Bank kutuma pesa kimakosa

Mzee wewe unge ila?
Unajua hiyo pesa kuingia kwenye account yake twice haikua bahati mbaya.
Hapo wajomba walichomeka mshahara wa mtu hewa kisha wakaupitisha kwenye account ya huyo jamaa then alipo ipata wakampigia kwamba imekosewa na wakamwambia airudishe kwenye account namba nyingine ambayo ndio yakwao
 
Mzee Wacha siasa, hebu sema unge zila?
 
Em waweke kwangu hizo pesa, mbona watafurahi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo bank huwashindi mbinu.

Hela ikiingizwa kwako kimakosa ukaila, elewa umejikopesha bila kujaza fomu.

Zipo sheria zinazokubana mteja kuwa mwaminifu na kurejesha fedha zinazotua kwako kimakosa, lakini bank huwa hawajishughulishi na kesi bali wanashughulika na account yako tu.

Kama ni mfanyakazi na mshahara wako unapitia bank hiyo ndiyo kabisaa, hawahangaiki na wewe!

Kuna program wanaitega kwenye account yako, kila pesa itakayoingia utaiona lakini ukiangalia salio utaikuta imening'inizwa juu, huwezi kuitoa.

Na hawana huruma hadi kiasi ulichochukua kitakapomalizika.
 
Ningeziacha kwenye account ili nione kama wamezihamisha then baada ya hapo ningeamua nini la kufanya
Wakizihamisha jukwaju hiyo inakuwa siyo fraud, inakuwa waliziingiza kimakosa kweli.

Ila wakikubembeleza uzihamishie account nyingine, elewa kuwa huo ni mchezo.
 
Pesa inachepushwa kimya kimya sahizi ipige ilikua ni shilingi ngapi
 
Ulipanic na kuchoma mafuta bure Moshi, msala haukukuhusu.
Kula naye siyo kufa naye.
 
Mkuu mwenyew imekuta desemba yaani sku mshagara unaingia ndo sku pesa imeingia kimaKosa tena kiasi kilekile,ila skuwa notified. Niljua baada ya kuchek balance maana nikuwa nmedepoisit vihela kadhaa sku chacche nyuma. Niliiacha wiki kadhaa then nkaenda kuchukua bank statement kujua pesa imetoka wap.

Baadae jua la January lilivyokuwa kali nkaipiga panga kias flan. Mwishon mwa Jan mwishon watu wa bank husika wakanipigia sim, nkawauliza how walikosea wakanieleza maelezo yaliyo nilidhisha nkawaomba wamwambie huyo mkoseaji asirudie kukosea staki usumbufu.
 
Noma mzee unatumika hapoo.. Kama wamekosea tena waambie watu wa bank nfo warudishe hizo hela ila Ukizituma wew kwa Acc namna nyingine Asilimia 100 kikiumana na wewe upo kwenye msalaaa..! Mambo ya hela noma mzeee unaweza jikuta kwenye majanga bila kutarajia.
 
Wakikudai tena waambie wajieleze kwa maandishi ni kwa nini kila wakati wanakosea kutuma mihamala halafu inakuja kwako.
Isije ikawa kuna wafanyakazi wanaiba hizo hela kijanja kwa kuzichepusha kwako sasa mwisho wa siku wakikamatwa na wewe utaonekana mnashirikiana kuiba pamoja.
Kwa hiyo lazima uweke njia za kuwa na ushahidi likitokea lolote baadae.
 
Usimuliaji wako unachekesha sana.
Kaka wamechukua yote sina hata 500 mfukoni.
Eti mwenzako yuko polisi huku njoo umsaidie si mlikuwa mnatumia wote.
Kaka nimetoka,mahabusu haina mwenyewe.
Hahahaha
 
Huo ni mtego. Kuna siku utakuta deni kwenye account yako hutaamini. Wakikwambia uitume kwenda account tofauti na ile iliyotuma pesa kuja kwako, nenda bank yako kisha hamisha pesa kutoka kwako kwenda kwenye account husika. Au omba kuonana na meneja wa tawi na umwambie warudishe muamala husika kwa aliyeutuma.

Hapo wanachofanya ni kutakatisha pesa na wakikamatwa wewe unakuwa mtuhumiwa pia kwasababu itaonekana ulikuwa ukipokea pesa hizo
 
Pesa ikiingizwa kimakosa kwenye akaunti ya mtu inatakiwa iwe reversed the same day kwa kutumia same system ilowekwa hio pesa kimakosa.
Ikitokea imelala kwenye akaunti ht siku 1 tu lazima ipatikane ridhaa ya aliewekewa hio pesa ndio pesa itoke......tena vyema aitoe mwenyewe mwenye akaunti. Bank kutoa hela toka kwenye akaunti ya mteja hata km ilikosewa ni makosa makubwa. Tena muhusika anaweza hata kui-sue bank km atataka.
Ndio maana huwa wanamtafuta mteja arudishe. Au wanai-hold asiweze kutoa kile kiasi. Au wanaondoa facilities zote za kutoa hela mpk ujipeleke bank mwenyewe...
Kuhusu kuwekwa mara ya pili inawezekana kuna uzembe toka kampuni ya wanaolipa huo mshahara ndio wamekosea namba. Tena inawezekana wanarusha wenyewe kwa EFT. Bank inawasaidia tu kukutafuta wewe kwa sababu ndio wana contacts zako.
Akaunti kutumika kwa money laundering sio rahisi kuchagua tu akaunti yyt. Wangefungua wao akaunti ya kuitumia na wanakuwa tayari ni mtu wao. Hawawezi kupick tu randomly akaunti ya mteja wasiemjua.
 
Kwa kuwarudishia kwa kuwatumia kwenda account nyengine unahalalisha wizi wao na huo mchezo mwisho wa siku itakuletea shida, Muhimu kama wamekosea kuweka pesa kwako wao wanapaswa kuitoa wenyewe kama walivyo iweka na si vinginevyo
 
Yani bank wanatuma hela kwenye laini yako au vipi mkuu
 
Yani bank wanatuma hela kwenye laini yako au vipi mkuu
WAlishanitumia hii mara ya tatu
Katika line yangu
Na benk ya kwanza mara mbili
Na hii ya hivi karibuni ni benki tofauti na ya mwanz mara 1
KIwango hakitofautiani sana kilichotumwa,ni 3k na kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…