Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Huu mradi ni mzuri Sana na unamanufaa makubwa tu,

Baada ya mh Rais aliyepita ambaye ni Hayati sasa kubainisha mapungufu yaliyomo kwenye Mkataba, kila mtu ulimtia kinyaa kuukubali lakini Mimi niliamini ni lazima Mkataba huu usainiwe upya baada ya kurekebishwa Baadhi ya vipengere kwenye Mkataba

Alichoweza kuanza nacho JPM ni kuziboresha Kwanza bandari zetu zote ili baada ya hapo kufanyike mazungumzo Kati ya serikali na wawekezaji hao kuona namna bora ya kuuingia huo Mkataba

Na Kwa kuwa bandari zetu sasa zimeboreshwa na kama Bado wamalizie ili sasa mwekezaji huyo aruhusiwe

Endapo kungesainiwa hivyohivyo bila kujali athari zilizomo kwenye Mkataba, bandari zetu zote zingekufa na Uchumi wetu ungeharibika vibaya na ikizingatiwa nchi yetu Kwa asilimia kubwa inategemea Uchumi wa bandari hizi

Mashariti mojawapo ya Mkataba huo, ilikuwa ni kutozikarabati bandari zetu zote Hadi miaka yote iliyopendekezwa na mwekezaji Kati ya miaka (99) na ndiyo maana JPM alianza na ukarabati wa Maana karibu bandari zote
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
Bandari ni kitu muhimu kwa maslahi ya taifa ni bora srikali ikawekeza yenyewe badala ya sekta binafsi. Hili ni suala la kiusalama tu
 
Km wanataka si wakajenge Mtwara wakainue na mikoa ya kusini...
kuna haja gani ya kujenga bandari mbili in a close proximity.

Tukishajenga bandari ya Bagamoyo hii ya Dar tunaifanya makumbusho au?

Na je bandari ya Dar imezidiwa mpaka tujenge nyingine?na km ndivyo kwann tusijenge wenyewe?
 
Bandari ijengwe maana itafungua fursa zaidi kuliko iligyo sasa

Hofu yangu ni je wawekezaji wale bado wako tayari kuwekeza au ndio wameshasepa maana tayari Lamu inafanya Kazi na bandari yenye ukubwa karibu na huo inajengwa Msumbiji kwa hiyo ile potential huenda kwa sasa ikawa haipo na wawekezaji wakasita kuleta pesa zao.

Mwisho Serikali ya mama ifanye tathmnini ya mradi na kuona kama wanaweza kuendelea nao na huu ndio utakuwa legacy yako mama itakahoishi miaka na miaka,kizazi na kizazi.

Hata hiyo sgr yenu Ili iwe na tija ni lazima kupatikane bandari kubwa itakayoweza kuifanya iwe operational vinginevyo maskini wa nchi hii hakuna siku watakuja kuona unafuu wa maisha
Wasepe waende wapi? Wana pa kwenda penye uchochoro wa bwereree kama Tanzania? Nchi nyingine zinajitambua na haziwezi kuingia mkataba wa kijinga namna hiyo. Ni Tanzania tu yenye viongozi wenye uchu wameona uwezekeno wa kuhonga ili wachukue hicho kipande. Hawa ni watu hatari sana sana na wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote.
 
Kwamba bandari ya Bagamoyo ikipokea mizigo itasambaza bidhaa Tanzania na nchi jirani kwa kutumia barabara za nchi gani vile?

Kwamba baada ya kujenga hiyo bandari ambayo wajanja mnahaha kuipamba chumba cha mwali itasafirishwa kwa njia ya reli itakayojengwa na nani vile?

Kwamba ukishajenga bandari Bagamoyo ni sharti ujenge pia barabara na reli kutoka hapo hadi iunganishe reli ya kwenda Tanga, Kilimanjaro na Arusha na kupitia Mlandizi au Chalinze na kuunganisha na reli ya kati

Kwamba ni sharti ujenge daraja himilivu kukatisha mto Ruvu ili kusambaza bidhaa husika kwa walengwa bara na nchi jirani?

Gharama hizi nani atazibeba?

Nchi itanufaika na kitu gani kwa kulinganisha na tulivyoambiwa nchi hairuhusiwi kudai kodi hapo kwa muda wa miaka 33?

Nani atakuwa mmilki wa ardhi ambayo uwekezaji huo utafanyika>

Bandari za Dar Es Salaam, Mtwara na Tanga zitakuwa zinafanya kazi gani kama mpaka sasa Mtwara na Tanga bado hazijatumika ipasavyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na wananchi wake?

Kwanini huo mkataba wa bandari ya Bagamoyo ni wa siri sana wakati unaonesha hauungwi mkono na walipa kodi wenyewe?

Je, uwekezaji wa bandari hio kama unavyopigiwa chapuo unatofauti gani na sera za kuweka rehani madini na rasilimali zingine za nchi kwa wageni kama ilivyonadiwa na mgombea mmojawapo katika uchaguzi mkuu uliopita 2020?

Huo mradi wa mwekezaji wa bandari kutoka China, ni akina nani wako kwenye umiliki na bodi ya wakurugenzi?

Kwanini mradi huo moja ya masharti yake ni kutoendeleza, kupanua au kushindana na bandari hiyo ya mabwanyenye wakiTanzania wanaojificha nyuma ya mgongo wa uwekezaji mkubwa?

Je, Kina cha bahari hapo Mbegani Bagamoyo ni kirefu kuzidi cha bandari ya Mtwara na Tanga?

Kitu gani kilichoshindikana kuongeza kina cha maji katika la kuingilia bandari ya Dar Es Salaam hivyo kufanikisha kuingiza meli kubwa za urefu wa mita 300 hadi400 kama inavyodaiwa?

Wapiga debe wa mradi huu wa bandari mnapoteza muda kama mlishakula mlungula mtazitapika muda sio mrefu
 
Km wanataka si wakajenge Mtwara wakainue na mikoa ya kusini...
kuna haja gani ya kujenga bandari mbili in a close proximity.

Tukishajenga bandari ya Bagamoyo hii ya Dar tunaifanya makumbusho au?

Na je bandari ya Dar imezidiwa mpaka tujenge nyingine?na km ndivyo kwann tusijenge wenyewe?
Hizi ni propaganda za watu wenye uchu kama mafisi na hakuna faida kwa nchi. Mwarabu anatumia nguvu kubwa kupora nchi yetu kwa kuhonga viongozi wetu. Kwanza kwa usalama wa nchi ni jambo baya sana kukabidhi milki ya bandari ya nchi kwa nchi nyingine. Itatumika kutoroshea raslimali zetu. Hilo ndolo lengo kubwa na haya mengine ni visingizio tu.
 
Km wanataka si wakajenge Mtwara wakainue na mikoa ya kusini...
kuna haja gani ya kujenga bandari mbili in a close proximity.

Tukishajenga bandari ya Bagamoyo hii ya Dar tunaifanya makumbusho au?

Na je bandari ya Dar imezidiwa mpaka tujenge nyingine?na km ndivyo kwann tusijenge wenyewe?
Kama umesoma vizuri makala hii majibu yako yanajibiwa
 
Bandari ni kitu muhimu kwa maslahi ya taifa ni bora srikali ikawekeza yenyewe badala ya sekta binafsi. Hili ni suala la kiusalama tu
Wwew unaona kama mimi. Ni ujinga kumkadhi mgeni ufunguo wa nyumba yako. Bandari na Airport siyo vitu vya kuendeshwa na nchi nyingine. Huu ni wendawazimu. Hata hao wanaoshawishi ijengwe kama kina Zitto wanapaswa kuwekwa kwenye kundi la wasaliti wa nchi. Wanasaliti nchi kwa vipande vya fedha walizoahidiwa. Madhara ya kuwapa watu wengine bandari yetu waisimamie ni makubwa sana.
 
Hoja MUFILISI
Eti bandari ya bagamoyo itaua bandari ya dar.
Kwani bagamoyo ipo KENYA?.
mapato si yataingia serikalini.?.
Hii bandari kujengwa ni hatari sana kwa usalama wa raslimali za nchi yetu. Unamjua mwarabu na mchina wewe? Wenzako wameshaona mbali na lengo kubwa la kujenga bandari hii ni kuitumia kutolea malighafi za viwanda vyao. Hata kwenye hiyo zone wakijenga viwanda lakini bado mali itakayozalishwa itachukuliwa juu kwa juu na kwenda kuuzwa sehemu nyingine. Wanajua hakuna wa kuwazuia kufanya hivyo kwa sababu watatumia rushwa.
 
According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
Hili nalo la muhimu kuangalia. Ni sawa na Dreamliner inaishia kwenda Mwanza.
 
Hakika, tutakuja kujuta. Nafuu hata ungekuwa uwekezaji wa wazawa tungebanana humu ndani, Wachina na WaOman tutawapata itakuwa kasheshe
Bandari ni kitu muhimu kwa maslahi ya taifa ni bora srikali ikawekeza yenyewe badala ya sekta binafsi. Hili ni suala la kiusalama tu
 
Back
Top Bottom