Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Wachina watatupiga km walivyowapiga Wakenya kwenye SGR, Siri Lanka and Eritrea kwenye Bandari.
Hii bandari tuijenge wenyewe taratibu, hatuna haraka nayo.
Km tumeweza SGR, bwawa la Nyerere hili haliwezi kutushinda.
 
Acha unafiki
 
Tuijenge wenyewe. Miaka kumi tu Au kumi na tano tutakuwa tumemaliza. Tuachane na mikataba ya ki-Chief Mangungu.
 
Bungeni kuna mtu wa kujadili mkataba uonavyo? Wenye akili wanasubiria tuu posho, hawana mpango na mijadala. Mijadala inatawaliwa na akina Lusinde, Msukama et al
When the geniuses are too silent and the laymen are too clever. It is a paradox.
 
Mimi najiuliza kama tumeweza kujenga bwawa la Rufiji,hii bandari kwa nini tusikomae nayo wenyewe

NGOJA TUMALIZE BWAWA LA RUFIJI NA STANDARD GAUGE RAILWAY PAMOJA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE NDIO TUFIKIRIE JINSI YA KUPAMBANA NA HIYO MIKUBWA MINGINE!!! HARAKA HARAKA YA NAMNA HIYO ITAKUJA KUTUPASUA.
 
Hakuna mkataba utakaopelekwa Bungeni. Kama tunakubali kuiuza nchi tuiuzeni tu. Wajukuu na vitukuu wetu watatuona wajinga na watamkubali sana our best president, Dr. JPM.
Mkataba uende bungeni, kwanini mikataba isiwe public kwanini ifichwe tu halafu mtu anakwambia kile anachotaka kukwambia.
Weka mikataba hadharani ijadiliwe ikataliwe kama haina faida tutafute njia nyingine za kusponsor miradi. Lakini inafichwa fichwa tu.
 
Good presentation haimanishi good mkataba.presentation ni just kama foot print.






Let's discuss in detail

Hapa wanaitajika watalaam wa mikataba
Siyo ati wazee wenye umri.mambo yanabadirika kulingana na muda na experience.

Tuache kudemka.,au kuzingua
 
BANDARI HII IJENGWE TU TIME IS MONEY HAKUNA MUDA WA KUPOTEZA ISPOKUWA MIKATABA YAKE LAZIMA IWE WAZI WATANZANIA WOTE WAUPITIE NA BUNGE NALO LIUPITIE PIA USIWE MREFU ZAIDI YA MIAKA 30,MAMLAKA ZETU ZA KODI ZIWEZE KUKUSANYA SHURU ZAKE HAPO.

Acha ujuha cc huku Tanga tuko bandarini tunashinda tumelala hakuna mizgo bado huko mtwara nako hali ndo ileile af ijengwe nyingine bagamoyo au unafikili kwa kutumia matako?
 
Mkataba upi ulishawahi kuwekwa hadharani tangu nchi yetu ilipopata uhuru?
 
Mkataba upi ulishawahi kuwekwa hadharani tangu nchi yetu ilipopata uhuru?
Ndiyo tuanze kuiweka hadharani tulikuwa tunaelekea huko ila mwendazake akajiondoa kwenye mkataba wa transparency😅😅😅
Sasa sijui aliogopa nini maana hakutaka hata aliyoingia yeye mheshimiwa aliyemaliza ufisadi, nabii mbeba maono, mzalendo namba moja tuijue
 
tuachane na Tanzania: nchi gani duniani ilishawahi kuweka mikataba ya aina hii hadharani?
 
Mkakati my ass@#$%*&!

Kwanini hao china wasitumie bandari ya dar ambayo ipo tayari na marekebisho yake hayataitaji pesa nyingi?
Umeshaambiwa Dar port ni ndogo ukilinganisha na Bagamoyo, kitu ambacho ni kweli...
 
Tujiulize hivi ni kwa nini historically Bandari ya Bagamoyo (kipindi cha ukoloni /biashara ya watumwa na meno ya tembo) ndiyo ilikuwa lango kuu la biashara?? Jibu ni kwamba iko centrally located na iko vizuri kwa meli kuingia na kutoka, tena bila kujengwa miaka hiyo. Ni bahati mbaya sana kwamba viongozi wetu hili hawakuliona, labda kwa sababu enzi hizo walichoona ni urahisi na kuiendeleza bandari ya Dar kwa sababu ya uwepo wa reli ya kati kipindi hicho, na pia urahisi wa kuisimamia bandari hiyo kwani ilikuwa jirani na maofisi ya nchi.
 
Unaelewa maana ya Trilioni 23???
 
Kwa taarifa za karibuni toka kwa Waziri wa Uchukuzi Engineer Leonard, ambaye sio mchumi kama ZZK, ni kwamba mradi huo sio viable kwani idadi ya mizigo bado ni kidogo, hivyo najiongezea wawekezaji anaweza kukaa miaka 200 badala 99
 
Ngoja tumalizie kujenga jiji la Chato kwanza! Lina faida zaidi kukiko Bandari ya Bagamoyo.

Yaani Propaganda 101 (ya 'mwalimu' JPM) ilikuwa hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…