Bandari ya Mombasa Yatoa Ofa Kwa Mizigo ya Congo DRC na Kutishia Uhai wa Bandari ya Dar. TPA na Serikali mmejipangaje?

DRC wakishaondoka bandari ya Dar tutapata majibu yake kwa ongezeko la wigo wa kodi ili kufidia pengo la makusanyo ya bandari.


Namshauri Rutto apunguze kodi ya mapato kufikia hata 49% off ataona namna makamouni makubwa yatakavhoenda kuwekeza pale Kenya.

Sisi tuendelee na upumbavu wetu wa kuwakamua wananchi bila huruma hadi tukome
 
Nyie endeleeni kubadili wakurugenzi wa bandari tu
 
Hayo mamuzi ya Kenya kuhusu bandari ya Mombasa si kwa manufaa ya Wakenya. Haya ni maamuzi ya kuwakomoa wale waliomkabidhi madaraka juzi haina tofauti na maamuzi ya kuhamia Dodoma ya lilenga pamoja na mambo mengine kuwanyi mapato ya pango wale waliowekeza biashara za rea estate DsM kwenye awamu ya 4.

Hilo la DRC kupewa Bandari kavu wala usidanganywe nalo kama ilivyo Tz bandari kavu ni mzinga wa babu tena wenye wale nyuki wadogo wa asali yenye thamani kubwa. VIvyo hivyo ungejiongeza kidogo tu hapo Kenya hiyo ardhi waliyopewa DRC inamikiwa na nani na kwa manufaa ya nani?
 
Mizigo ya DRC haiwezi kupita Tanga?
 
Ruto anaonesha sio tu kwanini aliutaka urais, ila pia, alijua akiupata ataufanyia nini kwa faida ya nchi yake, hawa ndio aina ya wale marais wanaolala na ma-file vitandani.
yaani hivyo tu!!??!!, Remember, RUTO ni mfanya biashara mkubwa, inawezekana ni kwa maslahi ya KENYA lakini yeye na watu wake wa karibu ndio wakawa wanufaika wakubwa. Rias mstaafu(UHURU) aliwahi kutahadharisha kuhusu huyu jamaa. ngoja tuone
 
Ufanisi wa bandari ya Dar ni mdogo na utaendelea hivyo kwa vile watawala wetu hawaangali ufanisi wa bandari kwa ujumla wake (holistically). Upakuaji wa haraka lazima uendane na usafirishaji wa haraka, kwa maana nyingine lazima kuwepo na access road za bandari tu. Kwa sasa malori yakienda na kutoka bandarini yanapishana na daladala, bajaj, boda boda, etc. Ndiyo maana kutoka bandarini hadi Kibaha inaweza kuchukua hata masaa 6, hapo hatujaweka msururu wa vikwazo vingine mpaka kufika mipakani.
 
mleta mada tukilalamikia utitiri wa kodi kwenye hii nchi,huwa unatetea serikali sijui leo umepatwa na nini mpaka kuona utitiri wa kodi ni tatizo!.
 
bado tunaweza kushindana na tukafanya vizuri tu, kwanza DRC tumepakana nayo bega kwa bega tena kwa strech ndefu tu, lakini pia TPA imejenga DRYPORT ndani ya DRC yenyewe,ikitumika vizuri bado tupo mbele ya Mr.bill. naamini barabara ya katavi ni nzuri, naamini pia kuna mpango wa kuiunganisha mtwara na katavi kwa lami, hapo tutaingia drc via mpulungu kiulaini tu.
 
Mazuzu yetu acha yajikanyage tupigwe KO mchana kweupe kama kawaida
 
Kwa akili za akina mwigulu hapo tunapigwa tatu bila, huko Rwanda na Burundi nao wamepewa ahueni mombasa sio muda wanahama kama kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…