Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 4,035
- 11,462
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Profesa Makame Mbarawa, ameipongeza Bandari ya Tanga kwa kuandika historia kwa kuwezesha kukusanya takribani bilioni 100 ndani ya miezi mitano.
Hayo ni matokeo ya uboreshaji wa miundombinu ya bandari hiyo uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliogharimu bilioni 429.1
Katika ukusanyaji wa mapato hayo, bilioni 38.53 zilikusanywa na Bandari ya Tanga na bilioni 57 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga.
Prof. Mbarawa ametoa Pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari ya Tanga ili kukagua maboresho makubwa yaliofanyika katika bandari ya hiyo.
Katika kipindi hicho cha miezi mitano pia Bandari ya Tanga imefanikiwa kuhudumia meli 172 ikiwa ni zaidi ya lengo la kuhudimia meli 90 kwa miezi mitano.
Mhe. Waziri huyo, aliendelea kwa kusema kuwa, mafanikio hayo ni matokeo ya uwekezaji wa sh. bilioni 429.1 uliofanywa katika kuboresha magati mawili yenye urefu wa mita 450 pamoja na ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo ya wateja.
“Matokeo yameonekana, ni wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo gharama za uwekezaji zitakuwa zimesharudi. Ajira zimeongezeka kwa sababu watu wanafanyakazi muda wote,” alibainisha.
Aidha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Juma Kijavara amesema, Serikali imetoa kibali cha kujenga gati maalum kwa ajili ya meli za makasha. Ujenzi wa gati hiyo ambayo itakuwa na urefu wa mita 300 mchakato wa kumpata mkandarasi karibu unakamilika. Pia itajengwa gati ya mita 50 kwa ajili ya meli za abiria.