Siku ya kwanza kufika Runzewe nilifika saa moja asubuhi bado Kuna ka Giza. Lkn supu zilikua tayari. Basi nikapata supu ya Moto, nikauliza mbona ka mji kenu kamepoa Sana. Nikaambiwa subiri. Basi nikatoka nikaitekenya 2.8 nikaenda Rusumo chap. Ile narudi saa nane, aloo ndio nikaona wanyama wenyewe. Twiga za kitusi, viboko vya kisukuma, miguu ya bia ya kihaya, swala za kinyaturu, digidigi za kiluguru, vifaru vya kisukuma na nyumbu zisizo na idadi. Nikaambiwa nyumbu huna haja ya kupeleka gesti. Subiri Giza kidogo omba mkeka wa taniboi Zama chini ya Lori. Buku yako tu.
Bahati nzuri nilikua muoga. Maana wakati unaingia Runzewe kuna kibao kimeandikwa kwa maandishi makubwa mno.
SASA UNAINGIA RUNZEWE
HAPA UKIMWI UPO.