Pre GE2025 Bango alilotoa Makonda linamhusu mnazi wa Mtama, Lindi

Pre GE2025 Bango alilotoa Makonda linamhusu mnazi wa Mtama, Lindi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu muungano wa ovyo kabisa , Tanganyika tunahishi bila kiongozi yoyote lakini Zanzibar inatoa maraisi wawili , mkoa wa Zanzibar ukapate mgao wa asilimia 20,
Tanganyika tutabaki kubwa jinga
 
View attachment 2874253
"Usibeze mtu kesho anaweza kuwa boss wako"

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo January 16,2024 ameongea na Waandishi wa Habari katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar wakati akitoa taarifa ya ziara ya kichama ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mikoa minne ya Unguja January 17-18,2024 ambapo pamoja na mambo mengine amesema CCM huwafundisha Watu kutodharauliana.

Makonda amenukuliwa akisema “Kwenye Chama chetu sisi tunasema uvumilivu ni jambo muhimu sana na kumuheshimu Mtu kwasababu leo unaweza ukambeza Mtu kesho ukamkuta ndio Boss wako, hupaswi kuwa na Adui kwamba Mwanachama mwenzako unamnunia, wewe Mzee wangu ulitegemea kuniona Mimi nimekaa hapa kwenye kiti!?”

“CCM ndio Chama pekee Duniani kinachowafundisha Watu kutokumdharau Mtu kwasababu ametoka kwenye nafasi, ni CCM tu kwasababu inakuonesha kabisa kwamba huyu uliyemdharau leo hii kesho huwezi kujua kwahiyo hata Mimi nafundishwa waliopo nje ambao hawana nafasi kama niliyonayo napaswa kuwaheshimu kwasababu kesho wanaweza kukaa kwenye kiti kama hiki halafu nikahitaji msaada wao wa kunisemea tu ili niende kuwa sehemu fulani na nafasi fulani “

Kuhusu ziara ya Rais Samia Makonda amesema itafanyika katika Mikoa ya Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini na Mkoa wa Magharibi “Bahati tuliyonayo anapotutembelea Mwenyekiti wa Chama ambaye ni Rais wa Nchi hata zile changamoto ambazo tulitamani Rais wa Nchi kuzitatua inakuwa nafasi nzuri ya kuzieleza”

Millard Ayo
Ajifunze kwanza alivyokuwa anamnyanyasa Chongolo wakati yeye ni RC dsm
 
Dongo lake mwenyewe maana alimwambia aliyekuwa boss wake Bw. Chongolo awe na adabu kipindi yeye ni RC. Ila Bw. Chongolo hakuwahi kulipa kisasi hata alipopata Ukatibu bado alisema sifa za ujenzi wa ofisi za chama DSM apewe Makonda.
Tenda wema nenda zako
 
Back
Top Bottom