Bapa limepita na mzee wa upako

Bapa limepita na mzee wa upako

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Alianza kama anatania vile mara... "... oooh kunywa pombe sio dhambi.." kumbe mzee wa upako alikuwa anagida bapa huku anaombea na kupaka mafuta ya 'upako' wagonjwa na wenye shida mbalimbali.

Akitoka kwenye huduma anapita na bapa, bapa likaweka maskani katika ubongo wake kisha likampotezea upako wake wote.

Leo hii mzee wa upako hamtambui Yesu kuwa ni Mungu.

Biblia inaonya... ".. Msilewe kwa mvinyo ambao kuna ufisadi ndani yake.."

Bapa limeshapita na mzee wa upako, hana upako tena, kwa sasa ni mlevi tu kama kina John Walker.

Wana familia wa madhabahu ya mzee wa upako pale Kibangu tujuane hapa.

1718079032693.jpg
 
Mwacheni na mambo yake
Kwake hiyo ni njia ya ujira na utafutaji kama walivyo wakulima na wafanye biashara wengine.

Unashangaa huyo
Vipi wale wanaobariki mashoga
Vipi wale wa mabikra 72 na moto ya pombe
Vipi wale wanaouziwa maji, mchanga na mafuta kwa pesa ndefu
 
Yuko sahihi:
Yohana 20:17
"Yesu akamwambia: “Acha kuning’ang’ania, kwa maana bado sijapanda kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu, nawe uwaambie, ‘Ninapanda kwenda kwa Baba yangu na Baba yenu na kwa Mungu wangu na Mungu wenu"
Itakuwa u mwanafamilia wa timu bapa wewe
 
Alianza kama anatania vile mara... "... oooh kunywa pombe sio dhambi.." kumbe mzee wa upako alikuwa anagida bapa huku anaombea na kupaka mafuta ya 'upako' wagonjwa na wenye shida mbalimbali.

Akitoka kwenye huduma anapita na bapa, bapa likaweka maskani katika ubongo wake kisha likampotezea upako wake wote.

Leo hii mzee wa upako hamtambui Yesu kuwa ni Mungu.

Biblia inaonya... ".. Msilewe kwa mvinyo ambao kuna ufisadi ndani yake.."

Bapa limeshapita na mzee wa upako, hana upako tena, kwa sasa ni mlevi tu kama kina John Walker.

Wana familia wa madhabahu ya mzee wa upako pale Kibangu tujuane hapa.
Mkuu pombe haijawahi kuwa dhambi wala Yesu sio Mungu kwa mujibu wa Bibilia

Ni kutokujua kwako maandiko ndio tatizo lako
 
Back
Top Bottom