Bandari ya Mombasa Yatoa Ofa Kwa Mizigo ya Congo DRC na Kutishia Uhai wa Bandari ya Dar. TPA na Serikali mmejipangaje?

Kijiografia nchi yetu ilivyo ni aibu kwa drc,rwanda na burundi kutumia bandari ya mombasa lakini hii yote inaletwa na uzembe wa viongozi wetu,viongozi uwezo wa kufikiri income itokane na kumnyonya mwananchi lakini si rasilimali,malawi mdogo mdogo anaacha kutumia bandari yetu anatumia ya maporini huko mozambique
 
Huwa sielewi kwanini Congo DRC anatumia bandari za nchi nyingine wakati yeye mwenyewe kapakana na bahari?

Kwa mwenye majibu tafadhali?
Sifahamu kuhusu bandari yao lakini hii mizigo inayopitia Mombasa na Dar huwa inatokea Asia, kwani nafuu kupitia nchi hizi kuliko kuzunguka hadi Atlantiki.
Pili Congo ni kubwa inaonyesha hii mizigo ni ya mashariki mwa Congo
 
Ngoja tunyoshwe tu hamna namna
Ndio maana Kagame aliwahi kutuambia tumpe bandari Dar, ili yeye aindeshe kutuonyesha vile hiyo bandari yaweza kuingiza pesa kibao kwa nchi, nyie mkatolea nje.....sasa ngoja Kenya wawaonyeshe jinsi ya kufanya, na sasa kila mtu ashinde mechi zake.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT, bila shaka mnaendelea kuchapa Kazi..

Kama inavyosomeka kwenye kichwa cha habari, Bandari ya Mombasa imetoa Ofa kabambe na kedekede Kwa Mizigo ya Congo DRC kupitia kwao, Kifurishi cha Ofa kinahusisha mambo yafuatayo;

1. Kupunguza gharama za kuhifadhi mizigo.

2. Kufuta gharama na vikwazo visivyo vya kikodi barabarani.

3. Kuwapa eneo Ili wajenge Dryport yao Ili wawe wanahifadhia mizigo yao hapo.

4. Ofa zingine za ki institutions.

Naomba ikumbukwe kwamba Bandari ya Dar inategemea zaidi mizigo ya Congo DRC kwa mapato sasa kwa Ofa hizi ni wazi bandari ya Dar inaenda kuwa tembo mweupe.

Ni vyema serikali kupitia TPA nao wakaja na counter offensive za kukabili ushindani wa kibiashara na kuongeza competitiveness yetu kwenye biashara ya logistics.

Tanzania inaongoza kwa kuwa na utitiri wa Kodi na tozo kwenye biashara bila kusahau utitiri wa vikwazo visivyo vya Kodi NTBs kama mamizani kila sehemu,traffic kila sehemu,sijui parking za malori za Halmashauri na blaa blaa zingine kama hizo.

Tukiendelea hivi bandari yetu itakuwa tembo mweupe na ikumbukwe kwamba hakuna kosa Wakenya Wamefanya ila ni mbinu za kukuza biashara.

Source> Uchumi Forum👇

View attachment 2357571View attachment 2357576View attachment 2357577
Tumepoteza bahati ya mtende ya kuwa na Bandari ya kisasa yenye uwezo wa kupokea meli kubwa za 4G, kwa ujinga wetu. Hakuna nchi yoyote hapa duniani inayoweza kukataa uwekezaji wa mradi wenye thamani ya USD 100B!! Sisi tungekuwa wakushindana na Durban, sio Mombasa.
Hiyo SGR itatengeneza faida kwa kubeba abiria mwaka gani?
 
Labda DRC ya upande wa Goma huko.
Kwa Lubumbashi haiwezekani kuikwepa bandari ya Dar.
 
Lissu anasemaje?

Ameiombea mabaya kwa muda mrefu sana Tanzania ashangilie sasa.
Wewe na mtoa mada wote ni makumbaff tu, huku mnatetea Tozo haramu halafu mnategemea kizazi hai chenye fikra tunduizi kama za Lissu kiwaunge mkono wajinga? Hapana, huyo sinked falla cost si huwa yupo humu akitetea ujinga 24/7?na wewe ndiye chawa wake? Wenye akili wanajua jinsi ya ku deal na uchumi bila kumuumiza mwananchi, nyie mkilala Tozo mkiamka Tozo, maujinga kabisa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Lipa tozo Kwa maendeleo ya Nchi yako.
 
Nawasalimu kwa jina la JMT, bila shaka mnaendelea kuchapa Kazi..

Kama inavyosomeka kwenye kichwa cha habari, Bandari ya Mombasa imetoa Ofa kabambe na kedekede Kwa Mizigo ya Congo DRC kupitia kwao, Kifurishi cha Ofa kinahusisha mambo yafuatayo;

1. Kupunguza gharama za kuhifadhi mizigo.

2. Kufuta gharama na vikwazo visivyo vya kikodi barabarani.

3. Kuwapa eneo Ili wajenge Dryport yao Ili wawe wanahifadhia mizigo yao hapo.

4. Ofa zingine za ki institutions.

Naomba ikumbukwe kwamba Bandari ya Dar inategemea zaidi mizigo ya Congo DRC kwa mapato sasa kwa Ofa hizi ni wazi bandari ya Dar inaenda kuwa tembo mweupe.

Ni vyema serikali kupitia TPA nao wakaja na counter offensive za kukabili ushindani wa kibiashara na kuongeza competitiveness yetu kwenye biashara ya logistics.

Tanzania inaongoza kwa kuwa na utitiri wa Kodi na tozo kwenye biashara bila kusahau utitiri wa vikwazo visivyo vya Kodi NTBs kama mamizani kila sehemu,traffic kila sehemu,sijui parking za malori za Halmashauri na blaa blaa zingine kama hizo.

Tukiendelea hivi bandari yetu itakuwa tembo mweupe na ikumbukwe kwamba hakuna kosa Wakenya Wamefanya ila ni mbinu za kukuza biashara.

Source> Uchumi Forum👇

View attachment 2357571View attachment 2357576View attachment 2357577
Hizoi ni ofa hewa! kenya haina ardhi ya kutoa bure kwa DRC ILI IJENGE BANDAR KAVU!
 
Back
Top Bottom