Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha unafikiHuyo nae alikuwa anajiendeshea nchi shaghla baghla,, wasiomjua wanaamini alikuwa bora lakini tulioishi kwenye uongozi wake mbele lilikuwa giza totolo.
Mtu asiyeshaurika hawezi kuwa bora.
Discussion huleta matokeo mazuri lakini kujiamlia tu kuna michemko sana.
Aliishi kwa uongo sana.
When the geniuses are too silent and the laymen are too clever. It is a paradox.Bungeni kuna mtu wa kujadili mkataba uonavyo? Wenye akili wanasubiria tuu posho, hawana mpango na mijadala. Mijadala inatawaliwa na akina Lusinde, Msukama et al
Mimi najiuliza kama tumeweza kujenga bwawa la Rufiji,hii bandari kwa nini tusikomae nayo wenyewe
Mkataba uende bungeni, kwanini mikataba isiwe public kwanini ifichwe tu halafu mtu anakwambia kile anachotaka kukwambia.Hakuna mkataba utakaopelekwa Bungeni. Kama tunakubali kuiuza nchi tuiuzeni tu. Wajukuu na vitukuu wetu watatuona wajinga na watamkubali sana our best president, Dr. JPM.
Umenena Vema.Hapa wanaitajika watalaam wa mikataba
Siyo ati wazee wenye umri.mambo yanabadirika kulingana na muda na experience.
Tuache kudemka.,au kuzingua
BANDARI HII IJENGWE TU TIME IS MONEY HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA ISPOKUWA MIKATABA YAKE LAZIMA IWE WAZI WATANZANIA WOTE WAUPITIE NA BUNGE NALO LIUPITIE PIA USIWE MREFU ZAIDI YA MIAKA 30,MAMLAKA ZETU ZA KODI ZIWEZE KUKUSANYA SHURU ZAKE HAPO.
Mkataba upi ulishawahi kuwekwa hadharani tangu nchi yetu ilipopata uhuru?Mkataba uende bungeni, kwanini mikataba isiwe public kwanini ifichwe tu halafu mtu anakwambia kile anachotaka kukwambia.
Weka mikataba hadharani ijadiliwe ikataliwe kama haina faida tutafute njia nyingine za kusponsor miradi. Lakini inafichwa fichwa tu.
Ndiyo tuanze kuiweka hadharani tulikuwa tunaelekea huko ila mwendazake akajiondoa kwenye mkataba wa transparency😅😅😅Mkataba upi ulishawahi kuwekwa hadharani tangu nchi yetu ilipopata uhuru?
tuachane na Tanzania: nchi gani duniani ilishawahi kuweka mikataba ya aina hii hadharani?Ndiyo tuanze kuiweka hadharani tulikuwa tunaelekea huko ila mwendazake akajiondoa kwenye mkataba wa transparency😅😅😅
Sasa sijui aliogopa nini maana hakutaka hata aliyoingia yeye mheshimiwa aliyemaliza ufisadi, nabii mbeba maono, mzalendo namba moja tuijue
Umeshaambiwa Dar port ni ndogo ukilinganisha na Bagamoyo, kitu ambacho ni kweli...Mkakati my ass@#$%*&!
Kwanini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Tujiulize hivi ni kwa nini historically Bandari ya Bagamoyo (kipindi cha ukoloni /biashara ya watumwa na meno ya tembo) ndiyo ilikuwa lango kuu la biashara?? Jibu ni kwamba iko centrally located na iko vizuri kwa meli kuingia na kutoka, tena bila kujengwa miaka hiyo. Ni bahati mbaya sana kwamba viongozi wetu hili hawakuliona, labda kwa sababu enzi hizo walichoona ni urahisi na kuiendeleza bandari ya Dar kwa sababu ya uwepo wa reli ya kati kipindi hicho, na pia urahisi wa kuisimamia bandari hiyo kwani ilikuwa jirani na maofisi ya nchi.Ni muhimu sana kusoma kabla ya kukurupuka,bandari kubwa ukanda wote wa Afrika unauliza nani ataleta meli? Kwani zinazotua dar kea sasa au mombasa serikali inazileta?
Afu uelewe maana ya kuwa lango na mfano wake ni ule wa port ya Dubai ambako 80% ya bidhaa zinazokuja Afrika zinapitia ,so kwa kuwepo Bagamoyo means kuchukua japo 20% ya share yake tayari ku lisha Afrika.
Tuulizane sgr ya tani zote hizo inajengwa itabeba mzigo gani wakati kabandari hakaruhusu mzigo mkubwa?
Afu tunavyodelay ndivyo Lamu na nakala ports zitakavyotake advantage .Nchi za kijamaa ni tatizo Sana maana watu ni waoga wa kutake risks as if Dunia inakusubiria.
Hii ni sawa na kusema eti tusivune madini tusubirie vizazi ,hii ni nonsense yeknology inabadilika huenda yakawa useless huko baadae lazima tuyavune sasa Ili tujenge msingi wa uchumi imara na kuandaa kizazi kijacho
Unapata wapi nguvu ya ku comment kitu ambacho hujakisoma??Maneno meeengi wala sikuyasoma.
Ila vizuri zaidi mtoa mada ungeuliza:
TUNAHITAJI MAENDELEO AU TUKAE TU, TUKISUBIRI KUDRA YA MOLA?
Unaelewa maana ya Trilioni 23???Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.
Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
Kwa taarifa za karibuni toka kwa Waziri wa Uchukuzi Engineer Leonard, ambaye sio mchumi kama ZZK, ni kwamba mradi huo sio viable kwani idadi ya mizigo bado ni kidogo, hivyo najiongezea wawekezaji anaweza kukaa miaka 200 badala 99MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.
Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.
Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wanchi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.
Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.
Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari.
Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.
Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari, Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.
Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika.
Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.
Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji.
Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.
Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka.
Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.
Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam.
Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.
Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).
Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited(China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute(STEPI)Korea Kusini.
Hofu ya Mradi wa Bagamoyo
Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka.
Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.
"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.
Spika Job Ndungai aliwahi kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa.
Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.
Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?
Mmoja wa viongozi wa juu katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambao mradi huo ulikuwa unaelekea kukamilika, ameniambia mengi ya yanayoyosemwa kuhusu mradi huo hayana ukweli na kwamba kulikuwa na upotoshaji mkubwa.
Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yake, kiongozi huyo alisema gharama pekee kubwa ambayo serikali ingetakiwa kuingia katika mradi huo ni ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa kupisha ujenzi wa bandari hiyo ambao kwa makisio ya mwaka 2016 yalikuwa kiasi cha dola takribani dola milioni 20.9 (shilingi bilioni 43).
" Gharama yetu ni hizo dola milioni 20 za kulipa wananchi lakini mengine yote ni siasa tu. Wanaokuja wanaleta shilingi trilioni 23 na ni uwekezaji wala si mkopo. Ni sawa na kampuni zinazokuja kuchimba madini hapa kwetu. Huwezi kusema wanakuja kutukopesha hela za kuchimba madini. Ni biashara yao.
" Jambo la muhimu kuliko yote ni kwamba huo mpango wa kuwa na Bandari ya Bagamoyo tulikuwa nao hata kabla wawekezaji hawajaja. Na wala hakuna masharti ya kutuzuia kujenga barabara wala miundombinu mingine. Hilo suala la miaka 33 ni la kawaida, yaani mtu aweke shilingi trilioni 23 na halafu asiweke muda wa kurudisha hela zake? Mwisho kabisa, baada ya miaka 33, bandari na hivyo viwanda havitahamishwa Tanzania na nina imani nchi yetu itakuwepo bado," alisema kiongozi huyo.
Huku Lamu, kule Bagamoyo
Kenya, kwa muda mrefu, ilikuwa ikitegemea Bandari ya Mombasa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo kwa wateja wake wa ndani na katika eneo la maziwa makuu. Kwa sababu ya ongezeko la mahitaji, yenyewe pia ikaamua kujenga Bandari ya Lamu - kwa sababu zilezile ambazo zimeifanya Tanzania kuwa na mpango wa Bagamoyo.
Hadi sasa, nchi hizi mbili zinashindana katika kuhakikisha ipi inakuwa ya kwanza kufanikisha mradi huo ambao unatarajiwa kuleta picha mpya ya ukuaji wa uchumi wa mataifa haya mawili jirani.
Bandari ni mojawapo ya maeneo ambayo yana fursa kubwa katika ukuaji wa uchumi na majirani hawa wote sasa wanatafuta wawekezaji katika miradi ya bandari lakini kwa kuiunganisha na ile ya miundombinu ya reli za kisasa.
Hata hivyo, kwa maana ya ukubwa na umuhimu, mradi wa Bandari ya Bagamoyo una faida kubwa na muhimu zaidi kwa Tanzania kwa sababu ya faida kubwa za viwanda na kilimo zitakazosababishwa moja kwa moja na uwepo wa bandari hiyo.
Rais Samia atafanya nini?
Katika muda wote aliowahi kuwa Makamu wa Rais, Samia hajawahi kutoa kauli yake rasmi kuhusu mradi wa Bagamoyo. Hata hivyo, sasa akiwa Rais, ni wazi washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.
Akiwa Rais, huenda washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na CCM , watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.
Dhana ya hofu dhidi ya Wachina ina mashiko miongoni mwa Watanzania wengi na ukweli kwamba hofu hiyo ilitangazwa na Rais Magufuli hadharani na katika namna ambayo ilikuwa rahisi kueleweka kwa Watanzania, inampa Rais Samia fursa ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuondoa mambo ambayo yanaweza kuwa hayana maslahi kwa taifa lake.
Bahati nzuri ambayo Watanzania wanayo kwasasa ni kwamba Samia ana asili ya Zanzibar na anajua nini maana ya bandari - pengine kuliko viongozi waliozaliwa mbali na pwani.
View attachment 1751788View attachment 1751789View attachment 1752847