liko tayari kusaidiana na serikali kuona ni namna gani masharti haya yanaboreshwa ili mradi uendelee kwa sababu baada ya kuboreshwa masharti utakuwa na faida kubwa.

Spika kapigia chapuo presentetion ya muwekezaji wa Kichina hapo unapata picha gani? Mradi hauna faida kama masharti ya kitapeli yata achwa ya endelee kama yalivyo. Hatuweze kuwa na ITPL nyingine ya Bandari ya Bagamoyo. Ukionja asali unachonga mzinga hakuna huo ujinga tena kwa Tanzania ya sasa.
 
Nikukumbushe tu aliyesema masharti ya proposal ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni mabovu alikuwa ni Rais wa JMT, kwa maneno mengine mtu aliyekuwa na access ya taarifa zote zinazohusu taifa wakati wowote; na kwa taarifa yako tu, si kuwa alikuwa anakuwa briefed tu, alikuwa anasoma yeye mwenyewe page kwa page most of the sensitive documents. Unahitaji niongeze sauti???
Hii pekee haitoshi kumwamini Magufuli kama alisema ukweli na sahihi. Why?
Kabla yake, Kikwete alikuwa Rais wa Tanzania na aliubariki ule mkataba. Kama tunaweza kumwamini Magufuli kwa aliyoyasema kama Rais, basi tujenge sababu pia ya Kumwamini Kikwete kwa kuwa yeye pia aliidhinisha uwekezaji ule akiwa Rais.

Upande wa pili tunajua Magufuli aliyasema yale mbele ya umma ili kujenga sababu za msingi za kuukataa ule uwekezaji. Kifupi Rais Magufuli alikuwa kipropaganda. Why?
Kama utatazama uwekezaji aliofanya Magufuli kule Chato basi utagundua Magufuli hakuwa mtu mkweli wala sahihi katika kupinga au kutetea uwekezaji fulani. He was not fair.
 
1. Faidi kwa wananchi pamoja na bandari kutajengwa viwanda zaidi 700 ambapo kutazalisha ajira zaidi ya 250,000

2. Mwekezaji ndiyo anaweka fedha yake trilioni 23, sisi tunaweka 48b tu za kulipa fidia wananchi

3. Masharti yanazungumzika
 
Tatizo sio kujengwa bandari ya Bagamoyo issue ni terms za kamtaba wenyewe. Uhalisia ni kwamba Dar aitoweza hudumia volumes za nchi zote zinazotumia bandari ya sasa iwapo hizo nchi zitafikia ukuaji wa 6%-7%.

Hivi leo tu kuna bandari ya nchi Kavu kubwa tu Pwani inayotumiwa na Dar kwa sababu ya mizigo, ina maana wanaanza kukosa nafasi Dar ya kutunza mizigo.

Wataiongeza hiyo bandari ya Dar ila kwa mazingira yake itafikia tu saturation point kutokana na kuongezeka kwa volumes za nchi jirani lazima kuwe na Mbadala.

If you ask me uwekezaji wa China wa $10 billion atuhitaji wote; TPA ijikite kwenye costs za bandari yenyewe pekee. Kama bandari na ofisi zake zitagharimu labda $4 billion huo ndio mkataba wa BOT unaouhusu serikali miaka mingapi wachina waendeshe port.

Hizo $6 billion zinazobaki kwenye miradi mingine zichukuliwe kama FDI subject to business taxation laws za Tanzania.

Wasituchanganyie 60% ya mahindi na 40% ya mchele kwenye gunia moja halafu wauze kwa bei ya mchele. Busara ni kuuweka huo mkataba wazi.
 
Sasa kwa nini wasishughulikie hayo masharti yakaboreshwa kwa faida za pande zote mbili. Wamekazana na kuitaka serikali ikubali kusaini huo mkataba. Ninge muelewa Ndungai kama angesema kwa uwazi kwamba masharti ya bandari ya Bagamoyo yana walakini mkubwa. Bunge liko tayari kusaidiana na serikali kuona ni namna gani masharti haya yanaboreshwa ili mradi uendelee kwa sababu baada ya kuboreshwa masharti utakuwa na faida kubwa.

Spika kapigia chapuo presentetion ya muwekezaji wa Kichina hapo unapata picha gani? Mradi hauna faida kama masharti ya kitapeli yata achwa ya endelee kama yalivyo. Hatuweze kuwa na ITPL nyingine ya Bandari ya Bagamoyo. Ukionja asali unachonga mzinga hakuna huo ujinga tena kwa Tanzania ya sasa.
Uwekezaji ni biashara sio msaada.
Hakuna mtu anakuja kuwekeza hapa Tanzania kwa sababu anawapenda au anawahurumia watanzania.

Kama uwekezekaji ule una masharti magumu maana yake ujue hapo hapo kwenye hayo masharti magumu ndipo hapo hapo pameficha faida ya mwekezaji. Mwekezaji akiondoa hayo masharti ujue atakwenda kuvuna hasara! Na hakuna mwekezaji mjinga hapa duniani.
Nani kauona huo mkataba?

#tupeweMKATABA
 
1. Faidi kwa wananchi pamoja na bandari kutajengwa viwanda zaidi 700 ambapo kutazalisha ajira zaidi ya 250,000

2. Mwekezaji ndiyo anaweka fedha yake trilioni 23, sisi tunaweka 48b tu za kulipa fidia wananchi

3. Masharti yanazungumzika
Hapo ndio serikali inatakiwa kuwa makini haya maswala ya viwanda ni aspect za FDI zenye rules nyingine.

Serikali aina interest na ubia wa ivyo viwanda, bali bandari. Cost za bandari ndio terms zake ziwe negotiated; costs za viwanda ziwe separated subject to TRA investment rules.

Wasituletee uhuni hapo ivyo viwanda wavimiliki wenyewe 100%, hatuna shida na ubia huko; tunachotaka bandari.

Kama kuna reli inayoenda unganisha bandari na mainline, hizo gharama ziwe mkopo kwa serikali 100% zilipwe kivingine.

Basically different constituents of the whole investment should be treated differently based on what is important to us. Sio watuletee uhuni wa kila kitu ndani ya gunia moja, mengine hatuna shida nayo sisi ni kwa faida zao.
 
1. Faidi kwa wananchi pamoja na bandari kutajengwa viwanda zaidi 700 ambapo kutazalisha ajira zaidi ya 250,000

2. Mwekezaji ndiyo anaweka fedha yake trilioni 23, sisi tunaweka 48b tu za kulipa fidia wananchi

3. Masharti yanazungumzika

Zilezi akili za kuachia makanikia ya kisafirishwa. Huku ukisema wananchi watafaidika na msaada wa vyandarua. Vyandarua vitasaidia kupambana na mbu wa Malaria, kutengeneza vichanja vifaranga wa kuku wasichukuliwe na mwewe, vipanga na kunguru na watazitumia kama nyavu za kivulia samaki. Zote hizi ni faida za vyandarua.

Nani aliye kudanganya kuwa viwanda vinajengwa tu kwa sababu bandari iko karibu?
 
Hii pekee haitoshi kumwamini Magufuli kama alisema ukweli na sahihi. Why?
Kabla yake, Kikwete alikuwa Rais wa Tanzania na aliubariki ule mkataba. Kama tunaweza kumwamini Magufuli kwa aliyoyasema kama Rais, basi tujenge sababu pia ya Kumwamini Kikwete kwa kuwa yeye pia aliidhinisha uwekezaji ule akiwa Rais.

Upande wa pili tunajua Magufuli aliyasema yale mbele ya umma ili kujenga sababu za msingi za kuukataa ule uwekezaji. Kifupi Rais Magufuli alikuwa kipropaganda. Why?
Kama utatazama uwekezaji aliofanya Magufuli kule Chato basi utagundua Magufuli hakuwa mtu mkweli wala sahihi katika kupinga au kutetea uwekezaji fulani. He was not fair.
Umeiweka vizuri sana, Magufuli alililisema hili hadharani, na siyo siri kuwa Kikwete alikuwa madarakani wakati mchakato huu unaanza na pia China inahusika na mradi huu. Kama ni hivyo, kwanini China haijajitokeza hadharani kukanusha? China hawajawahi kuwa na unafiki, kila siku wanaparurana na Marekani huko kwenye MSM. Kwa nini Kikwete hajatoka hadharani kukanusha? Bila shaka wanajua alichosema Magufuli ndio ukweli. Hata yule Kakoko wa bandari alisema the same, sijaona aliyekanusha.

Ya Chato ni muktadha tofauti na huu. Tumalize hili kwanza.
 
Back
Top Bottom