Bandari ya Bagamoyo ikijengwa CCM ijindae kwa adhabu pia

Bandari ya Bagamoyo ikijengwa CCM ijindae kwa adhabu pia

rugumye

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
561
Reaction score
179
Wakati sakata la gesi ya Mtwara halijaisha CCM kupitia kwa Mwenyekiti wake Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete amesaini mktaba wa kujenga bandari nyingine huko Mbegani Bagamoyo Nyumbani kwa Rais, huku zile za Mtwara na Tanga zikiachwa hoi, CCM ikumbuke kuwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni kaburi lake katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Tanga, Lindi na Mtwara ni ngome za CCM zilizobaki na itakuwa ni kura ya turufu kwa kambi ya upinzani.

Baada ya sakata la gas wananchi wa Mtwara wasikie tena bandari yao kwisha kazi na gas inatakiwa kutoka Mtwara kwenda Bagamoyo kwenye eneo maalumu la viwanda-EPZ, huku, Tanga nao matumaini ya kuboreshwa kwa bandari yao sasa itakuwa ni ndoto kwa kuwa bandari mbadala itajengwaBagamoyo kwa nini wananchi wasichukue hatua dhidi ya CCM? bandari ya bagamoyo jengeni lakni jiandaeni kwa adhabu pia, kanda ya ziwa CCM ni taabani, Mbeya kwisha, Kaskazini hakuna kitu, Magharibi CCM chupuchupu kukosa mbunge hata mmoja katka uchaguzi uliopita.

Nawasilisha.
 
Bado nakosa imani na baraza la mawaziri lililojaa watu wanaojiita ma Dr. na ma Prof.

Kama watu wa mikoa hiyo wakiendelea kuichagua CCM basi umasikini ni haki yao na waendelee kuwa nao tu

Hivi ule mpango wetu wa miaka mitano uliozinduliwa kwa mbwembwe ni serikali ipi inatekeleza?
 
Kujenga bandari Bagamoyo wakati ile ya Dar haijaboreshwa ilivyo ni matusi ya Kikwete kwa wananchi wa Tanzania kwani anaonesha wazi ubabe wa kupendelea sehemu anayotoka; siku hizi kila uwekezaji ni Bagamoyo ili kumpendezesha Mfalme lakini ijulikane tu kuwa kila jambo lina mwisho wake!!
 
Nchi hii sasa kila kitu siasa

Kuna siku hata mkifunga choo mtakuja kulalama chadema au ccm zimeleta hayo

We will never progress with our current mindset
 
Well said Mkuu!!
Halafu kwa akili finyu ya JK anafikiria akiwajengea bandar wakwele wenzie watapata maendeleo!! Ki vipi? Bandari pekee haiwezi kuwaenedelelza wakwere. Ili waendelee lazima wasome. Bahati mbaya JK kashindwa kuwashawishi nduguze wasome.

Kama bandari ingekuwa na uwezo wa kuendeleza watu wanaoizunguka, Wazaramo wasingekuwa hivi walivyo. Wageni ndiyo wanaendelea wakati wao wanazidi kuuza maeneo yao na kutokomea kusikojulikana. Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa wakwele. Watu wa mbali wataenda Bagamoyo na kuwanunua wakwere. Kwa kupeleka bandari huko ni sawa na kuchangia kutoweka kwa wakwele. JK halijui hili.

Hebu niwahi Bagamoyo nikanunue ardhi kabla haijaisha!!
 
Watu wamenyang'anywa ardhi bagamoyo (kable ya bagamoyo mjini) kwa ajiri ya ujenzi wa eneo maalumu la viwanda yaani EPZ, pale chalinze shirika la nyumba lilijenga maghorofa 2 apartment polini, kwa sasa kuna mradi mkubwa wa maji yanasambazwa chalinze na vijiji vyote kutoka mto wami, na kuna phase 2 inaanza muda wowote, kama Kila Rais atakuwa selfish basi ni hakika kila kabila litapigana Rais atoke kwao. ALitaka kubomoa barabara chalinze segela mbunge seleli kutoka Nzega Tabora akahoji bajeti ilikotoka sasa tumemsahau kwenye siasa.
 
Well said Mkuu!!
Halafu kwa akili finyu ya JK anafikiria akiwajengea bandar wakwele wenzie watapata maendeleo!! Ki vipi? Bandari pekee haiwezi kuwaenedelelza wakwere. Ili waendelee lazima wasome. Bahati mbaya JK kashindwa kuwashawishi nduguze wasome.

Kama bandari ingekuwa na uwezo wa kuendeleza watu wanaoizunguka, Wazaramo wasingekuwa hivi walivyo. Wageni ndiyo wanaendelea wakati wao wanazidi kuuza maeneo yao na kutokomea kusikojulikana. Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa wakwele. Watu wa mbali wataenda Bagamoyo na kuwanunua wakwere. Kwa kupeleka bandari huko ni sawa na kuchangia kutoweka kwa wakwele. JK halijui hili.

Hebu niwahi Bagamoyo nikanunue ardhi kabla haijaisha!!

Kama Mwl angekuwa mbinafsi basi butiama ingekuwa London ya bongo. akumulikae mchana usiku anakuchoma. haya ni ya wzi je tusiyoyajua?
 
Huu mradi ni vema tukautumia vema ili kuichonganisha CCM na wnanchi wa maeneo yalioshaulika.ANIA
WATANZANIA WATAMBUE KUWA CCM NI CHAMA CHA FAMILIA YA KIKWETE NA KWA SASA KINATEKELEZA MIPANGO YA KUINDELEZA BAGAMOYO NA KUYATELEKEZA MAENEO MENGINE YA TANZANIA.
CHAMA HIKI HAKIFAI KUENDELEA KUITAWALA NCHI HII KWA NGAZI YOYOTE ILE.......TUKATAE KABISA!
 
Kuwa na baba masikini sio kosa, ila kuwa na baba mkwe masikini ni kosa kwani tunachagua. So watanga, wamtwara na kanda zingine kazi kwenu
 
Wakati sakata la gesi ya Mtwara halijaisha CCM kupitia kwa Mwenyekiti wake Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete amesaini mktaba wa kujenga bandari nyingine huko Mbegani Bagamoyo Nyumbani kwa Rais, huku zile za Mtwara na Tanga zikiachwa hoi, CCM ikumbuke kuwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni kaburi lake katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Tanga, Lindi na Mtwara ni ngome za CCM zilizobaki na itakuwa ni kura ya turufu kwa kambi ya upinzani.

Baada ya sakata la gas wananchi wa Mtwara wasikie tena bandari yao kwisha kazi na gas inatakiwa kutoka Mtwara kwenda Bagamoyo kwenye eneo maalumu la viwanda-EPZ, huku, Tanga nao matumaini ya kuboreshwa kwa bandari yao sasa itakuwa ni ndoto kwa kuwa bandari mbadala itajengwaBagamoyo kwa nini wananchi wasichukue hatua dhidi ya CCM? bandari ya bagamoyo jengeni lakni jiandaeni kwa adhabu pia, kanda ya ziwa CCM ni taabani, Mbeya kwisha, Kaskazini hakuna kitu, Magharibi CCM chupuchupu kukosa mbunge hata mmoja katka uchaguzi uliopita. Nawakilisha.

Nimelikumbuka lile bango la maandamana ya Mtwara "BANDARI BAGAMOYO, GESI BAGAMOYO, VIWANDA BAGAMOYO, MTWARA WAPUUZI". Tembelea link
JUMA MTANDA: WANANCHI WA MKOA WA MTWARA WAANDAMANA KUPIGA GESI KWENDA DAR ES SALAAM.
 
Kujenga bandari Bagamoyo wakati ile ya Dar haijaboreshwa ilivyo ni matusi ya Kikwete kwa wananchi wa Tanzania kwani anaonesha wazi ubabe wa kupendelea sehemu anayotoka; siku hizi kila uwekezaji ni Bagamoyo ili kumpendezesha Mfalme lakini ijulikane tu kuwa kila jambo lina mwisho wake!!
mimi nafikia sehemu na kuanza kuamini kuwa mwenyekiti anaweza either kwa makusudi au kutooelewa akawa na mpango wa kuifikisha nchi hii anakojua yeye na baadhi ya wenzie wachache. Hii ni kufuatilia matendo yake na zile nyimbo za washauri wabaya kila kukicha huku akijua kinachoendelea.
Ingelikuwa sio hivyo basi angelimfukuza kazi hata Mh. Mulugo/Hamimu/Milambo ambaye chini yake matokeo ya mitihani ni mabaya na imeundwa hata tume lakini pia imedhihirika ana vyeti vya bandia!
Siwaamini CCM kwenye mambo yanayohusiana na mikataba na hasa hii CCM ya sasa!

Hawa jamaa wajapani wamejipanga hadi basi every data and information about our resources and opportunities they have on hand kuna kavita ka interest wanashindana na wachina parallel to our expectation. Si ajabu ukakuta hakuna policy analyst or planner kutoka ikulu aliyesoma mpango huu au huenda waliifanyia skimming tu hyo report ya wajapani kama gazeti la udaku. Bandari ya bagamoyo? wakati Bandari ya mtwara na Tanga zipo katika regional agreement za SADC Hivi akizikacha atajibu nini huyu JK Kwa SADC na partinership ya Mtwara Development Corridor?
 
Wananchi wameishaichoka CCM na sasa wanasubiri kuipa adhabu 2015,,,

Hata kama angejenga bandari pale Msoga, kichapo kutoka kwa watanzania kiko pale pale, watanzania tumeamua kwa dhati kuhakikisha CCM inazifuata KANU na UNIP
 
Hii kali. Maana kama kusoma hatukusoma waTZ ila hata kuona hatuoni?
 
Natamani siku moja bahari iende Moshi, tuone kama jamaaa hawatajenga Bandari Kilimanjaro with a lot of reasons. Kila Mradi wa Umoja wa Mataifa unajengwa Arusha mbona hatulalamiki? Au hakuna Mikoa mingine yenye Ardhi ya kujengwa majengo hayo? Nawaambia kila Raisi wa kizazi cha sasa atakaye ingia madarakani kamwe hata acha kupendelea kujenga nyumbani kwao TUSIDANGANYIKE. KUMBUKENI KIPINDI CHA MAWAZIRI WAKUU KUTOKA KANDA YA KASKAZINI PAMOJA NA WAZIRI WAO WA FEDHA NA UJENZI KIPINDI HICHO ,KILA MRADI ULIKUWA UNAPELEKWA MOSHI mbona hatusemi. Hii dhambi ya JK waliianzisha Viongozi wanaotokea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
 
Hii kali. Maana kama kusoma hatukusoma waTZ ila hata kuona hatuoni?

Zuzu linaona mkuu? acha tu wafanye watakavyo si watanzania kondoo? akupigaye kofi shavu la kushoto mgeuzie na la kulia. Reli ya kati hoi bin taabani, Mwakyembe anajaribu kuchacharika lakini mwisho ataishiwa nguvu tu.
 
Ila usishangae bado kuna watu hawaambiwi kitu Juu ya CCM.
 
Back
Top Bottom