Bandari zetu ni masalia tusikubali nazo zitutoke

Hii nchi ina utajiri mwingi sana ila wananchi wake ni masikini balaa. Mchina, mwarabu, mrusi na mzungu anatamani sana atapataje mali hizi kwa masikini, anatumia kila njia ikiwemo amani na vita. Njia ya amani ni hiyo mikataba ya kijuha, akiona hutaki amani anakupandikizia vita kwa kuunda vikundi vya waasi wenye itikadi kali za kidini, kikanda au kikabila mvurugane msiwe pamoja ili apore rasilimali kiurahisi. Taifa likiwa na wajinga wengi wasomi matokeo yake ni kugawa rasimali za nchi kama njugu kijuha
 
CCM wamejiapiza kwamba lazima wauze kila tulichonacho
 
Kuna Jaji mzalendo jina kapuni, Amegoma kabisa kununuliwa. Tulia katumia kila njia kagoma. Samia katuma watu amegoma. Tusubirie ili tusivuruge kesi. Huyu Jaji mtamjua tu. Ni mzalendo wa hali ya juu. Vitisho vya Tulia na usalama havijamteteresha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hivyo tujue tu wananunua kesi. Majaji watavunja heshima yao. Wazalendo wanajiandaa kukata rufaa mahakama ya rufaa.
Hakika tutashinda hauzi mtu bandari zetu uarabuni.
 
Mbona unahangaika sana mtu mzima?!!! Mwanahisa wa TICS nini?!!!

Ingependeza ukaweka hoja zako bila kuzushia wengine kwa vijiuzushi vya kitoto.......yaani Mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, ahangaike na kina mwabukusi sijui mwambusi?!!!!!🤣🤣🤣🤣
She's more than that!!
 
 
Mkuu kitendo cha Jaji mmoja kupata dharula, kumbe ni mbinu chafu na imeshaongelewa sana kwenye "supesi",kwamba ni rafu ambayo huchezwa na maJaji wa serikali wanapoona "hukumu" imeegemea upande wao.

Ni mbinu ambayo hutumika kutaka kuchezea hukumu ya haki ambayo haina maslahi kwao.

Kama "Jamhuri" ingelikuwa ndiye mlalamikaji na wanaenda kushinda, siku ya hukumu hauwezi kusikia eti Jaji ana udhuru ama dharula nk nk na mifano ikatolewa mingi tu!

Hukumu imeshaonesha imeegemea kwa "mlishi", sasa wanaenda kuuliza: ..."eti mkuu tuhukumu hivyo hivyo au tutamuudhi mama ...?"

Kama itakuwa ndiyo kweli mbinu hizo chafu zinachezwa, wewe unategemea nini cha maana hapo?

Na kuna viashiria kwa mfano, kuna "Siaijii" mwandamizi anayechukuliwa kama kioo cha jamii, kuweza kuweka maoni yaliyoegemea kutetea mkataba kabla ya hukumu, kuna cha maana hapo jamani?

Kumbe hapa Tz usitegemee usomi ama title ya mtu kuisaidia nchi hasa linapokuja suala la uchama na takataka zingine!

Kesho natabiri dana dana kuendelezwa kwa sura nyingine ama kutolewa hukumu ya aibu itakayoligawa Taifa.
 
Hukumu imeshaonesha imeegemea kwa "mlishi", sasa wanaenda kuuliza: ..."eti mkuu tuhukumu hivyo hivyo au tutamuudhi mama ...?"[emoji3064][emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…