Bandari ya Bagamoyo ikijengwa CCM ijindae kwa adhabu pia

Bandari ya Bagamoyo ikijengwa CCM ijindae kwa adhabu pia

Watu wamenyang'anywa ardhi bagamoyo (kable ya bagamoyo mjini) kwa ajiri ya ujenzi wa eneo maalumu la viwanda yaani EPZ, pale chalinze shirika la nyumba lilijenga maghorofa 2 apartment polini, kwa sasa kuna mradi mkubwa wa maji yanasambazwa chalinze na vijiji vyote kutoka mto wami, na kuna phase 2 inaanza muda wowote, kama Kila Rais atakuwa selfish basi ni hakika kila kabila litapigana Rais atoke kwao. ALitaka kubomoa barabara chalinze segela mbunge seleli kutoka Nzega Tabora akahoji bajeti ilikotoka sasa tumemsahau kwenye siasa.

Napita tu!
 
Kwa hili ninasema tutafanya liwezekanalo, afadhali tuwe na mpango wa majimbo kila mtu ajijue kivyake, ni shida kuwa na baba mdini, mkabila na mfitinishaji wa watu wake kwa mipango dhaifu. Tunahitaji kukasirika na kuamua kwa hasira sasa.

Mkuu toa suluhisho la nini serikali ya CCM ifanye maana kila inachokifanya kinaonekana kibaya. Ijenge Bandari-vibaya tu; ijenge barabara-vibaya tu; inunue meli-vibaya tu; ibadili katiba kwa matakwa yenu-vibaya tu; iteue wakuu wa mikoa-vibaya tu; iwahamishe wafugaji kwa kuwa mifugo yao inasababisha mmomonyoko wa udongo-kwetu vibaya tu...... Sasa ishaurini ifanye nini? As to remain at home doing nothing is not a good option.
 
Kwa hili ninasema tutafanya liwezekanalo, afadhali tuwe na mpango wa majimbo kila mtu ajijue kivyake, ni shida kuwa na baba mdini, mkabila na mfitinishaji wa watu wake kwa mipango dhaifu. Tunahitaji kukasirika na kuamua kwa hasira sasa.

This is not a wise of a great thinker........
 

Hivi Chama Cha Mapinduzi kiliwakosea nini haswa mpaka kila kitu mnakiona kibaya tu? Mnadhani hao mnaowafikiria siku wakichukua madaraka mnadhani mtabaki salama?Fikiria hao jamaa zenu mnaodhani ni watu bora wakati wamejaa ukabila wamepewa tu….mfano kuna ka-taasisi kamoja ka serikali wameendekeza ukabila mpaka kataasisi hako kanakaribia kufariki dunia-wameendekeza ukabila seuze wapewe nchi? Mtakuja kunikumbuka na kuikumbuka CCM sana tu. Waulizeni watu wa Misri walioshabikia mageuzi na leo hii mnajua position yao ilivyo… Kama ilivyo Libya pia.Tusijadili watu bali tujadili hoja kwa manufaa ya Tanzania.

Labda waTanzania wamewachukia pia kwa propaganda chafu na za kibaguzi. Udini na ukabila mnaujenga nyie, ona hapo penye Bluu. Unaweza kubisha kuwa hujaawashawishi waTanzania wenzio kulichukia hilo kabila ambalo hukulitaja (Wachaga)? Mimi naona watu wa aina yako kama ndio wako kwenye hiyo CCM basi haina sababu hata kidogo ya kupendwa. Tukianzia hapohapo, wachaga watakupenda je?

Hivi nikuulize, katika Propaganda zenu, manpofanya mikutano Kilimajnaro, huwa mnawaambia haya, na kuwa hawana haki tena kwa kuwa wao ni WAKABILA? JK alipofanya kampeni na timu yake hawakuwaambia kuwa wao ni wakabila, ila atauzungusha mlima kilimanjaro kwa barabara za LAMI.

CCM waangalie nchi hii itakuwepo hata bila ya ccm au chadema. Tuijenge nchi itakayokuwa mahali pema pa kuishi wajukuu na vitukuu vyetu vya vitukuu vyetu, nao watafanya vivyo hivyo.

Kuna mifano mingi sana mibaya dhidi ya ccm na serikali yake. Leo wanatugawa hata jinsi ya kujipatia kitoweo. Iliwahi kutokea kipindi yakatowa matamko mazito tena yakimlenge mkuu wa nchi kwa kiasi hiki? Jiulizeni na myatendee kazi. Kwanini mchukiwe leo na sio jana? Hamjiulizi, nyie mnawacheki chadema, wakati nyie ndio wenye nchi!

Kama sio upuuzi, basi nyie ni Wapuuzi.

*Upuuzi linatokana na neno puuza, hivyo mtu mpuuzi ni mtu anayepuuza mambo.
 
Mkuu toa suluhisho la nini serikali ya CCM ifanye maana kila inachokifanya kinaonekana kibaya. Ijenge Bandari-vibaya tu; ijenge barabara-vibaya tu; inunue meli-vibaya tu; ibadili katiba kwa matakwa yenu-vibaya tu; iteue wakuu wa mikoa-vibaya tu; iwahamishe wafugaji kwa kuwa mifugo yao inasababisha mmomonyoko wa udongo-kwetu vibaya tu...... Sasa ishaurini ifanye nini? As to remain at home doing nothing is not a good option.

Sio kweli kuwa hawafanyi jambo, jambo lenyewe wamefanya nalo nikusema kuwa ni vibaya! Kama mnataka watende, basi wapeni nafasi muone. (Haya ni majibu mepesi kwa hoja nyepesi)

Nadhani ungechambua kwanini watu wanahoji, tungekuwa na mahali pa kusimama kuenda jambo!
Lakini nchi ya ajabu inayoongozwa na viongozi wa ajabu wasiokuwa na vipaumbele wala maono, ndio maana hawajui sababu ya umaskini wetu nini. Wataweza je kututoa hapa tulipo?

Jengeni bandari, kama mlivyojenga shule za voda faster, mkimaliza jengeni zahanati, barabara n.k Akili yenu inawatuma kuwa maendeleo ya watu ni material
 
I would like to know which wise word should be of a wise thinker, when after all wisdom, sharing, tolerance and patience you end up having the plans that are changing with the blow of wind. You are given a plan in the morning, by noon they are no more, you are given a promise in noon, by evening they are no more. You better get angry.

By the way you might be afraid of the word, angry, but it is even the words of the former wise men, be angry but do not late your anger lead you to sin. So I mean we need to get angry, and through the anger and agitation of what is not been done properly we will be able to force our way to what it should stand; being angry does not mean, been un-wise. otherwise supply me with your expression " this is not a wise of a great thinker..."
 
Huu mradi ni vema tukautumia vema ili kuichonganisha CCM na wnanchi wa maeneo yalioshaulika.ANIA
WATANZANIA WATAMBUE KUWA CCM NI CHAMA CHA FAMILIA YA KIKWETE NA KWA SASA KINATEKELEZA MIPANGO YA KUINDELEZA BAGAMOYO NA KUYATELEKEZA MAENEO MENGINE YA TANZANIA.
CHAMA HIKI HAKIFAI KUENDELEA KUITAWALA NCHI HII KWA NGAZI YOYOTE ILE.......TUKATAE KABISA!
maneno yako ni mazuri sana ila wakusikiao huko vijijini 90% yao huabudu chama na wala sio kupima maendeleo waletwayo na chama! kazi ipo kumuambia mtu kuwa upo matesoni!!!
 
bado nakosa imani na baraza la mawaziri lililojaa watu wanaojiita ma Dr. na ma Prof.

kama watu wa mikoa hiyo wakiendelea kuichagua CCM basi umasikini ni haki yao na waendelee kuwa nao tu

hivi ule mpango wetu wa miaka mitano uliozinduliwa kwa mbwembwe ni serikali ipi inatekeleza?

mkuu ule mpango zilikuwa mbwembwe tu kama zile za wachina kuchimba barabara katikati ya jiji kwa kisingizio cha kurekebisha sewage system mvua ikinyesha kidogo tu barabara zinageuka mabwawa ya samaki.
This is tanzania special
 
Iondoke madarakani na kupisha wengine we are tired of it. Huo ndio ushauri wangu, anyway kwa mipango hii tayari imeshaanza kuonesha inajipanga kuondoka.

Yote uliyotaja hapo juu yakitekelezwa kwa kulenga faida na mafanikio na sio kuweka bomba la gesi toka Mtwara kuja Dar, au kuhamisha goal posts after every aid promise basi tusingekuwa na la kusema. Kwa hiyo suala sio kuwa kila wafanyacho, ila wanapofanya vibaya hicho wafanyacho. Yote uliyotaja hapo juu ukiyaangalia bila kuwa na itikadi ya kupendelea upande utaona kuwa ni mazuri ila yanaharibiwa na mipango mibovu ya kuyatekeleza--- na hiyo ndio kero inayofanya tusichoke kupiga kelele.
 
Mkuu toa suluhisho la nini serikali ya CCM ifanye maana kila inachokifanya kinaonekana kibaya. Ijenge Bandari-vibaya tu; ijenge barabara-vibaya tu; inunue meli-vibaya tu; ibadili katiba kwa matakwa yenu-vibaya tu; iteue wakuu wa mikoa-vibaya tu; iwahamishe wafugaji kwa kuwa mifugo yao inasababisha mmomonyoko wa udongo-kwetu vibaya tu...... Sasa ishaurini ifanye nini? As to remain at home doing nothing is not a good option.

Iondoke madarakani na kupisha wengine we are tired of it. Huo ndio ushauri wangu, anyway kwa mipango hii tayari imeshaanza kuonesha inajipanga kuondoka.

Nyongeza: Yote uliyotaja hapo juu yakitekelezwa kwa kulenga faida na mafanikio na sio kuweka bomba la gesi toka Mtwara kuja Dar, au kuhamisha goal posts after every aid promise basi tusingekuwa na la kusema. Kwa hiyo suala sio kuwa kila wafanyacho, ila wanapofanya vibaya hicho wafanyacho. Yote uliyotaja hapo juu ukiyaangalia bila kuwa na itikadi ya kupendelea upande utaona kuwa ni mazuri ila yanaharibiwa na mipango mibovu ya kuyatekeleza--- na hiyo ndio kero inayofanya tusichoke kupiga kelele.
 
Wakuu kwa kunisaidia mawazo,kwanza bandari ya Dar ni muhimu sana kama jiji kuu lakini hivi ile bandari haiewezi kupanuliwa kukidhi viwango?

Kama ni ngumu kupanuliwa hamuoni ni bora ijengwe kubwa nyingine bagamoyo?

Kuhusu utaratibu wanabodi wa JF!
 
Huu mradi ni vema tukautumia vema ili kuichonganisha CCM na wnanchi wa maeneo yalioshaulika.ANIA
WATANZANIA WATAMBUE KUWA CCM NI CHAMA CHA FAMILIA YA KIKWETE NA KWA SASA KINATEKELEZA MIPANGO YA KUINDELEZA BAGAMOYO NA KUYATELEKEZA MAENEO MENGINE YA TANZANIA.
CHAMA HIKI HAKIFAI KUENDELEA KUITAWALA NCHI HII KWA NGAZI YOYOTE ILE.......TUKATAE KABISA!

keshajibinafsishia mpaka chama kwahiyo tutarajie mama salma ama riz1 kugombea upresidaa next election?
 
Wakati sakata la gesi ya Mtwara halijaisha CCM kupitia kwa Mwenyekiti wake Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete amesaini mktaba wa kujenga bandari nyingine huko Mbegani Bagamoyo Nyumbani kwa Rais, huku zile za Mtwara na Tanga zikiachwa hoi, CCM ikumbuke kuwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni kaburi lake katika uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Tanga, Lindi na Mtwara ni ngome za CCM zilizobaki na itakuwa ni kura ya turufu kwa kambi ya upinzani.

Baada ya sakata la gas wananchi wa Mtwara wasikie tena bandari yao kwisha kazi na gas inatakiwa kutoka Mtwara kwenda Bagamoyo kwenye eneo maalumu la viwanda-EPZ, huku, Tanga nao matumaini ya kuboreshwa kwa bandari yao sasa itakuwa ni ndoto kwa kuwa bandari mbadala itajengwaBagamoyo kwa nini wananchi wasichukue hatua dhidi ya CCM? bandari ya bagamoyo jengeni lakni jiandaeni kwa adhabu pia, kanda ya ziwa CCM ni taabani, Mbeya kwisha, Kaskazini hakuna kitu, Magharibi CCM chupuchupu kukosa mbunge hata mmoja katka uchaguzi uliopita. Nawakilisha.

Bandari zingejengwa Arusha/kilimanjaro ingekuwa sawa. Zinajengwa Uzaramoni inakuwa Nongwa! Acheni bana, kwani kukiwa kuna bandari kote, Dar, Tanga, Mtwara na Bwagamoyo kwani kunashida gani! Mbona SA wana bandari nyingi tu, ebu tazama link hii http://www.southafrica.com/ports/. Achane hizo, kuwa na bandari nyingi ni maendeleo wakuu.
 
Hii kali. Maana kama kusoma hatukusoma waTZ ila hata kuona hatuoni?

kuona tunaona ila kuthubutu kuhoji na kutojua wajibu wetu ndo tatizo ukizingatia na hili la sasa walilokuja nalo la kuteka na kutesa na kuishia kuunda tume isiyokuja na majibu ndo inayowapa woga kabisa waTZ
 
Natamani siku moja bahari iende Moshi, tuone kama jamaaa hawatajenga Bandari Kilimanjaro with a lot of reasons. Kila Mradi wa Umoja wa Mataifa unajengwa Arusha mbona hatulalamiki? Au hakuna Mikoa mingine yenye Ardhi ya kujengwa majengo hayo? Nawaambia kila Raisi wa kizazi cha sasa atakaye ingia madarakani kamwe hata acha kupendelea kujenga nyumbani kwao TUSIDANGANYIKE. KUMBUKENI KIPINDI CHA MAWAZIRI WAKUU KUTOKA KANDA YA KASKAZINI PAMOJA NA WAZIRI WAO WA FEDHA NA UJENZI KIPINDI HICHO ,KILA MRADI ULIKUWA UNAPELEKWA MOSHI mbona hatusemi. Hii dhambi ya JK waliianzisha Viongozi wanaotokea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Kama ni hivyo mwenzako akitenda na kufa kwa dhambi na wewe utataka kuwa hivyo?
 
Ila siku zote mbio za sakafuni huishia ukingoni nao ukingo wenyewe uko jirani
 
Tuliodhani wana uchungu na nchii hii ni sifuri kabisa. Walivaa ngozi ya kondoo kumbe wao ni mbwa mwitu. Masikini Tanzania unaongozwa na wenye tamaa kupitiliza.
 
Nafikiri mtoa mada anatupa ujumbe kuwa, pamaoja na malengo mazuri ya mradi huu kwa Taifa, tatizo hakuna information flow na mikataba inabaki kuwa siri ya wakubwa. kama una maana tuwe great thinkers wote, lazima tusome na kuelewa kwa nini wakoloni walibuni bandari za Tanza na Mtwara. je wewe umefanya utafiti ukajua haya? nafirki ni rahisi kusafirisha mizigo ya Malawi, Zambia kupitia bandari ya Mtwara, kwa kuwa bandari ya Dar es salaam imezidiwa muafaka ni kutumia bandari ya Tanga kwa mizigo ya DRC, Burundi na Rwanda. Tuna plan ngapi katika nchi hii ambazo zimetelekezwa? tujuze plan ya Bandari ya Mtwara.

Ndugu Watanzania wenzangu, tunakwenda wapi? Here is the Home of Great Thinkers lakini kwa maoni yangu siku hizi sisi wadau (na Si JF) tumekuwa dhaifu sana katika kutoa hoja…..Tumekuwa tunajadili watu badala ya kujadili Ideas. Tumekuwa tukikosoa bila kuleta alternative solution na pia tumekuwa hatusomi ama kufanya rejea.Watanzania wenzangu mnataka nini zaidi ndo mridhike? Kujenga bandari Bagamoyo imekuwa nongwa? Sasa mlitaka ikajengwe wapi ? Maana mimi kwetu ni Tabora ukiniambia utanijengea bandari nitakuona wewe una akili timamu kweli ? Na hivi ninyi mnaoiponda CCM iliwakosea nini ? Maana kila inachokifanya CCM ninyi kwenu ni kibaya tu…. Ina maana haijafanya kitu (japo kimoja) kizuri ?

Na huyu Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete aliwakosea nini maana kila kukicha ni kumsema vibaya tu…Hakuna sifa hata kidogo ? Au kwa kuwa alimshinda mtu wa kwenu katika uchaguzi wa Urais ? Huyo Rais mnayemtaka ninyi aje awe rais wa ukanda ataweza kutenda kama mnavyofikiri ? Ataweza kweli maana katika hali ya kawaida Demand mnayomtaka Rais kikwete au hata serikali yake ifanye in no circumstances haiwezekani….. Demand ni kubwa kiliko uwezo…..
Wengi mliochangia mpaka sasa mnajadili individual weakness za mtu badala ya utendaji kazi wake. Halafu hakuna rejea yoyote ya kisayansi mnayoifanya.Nani kasema Bandari ya Tanga ama Dar es Salaam haitajengwa ? Mbona ilitangawza kuwa bandari ya Tanga na Dar es Salaam zitanjengwa (kupanuliwa) na gharama yake kwa ujumla itagharimu dola za marekani bilioni moja na point nne ($1.4bil)…. Hamkusoma ama taarifa ya ujenzi ndo hamuiamini ? Hebu soma hapa : Tanzania to expand Dar, Tanga ports - Business - www.theeastafrican.co.ke

Au kama huwezi soma bila kudownloan soma hapa :Tanzania to expand Dar, Tanga portsThe Tanzania Ports Authority has embarked on an expansion exercise to increase capacity by dredging and construction of two new berths.According to the TPA, the massive $1.4 billion expansion drive aims to serve new markets in South Sudan and neighboring landlocked countries specifically, Uganda, DR Congo and Zambia. TPA Deputy Director General, Julius Mfuko said the authority has set aside $600 million for the construction of Tanga’s new Mwambani port. “Meanwhile the Dar es Salaam port’s, excluding dredging of the channel depth, is estimated to be $523 million,” said Mr Mfuko.
This will also comprise the building of new berths number 13 and 14 adjacent to Kurasini Oil Jetty and turning the single point mooring into a multipurpose facility, Mr Mfuko said. Cassian Ng’amilo, Dar es Salaam port manager, said the construction of berth 13 and 14 would cost $400 million, to be funded by China.
Mr Mfuko said that in two years, the principal ports will have the capacity to cater for one million 20-feet equivalent units per year. TPA is also working on creating a dry port at Kisarawe in the Coast Region in order to decongest the port. The Kisarawe dry port will be developed into a cargo freight station able to handle both containers and vehicles in large numbers. The European Union mission in the country had warned TPA management that it stands to lose business if it does not take urgent measures to fast track cargo clearance at the port. Tanga port, located on the north-eastern Indian Ocean coast close to the Kenya border is the second biggest in Tanzania after Dar es Salaam. Currently, the port has the capacity to handle 500,000 tonnes of cargo annually, but utilises only 76.5 per cent of that capacity. According to Mr Mfuko, most goods passing through Tanga port are imports which include liquid bulk and break bulk cargo, chemicals, machinery and vehicles. The governments of Tanzania and Uganda early this month agreed to fast track the construction of the Tanga-Musoma-Uganda railway line to enable speedy movement of goods between the two countries. According to the agreement, the two countries will expand Tanga and Musoma ports in Tanzania, and build a new port in Uganda to serve the new railway line. The construction of the railway line will fulfil the wishes of Tanzania’s founder, the late Julius Nyerere, who wished to link Uganda directly to the Indian Ocean. It is also expected to open up athird gateway for Ugandan goods to the sea. Uganda’s other alternative are the Mombasa-Kampala route, the Northern Corridor and the Dar-Mwanza to Kampala route, also known as the Central Corridor.
Mr Mfuko said that an environment impact assessment has given the project clearance and the first phase of the construction would start later this year. The port depth would also be increased to cater for larger ships in efforts to increase efficiency. The Kurasini Oil Jetty and single point mooring projects will cost $60 million; the former will have the ability to carry 45,000 tonnes to 80,000 tonnes; while the latter will be receiving multiple products and not handle crude oil as before. “Expansion of these oil delivery points will be completed in 2012, with the single point mooring gearing to handle ships with 120,000 tonnes,” said Mr Ng’amilo. By Leonard Magomba and John Mbalamwezi
Mmejirisha ama hamuyaamini na hayo pia?
Hivi Chama Cha Mapinduzi kiliwakosea nini haswa mpaka kila kitu mnakiona kibaya tu? Mnadhani hao mnaowafikiria siku wakichukua madaraka mnadhani mtabaki salama?Fikiria hao jamaa zenu mnaodhani ni watu bora wakati wamejaa ukabila wamepewa tu….mfano kuna ka-taasisi kamoja ka serikali wameendekeza ukabila mpaka kataasisi hako kanakaribia kufariki dunia-wameendekeza ukabila seuze wapewe nchi? Mtakuja kunikumbuka na kuikumbuka CCM sana tu. Waulizeni watu wa Misri walioshabikia mageuzi na leo hii mnajua position yao ilivyo… Kama ilivyo Libya pia.Tusijadili watu bali tujadili hoja kwa manufaa ya Tanzania. Utaona mtu anaandika ukwere na Upwani kana kwamba kwake yeye ni ufahari sana. Barabara za kwanza kujengwa Tanzania ni za Dar-Moshi-Arusha lakini hakuna mtu alikuwa analalamika maana tulijua ukishamaliza kujenga Dar-Moshi-Arusha basi next step ni kujenga Dar-Dodoma-Mwanza etc, etc kisha nchi nzima inaenea barabara, na ndicho serikali ya CCM ilichokifanya miaka yote hiyo. Au mmesahau jinsi mlivyokuwa mnakanyaga matope magari yakizama kisha mkaambiwa mshuke ili msukume maana gari limezama kwenye matope? Sasa maendeleo yapo kila kona bado tu hamridhiki? Mnataka nini hasa?

UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYOBandari ya Bagamoyo inajengwa kwa malengo maalum mojawapo ni kuwa bandari ya kisasa Afrika mashariki. Pia itahudumia nchi nyingi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.Hizo Bandari mnazozilalamikia eti kwa nini zisijengwe ni kwamba zilijengwa zamani sana hivyo kwa sasa haziwezi kumudu mikiki ya teknologia ya sasa. Zimejengwa kwa kujibana mno na miundo mbinu yake haifai kwa matumizi ya sasa. Kuzijenga upya ni gharama kubwa na pia miundombinu yake ni finyu sana. Ndo maana mahala ambapo pameoneka kukidhi matarajio ya sasa (mojawapo ni nafasi na miundombinu bora) ni Bagamoyo. Haiyumkini kujenga Bandari kwa dola za kimarekani zaidi ya bilioni kumi katika eneo finyua na miundombinu ya kizamani kisa kuwaridhisha watu ili wasiione CCM inakufa…..Haiingii akilini kabisa na haikubaliki!!!!!!Pamoja na kuwa na bandari za kizamani na miundo mbinu haifai kwa sasa lakini Serikali imeamua kuzipanua nazo zilingane na hali ya sasa. Yote hayo ninyi mnaopinga kama wasomi mnayajua yoye haya lakini hamtaki kukubali ukweli. Inauma sana kwa mtanzania wa sasa anayeshabikia kuzorotesha maendeleo kwa kisingizio chochote kile.Je, hao mnaowatukuza na kudhani watakuja kuwaletea maendeleo pindi wakiingia madarakani wameshawahi kujenga japo barabara ya kilomita moja?????
Basi kama mna alternative solution ya ujenzi wa bandari semeni na muishauri serikali ikajenge wapi hizo bandari maana sehemu zenye bahari ni chache-si kila mkoa una bahari.
 
Sio kweli kuwa hawafanyi jambo, jambo lenyewe wamefanya nalo nikusema kuwa ni vibaya! Kama mnataka watende, basi wapeni nafasi muone. (Haya ni majibu mepesi kwa hoja nyepesi)

Nadhani ungechambua kwanini watu wanahoji, tungekuwa na mahali pa kusimama kuenda jambo!
Lakini nchi ya ajabu inayoongozwa na viongozi wa ajabu wasiokuwa na vipaumbele wala maono, ndio maana hawajui sababu ya umaskini wetu nini. Wataweza je kututoa hapa tulipo?

Jengeni bandari, kama mlivyojenga shule za voda faster, mkimaliza jengeni zahanati, barabara n.k Akili yenu inawatuma kuwa maendeleo ya watu ni material

Aliyewanyima nafasi ni nani? Kutokukubalika kwa wananchi isiwe hasira zao kuzimalizia CCM!!! Wawakasirikie wananchi na si CCM maana CCM haipigi kura bali nayo inapigiwa kura na wananchi. Kama wananchi hawawapigii kura watu mnaowapenda lawama zisitupiwe CCM bali ni ninyi mnaowapenda watu wasiopendwa na wananchi.
 
maneno yako ni mazuri sana ila wakusikiao huko vijijini 90% yao huabudu chama na wala sio kupima maendeleo waletwayo na chama! kazi ipo kumuambia mtu kuwa upo matesoni!!!

Kumbe suluhisho mnalo!!! Kushindwa kwenu katika uchaguzi kunachangiwa na hilo hapo juu kwenye red. Sas hasira za kuichukia CCM zinatoka wapi??? Kwa nini msichukue hatua kuwashawishi watu wawapende na ninyi na si kuichukia CCM kwa vile inapendwa na wananchi.
 
Back
Top Bottom