Bandari zetu ni masalia tusikubali nazo zitutoke

Hivi Abu Dhabi wana migodi kama sisi?

Wana Bahari na Maziwa kama sisi?

Wana Mbuga za wanyama kama sisi?

Wana gesi kama sisi?

Wana Nickel kama sisi?

Wana uoto mzuri wa Asili kama sisi?

Wana vivutio vya utalii kama sisi?

Wana Mlima Kilimanjaro kama sisi?



TUMESHAUZA VYOTE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waacheni: "Nimeacha kusemasema kwa sababu waTz wanaojua zaidi ni wengi na wanaamini zaidi wanayoyajua.

Katika Misc CrimCause no. 2/2023 kuna hoja ya Kamishina Jenerali wa Magereza wa sasa ambaye rekodi zipo alikufa 1993. Ukiwambia mkopo wa AbuDhabi ulikotoka wataelewa?"...Mwalimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kwa hisia sana mkuu!

Ila usijali, kuna kitu kinaniambia kuwa bandari hazitachukuliwa.... hata vilivyochukuliwa kienyeji vitarudi.

Kwa imani yangu siachi kusali na kuliombea taifa langu.
Kusali tu hakutoshi lazima kuchukua hatua , nchi haikombolewi kwa kusali tu bali kwa kufanya maamuzi magumu! Watu ni lazima tujitoe muhanga kama sadaka nchi ikombolewe kwa faida ya vizazi vijavyo.

Hukumu itakayotolewa na mahakama kwa kukandamiza haki itachochea ukombozi wa nchi hii!
 
Umeongea kwa hisia sana mkuu!

Ila usijali, kuna kitu kinaniambia kuwa bandari hazitachukuliwa.... hata vilivyochukuliwa kienyeji vitarudi.

Kwa imani yangu siachi kusali na kuliombea taifa langu.
Una sali? [emoji848]
 
Kwenye hii Tanzania ya sasa [emoji848]itakuwa miujiza atokee mtu aache tumbo lake na njaa
 
Mkuu nimeisoma sijaielewa!

Nimeigeuza geuza wee, lakini hola!

Kwamba huyu mjelajela #1 original kuna hukumu ilitoka kueleza kadanja?

Kesi ilihusu nini mkuu, embu tia tia nyama kdogo.
 
Mawakili wanaoshitaki wenyewe hawana hofu. Wewe hofu ya nini. Subiri hukumu. Iwe masika kuna nafasi ya kukata rufaa. Iwe kiangazi kuna nafasi ya kukata rufaa. Jiandae tu kwa lolote kati ya kushinda au kushindwa. Rufaa ni haki ya wote. Mguu sawaaa!
 
Nimekumbuka maneno ya Azizi Ki wa Yanga Yangu.
Ni simu tu zinatembea kwa sasa na vocha za tiGo.
 
Kamanda naona unashusha vitisho si mchezo, tunakutegemea kuanzia kesho tukuone 'live', na si kuona maneno yako tu humu, ukituongoza katika kulianzisha kuelekea ikulu kumtoa Samia akae Mbowe au Tundu lissu!!
 
Kamanda naona unashusha vitisho si mchezo, tunakutegemea kuanzia kesho tukuone 'live', na si kuona maneno yako tu humu, ukituongoza katika kulianzisha kuelekea ikulu kumtoa Samia akae Mbowe au Tundu lissu!!
Nadhani muda si mrefu tutakuwa Niger! Mapinduzi ya wananchi! Sio Mbowe wala lissu wote ni hao hao !
 
Mawakili wanaoshitaki wenyewe hawana hofu. Wewe hofu ya nini. Subiri hukumu. Iwe masika kuna nafasi ya kukata rufaa. Iwe kiangazi kuna nafasi ya kukata rufaa. Jiandae tu kwa lolote kati ya kushinda au kushindwa. Rufaa ni haki ya wote. Mguu sawaaa!
Hofu sina pia, ninajua ngoma hii ni mbichi, maana kila upande umeangalia hapo hapo.

Hatuwezi kuelewa siri ya M/Mungu kutupitisha kwenye tanuri hili.

Mimi ndivyo naamini kuwa hukumu mbovu yaweza kuwa na manufaa kwa jamii, kwa sababu inaweza kuwa ndiyo chanzo cha jamii kujitambua ama kutambua ya sirini ambayo yalifichwa na sasa kwa kupitia hili saga mambo yakaeleweka hata na mpumbafu.

Tuombe uzima, twaweza kuona mengi yajayo kwa muda mfupi tukayastaajabia!
 
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na wakili Boniface Mwabukusi na wenzake iliyokuwa inapinga serikali ya Tanzania kuingia mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na serikali ya Dubai ikilenga kushirikiana katika Uwekezaji Bandarini ambapo kampuni ya DP WORLD kwa niaba ya Dubai watashirikiana na TPA kwa niaba ya Tanzania zitashirikiana kuendeleza maeneo maalum ya kiuchumi ikiwemo uendeshaji wa Bandari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaji Dunstan Ndunguru anasema Mahakama inakubaliana na hoja ya waleta maombi, kwamba ibara za IGA zimevunja sheria za ulinzi wa Rasilimali, kwa kupeleka migogoro nje ya nchi.Lakini anasema dosari hiyo haitatumika kutangaza IGA kuwa ni batili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hila ya Majaji mbona tuliigundua mapema sana tangu siku waliposema kuwa mmoja wao ana udhuru?

Na hayo tuliyaongea kabla ya hukumu, tuliyabashiri haya kwa usahihi kutokea na ndivyo ilivyokwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…